Ni ukweli kwa asilimia 80 mbaya Zaid watanzania wengi hawasemi ukweli wakirudi huku full kupasifia, inabid uwe na maajabu ndo utafurahia maisha ya kule hivi hivi utajikuta unaingia katika depression, stress, ya kufa mtu
Science Priest: Niko US, najaribu kutoa experience yangu tu, Ni vigumu kulinganisha Marekani na Tanzania, inategemea unalinganisha nini! Chungwa na pera yote ni matunda, lakini huwezi kuyangalinisha kabisa, lazima utoe sababu kwa nini unayalinganisha! Hata sisi Wabongo tuliokuja huku, kila mtu ana experience yake, nchii hii (US) ni kubwa mno kutoa experience ya aina moja!
Jinsi ulivyoingia Marekani, elimu yako, jimbo uliloingilia, watu waliokupokea vinaweza kuleta experience tofauti kabisa kabisa! Hata Tanzania iko hivyo! Kijana aliyeingia bongo akiwa na elimu yake toka Moshi, akafikia kwa mjomba/baba mdogo anayeishi Masaki, akamtafutia kazi Voda, baada ya muda akamtafutia nyumba ya kupanga Sinza, ni tofauti kabisa na kijana aliyeingia toka Mtwara akafikia Mbagala, kazi ya kwanza akapewa kufanya umachinga! Wote wako Dar yenye fursa kwa mtu aliyetoka mkoani! Lakini wote watasimulia tofauti kabisa! Ndivyo ilivyo US.
Wengine walikuja kwa mwaliko wa harusi, wengine na Visa ya shule, wengine na Green Card, wengine just form 4 or six, wengine graduates or with high techinical skills tegemea experience zao zitakuwa tofauti!
Dhana mbovu kwa wengi Tanzania ni kuwa ukiingia tu Marekani umeukata! Sio Kweli! Marekani ni nchi yenye mfumo wa maisha tofauti kabisa na Tanzania, unaanza kwanza na kazi kubwa ya ku adapt maisha ya hapa! Hiyo tu ni shule tosha! Wengine wanashindwa hapo mapema kabisa! Hakuna kupoteza muda, kila saa akili inabidi ifanye kazi.
Nawafahamu baadhi ya Watanzania walioko Marekani ningekuwa na uwezo ningewarudisha nyumbani! Maisha yamewakataa! Hawana vibali. hawajaenda shule, maisha yao ni shida sana, kwangu mimi afadhali kurudi nyumbani! Lakini pia nafahamu Watanzania si haba! wanaishi maisha ambayo wanayaita "American Dream" ambayo Tanzania ni wachache wanafika hatua hiyo!
Lakini pia nikija Tanzania kuna vijana wako hapo nyumbani, natamani ningekua na uwezo ningewaleta US, wako aggressive wanajua nini wanatafuta maishani, lakini hawana fursa wala connection ya kuwatoa walipo! Lakini pia kuna vijana wengine wanalilia kuja Marekani, ukiwaangalia tu unajua wanadhani Marekani ni kula bata tu! unajua wakija hapa hawatatoka afadhali wabaki bongo!