Ukitaka kwenda kuishi Marekani inabidi ujipange

37 +10 ya kusawazisha mambo =47 hapo hata kibibi cha kizungu hakikutamani,kazi utaishia kupiga deki au kusukuma vizee.km una issue hapo mjini komaa nayo tu
Usimkatishe tamaa jamaa[emoji28]hujui anajipanga vipi. Pengine ana mtaji mzuri. Akiwa na uelekeo mzuri atatusua. Kuna hatua ukifika ni bora uende US wanaheshimu sana mitaji kuliko kuendelea Tz.

Kuna sababu nyingi kwann wafanyibiashara wengi wakubwa sio asili ya Afrika. Kuna kukwamishwa sana kwa sababu za kisiasa na kijamii.
 
Tanzania kwetu na Nigeria tofauti mno. Tuweke context sawa. Pili, hizo basic needs kwa immigrant anayetoka kwetu kishida shida bila mchongo au connection ataweza? Ataweza kulipia housing? Tuition fees za US? Bima au kama hana health bills?

Kimtazamo wangu kwa anayeanza asikurupuke kuzamia asikokufahamu bila kuwa na kianzio cha kueleweka. Utaishia pabaya. Umasikini Amerika ni kitu mtambuka. Pandemic ilichora picha nzuri. Nina uhakika ulijionea unless kama unaishi maeneo affluent na mbali na mmarekani wa kawaida. Hoja yangu ndio hiyo. Kwa anayetaka hebu aje ajionee kwanza hali halisi kwanza halafu achanganye uzoefu wake na wa kuambiwa. Halafu ajiulize... je, yaliyomo yamo?
Masdinero: Nadhani tuko pamoja, maybe the way we presents our ideas, mimi kama wewe nasema usikurupuke kuja Marekani! Narudia tena usikurupuke kuja US. Katika maandiko yangu nimesema usije Marekani bila aina ya vibali, legal papers! Visa ya uanafunzi kwangu mimi ndio visa ya kuanzia kama huna Green Card. Umetumia neno zuri "asikurupuke kuzamia usikokufahamu bila kuwa na kianzio cha kueleweka" Nimerudia sana hilo.
Nimeeleza pia katika posts zangu nyingine kuwa Marekani ni kubwa sana, inategemea umeingilia State gani, nani ni mwenyeji wako anayekupokea na kukushauri/kukusaidia kuanza maisha hapa! Nimesadia baadhi ya watu ku setlle US, najua nachokisema, na nimeshauri kwa baadhi ya watu kurudi Bongo! Na mpaka leo wananishukuru, nimesaidia pia badhi ya watu kulipia Tuition fee ili wasitoke nje ya Status.
Na umesema Pandemic ilichora picha nzuri, lakini pia haikutoa picha sahihi pia, Niko Texas, siishi affluent area, ni mji mdogo, predominantly Whites and few blacks, Walmart amabayo ni kimbilio la mtu wa kawaida haikufungwa! Kazi nayofanya ( haihusiani kabisa na na maswala ya afya haikufungwa) Ilikuwa ni mask tu! Watoto wangu wanaofanya proffesional jobs walifanyia kazi nyumbani, gharama za maisha kwangu zilishuka sana! Na support pesa za serikali nadhani unajua zilivyokuwa, ziliongeza kipatao changu kwa sehemu kubwa! Mwajiri wangu alikua anaotoa assistance ya fedha kila baadhi ya miezi mitatu! Hivyo Pandemic haikuniacha pabaya kabisa! In short iliniacha vizuri!
Nakuunga mkono kwa hilo usike kwa mchongo mchongo! Lakini pia nimeona watu wakija hawana Tuion fee, hawana bima ya maisha, majuzi kuna dada alikuja hivyo, ame graduate Nursing, na sasa kuna kampuni ina msadia kupata Green Card! Nawafahamu wengi wa aina hiyo! Pasipo chochote ulichokisema walitoka kimaisha! Sasa utasemaje? Naona kila mtu na bahati yake.
 
Maybe Masdinero nipe experience yako ya US je hauna success story ya Mtanzania aliyefanikiwa? Naona labda nakosea, uzoefu au ufahamu wako wa Marekani ni negative kabisa! Niliingia Marekani mara ya kwanza kikazi miaka ya 2005, ilikuwa ni just for a month for a workshop, nilikua North Carolina, kisha nikaja Atlanta, baada ya hapo nilitembelea jamaa zangu kabla ya kurudi Tanzania. Kwa kifupi Marekani ilinivutia, na wenzangu wakati huo walinipa picha kamili ya hapa, usije bila karatasi! uje ukiwa umejipanga. Na nilipoingia kuja kuishi walinipa support ya mawazo na mali, na sijutii kuwepo kwangu Marekani.Huo ndio msimamo wangu.
 
IMG_1795.jpg

Stereotypes za kuhusu Texas [emoji28]
 
Jibu: Maeneo ambayo yanasemwa kuendelea na kodi ziko juu watu wanaishi kwa amani zaidi ya maeneo kama US! Jibu lingine: Wengi hawaondoki kwa kushindwa uwezo, ufahamu na elimu ya kulingana na nchi zilizoendelea zaidi. Sekta ya elimu US imeyumba sana na kuachwa nyuma. Huu ni mjadala mwingne mpana tuuache.

Suala la kuhenya lazima lakini kuwe na sheria basi za kukinga wafanyakazi hata kidogo. Hivi ni ubinadamu kufanya kazi masaa zaidi ya 10 mfululizo? IKEA ina wamiliki na washika dau wanaotaka faida. Makampuni kwa asili yakiachwa huru yataenda popote au kufanya chochote ili tu kuongeza faida na kukua bila hvyo yataanguka. Sio kigezo cha maendeleo US, sana sana inakazia hoja ya US ni sehemu ya unyonyaji na kuchota huku wengi wakifa wanalia!

Kwenye kuhenya umeamua kutaja nchi zilizo chini ya marekani kwa maendeleo, sawa kazia hoja yako.

Una mtazamo wa kizamani sana kuhusu ujamaa. Serikali ili ilinde maslahi ya watu na nchi inayoongoza sio lazima imiliki njia za kuzalisha mali kama mwalimu na wenzie walivyojaribu. Umetaja China, ni mfano mzuri wa nchi inavyoweza kukua kiuchumi, kuondoa au kupunguza umasikini huku ikisimamia sekta zote bila kuzimiliki moja kwa moja. Hapo kwenye umiliki pia wamefeli kwa sababu ukienda Beijing utajionea kuna viashiria vikali vinaanza kutawala vya mambo kama ya US... mnahenya tu halafu wachache wanakula nchi.

Marekani kuna uongo unaotawala kwamba mtu unaweza tu kutoka. Kuna jamaa wanajiita mabosi wao wenyewe kwa kuendesha Lyft. Be your own boss. Propaganda hiyo imekuteka na wewe ndugu yangu.

Kijana aliyemaliza chuo bongo miaka michache tu iliyopita unamshaurije azamie US? Au una kitu mbele unaenda kuwasaidia? Una mpango gani ndugu "Kisamvu"? Akifeli utamrudisha au ndio shauri lake?
Mada ya mawazo ya Ujamaa wa zamani na leo mada ni nyingine! Sitaenda huko, Hebu nijibu aya yako ya mwisho.

1. Nimesaidia baadhi ya Vijana waliokwama na Tanzania ambao wameingia US nilioweza kufahamiana nao , si wengi, na wanafanya vizuri US through my guidance + juhudi zao wenyewe naona wanatoka kimaisha! Kule kukata tamaa ambao ndio wimbo waliokuwa nao bongo haupo tena.

2. Nimesadia baadhi wanafunzi walikokwama na ada kusoma US, Kijana mmoja nilimsadia Tution fee ya semester nzima, asije toka nje ya status

3.Kwa kijana aliyemaliza chuo Tanzania Akakwama kabisa hakuna mlango ulio wazi mbele yake, namshauri kama anaweza ajaribu US, nawafahamu vijana waliofanya hivyo! Si njia nyepesi but is worth trying, kuliko kulia kulia huna connections au huna mtaji!

4.Nimeshauri watu wacheze Greencard kujaribu bahati zao! Miaka miwili iliyopita jaam yangu mmoja alifanikiwa, nilimsadia process zote hapa anaendelea na maisha yake vizuri.

5. Nimewasadia baadhi ya vijana kama watatu hivi, waliokuja kusoma US na kutaka kuzamia pasipo plan yoyote warudi Bongo! Kuna binti mmoja niliwatafuta hata wazazi wake bongo wamshauri binti yao arudi nyumbani! Hiyo degree yake aliyosoma ina soko nyumbani, sio US alifanya hivyo, na mpaka kesho ananinishukuru.

Huo ndio mchango wangu ndugu Masdinero! Hebu na wewe toa ushauri kwa kijana ambaye kashindwa kabisa Tanzania, yaani mlango umefungwa! Kakosa ajira, hana mtaji, wala connection.Umeeleza baadhi ya nchi kama 30 ambazo ni bora kuishi na kuingia kuliko US, zitaje nchi hizo basi angalau ziwasaidie vijana waliokwama bongo wanaotaka kujaribu nje.
 
Masdinero: Nadhani tuko pamoja, maybe the way we presents our ideas, mimi kama wewe nasema usikurupuke kuja Marekani! Narudia tena usikurupuke kuja US. Katika maandiko yangu nimesema usije Marekani bila aina ya vibali, legal papers! Visa ya uanafunzi kwangu mimi ndio visa ya kuanzia kama huna Green Card. Umetumia neno zuri "asikurupuke kuzamia usikokufahamu bila kuwa na kianzio cha kueleweka" Nimerudia sana hilo.
Nimeeleza pia katika posts zangu nyingine kuwa Marekani ni kubwa sana, inategemea umeingilia State gani, nani ni mwenyeji wako anayekupokea na kukushauri/kukusaidia kuanza maisha hapa! Nimesadia baadhi ya watu ku setlle US, najua nachokisema, na nimeshauri kwa baadhi ya watu kurudi Bongo! Na mpaka leo wananishukuru, nimesaidia pia badhi ya watu kulipia Tuition fee ili wasitoke nje ya Status.
Na umesema Pandemic ilichora picha nzuri, lakini pia haikutoa picha sahihi pia, Niko Texas, siishi affluent area, ni mji mdogo, predominantly Whites and few blacks, Walmart amabayo ni kimbilio la mtu wa kawaida haikufungwa! Kazi nayofanya ( haihusiani kabisa na na maswala ya afya haikufungwa) Ilikuwa ni mask tu! Watoto wangu wanaofanya proffesional jobs walifanyia kazi nyumbani, gharama za maisha kwangu zilishuka sana! Na support pesa za serikali nadhani unajua zilivyokuwa, ziliongeza kipatao changu kwa sehemu kubwa! Mwajiri wangu alikua anaotoa assistance ya fedha kila baadhi ya miezi mitatu! Hivyo Pandemic haikuniacha pabaya kabisa! In short iliniacha vizuri!
Nakuunga mkono kwa hilo usike kwa mchongo mchongo! Lakini pia nimeona watu wakija hawana Tuion fee, hawana bima ya maisha, majuzi kuna dada alikuja hivyo, ame graduate Nursing, na sasa kuna kampuni ina msadia kupata Green Card! Nawafahamu wengi wa aina hiyo! Pasipo chochote ulichokisema walitoka kimaisha! Sasa utasemaje? Naona kila mtu na bahati yake.
Ndio, kila mtu na bahati yake. Sio kila mtu ana shangazi US. View point yangu iko kitahadhari zaidi. Ukisoma kwa haraka utaona niko -ve tu. Hapana. Huku utamaduni uko tofauti na Tz. Mambo ya kusaidiana na kubebana ni haba sana kwa uzoefu wangu. You are on your own. Lazima mtu aje akijua anafika wapi au kama ulivyosema, kwa nani na huyo mwenyeji wake awe wa uhakika. Wapo waliofanikiwa, kama wewe obviously, unless hujichukulii kama hadithi ya mafanikio ya mhamiaji Amerika. Wapo waliosoma kupata kazi wapo, wengne hata sio tu kusoma ni vipaji au ubunifu wamepata pa kujishkiza. Wengne jeshini.

Nilikuwa najaribu kuleta uwiano kwenye mtazamo ambayo nilihisi iko too +ve kutoka kwako Cassavaleaves. Sio kupinga kwamba fursa hamna bali kutoa changamoto zilizopo. Mfano suala la afya yaweza kuwa sio ishu; kuna njemba ni kama huwa haziumwi kuhitaji kwenda ER unless apate ajali na hata hapo kuna anayegongwa na gari akainuka na kusepa kabla paramedic kufika, hawa huduma ya bima ya afya ya nn? Wangapi wanazaa nyumbani? Mfano mwingne ni wewe Pandemic haikukuacha barabarani na vitu vyako lakini wangap wamemwagwa nje? Wangapi wamekufa kimzaha kwa kutopata huduma? Hasa kundi la watu fulani, sio siri iliongelewa nchi nzima. Sasa hapo wao kwa wao wewe mtz sijui uliyeanguka sijui utalia na nani. Wangapi wamepoteza akiba zote kipindi shughuli nying zimesimama? Hapa inaonyesha jinsi vipato ving huku ni "pokea mkononi mdomoni twende". Saving haiwezekani kwa payment ya kazi nyingi za kawaida. Labda wewe unalipwa mbali sana na $15/saa. Wengi wanalipwa chini ya hapo. Illegal but preverant. Mfumo uliopo huku unalazimisha mtu awe na nidhamu sana & mpango juu ya mipangilio yote. Hoja hapo nikachomekea ambay haikueleweka sijui au kutopendwa... anayway ni kwamba level itakayotumika "kufanikiwa" US hata Tz inawezekana sana. Mfano lifestyle atakayoishi mbongo mbele hawezi kabisa akiwa nyumbani. Kuna watu wanakomaa tu huku kwa ishu ambazo home hawawezi kufanya kwa ujira huohuo. Nyingne aibu hata kusema mwa watu. Mwambie rudi hawezi kwa ule msukumo wa ataonekana kafeli au hajafanya lolote la maana.

Tufate ushauri wa topic inavyosema tujipange sana kabla kuzamia ugenini. Fanya research, tembea kajionee kama unaweza, angalia njia zilizopitiwa na waliotangulia kwa umakini yawezekana uchochoro una kichaka mbele haufai tena.

Cassavaleaves sijui umenisoma? Karibu kahawa.
 
Mada ya mawazo ya Ujamaa wa zamani na leo mada ni nyingine! Sitaenda huko, Hebu nijibu aya yako ya mwisho.

1. Nimesaidia baadhi ya Vijana waliokwama na Tanzania ambao wameingia US nilioweza kufahamiana nao , si wengi, na wanafanya vizuri US through my guidance + juhudi zao wenyewe naona wanatoka kimaisha! Kule kukata tamaa ambao ndio wimbo waliokuwa nao bongo haupo tena.

2. Nimesadia baadhi wanafunzi walikokwama na ada kusoma US, Kijana mmoja nilimsadia Tution fee ya semester nzima, asije toka nje ya status

3.Kwa kijana aliyemaliza chuo Tanzania Akakwama kabisa hakuna mlango ulio wazi mbele yake, namshauri kama anaweza ajaribu US, nawafahamu vijana waliofanya hivyo! Si njia nyepesi but is worth trying, kuliko kulia kulia huna connections au huna mtaji!

4.Nimeshauri watu wacheze Greencard kujaribu bahati zao! Miaka miwili iliyopita jaam yangu mmoja alifanikiwa, nilimsadia process zote hapa anaendelea na maisha yake vizuri.

5. Nimewasadia baadhi ya vijana kama watatu hivi, waliokuja kusoma US na kutaka kuzamia pasipo plan yoyote warudi Bongo! Kuna binti mmoja niliwatafuta hata wazazi wake bongo wamshauri binti yao arudi nyumbani! Hiyo degree yake aliyosoma ina soko nyumbani, sio US alifanya hivyo, na mpaka kesho ananinishukuru.

Huo ndio mchango wangu ndugu Masdinero! Hebu na wewe toa ushauri kwa kijana ambaye kashindwa kabisa Tanzania, yaani mlango umefungwa! Kakosa ajira, hana mtaji, wala connection.Umeeleza baadhi ya nchi kama 30 ambazo ni bora kuishi na kuingia kuliko US, zitaje nchi hizo basi angalau ziwasaidie vijana waliokwama bongo wanaotaka kujaribu nje.
Cassavaleaves: Nimegundua wewe pia ni mjamaa angalau kwa uchache kwa hiyo misaada unayotoa (unless kuna kitu cha ziada hutuambii na kama ni kweli). Ujamaa dhana pana sana, ya siku ingne.

Siwezi kutoa wazo ambalo siwezi kulifata. Nilikuwa na ndoto ya kutoka na kuishi sehemu bora zaidi ya nilikozaliwa. Kuzaliwa sehemu sio nongwa ufe hapo hapo ndio mtazamo wangu. Sipendi kasumba za ufungwa au ufahari usio na msingi. Hata hivyo sikutaka kuwa mkimbizi wa kiuchumi kwahiyo dhana yangu ilikuwa nijijenge nilikokuwa napajua zaidi kabla ya kutoka kwenda nisikokuwa na ndugu au msaada wowote iwapo nikikwama. Nilitoka Tz kama mtembezi tu, mara kadhaa kuja kikazi US kwa ushirikiano wa taasisi fulani nyumbani. Hata sasa niko kwa muda kwa ajili ya utafiti fulani, zaidi ya hapo shughuli binafsi za uwekezaji. Uwekezaji US unalipa sana. Mfano miaka hii ya uviko kuna returns nimezipata ambazo Tz ni ndoto. Lakini mtaji wake sio lelemama. Na pia ni aina ya mtaji ambao ningekuwa mtumishi US nisingeweza kuuweka na kupata rejeo la maana kwa vipato vya Amerika. Siwezi kutoa ushauri general kila mtu ana hali tofauti na malengo tofauti. Itoshe kutoa angalizo ndugu zetu tahadhari muhimu sana au lazima wote tuchangie upande wa encouragement?
 
Lakini Cassavaleaves kuna jipu unalilea hapo kwenye maelezo yako. Dhana ya "mlango umefungwa" siikubali. Mtu aliyesoma kwa malengo akaelimika ni ngumu kuishia kinyonge eti mlango umefungwa. Kuna shida sehemu nadhani. Anyway ni mjadala mwingine.
 
Cassavaleaves: Nimegundua wewe pia ni mjamaa angalau kwa uchache kwa hiyo misaada unayotoa (unless kuna kitu cha ziada hutuambii na kama ni kweli). Ujamaa dhana pana sana, ya siku ingne.

Siwezi kutoa wazo ambalo siwezi kulifata. Nilikuwa na ndoto ya kutoka na kuishi sehemu bora zaidi ya nilikozaliwa. Kuzaliwa sehemu sio nongwa ufe hapo hapo ndio mtazamo wangu. Sipendi kasumba za ufungwa au ufahari usio na msingi. Hata hivyo sikutaka kuwa mkimbizi wa kiuchumi kwahiyo dhana yangu ilikuwa nijijenge nilikokuwa napajua zaidi kabla ya kutoka kwenda nisikokuwa na ndugu au msaada wowote iwapo nikikwama. Nilitoka Tz kama mtembezi tu, mara kadhaa kuja kikazi US kwa ushirikiano wa taasisi fulani nyumbani. Hata sasa niko kwa muda kwa ajili ya utafiti fulani, zaidi ya hapo shughuli binafsi za uwekezaji. Uwekezaji US unalipa sana. Mfano miaka hii ya uviko kuna returns nimezipata ambazo Tz ni ndoto. Lakini mtaji wake sio lelemama. Na pia ni aina ya mtaji ambao ningekuwa mtumishi US nisingeweza kuuweka na kupata rejeo la maana kwa vipato vya Amerika. Siwezi kutoa ushauri general kila mtu ana hali tofauti na malengo tofauti. Itoshe kutoa angalizo ndugu zetu tahadhari muhimu sana au lazima wote tuchangie upande wa encouragement?
Samahani mkuu hivi kwa wakimbizi kutoka sudan na congo huwa wanasaidiwa na serikali ya marekani au inakuaje maana naona wanaenda makundi kwa makundi,unakuta familia ina watoto kumi na nne na wazazi.nilitaka nijue tu maana nimeuliza hapo juu sijapata jibu.
 
Labda sio Texas nayoishi! Kumbuka Texas ukubwa wake si Mbali na Tanzania! Texas NEVER stopped during the Pandemic! labda miji ndani ya Texas! Baadhi ya shughuli kusimama nakubali! Labda TEXAS ya kwenye Comedy! Nimepokea wagene Dallas Fortworh aiport kipindi cha COVID!

Maelezo mazuri
 
Samahani mkuu hivi kwa wakimbizi kutoka sudan na congo huwa wanasaidiwa na serikali ya marekani au inakuaje maana naona wanaenda makundi kwa makundi,unakuta familia ina watoto kumi na nne na wazazi.nilitaka nijue tu maana nimeuliza hapo juu sijapata jibu.
Ndio, sidhani mtu mmoja mmoja ataweza saidia watu wanaokimbia vita. Ni serikali pekee yenye mamlaka ya kuruhusu kuingia kwenye nchi kama waathirika wa machafuko na uwezo wa jinsi ya kuwapa kianzio kipya cha maisha. Sio wote wanaohitaji hupata fursa hii. Kuna utaratibu wa kupata msaada. Rasilimali hata za nchi kubwa kama Marekani haziwezi kubeba wakimbizi wote. Sijui kiundani taratibu na nyaraka na kupokea wakimbizi. Kwann umeuliza? Labda kuna mtu hapa anaweza kukusaidia.
 
Ukitaka kujua life la state sikiliza hiphop.

Lighters up - Lil kim
Brooklyn Anthem - Foxy Brown.
Chicago - L.E.P Bogus
Welcome to ATL - J.Dupri
Welcome to Detroit - Trick ft Eminem
We built this city - Diplomat
Ghetto- Akon
Lighters Up - Lil Kim
[emoji91][emoji91][emoji91][emoji91][emoji91][emoji91][emoji91][emoji91]
 
Cassavaleaves: Nimegundua wewe pia ni mjamaa angalau kwa uchache kwa hiyo misaada unayotoa (unless kuna kitu cha ziada hutuambii na kama ni kweli). Ujamaa dhana pana sana, ya siku ingne.

Siwezi kutoa wazo ambalo siwezi kulifata. Nilikuwa na ndoto ya kutoka na kuishi sehemu bora zaidi ya nilikozaliwa. Kuzaliwa sehemu sio nongwa ufe hapo hapo ndio mtazamo wangu. Sipendi kasumba za ufungwa au ufahari usio na msingi. Hata hivyo sikutaka kuwa mkimbizi wa kiuchumi kwahiyo dhana yangu ilikuwa nijijenge nilikokuwa napajua zaidi kabla ya kutoka kwenda nisikokuwa na ndugu au msaada wowote iwapo nikikwama. Nilitoka Tz kama mtembezi tu, mara kadhaa kuja kikazi US kwa ushirikiano wa taasisi fulani nyumbani. Hata sasa niko kwa muda kwa ajili ya utafiti fulani, zaidi ya hapo shughuli binafsi za uwekezaji. Uwekezaji US unalipa sana. Mfano miaka hii ya uviko kuna returns nimezipata ambazo Tz ni ndoto. Lakini mtaji wake sio lelemama. Na pia ni aina ya mtaji ambao ningekuwa mtumishi US nisingeweza kuuweka na kupata rejeo la maana kwa vipato vya Amerika. Siwezi kutoa ushauri general kila mtu ana hali tofauti na malengo tofauti. Itoshe kutoa angalizo ndugu zetu tahadhari muhimu sana au lazima wote tuchangie upande wa encouragement?
Masdinero: Nakubaliana na wewe mahali bora kabisa kuishi duniani ni mahali ulipozaliwa, nikiwa na maana unajua tamaduni na mila, uko connected na jamii unayoifahamu. Lakini wewe unajua wazi si kila mtu alipozaliwa panaweza kumwezesha mtu kuyatunza maisha yake na kumpa mahitaji anayoyatafuta, Si Tanzania tu, is just a global trend, watu wanatoka vijijini kuja kuishi mijini, unajua ni nini wanachokitafuta. Nchi nyingi Africa zimeshindwa kabisa katika hilo.Ulisema Nigeria tuiweke kando, lakini na pia Tanzania tunaelekea huko huko Taratibu kama sera za kutengeneza ajira na kukuza uchumi zisipoangaliwa tena, nadhani ndio kiini cha mada hii, kuna kundi la vijana wanaona fursa nyumbani zimebuma, wewe umeweza kukomaa, kuna wengi wameshindwa.
Hivyo sio wote tumekuja huku kwa sababu ya Propaganda za Hollywood au MTV, hapana kuna maisha fulani tulikuwa tunayatafuta, ambayo Tanzania tusingeweza kuyapata. Naweza kusema returns ni kubwa mno kwa kazi nayofanya Marekani nikilinganisha na kazi yenye wadhifa niliyokuwa nafanya Tanzania.
Kwa mtu wa level yako kama unavyonieleza, nyumbani kunalipa, na hapa Marekani kama ukiwa na uwezo wa kufungua biashara zinalipa pia, nawafahamu baadhi ya Watanzania, si tu kwamba ni madereva wa magari makubwa, wana own kampuni za usafirishaji, hali zao za kiuchumi ni kubwa na wako mbali kimafanikio.
Marekani ina changamoto nyingi, nakubali kabisa, lakini pia ina fursa nyingi pia.

Naukubali mwaliko wako wa Kahawa, Shukran, Karibu Texas.
 
Ndio, sidhani mtu mmoja mmoja ataweza saidia watu wanaokimbia vita. Ni serikali pekee yenye mamlaka ya kuruhusu kuingia kwenye nchi kama waathirika wa machafuko na uwezo wa jinsi ya kuwapa kianzio kipya cha maisha. Sio wote wanaohitaji hupata fursa hii. Kuna utaratibu wa kupata msaada. Rasilimali hata za nchi kubwa kama Marekani haziwezi kubeba wakimbizi wote. Sijui kiundani taratibu na nyaraka na kupokea wakimbizi. Kwann umeuliza? Labda kuna mtu hapa anaweza kukusaidia.
 
Wakimbizi wanaoingia Marekani wanapata msaada kutoka serikalini ili ku settle US, kwanza wanaandaliwa mahali pa kukaa kwa kipindi cha kama miezi mitatu, huku wanalipwa, na halafu wanatafutiwa kazi na serikali. Na pia wanaendelea kupata msaada wa "food stamp" na huduma za matibabu kama hawajiwezi mpaka watakapoweza kusimama na miguu yao. Niko connected na wakimbizi toka Burundi na Zaire, maana nimefanya kazi katika mashirika ya kuhudumia wakimbizi Tanzania, na nimeona jinsi wanavyoanza maisha US, wengi hawajui kiingereza, kuna taasisi zinazolipwa na serikali kuwasaidia na mashirika mengi ya kidini na na kibinasfi hupewa tenda hizo.
 
Masdinero: Nakubaliana na wewe mahali bora kabisa kuishi duniani ni mahali ulipozaliwa, nikiwa na maana unajua tamaduni na mila, uko connected na jamii unayoifahamu. Lakini wewe unajua wazi si kila mtu alipozaliwa panaweza kumwezesha mtu kuyatunza maisha yake na kumpa mahitaji anayoyatafuta, Si Tanzania tu, is just a global trend, watu wanatoka vijijini kuja kuishi mijini, unajua ni nini wanachokitafuta. Nchi nyingi Africa zimeshindwa kabisa katika hilo.Ulisema Nigeria tuiweke kando, lakini na pia Tanzania tunaelekea huko huko Taratibu kama sera za kutengeneza ajira na kukuza uchumi zisipoangaliwa tena, nadhani ndio kiini cha mada hii, kuna kundi la vijana wanaona fursa nyumbani zimebuma, wewe umeweza kukomaa, kuna wengi wameshindwa.
Hivyo sio wote tumekuja huku kwa sababu ya Propaganda za Hollywood au MTV, hapana kuna maisha fulani tulikuwa tunayatafuta, ambayo Tanzania tusingeweza kuyapata. Naweza kusema returns ni kubwa mno kwa kazi nayofanya Marekani nikilinganisha na kazi yenye wadhifa niliyokuwa nafanya Tanzania.
Kwa mtu wa level yako kama unavyonieleza, nyumbani kunalipa, na hapa Marekani kama ukiwa na uwezo wa kufungua biashara zinalipa pia, nawafahamu baadhi ya Watanzania, si tu kwamba ni madereva wa magari makubwa, wana own kampuni za usafirishaji, hali zao za kiuchumi ni kubwa na wako mbali kimafanikio.
Marekani ina changamoto nyingi, nakubali kabisa, lakini pia ina fursa nyingi pia.

Naukubali mwaliko wako wa Kahawa, Shukran, Karibu Texas.
Mkuu kweema mkuu
 
Wakimbizi wanaoingia Marekani wanapata msaada kutoka serikalini ili ku settle US, kwanza wanaandaliwa mahali pa kukaa kwa kipindi cha kama miezi mitatu, huku wanalipwa, na halafu wanatafutiwa kazi na serikali. Na pia wanaendelea kupata msaada wa "food stamp" na huduma za matibabu kama hawajiwezi mpaka watakapoweza kusimama na miguu yao. Niko connected na wakimbizi toka Burundi na Zaire, maana nimefanya kazi katika mashirika ya kuhudumia wakimbizi Tanzania, na nimeona jinsi wanavyoanza maisha US, wengi hawajui kiingereza, kuna taasisi zinazolipwa na serikali kuwasaidia na mashirika mengi ya kidini na na kibinasfi hupewa tenda hizo.
@mkosa shingo
 
Ina maana captalism ipo hadi kwenye love? Mimi nijuavyo mapenzi hayana upendeleo ukiwa poor una wakwako na tajir ana wakwake vilio vipo kwa woote kupigwa chini hata Billgates yamemkuta je mimi wewe ni nani? Inaonekana mleta mada ulikuwa bussy sana mbususu ukapiga chini.
 
Habari zenu wana jamvi. Mimi naomba nichepuke kidogo nje ya mada. Natamani kwenda vacay U.S/ U.K / Canada. Ni familia yenye 4 kids. Swali langu ni njia gani rahisi naweza kuitumia kufika mojawapo kati ya nchi hizo nikimaanisha unafuu wa gharama. Je naweza kwenda tu na nikajitembeza mwenyewe au ni lazima niwe na mwenyeji au nitumie makampuni? Naombeni gharama makadirio ya gharama za maisha kwa mwezi mmoja kwa kila nchi tajwa hapo juu kuanzia cheap return tickets, malazi, chakula na mizunguko.
NB: Lengo sio kuzamia, kipato changu ni cha uhakika na kinaniruhusu kwenda kuosha macho mbele na kurudi home. Natanguliza shukrani!
 
Back
Top Bottom