Ukitaka kwenda kuishi Marekani inabidi ujipange

Ukitaka kwenda kuishi Marekani inabidi ujipange

mkuu umeng'ang'ania ukimbizi, kuna vita gani tanzania!? kwa mipango hii wala usiende huko maana utakufa njaa kabla hujatua uwanja wa ndege..
Mkuu shemeji yako kaenda kama mkimbizi ndio maana nauliza kwani kuna shida kujua, ndugu yangu.yeye ni raia wa congo na hapa tunaongea hajamaliza hata mwezi.ndio maana nataka nijue kwa upana maana mpaka sasa bado hajaanza kazi
 
Tatizo wenye ndoto za kwenda marekani kuishi wengi wao wanakimbilia kwenye miji mikubwa kama new york, california, Chicago, Boston, Manhattan ambayo ni very expensive!. Kuna miji ni very cheap na watu weusi wapo tu + huduma zote za kijamii zipo.
 
Mkuu shemeji yako kaenda kama mkimbizi ndio maana nauliza kwani kuna shida kujua, ndugu yangu.yeye ni raia wa congo na hapa tunaongea hajamaliza hata mwezi.ndio maana nataka nijue kwa upana maana mpaka sasa bado hajaanza kazi
ahaa hapa sawa mkuu..
 
Watanzania fungukeni akili

Unapotak kwenda nje ujue lengo ni lipi, kama lengo ni kutafuta pesa hata uwe na PhD kwa nchi kama Canada utachoma mahindi, yaani hawaitambui elimu yako.

Mfano mimi, lengo langu la kuondoka nchini sio kupata pesa nje ya nchi HAPANA, lengo ni elimu bora kwa watoto

Sin uwezo wa kusomesha Feza and the like nikatafuta ahueni nikapata CANADA sas uniambie nisiende?

Fungukeni Watz
 
Wale homeless people wanatokeaje ikiwa kazi ni bwerere?
Lazima watokee jamaa yangu, wengine ni mfumo , lakini wengine wamejikosesha wao wenyewe! umegoma kwenda shule, umejiingiza kwenye madawa ya kulevya, kutumia ama kuuza, ulevi nk. Hivyo Umetengeneza rekodi mbaya ya kutolipa madeni nk. Zile safety nets zilizowekwa na serikali kumsadia maskini umezitumia vibaya. Na tabu kubwa ya Marekani ni records! Kumbukumbu zako zote zinapatikana kirahisi, hizi mara nyingi zitakuandama maisha yako yote. Hivyo unapomuona Homeless kwa upande mwingine unajua kuna sehemu fulani amefanya kumfikisha hapo.
Hata wewe Panzi mbishi, utaajiri mtu mwenye rekodi mbaya kwenye kazi yako, Marekani background check ni lazima kwa kazi yoyote ile. Haya ndio maswala muhimu ambayo tunawaambia watu wanaoingia Marekani au tulio na watoto huku, kosa ambalo wewe unaliona dogo linaweza ku cost maisha yako forever! Hulipi tickets za makosa ya barabarani, unafukuzwa kwenye nyumba uliyopanga ni rahisi vutu kama hivyo kukupelea kuwa homeless, na inasikitisha kukutana na mtu kutoka nchi kama Tanzania kwa homeless, na inatokea.
 
Hongera kwa kutokata tamaa kupambana ni muhimu sana ..

For more than 20+ years and still kicking no turning back.

Nyumbani wengine imebaki ni humu humu JF na physically kuja kusalimia na kwenye matukio muhimu tu.

Nawashauri vijana wakipata fursa wapambane kikwelikweli wasiishi kwa kuangalia na kubeba fikra za kwenye filamu za Hollywood.

Kiufupi US ni land of opportunities na kama ukiweza kuishi US basi pasipo shaka waweza ishi sehemu yoyote duniani.

Vipi ulifanikiwa kuacha damu yako huku pia hahaha?
 
Mkuu shemeji yako kaenda kama mkimbizi ndio maana nauliza kwani kuna shida kujua, ndugu yangu.yeye ni raia wa congo na hapa tunaongea hajamaliza hata mwezi.ndio maana nataka nijue kwa upana maana mpaka sasa bado hajaanza kazi
Hao wakimbizi wanapewa green card,
Je mlifunga ndoa ,una cheti cha ndoa?
 
Habari zenu wana jamvi. Mimi naomba nichepuke kidogo nje ya mada. Natamani kwenda vacay U.S/ U.K / Canada. Ni familia yenye 4 kids. Swali langu ni njia gani rahisi naweza kuitumia kufika mojawapo kati ya nchi hizo nikimaanisha unafuu wa gharama. Je naweza kwenda tu na nikajitembeza mwenyewe au ni lazima niwe na mwenyeji au nitumie makampuni? Naombeni gharama makadirio ya gharama za maisha kwa mwezi mmoja kwa kila nchi tajwa hapo juu kuanzia cheap return tickets, malazi, chakula na mizunguko.
NB: Lengo sio kuzamia, kipato changu ni cha uhakika na kinaniruhusu kwenda kuosha macho mbele na kurudi home. Natanguliza shukrani!
Mkuu mbona maisha simple sana kwa sasa.

1) Kuhusu flight ticket, ingia online uangalie mashirikia makubwa ya ndege yanayokuja bongo kama Qatar, KLM, Turkish, Ethiopian Airlines kisha utaona gharama zote.
2) Kuhusu Malazi ingia pia online google uandike affordable hotels katika mji unaopenda kwenda utapata details zote. Kiufupi unaweza kufanya booking ya hotels LONDON hata ukiwa Namanyere au Ukara Ukerewe.
3) Kuhusu chakula vivyo hivyo ingia online uangalie affordable hotels katika mji unaotaka kwenda.
4) Kuhusu gharama za mizunguko: Nchi za wenzetu usafiri ni wa uhakika na affordabe kabisa. Usafiri mkubwa ni Train, ndege na BUS. Unweza pia kuingia online ukaangalia unapenda kwenda wapi na wapi na utapata details zote.
5) Kiufupi mkuu nchi za wenzetu siyo kama sisi. Kila kitu unapata online na kuna wakati unaweza kumwuliza mtu mtaani ikabidi na yeye ndio aingie kwanza online kuangalia ndio anakupa majibu. Muhimu wewe unafahamu lugha ya malkia kwahiyyo hakuna kitu kitakuwa kigumu kwako. Jipe muda wa kutosha ufanye ka-research kadogo utapata details zote unazotaka. Kwa wenzetu unaweza kuingia Supermarket ukajihudumia mwenyewe kila kitu mpaka kulipia bila kuzungumza na mtu. Kila kitu ni digitalized. Kila la kheri mkuu.
 
Aliniambia mambo yakiwa safi atanifanyia mpango niende.sasa kwa wenyewe hawa mambo huwa safi baada ya muda gani?
Huo mpango anakufanyiaje (kuhusu visa)?? Unaenda kama mme wake?, tourist, student, worker??

Huwa wanapewa nyumba, na allowance wanapokea za kuqnzia maisha wakati bado wana settle
 
Back
Top Bottom