Ukweli kuhusu Jane Urassa - mke aliyeuawa kwa risasi 💔

Ukweli kuhusu Jane Urassa - mke aliyeuawa kwa risasi 💔

Sasa kama tayari wewe umeshagundua kuwa Jamaa Hana akili, basi we Baki na ukweli wako!! Maana umekuja hapa tayari ukiwa na hukumu yako!!
Sina hukumu ila mauaji hayana utetezi, hata kama Jane naye alikua na makosa, hakustahili kifo.
 
Sijui Mahi, ila inaonekana kulikua tayari na migogoro na changamoto nyingine.

Navyoona mwanaume kajenga kwa mke akakosa sauti ya maamuzi, na Jane naye akatumia ubavu wa umiliki wa kiwanja, kufanya maamuzi yanayopingana na matakwa ya Kweka. Mwishowe, wote wamekosa.
Duuh hii hatari, najiuliza hawakuwashirikisha hata wazazi/ndugu wa pande zote? Ili kupata suluhu ya hili suala, maana inaonekana ilifikia hatua mbaya sana.
 
#FACT-CHECKING

Usidanganyike, mambo kwa ground yapo tofauti sana. Kwa ushahidi, tupitie ni yapi ya kweli na yapi si kweli kuhusu kifo cha Jane Maloo Urassa ⚰️ aliyeuawa na Laurence Kweka, mwanaume aliyekosa akili, busara na utashi wa kibinadamu.


View attachment 3686843

  1. Jane na Bw. Kweka waliishi kwenye ndoa kwa miaka 18 na miezi 8 na wana watoto 4 - KWELI

  2. Jane alikua mtumishi aliyeajiriwa, mwenye kipato chake binafsi, na elimu ya chuo kikuu (Masters) - KWELI

  3. Jane alimiliki mali binafsi alizotafuta kabla ya ndoa ikiwemo kiwanja kilichojengwa nyumba iliyoleta mgogoro - KWELI

  4. Jane alikua ameshaondoka hapo nyumbani kwenye migogoro kwa zaidi ya miezi miwili na kwenda kuishi kwa ndugu zake na alimuachia bwana Kweka nyumba na pamoja na watoto wote aishi nao - KWELI

  5. Mgogoro mkubwa ulijitokeza miezi kadhaa nyuma baada ya hati ya nyumba kutoka na majina ya watoto na Jane kama msimamizi mpaka pale mtoto wao wa kwanza atakapofikisha miaka 18 - KWELI

  6. Jane alitaka hati ya nyumba iwe kwa jina lake - SI KWELI

  7. Jane aliweza kutengeneza hati sababu kiwanja kilikua mali yake na bwana Kweka hakutaka majina ya watoto kwenye hati bali jina lake mwenyewe, sababu aliamini nyumba ameijenga kwa jasho lake - KWELI

  8. Jane alirudi nyumbani kwao masaa machache kabla ya kuuawa, kuwapelekea watoto wake chakula kwa sababu walikua wameishiwa na baba wa watoto alikua safarini Moshi - KWELI

    PS:
    Mtoto wao mkubwa aliyempigia simu mama yake ataishi kwa uchungu maisha yake yote, akijua bila ya simu yake, mama yao angekua hai leo.

    View attachment 3686846

  9. Kabla ya mauaji, tayari kulikua na kesi polisi na ustawi wa jamii dhidi ya bwana Kweka kuhusu ukatili wa kijinsia na kumtishia mkewe maisha - KWELI

Vyanzo vya taarifa / Sources: (Ukija kubisha na wewe ulete vyanzao vyako)

Tofauti na mambo yanayoendelea mtandaoni na watu wanavyoleta mizaha kuhusu ukatili wa kijinsia na mauaji, Jane Urassa aliuawa kwa sababu alikua tayari kuachana na mume wake na kuhakikisha mali zao walizochuma pamoja zinabaki kwa watoto wao.

Alifanya vile ambavyo wanaume wanashauri humu jukwaani kwamba, using’ang’anie mali ambayo si yako, akampisha mwanaume kwenye nyumba yao, akaacha watoto bila kuwang'ang'ania na bado akauawa kikatili.


Hitimisho:

Jane alifikia mwisho kwenye maisha ya ndoa ila Mr. Kweka hakuwa tayari kuona mwisho wa ndoa yao pekee, alitaka pia kuhakikisha ni mwisho wa maisha yake pia - kusudi lake limetimia.

R.IP Jane 💔

Tupinge Femicide / mauaji ya wanawake

Alamsiki!
She was perfect everywhere!
 
Sasa mahi, kwanini Huyo Jane asingeacha utambulisho usome wa kweka, hadi mtoto akifikisha umri wa 18yrs ndipo wafanye taratibu za kubadilisha? Tatizo lilikua nini yaani?
... ukifa mimi na watoto tutaishije? Ndugu zako (mume) watatudhulumu! Nadhani alikuwa anajaribu ku-fast track given the unforseen future!
 
Tangu mwanzo hati ilikuwa inasoma majina ya mwanamke tu maana alinunua kabla hawajaoana. Huyo kweka alitaka ikabadilishwe jina lake ndio liwekwe baada ya kuona mke kagoma kuuza. Yeye alikosea kujenga kwenye kiwanja cha mwanamke , hapo ni sawa na kujenga kwenye kiwanja ulichopewa na baba mkwe zawadi siku ya harusi😝😝😝
Sasa mahi nini kilifanya hadi wafikie hatua hiyo, naamini kulikua na kitu kilichofanya hawa waanze kuwa na migogoro hadi kufikia kuanza kugombania nyumba. Ila mmmh hizi ndoa.
 
Aunt ninaomba uniwie radhi kwa sababu majibu yangu ni mafupi,ninashukuru utayaelewa.
Kwanini huamini mpwa?
Mimi siwezi kuamini maandishi yenu hadi nitakapompata mtu wa karibu na nitampata tu.
Ni kweli migogoro ya ndoa ni mingi na kuna mingine wanawake ndiyo chanzo na mingine wanaume ni chanzo.
Wote inabidi kuingia kwenye hizi taasisi tukiwa tayari na kupunguza tamaa, ziwe za kifedha au kimwli.
Asante sana na ninaamini utalisimamia au kuchangia kitu kwenye hili hata ikitokea kwa upande wangu.
Unamaanisha nini?
Sasa imagine mtu anakuja kusifia mauwaji na wengine wanaanzisha nyuzi kabisa…hata hayo mabunduki yenyewe hatuyajui.
 
Kwa Nini awe na mshahara wake binafsi akiwa kwenye ndoa.Na kwa Nini awapende watoto ashindwe kumpenda mume aliyezaa naye watoto?Tatizo sio nyumba Kuna shida mahali
 
Pamoja na elimu yangu, sikutaka kabisa kujipa stress ya kuoa mwanamke aliyesoma. Mtasema sijiamini, lakini kama ni kutojiamini, basi bora niendelee kutojiamini ili nijue nimekaa sehemu salama na yenye amani kwangu.

Ukitaka kuamini hili, angalia hata historia ya wake wa baadhi ya viongozi wetu. Mama Janeth Magufuli alikuwa mwalimu wa shule ya msingi, Salma Kikwete alikuwa na elimu ya ualimu, na hata wake wa viongozi kama Nyerere na Mwinyi hawakuwa na hizo elimu kubwa tunazoziona leo.

Kwa hiyo, kwangu mimi elimu kubwa kwa mwanamke si lazima iwe kipimo cha kumfanya awe chaguo bora la ndoa. Muhimu zaidi ni tabia, heshima, busara, utulivu na namna anavyoijenga familia.
 
Mimi Niko na Kweka Hadi mwisho,kama hakununua kiwanja si anajasho lake kwenye ujenzi?kama ni kuandika majina kwanini mama aandike jina peke yake na watoto?kama ni equal basi yangeandikwa majina yote yaani mke,mume na watoto tatizo mama alishaa pata duduwasha nje likamshawishi usengerema.
 
Issue ni kuwa wanawake huwa na jeuri mno, hasa wachaga huwa ni vichwa ngumu mno.

Kuchapwa risasi kajitakia yeye mwenyewe..

Lakini pia, kuna namna na yeye alikuwa na kiburi, mtu hata kama awe narcissist like hell, hawezi tu kuuwa for no reason.

Dysfunction katika hiyo familia ili build up na yeye mwanamke alidhani kuwa na jeuri ni sawa tu mpaka umati ulivyo mkuta

Mwisho wa kiburi na jeuri ni mauti
 
Back
Top Bottom