Ukitaka kwenda kuishi Marekani inabidi ujipange

Ukitaka kwenda kuishi Marekani inabidi ujipange

Miaka flani Niko bongo sielewi mambo hayaeleweki, nina sista angu yuko U.S nkaongea nae kuhusu mi kwenda Marekani kujaribu maisha anakubali, mipango inakamilika kijana nkatua Jackson heartsfield Atlanta lengo kubwa la kwenda Marekani ni kupata exposure na kutafuta maisha.

Harakati zinazofuata ni mim kutafuta kazi, Marekani kazi zipo Ila sasa kule ukisikia kazin kazini kweli full supervision unafanya kazi masaa 10 mpaka 12 hiyo ni uongeze kipato ukizingatia kazi zenyenyewe unalipwa kwa masaa, kwa hiyo lazima ukomaee Ila kazi tu zipo, baada ya mda kudunduliza ela nahama kwenye basement nikahamia kwenye chumba kimoja sehemu moja hivi inaitwa sandy springs.

Tatizo la Marekani maisha expensive kipato cha kawaida ukizingatia nilienda kama mtu wa Kawaida, kila kitu ni ela yaan ukisikia capitalism kule ndo inakua practice 💯 swala la kuwa na depression, loneliness ni moja ya vitu lazima ukumbane navyo usipokua makini lazima uingie kwenye matumizi ya madawa ya kulevya.

Ukikaa Marekani kitu unachoombea kila siku ni usiumwe sababu ni balaa, kuhusu starehe nayo pia ni mtihan kwa mtu mwenye kipato cha kawaida, wanawake wengi wa Atlanta ni materials things inabidi kuwapata ni gharama wako after money.

Kwa sasa hivi nilisharudi tz sababu za kifamili, na maisha ya marekani ili yakuendee vizuri uwe na professional means at least umesomea master kule kama hujasoma bachelor kwenye fani za science, au unakipaji kitu ambacho kwa watanzania wengi mpaka wanakua hawajui vipaji vyao, kwenda marekani hivi hivi ni kugumu sana kwa sababu kwa maisha utajikuta unapata ela ya kawaida alafu unaishi kwa mawazo sana in short unataka kwenda marekani kutafuta maisha jipange na uwe mtu wa kujiongeza sana, na uwe competent hivi hivi sikushauri hata kidogo.

California, new York, Illinois, Massachusetts, na Washington state hayo ni majimbo ya kuyaepuka Kodi na gharama za maisha ziko juu. Ila Texas, Florida, Georgia, na north Carolina haya majimbo maisha yako cheap.

Vitu nilivuomiss marekani ni exposure Ila mwaka huu ntarudi nikiwa nimejipanga zaidi, kunakikampuni ntaenda kukifungua deleware kama domestic company, alafu baadae Virginia na Texas kama foreign company.
mmmmm... Watanzania kweli miamba. Mpaka USA mnashabikia kampuni za mifukoni. Jimbo la Delaware linasifika kwa uandikishaji wa kampuni za mifukoni!
 
Kwa mwezi unakunja $2,400 si haba hata kama utalipa chumba $400-$800
Katika hizo $2,400 inabidi utoe state tax, federal tax, Medicare contributions, social security contributions, na unemployment contributions. Ukiwa na bahati unaweza kuwa na take home ya $1,700. Katika hiyo take home bado hujalipia cable TV ($40), internet ($45), cellphone ($35), apartment ($500) maji/umeme ($75), bima ya gari ($70). Hiyo take home huenda ukabakiza $1000. Kwenye hiyo 1000 ndiyo ulipie mafuta ya gari, chakula, na vitu vingine. Hizo gharama nilizozitaja ni kwa majimbo ya gharama nafuu. Vitu vingine kama bima ya gari inategemea uendeshaji wako na pengine na umri na miaka ya leseni. Kila ukipata tiketi, bima yako inapanda; ticketi zikizidi wenye bima wanakukataa (risky driver). Inabida upate bima special ambayo unaweza ukalipia zaidi ya $200 kwa mwezi...hapo unatamani urudi TZ maana huo mshahara haukupi hamasa ya kutoboa!

Pamoja na vijana wengi waliyopata green card kuamua kufanya kazi, lakini in the end anayekamata shule atafanikiwa zaidi kuliko anayesema ngoja nikusanye pesa. Lakini ndiyo hivyo, wengine shule inawapa shida kwa sababu ya ung'eng'e
 
mmmmm... Watanzania kweli miamba. Mpaka USA mnashabikia kampuni za mifukoni. Jimbo la Delaware linasifika kwa uandikishaji wa kampuni za mifukoni!
Makampuni makubwa mia Tano asilimia almost 70 yamesajiliwa deleware as a domestic company na majimbo mengine kama New York, CA au Texas as a foreign company

Ajabu ni nin kama sio Kosa kisheria uoga wako ndo umaskini wako
 
Katika hizo $2,400 inabidi utoe state tax, federal tax, Medicare contributions, social security contributions, na unemployment contributions. Ukiwa na bahati unaweza kuwa na take home ya $1,700. Katika hiyo take home bado hujalipia cable TV ($40), internet ($45), cellphone ($35), apartment ($500) maji/umeme ($75), bima ya gari ($70). Hiyo take home huenda ukabakiza $1000. Kwenye hiyo 1000 ndiyo ulipie mafuta ya gari, chakula, na vitu vingine. Hizo gharama nilizozitaja ni kwa majimbo ya gharama nafuu. Vitu vingine kama bima ya gari inategemea uendeshaji wako na pengine na umri na miaka ya leseni. Kila ukipata tiketi, bima yako inapanda; ticketi zikizidi wenye bima wanakukataa (risky driver). Inabida upate bima special ambayo unaweza ukalipia zaidi ya $200 kwa mwezi...hapo unatamani urudi TZ maana huo mshahara haukupi hamasa ya kutoboa!

Pamoja na vijana wengi waliyopata green card kuamua kufanya kazi, lakini in the end anayekamata shule atafanikiwa zaidi kuliko anayesema ngoja nikusanye pesa. Lakini ndiyo hivyo, wengine shule inawapa shida kwa sababu ya ung'eng'e
Florida, Texas, Tennessee, Washington hawana state income tax
 
Mkuu mimi sasa hivi nina 37 nafanyiwa mpango wa kwenda je ni umri sahihi au niahirishe?
Nenda haraka sana , usiangalie nyuma ukifika huko chapa kazi aanza na kazi hata wanazolipa 12/hr kwa miezi kadhaa wakati unatafuta kazi ya fani yako na yenye kipato kizuir..

Hukiwa huna matumizi ya aajabu ajabu utamake sana
 
nakwambiaje mtaalam maisha ya kule hatuyawez kule hakun kula kwa mjomb tena uanapakua mavipande ya kuku na umeend bila appointment na chumba kwa anko unapewa unallala hata siku 3 kule maisha ya kibepar kila mtu anakufa kivyake watoto hawan adab na wazaz wao ukifika 18 umemaliza masom yote na kaz unapiga

Sent from my TECNO CF7 using JamiiForums mobile app

[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Science Priest: Niko US, najaribu kutoa experience yangu tu, Ni vigumu kulinganisha Marekani na Tanzania, inategemea unalinganisha nini! Chungwa na pera yote ni matunda, lakini huwezi kuyangalinisha kabisa, lazima utoe sababu kwa nini unayalinganisha! Hata sisi Wabongo tuliokuja huku, kila mtu ana experience yake, nchii hii (US) ni kubwa mno kutoa experience ya aina moja!

Jinsi ulivyoingia Marekani, elimu yako, jimbo uliloingilia, watu waliokupokea vinaweza kuleta experience tofauti kabisa kabisa! Hata Tanzania iko hivyo! Kijana aliyeingia bongo akiwa na elimu yake toka Moshi, akafikia kwa mjomba/baba mdogo anayeishi Masaki, akamtafutia kazi Voda, baada ya muda akamtafutia nyumba ya kupanga Sinza, ni tofauti kabisa na kijana aliyeingia toka Mtwara akafikia Mbagala, kazi ya kwanza akapewa kufanya umachinga! Wote wako Dar yenye fursa kwa mtu aliyetoka mkoani! Lakini wote watasimulia tofauti kabisa! Ndivyo ilivyo US.

Wengine walikuja kwa mwaliko wa harusi, wengine na Visa ya shule, wengine na Green Card, wengine just form 4 or six, wengine graduates or with high techinical skills tegemea experience zao zitakuwa tofauti!

Dhana mbovu kwa wengi Tanzania ni kuwa ukiingia tu Marekani umeukata! Sio Kweli! Marekani ni nchi yenye mfumo wa maisha tofauti kabisa na Tanzania, unaanza kwanza na kazi kubwa ya ku adapt maisha ya hapa! Hiyo tu ni shule tosha! Wengine wanashindwa hapo mapema kabisa! Hakuna kupoteza muda, kila saa akili inabidi ifanye kazi.

Nawafahamu baadhi ya Watanzania walioko Marekani ningekuwa na uwezo ningewarudisha nyumbani! Maisha yamewakataa! Hawana vibali. hawajaenda shule, maisha yao ni shida sana, kwangu mimi afadhali kurudi nyumbani! Lakini pia nafahamu Watanzania si haba! wanaishi maisha ambayo wanayaita "American Dream" ambayo Tanzania ni wachache wanafika hatua hiyo!

Lakini pia nikija Tanzania kuna vijana wako hapo nyumbani, natamani ningekua na uwezo ningewaleta US, wako aggressive wanajua nini wanatafuta maishani, lakini hawana fursa wala connection ya kuwatoa walipo! Lakini pia kuna vijana wengine wanalilia kuja Marekani, ukiwaangalia tu unajua wanadhani Marekani ni kula bata tu! unajua wakija hapa hawatatoka afadhali wabaki bongo!
Una washauri nini vijana ... What are the pathways wanazoweza kutumia kuhamia Marekani?
 
Habari zenu wana jamvi. Mimi naomba nichepuke kidogo nje ya mada. Natamani kwenda vacay U.S/ U.K / Canada. Ni familia yenye 4 kids. Swali langu ni njia gani rahisi naweza kuitumia kufika mojawapo kati ya nchi hizo nikimaanisha unafuu wa gharama. Je naweza kwenda tu na nikajitembeza mwenyewe au ni lazima niwe na mwenyeji au nitumie makampuni? Naombeni gharama makadirio ya gharama za maisha kwa mwezi mmoja kwa kila nchi tajwa hapo juu kuanzia cheap return tickets, malazi, chakula na mizunguko.
NB: Lengo sio kuzamia, kipato changu ni cha uhakika na kinaniruhusu kwenda kuosha macho mbele na kurudi home. Natanguliza shukrani!
Angalia requirements za visiting visa kutoka US embassy official website.!
 
Miaka flani Niko bongo sielewi mambo hayaeleweki, nina sista angu yuko U.S nkaongea nae kuhusu mi kwenda Marekani kujaribu maisha anakubali, mipango inakamilika kijana nkatua Jackson heartsfield Atlanta lengo kubwa la kwenda Marekani ni kupata exposure na kutafuta maisha.

Harakati zinazofuata ni mim kutafuta kazi, Marekani kazi zipo Ila sasa kule ukisikia kazin kazini kweli full supervision unafanya kazi masaa 10 mpaka 12 hiyo ni uongeze kipato ukizingatia kazi zenyenyewe unalipwa kwa masaa, kwa hiyo lazima ukomaee Ila kazi tu zipo, baada ya mda kudunduliza ela nahama kwenye basement nikahamia kwenye chumba kimoja sehemu moja hivi inaitwa sandy springs.

Tatizo la Marekani maisha expensive kipato cha kawaida ukizingatia nilienda kama mtu wa Kawaida, kila kitu ni ela yaan ukisikia capitalism kule ndo inakua practice 💯 swala la kuwa na depression, loneliness ni moja ya vitu lazima ukumbane navyo usipokua makini lazima uingie kwenye matumizi ya madawa ya kulevya.

Ukikaa Marekani kitu unachoombea kila siku ni usiumwe sababu ni balaa, kuhusu starehe nayo pia ni mtihan kwa mtu mwenye kipato cha kawaida, wanawake wengi wa Atlanta ni materials things inabidi kuwapata ni gharama wako after money.

Kwa sasa hivi nilisharudi tz sababu za kifamili, na maisha ya marekani ili yakuendee vizuri uwe na professional means at least umesomea master kule kama hujasoma bachelor kwenye fani za science, au unakipaji kitu ambacho kwa watanzania wengi mpaka wanakua hawajui vipaji vyao, kwenda marekani hivi hivi ni kugumu sana kwa sababu kwa maisha utajikuta unapata ela ya kawaida alafu unaishi kwa mawazo sana in short unataka kwenda marekani kutafuta maisha jipange na uwe mtu wa kujiongeza sana, na uwe competent hivi hivi sikushauri hata kidogo.

California, new York, Illinois, Massachusetts, na Washington state hayo ni majimbo ya kuyaepuka Kodi na gharama za maisha ziko juu. Ila Texas, Florida, Georgia, na north Carolina haya majimbo maisha yako cheap.

Vitu nilivuomiss marekani ni exposure Ila mwaka huu ntarudi nikiwa nimejipanga zaidi, kunakikampuni ntaenda kukifungua deleware kama domestic company, alafu baadae Virginia na Texas kama foreign company.
Kasie Usipite huku usije ukaniacha...
 
Ngoja nikatafute maisha Ukraine, kule kila kitu cheap, mgahawa buku ya huku kwa fedha ya Ukraine unakula unashiba ...pisi za kule hazipo after money zinapenda kwa dhati hasa hasa doneskt wako poa sana..😅😅😅😅😢
😄😄😄lakini ni walevi na wavutaji tuulize tuliokimbia
 
Una washauri nini vijana ... What are the pathways wanazoweza kutumia kuhamia Marekani?

According to opportunities na system ya maisha kwa wenzetu ilivyo Ndo maana vijana wengi wa kiafrika wanalaani sana Afrika yao na viongozi. Na hiyo ndo source ya kuzaliwa neno hili “Ahh! Bora kuzaliwa/ningezaliwa mbwa Ulaya au Marekani” hawakukosea [emoji4] ingawa si kauli njema. Kama kiongozi au mtu mzima anajitambua ataichambua kauli hii kwa urefu na upana na kuitathmini pamoja na kuifanyia upembuzi yakinifu.

Hivi we huoni hao walioko huko jinsi wanatupa madini hapa?! Hata waliowahi kuishi huko?! Tukabali au tukatae huko maisha yapo na ukituliza akili na kujitambua uta-pursue zaidi.

Tujiulize hamuoni hao viongozi wenyewe wanapeleka watoto wao kusoma huko?! [emoji2] hamuoni kila baada ya muda wanaenda huko?! [emoji2] na cha kushangaza zaidi walisoma na kuishi huko [emoji2]

Wana exposure za kiwango cha hali ya juu! [emoji92][emoji1476]

Napenda nimalize kwa kusema “Bora kuzaliwa mbwa Ulaya/Marekani kuliko kuwa mtu Afrika”
 
Back
Top Bottom