Ukitaka kwenda kuishi Marekani inabidi ujipange

Ukitaka kwenda kuishi Marekani inabidi ujipange

Bongo maisha rahisi sana hata ukiwa na net ya 1.5m unaishi kwa raha.
Nyumba nzima ya 3 bedrooms Bongo unapanga kwa 300k kwa mwezi,wakati majuu master room moja kodi yake kwa mwezi ni zaidi ya 2m.
So majuu ukiyumba kidogo tu utalala nje,hakuna kulala ni mchakamchaka masaa 24.
Bongo hata ukiwa jobless hukosi mahali pa kula na kulala I mean hata kwa mjomba au shemeji utaenda kulala life linasonga na kitambi kinaota kabisa,Majuu hakuna ndugu wala mjomba wala jirani na hata kama kuna ndugu yako kule watu hawataki mazoea na mtu kila mtu yuko na stress zake.
So tafakari kabla ya kufanya maamuzi.

Sent from my SM-C7000 using JamiiForums mobile app
Umeeleweka mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Shida sio njaa ya mafanikio. Shida siwezi kuishi kwenye utamaduni wa design hiyo ya Marekani. Maisha sio kutafuta pesa tu.

Kuna mdau huko juu kasema, ukiwa unasaka maisha huko hata ukipata mtoto ni tabu nyingine umejiletea. Kwa mimi hiyo naona ni mateso tupu

Nchi huwezi kupiga story hata na jirani kila mtu bussy na mambo yake, hapohapo hata mtoto kuzaa ni kwa mahesabu makali aisee! Mimi loniless ingeniua. Nendeni mnaoweza sie hapahapa kwa Nyerere panatutosha, tena ukiwa na hela hapa bongo mbona tambarare tu.
Kwa kwl maosha ya upweke noma asee
 
Bongo maisha rahisi sana hata ukiwa na net ya 1.5m unaishi kwa raha.
Nyumba nzima ya 3 bedrooms Bongo unapanga kwa 300k kwa mwezi,wakati majuu master room moja kodi yake kwa mwezi ni zaidi ya 2m.
So majuu ukiyumba kidogo tu utalala nje,hakuna kulala ni mchakamchaka masaa 24.
Bongo hata ukiwa jobless hukosi mahali pa kula na kulala I mean hata kwa mjomba au shemeji utaenda kulala life linasonga na kitambi kinaota kabisa,Majuu hakuna ndugu wala mjomba wala jirani na hata kama kuna ndugu yako kule watu hawataki mazoea na mtu kila mtu yuko na stress zake.
So tafakari kabla ya kufanya maamuzi.

Sent from my SM-C7000 using JamiiForums mobile app
Duh
 
Miaka flani niko Bongo sielewi mambo hayaeleweki, nina sista angu yuko U.S nikaongea nae kuhusu kwenda Marekani kujaribu maisha anakubali, mipango inakamilika kijana nikatua Jackson Heartsfield Atlanta lengo kubwa la kwenda Marekani ni kupata exposure na kutafuta maisha.

Harakati zinazofuata ni mimi kutafuta kazi, Marekani kazi zipo ila sasa kule ukisikia kazi ni kazini kweli full supervision unafanya kazi kwa muda wa saa 10 mpaka 12, hiyo ni uongeze kipato ukizingatia kazi zenyewe unalipwa kwa saa, kwa hiyo lazima ukomaee ila kazi tu zipo.

Baada ya muda kudunduliza hela nahama kwenye basement nikahamia kwenye chumba kimoja sehemu moja hivi inaitwa Sandy Springs.

Tatizo la Marekani maisha expensive kipato cha kawaida ukizingatia nilienda kama mtu wa kawaida, kila kitu ni hela yaani ukisikia capitalism kule ndo inakuwa practice [emoji817]

Suala la kuwa na depression, loneliness ni moja ya vitu lazima ukumbane navyo usipokuwa makini lazima uingie kwenye matumizi ya madawa ya kulevya.

Ukikaa Marekani kitu unachoombea kila siku ni usiumwe sababu ni balaa, kuhusu starehe nayo pia ni mtihan kwa mtu mwenye kipato cha kawaida, wanawake wengi wa Atlanta ni materials things inabidi kuwapata ni gharama wako after money.

Kwa sasa hivi nilisharudi TZ sababu za kifamilia.

Maisha ya Marekani ili yakuendee vizuri uwe na professional means at least umesomea master kule kama hujasoma bachelor kwenye fani za science, au una kipaji kitu ambacho kwa Watanzania wengi mpaka wanakua hawajui vipaji vyao.

Kwenda Marekani hivihivi ni kugumu sana kwa sababu kwa maisha utajikuta unapata hela ya kawaida alafu unaishi kwa mawazo sana in short unataka kwenda Marekani kutafuta maisha jipange na uwe mtu wa kujiongeza sana, uwe competent, hivihivi sikushauri hata kidogo.

California, New York, Illinois, Massachusetts na Washington hayo ni majimbo ya kuyaepuka, kodi na gharama za maisha ziko juu ila Texas, Florida, Georgia, na north Carolina haya majimbo maisha yako cheap.

Vitu nilivyomiss Marekani ni exposure ila mwaka huu ntarudi nikiwa nimejipanga zaidi, kuna kikampuni nitaenda kukifungua deleware kama domestic company, baadae Virginia na Texas kama foreign company.
Kama umeweza ku-budget ghalama mpaka za wanawake utaonaje kua panatufaa, we Kaa TZ na wanao thubutu waache waende maana wengine hawapigii ghalama zingine za wanawake, hiyo kwao ni ziada tu
 
Malengo tu mkuu wangu. Na penye nia pana njia. Japo ili kupata visa kiurahisi.. pata passport hata mwaka mmoja kabla ya kwenda embassy. Itumie kwenda hata kenya hivi.. Huwa wanasema sometimes kama we hata kenya haujafika, kwa nini tukupe visa ya kwenda usa?. Wanaringa sana na visa ya nchi yao wakati watu tukifika huku ni kupigika kweli kweli kwanza kama nyani aliyepigwa marungu kichwani. Ila ndio hivyo.. mambo yakitulia. Yanatulia kwelikweli.
😁😁😁
 
Kuna yule dogo anajiita dullarstar anapiga box USA 🇺🇸 kila mara anakuja bongo sjui anatumia visa gani
 
Uwa najiuliza watu wanasema upweke ni kitu Gani uko majuu maana uwa sielewi .
Wabongo si wamezoea mara Shangazi kaja, mara shemeji katutembelea. Mara niende kwa washkaji hapo kitaa nikapige stories. Ukiwa ghetto mara utoke nje kuongea na majirani. Sasa huko kwa wenzetu mambo yote hayo hayapo. Kila mtu na maisha yake. Unaweza kuwa unaishi kwenye apartment moja na watu na vyumba vyenu vinatazamana ila hamjuani miaka yote.
 
Mbona tukiangaliaga movies hasa za ma black unakuta wako vijiweni au maghettoni wame chill au hao bills haziwahusu
 
Back
Top Bottom