Ukweli kuhusu Jane Urassa - mke aliyeuawa kwa risasi 💔

Ukweli kuhusu Jane Urassa - mke aliyeuawa kwa risasi 💔

Mara zote huwa nasema huku ndani, mwanaume kukosa akili ndio chanzo cha matatizo mengi kwenye ndoa sababu kuanzia kwenye uchaguzi wa mwanamke wa kuishi nae mwanaume unatakiwa kumsoma huyu mtu atakuja kubadilika au la

Hapa bwana Kweka alikosa akili tokea mwanzo kwa kukubali kujenga kwenye kiwanja cha mwanamke maana ndio makosa yalipoanzia
 
Mara zote huwa nasema huku ndani, mwanaume kukosa akili ndio chanzo cha matatizo mengi kwenye ndoa sababu kuanzia kwenye uchaguzi wa mwanamke wa kuishi nae mwanaume unatakiwa kumsoma huyu mtu atakuja kubadilika au la

Hapa bwana Kweka alikosa akili tokea mwanzo kwa kukubali kujenga kwenye kiwanja cha mwanamke maana ndio makosa yalipoanzia
Mkuu,unapokuwa chumbani na mwanamke ,amekulalia KWENYE kifua haya mengine utayakumbuka kweli ?
 
Jane alikua mtumishi aliyeajiriwa, mwenye kipato chake binafsi, na elimu ya chuo kikuu (Masters) - KWELI
1. Alikuwa anafanya kazi wapi?
2. Alisomea masomo gani?
3. Mume wake alikuwa na elimu gani?
4. Kama alikuwa ameajiriwa akanunua kiwanja,kwanini alishindwa kujenga nyumba kwenye eneo hilo mwenyewe?
 
Naamini ukweli halisi wanaujua wao wenyewe, sisi huku nje ni speculations tu.

Sasa kama mwanaume alikuwa safarini watoto wakamlilia mama yao njaa, kwanini marehemu asingetuma take away wapelekewe kama hakutakiwa kuingia ndani?

Ina maana Kweka alimkuta marehemu ndani bahati mbaya kisha akamwambia twende chumbani?

If yes, kwanini marehemu akakubali kwenda chumbani huku akijua yeye na mumewe hawana maelewano mazuri?
 
Tufanye yote ni sahihi kuwa Jane ana tamaa na mlafi wa mali

Ila kama mwanaume si hitimisho kumuua mwanamke

Kivipi aani tunashangilia mauaji alichokifanya kweka kuna utofauti gani na walichokifanya ccm kuua wananchi kwaajili ya kujilindia mali

Uwanaume haupimwi kwa misuli tu pia kudhibiti hisia zako demu,mke hata malaya akizingua piga chini tafuta njia ya kujilinda wewe na mali zako ila sio kumuuaaa
 
Mkuu,unapokuwa chumbani na mwanamke ,amekulalia KWENYE kifua haya mengine utayakumbuka kweli ?
😂 😂 Hapo ndiyo inakuwaga kamzozo, nyonyo ziko mkononi bibie anakwambia nina kiwanja basi tujenge, unajikuta umekubali tu. Mapenzi yakipungua akili ikakukaa sawa, tayari ushamwaga milioni 100 nyumba iko kwenye finishing, hapo ndiyo hasira zinapofukuta sasa.
 
#FACT-CHECKING

Usidanganyike, mambo kwa ground yapo tofauti sana. Kwa ushahidi, tupitie ni yapi ya kweli na yapi si kweli kuhusu kifo cha Jane Maloo Urassa ⚰️ aliyeuawa na Laurence Kweka, mwanaume aliyekosa akili, busara na utashi wa kibinadamu.


View attachment 3686843

  1. Jane na Bw. Kweka waliishi kwenye ndoa kwa miaka 18 na miezi 8 na wana watoto 4 - KWELI

  2. Jane alikua mtumishi aliyeajiriwa, mwenye kipato chake binafsi, na elimu ya chuo kikuu (Masters) - KWELI

  3. Jane alimiliki mali binafsi alizotafuta kabla ya ndoa ikiwemo kiwanja kilichojengwa nyumba iliyoleta mgogoro - KWELI

  4. Jane alikua ameshaondoka hapo nyumbani kwenye migogoro kwa zaidi ya miezi miwili na kwenda kuishi kwa ndugu zake na alimuachia bwana Kweka nyumba na pamoja na watoto wote aishi nao - KWELI

  5. Mgogoro mkubwa ulijitokeza miezi kadhaa nyuma baada ya hati ya nyumba kutoka na majina ya watoto na Jane kama msimamizi mpaka pale mtoto wao wa kwanza atakapofikisha miaka 18 - KWELI

  6. Jane alitaka hati ya nyumba iwe kwa jina lake - SI KWELI

  7. Jane aliweza kutengeneza hati sababu kiwanja kilikua mali yake na bwana Kweka hakutaka majina ya watoto kwenye hati bali jina lake mwenyewe, sababu aliamini nyumba ameijenga kwa jasho lake - KWELI

  8. Jane alirudi nyumbani kwao masaa machache kabla ya kuuawa, kuwapelekea watoto wake chakula kwa sababu walikua wameishiwa na baba wa watoto alikua safarini Moshi - KWELI

    PS:
    Mtoto wao mkubwa aliyempigia simu mama yake ataishi kwa uchungu maisha yake yote, akijua bila ya simu yake, mama yake angekua hai leo.

    View attachment 3686846

  9. Kabla ya mauaji, tayari kulikua na kesi polisi na ustawi wa jamii dhidi ya bwana Kweka kuhusu ukatili wa kijinsia na kumtishia mkewe maisha - KWELI

Vyanzo vya taarifa / Sources: (Ukija kubisha na wewe ulete vyanzao vyako)

Tofauti na mambo yanayoendelea mtandaoni na watu wanavyoleta mizaha kuhusu ukatili wa kijinsia na mauaji, Jane Urassa aliuawa kwa sababu alikua tayari kuachana na mume wake na kuhakikisha mali zao walizochuma pamoja zinabaki kwa watoto wao.

Alifanya vile ambavyo wanaume wanashauri humu kwamba using’ang’anie mali ambayo si yako, akampisha mwanaume kwenye nyumba yao, akaacha watoto bila kuwang'ang'ania na bado akauawa kikatili.


Hitimisho:

Jane alifikia mwisho kwenye maisha ya ndoa ila Mr. Kweka hakuwa tayari kuona mwisho wa ndoa yao pekee, alitaka pia kuhakikisha ni mwisho wa maisha yake pia - kusudi lake limetimia.

R.IP Jane 💔

Tupinge Femicide / mauaji ya wanawake

Alamsiki!
RIP Jane! Ila ubabe ulikuwa nao!
 
Back
Top Bottom