Ukweli kuhusu Jane Urassa - mke aliyeuawa kwa risasi 💔

Ukweli kuhusu Jane Urassa - mke aliyeuawa kwa risasi 💔

Yote ya yote hata kama siamini ulichokiandika Aunt,
Kwanini huamini mpwa?
ukweli ni kwamba jamaa alikosea kumuua mzazi mwenzake kisa mali.
Ni kweli
Nje ya hayo mbona matukio yapo mengi na wanajamiiforums wengi wanapitia.
Ni kweli migogoro ya ndoa ni mingi na kuna mingine wanawake ndiyo chanzo na mingine wanaume ni chanzo.
Wote inabidi kuingia kwenye hizi taasisi tukiwa tayari na kupunguza tamaa, ziwe za kifedha au kimwili.
Ni vile wengi tunacomment kwa sifa na ni bongo zilizolala.
Unamaanisha nini?
 
Sasa mahi, kwanini Huyo Jane asingeacha utambulisho usome wa kweka, hadi mtoto akifikisha umri wa 18yrs ndipo wafanye taratibu za kubadilisha? Tatizo lilikua nini yaani?
Sijui Mahi, ila inaonekana kulikua tayari na migogoro na changamoto nyingine.

Navyoona mwanaume kajenga kwa mke akakosa sauti ya maamuzi, na Jane naye akatumia ubavu wa umiliki wa kiwanja, kufanya maamuzi yanayopingana na matakwa ya Kweka. Mwishowe, wote wamekosa.
 
Kila binadamu ni mbaya.

Si wanaume wala wanawake.

Lakini jamii inataka kuaminishwa kwamba wanawake ni innocent people.

Kwamba wanaume ndio wabaya tu.
Mimi siamini wanawake wote ni innocent.

Wapo wanawake wengi ambao ni chanzo cha matatizo kwenye mahusiano yao, ila pia wapo wanaume wengi ambao ni chanzo cha matatizo vile vile.

Wote tutumie busara kwenye maamuzi, naamini Kweka alitumia hisia kukubali kujenga kwenye kiwanja cha mkewe, majuto yalifuata baadaye.
 
Ukishaoa Mwanamke anayechangia Kipato kwa familia ni mambo Mawili tu, mtaachana au kubali Kuishi Kama Kondoo.

Akina Elon, akina Dangote akina Mengi walikataa haya, Bora Mo, Manji na kina JK walioa house wife kwa Amani zao.

Mwanaume ili uwe na amani na Uhuru na utulivu wako, kubali kuwa Baba n kiongozi wa familia anayetimiz majukumu yake mwenyewe.

Mara utakapotaka Mke akusaidie majukumu basi kubali ia mgawane power yako nje ya hapo uwe na basta tu
Shida yao wakishakuzidi kipato ni tatizo
 
Point to remember.

Ruthlessness is rarely born in a single moment.

It is forged through years of silent wounds, betrayal, humiliation, and pain left to rot in the dark.

A person can endure only so much before something inside them dies...

And sometimes, when the pain has nowhere left to go, the final chapter is written in blood.

Let that sink in.....
 
Nilishamwambia wife kitambo na hua naendelea kumkumbusha kwamba, siku ikitokea tumechokana, hakuna haja ya kusumbua watu, ntaondoka na kuacha kila kitu ilimradi najua wanangu wanapakuishi na wako na mama yao.

Lakini pia akiona watoto wanamzonga, ntaondoka nao. Ila suala la kugawana mali au kushughulisha watu kuamua kesi halipo.

Na kuthibitisha hilo, nilibadili hati inasoma jina lake peke yake, akashauri basi badala ya kuweka lake, na kuondoa langu, tuweke yote. Nikamwambia mimi ndio nimeamua liwe jina lako. Nikitangulia mbele ya haki, haubughudhiwi na mtu.
 
Jane alikua analinda urithi wa watoto wake.!
... hizi thinking ndio chanzo cha matatizo ikiwemo kuuliwa kipumbavu! Hilo neno moja tu "wake" kwenye ndoa ni hatari kuliko nyuklia. Why not "wao"?
 
Back
Top Bottom