zee_latown
JF-Expert Member
- Feb 21, 2026
- 523
- 927
Habari kila mmoja humu jukwaani. Maisha ni kutofautiana, na kutofautiana ndiyo maisha yenyewe.
Mimi binafsi niliwahi kwenda US kwa shughuli mahususi za kimasomo, wakati huo nikiwa kijana mdogo sana.
Nilimaliza, na nilikuwa na wenzangu.
Wenzangu walipenda sana kuendelea kuishi huko na walikuwa na mipango ya muda mrefu US. Hali kwangu ilikuwa tofauti sana. Kwa mara ya kwanza nikawa tofauti na wengi sana kimtazamo.
Na hili nitalidadavua leo hapa. Mimi nilikuwa na sababu zangu, ingawa wengine waliona za kipuuzi.
Kwanza niligundua si rahisi kumiliki nyumba ya kuishi kwa wakati huo, na hata sasa si rahisi, kutokana na vyanzo vinavyoaminika. Mimi napenda mno kitu kinachoitwa kumiliki nyumba. Na hili limefanya nijinyime, nidundulize, na kufanikiwa kumiliki nyumba mbili Oysterbay (kwa jasho langu mwenyewe), pamoja na maeneo mengine mengi DSM.
Ile hali ya ugumu wa kumiliki nyumba ilinikatisha sana tamaa. Sikukaa miaka mingi, nikaanza kuichukia sana America. Mpaka leo nadhani hapanishtui; bado ile hali ya kutopapenda ipo, ingawa nikiamua kwa hali ya sasa naweza kununua nyumba.
Huwa nafikiria na kujiuliza, sijui nirudi nikaishi US upya au nighairi. Ila najikuta naghairi, ukizingatia umri umesogea mno. Napenda mno kitu kinachoitwa "kumiliki nyumba."
Wenzangu (RIP) walibaki wakaendelea na maisha, lakini mimi nikaona nirudi nyumbani nitumie fursa za hapa, kwa sababu niliona ni rahisi kumiliki nyumba kuliko kule US.
So napachukia bado till to date. 😄
Nawaheshimu sana wanaomiliki majengo US.
Na wish siku moja moyo wangu ufunguke nipapende tu US, ila nadhani nimetokea kutopaelewa.