Ukweli kuhusu Jane Urassa - mke aliyeuawa kwa risasi 💔

Ukweli kuhusu Jane Urassa - mke aliyeuawa kwa risasi 💔

Je ni kweli huyo bwana aliwahi kuwa Terminal Ill ? Na je kipindi hicho nani alihudumia familia ? Kuna uwezekano wa kuwepo kwa sponsor in between aliyesaidia familia izidi kusonga mbele ila kwa malipo ya sio na staha kwenye ndoa ?
 
Tufanye yote ni sahihi kuwa Jane ana tamaa na mlafi wa mali
Mpwa, umeanza lini uongo na unafiki 😂
Ila kama mwanaume si hitimisho kumuua mwanamke

Kivipi aani tunashangilia mauaji alichokifanya kweka kuna utofauti gani na walichokifanya ccm kuua wananchi kwaajili ya kujilindia mali

Uwanaume haupimwi kwa misuli tu pia kudhibiti hisia zako demu,mke hata malaya akizingua piga chini tafuta njia ya kujilinda wewe na mali zako ila sio kumuuaaa
Umesema kwa busara sana, kudos kwa mchango huu!
 
SWALI (hasa kwa wanaume walioreply wakiunga mkono mauaji na huyu mama kwenye nyuzi zilizopita)
  • JANE ALIKOSEA NINI?
  • NI NINI KIFANYIKE ILI MAUAJI NA UKATILI KAMA HUU USIENDELEE KUTOKEA?
mama angeandika majina ya watoto tu au watoto na mme na mke...njia bora angeandika majina ya mume na mke na watoto si vinginevyo ...mnapokuwa na magomvi jiepusheni na kuchochea moto ..kitendo cha mke kwa wakati huo akikuonyesha mwelekeo mzuri hata chembe.
 
Je ni kweli huyo bwana aliwahi kuwa Terminal Ill ? Na je kipindi hicho nani alihudumia familia ? Kuna uwezekano wa kuwepo kwa sponsor in between aliyesaidia familia izidi kusonga mbele ila kwa malipo ya sio na staha kwenye ndoa ?
Mke ni mtumishi alikua na kazi, sina hakika ila nafikiri wote walikua wanachangia kwenye familia yao.
 
Tukiacha utani, hoja kama hizi na mada zinazohusiana na haya mambo ya ndoa Kuna muda wale jamaa wa kataa ndoa wanakuwaga sahihi sana ili kuepusha mambo ya homicide kama haya.
 
mama angeandika majina ya watoto tu au watoto na mme na mke...njia bora angeandika majina ya mume na mke na watoto si vinginevyo ...mnapokuwa na magomvi jiepusheni na kuchochea moto ..kitendo cha mke kwa wakati huo alikuonyesha mwelekeo mzuri hata chembe.
Nakubaliana na wewe, kama baba alikua na mipango mingine kama kuuza nyumba au kurithisha wengine, basi swala la kuandika majina ya watoto bila majina yao wenyewe, lilichochea ugomvi na kuwafikisha mahali pabaya.
 
Umesoma uzi?

Hakubadili alitengeneza (kwa sababu yeye ndiye alikua mmiliki wa kiwanja) na akaweka majina ya watoto badala ya jina lake na la mumewe.
Hayo aliyoyafanya mume wake aliyaridhia ? Na hata kama yeye alikuwa mmiliki wa kiwanja , nyumba alijenga nani? Na kwanini aliweka majina ya watoto lakini siyo ya kwao pia kama wazazi.?
 
SWALI (hasa kwa wanaume walioreply wakiunga mkono mauaji na huyu mama kwenye nyuzi zilizopita)
  • JANE ALIKOSEA NINI?
  • NI NINI KIFANYIKE ILI MAUAJI NA UKATILI KAMA HUU USIENDELEE KUTOKEA?
Hizi taarifa za ndugu wa Jane ni maoni ya upande mmoja tu.

Na wala sio facts.

Vipi taarifa za upande wa Mwanaume Kweka?

Taarifa za upande mmoja tu, sio hitimisho la kumtetea Jane.

Huwezi kuita taarifa za upande mmoja facts, wakati hujasikiliza taarifa za upande wa pili. Kulinganisha ukweli ni upi.

Kwa sababu kwenye issue kama hizi, kila ndugu atatetea upande wa ndugu yao.
 
#FACT-CHECKING

Usidanganyike, mambo kwa ground yapo tofauti sana. Kwa ushahidi, tupitie ni yapi ya kweli na yapi si kweli kuhusu kifo cha Jane Maloo Urassa ⚰️ aliyeuawa na Laurence Kweka, mwanaume aliyekosa akili, busara na utashi wa kibinadamu.


View attachment 3686843

  1. Jane na Bw. Kweka waliishi kwenye ndoa kwa miaka 18 na miezi 8 na wana watoto 4 - KWELI

  2. Jane alikua mtumishi aliyeajiriwa, mwenye kipato chake binafsi, na elimu ya chuo kikuu (Masters) - KWELI

  3. Jane alimiliki mali binafsi alizotafuta kabla ya ndoa ikiwemo kiwanja kilichojengwa nyumba iliyoleta mgogoro - KWELI

  4. Jane alikua ameshaondoka hapo nyumbani kwenye migogoro kwa zaidi ya miezi miwili na kwenda kuishi kwa ndugu zake na alimuachia bwana Kweka nyumba na pamoja na watoto wote aishi nao - KWELI

  5. Mgogoro mkubwa ulijitokeza miezi kadhaa nyuma baada ya hati ya nyumba kutoka na majina ya watoto na Jane kama msimamizi mpaka pale mtoto wao wa kwanza atakapofikisha miaka 18 - KWELI

  6. Jane alitaka hati ya nyumba iwe kwa jina lake - SI KWELI

  7. Jane aliweza kutengeneza hati sababu kiwanja kilikua mali yake na bwana Kweka hakutaka majina ya watoto kwenye hati bali jina lake mwenyewe, sababu aliamini nyumba ameijenga kwa jasho lake - KWELI

  8. Jane alirudi nyumbani kwao masaa machache kabla ya kuuawa, kuwapelekea watoto wake chakula kwa sababu walikua wameishiwa na baba wa watoto alikua safarini Moshi - KWELI

    PS:
    Mtoto wao mkubwa aliyempigia simu mama yake ataishi kwa uchungu maisha yake yote, akijua bila ya simu yake, mama yao angekua hai leo.

    View attachment 3686846

  9. Kabla ya mauaji, tayari kulikua na kesi polisi na ustawi wa jamii dhidi ya bwana Kweka kuhusu ukatili wa kijinsia na kumtishia mkewe maisha - KWELI

Vyanzo vya taarifa / Sources: (Ukija kubisha na wewe ulete vyanzao vyako)

Tofauti na mambo yanayoendelea mtandaoni na watu wanavyoleta mizaha kuhusu ukatili wa kijinsia na mauaji, Jane Urassa aliuawa kwa sababu alikua tayari kuachana na mume wake na kuhakikisha mali zao walizochuma pamoja zinabaki kwa watoto wao.

Alifanya vile ambavyo wanaume wanashauri humu jukwaani kwamba, using’ang’anie mali ambayo si yako, akampisha mwanaume kwenye nyumba yao, akaacha watoto bila kuwang'ang'ania na bado akauawa kikatili.


Hitimisho:

Jane alifikia mwisho kwenye maisha ya ndoa ila Mr. Kweka hakuwa tayari kuona mwisho wa ndoa yao pekee, alitaka pia kuhakikisha ni mwisho wa maisha yake pia - kusudi lake limetimia.

R.IP Jane 💔

Tupinge Femicide / mauaji ya wanawake

Alamsiki!
Mimi nachokiona ni wahuni wame wahiana tu, hata huyo Mama angemuwahi jamaa angemuua
 
Ila Kweka.! Nashauri kabla ya kuhusiana na mtu angalia jinsi anavyowatendea watu wengine.

Kuna watu hawatoi heshima kwa wazazi wao, ndugu na jamii inayowazunguka.
Wamejawa viburi na majivuno.

Sasa mtu kama huyu asiyejali kuhusu wazazi wake, vipi awaze kuhusu wewe.

Tukifatilia uhusiano wa Kweka na wazazi wake, kazini, majirani utakuta tu alikua mtu wa matatizo.
Ni kweli kabisa, lazima kuna chimbuko na matukio mengine ambayo si mazuri kwenye historia yake.
Ukatili wa hali ya juu kumuua mama watoto wako.
Na amemuua nyumbani na watoto wake wote wakiwemo ndani.
YANI UNAWEZAJE 💔
 
Back
Top Bottom