Miaka flani Niko bongo sielewi mambo hayaeleweki, nina sista angu yuko U.S nkaongea nae kuhusu mi kwenda Marekani kujaribu maisha anakubali, mipango inakamilika kijana nkatua Jackson heartsfield Atlanta lengo kubwa la kwenda Marekani ni kupata exposure na kutafuta maisha.
Harakati zinazofuata ni mim kutafuta kazi, Marekani kazi zipo Ila sasa kule ukisikia kazin kazini kweli full supervision unafanya kazi masaa 10 mpaka 12 hiyo ni uongeze kipato ukizingatia kazi zenyenyewe unalipwa kwa masaa, kwa hiyo lazima ukomaee Ila kazi tu zipo, baada ya mda kudunduliza ela nahama kwenye basement nikahamia kwenye chumba kimoja sehemu moja hivi inaitwa sandy springs.
Tatizo la Marekani maisha expensive kipato cha kawaida ukizingatia nilienda kama mtu wa Kawaida, kila kitu ni ela yaan ukisikia capitalism kule ndo inakua practice [emoji817] swala la kuwa na depression, loneliness ni moja ya vitu lazima ukumbane navyo usipokua makini lazima uingie kwenye matumizi ya madawa ya kulevya.
Ukikaa Marekani kitu unachoombea kila siku ni usiumwe sababu ni balaa, kuhusu starehe nayo pia ni mtihan kwa mtu mwenye kipato cha kawaida, wanawake wengi wa Atlanta ni materials things inabidi kuwapata ni gharama wako after money.
Kwa sasa hivi nilisharudi tz sababu za kifamili, na maisha ya marekani ili yakuendee vizuri uwe na professional means at least umesomea master kule kama hujasoma bachelor kwenye fani za science, au unakipaji kitu ambacho kwa watanzania wengi mpaka wanakua hawajui vipaji vyao, kwenda marekani hivi hivi ni kugumu sana kwa sababu kwa maisha utajikuta unapata ela ya kawaida alafu unaishi kwa mawazo sana in short unataka kwenda marekani kutafuta maisha jipange na uwe mtu wa kujiongeza sana, na uwe competent hivi hivi sikushauri hata kidogo.
California, new York, Illinois, Massachusetts, na Washington state hayo ni majimbo ya kuyaepuka Kodi na gharama za maisha ziko juu. Ila Texas, Florida, Georgia, na north Carolina haya majimbo maisha yako cheap.
Vitu nilivuomiss marekani ni exposure Ila mwaka huu ntarudi nikiwa nimejipanga zaidi, kunakikampuni ntaenda kukifungua deleware kama domestic company, alafu baadae Virginia na Texas kama foreign company.