masdinero masproblemas
JF-Expert Member
- Mar 19, 2022
- 224
- 178
Sasa unarudia nilichoandika[emoji1]kwa mara ingine kama una uwezo wa kuchagua pakwenda kuishi US sio no1. Sikuongelea watu waliodesperate, mwenye njaa hana uchaguzi.Labda sikukuelewa jamaa yangu, na pia kwa lugha uliyotumia! Kwanza Hakuna jamii isiyo na shida ulimwenguni! Kitabu cha dini ya Kikristo kinasema katika aya fulani, maskini mnao siku zote ulimwenguni! Ndio maana hata sera za Ujamaa zenye kutaka kuondoa Umaskini kwa huwa zinashindwa! Marekani inaweza kuwa na 1% inayomiliki uchumi, Je nchi nyingine huwa na nini? Ni jamii gani isiyo na tabaka la Juu! Umeeleeza ju ya Scandnavia countries, nadhani uko informed juu ya mabadiliko mengi kuhusu wageni katika nchi hizo, Scandnavia countries za miaka ya nyuma kuingia, kupata kazi na maisha hata kwa wakimbizi tu si rahisi tena! Hapa tunazumgumzia mtu wa KUJA anayetafuta maisha ugenini! Jinsi ya kuingia na kupata au kutengeza maisha yake ukilinganisha na alikotoka! Sidhani kama tunalinganisha quality of life! Hicho ni kitu kingine kabisa.
Umeeleza mambo mengi yenye negative kama shida za usalama, niko Marekani na Marekani ni kubwa sana, hivyo unapozungumizia violence uwe makini sana, sio kama unavyoona kwenye Media! Labda hofu yangu ya maisha Marekani niliyopo ni kufa kwa ajali barabarani sio risasi! Maana licha ya bararabara kuwa kubwa tunaendesha kwa kasi sana hasa huku Texas! Siogopi hata kidogo kupoteza maisha kwa bunduki!
Kuhusu ubaguzi, nayo pia unahitaji kuwa naungalifu, Nimekamatwa sio mara moja na polisi kwa kuvunja sheria za barabarani, sikubaguliwa, sikuonewa na wala kudhalilishwa! Nilionyeshwa makosa yangu na kuambiwa nilipe faini! Actually nimewahi kukamatwa nikiwa na arrest warrant, yaani kesi yangi imesomwa Mahakamani sikutokea, kwa makosa ya barabarani, Polisi mweupe aliniambia kwa nini nisilipe faini kuliko kunipeleka Jela! Nilifanya hivyo mambo yakaisha! Watoto wangu ni vijana, wanatoka usiku, wanaenda viwanja hawajawahi hata kidogo kusimamishwa na polisi sababu n iweusi! Sio kwamba wana bahati, bali wanafuata sheria! Ni vigumu kwa mtazamo wangu Polisi kukuamkia tu mahali kwa sababu ni mweusi, inategemea wapi au maeneo gani! Na kipi hasa kimemfanya Polisi akufuate wewe! Hiyo knife violence mkuu ipo kila mahali!
Kuhusu bima za Afya nakubali ni ghali ukilinganishwa na nchi nyingine, napenda kutumia mfano wangu, mimi ni kama mtu kawaida, I dont think I'm really middle class American, napiga kazi Kiwandani, nina Medical Insurance mbili ya Kawaida na meno, nalipa roughly $400 kwa mwezi, napata matibabu mazuri na pia Kiwanda nachopiga mzigo naweza kwenda wakati wowote kupata matinabu kwa $40 kwa mwezi. Sasa unataka niseme Huduma za Afya Mbovu? Unalinganisha na wapi hasa? Hasa kwa mimi mtu wa KUJA toka bongo!
Nasema tena Marekani sio Paradiso, kila Nchi ina upper class! kumbuka hiyo 1% unayoizungumza hai control Marekani peke yake, ina control ulimwenguni kote, hata wewe uliko pengine kwa sehemu inakukaba pasipo kujitambua!
Hivyo kama Scandanavia, New Zealand ni rahisi kuishi, wasaidie vijana wa kibongo watafute fursa huko! Kwangu Marekani from my own practical experience ni rahisi kuingia na ku establish maisha kuliko hizo sehemu ulizo zitaja.
Polisi US wa hovyo ni wengi mno. State zote. Huwezi kunidanganya. Sijui uliingia mwaka gani US huko Texas. Mfano mmoja nilishuhudia ufedhuli kati ya Nov mwaka 1999 na Dec 2000 nikiwa kwenye assoc fulani iliyokuwa ikishirikiana na ACLU, kulikuwa na movement za kupinga WTO na mashirika ya kifedha ya kimataifa... maandamano ya amani yalitembezewa kipigo miji yenye hadhi ya juu. Nilinusurika Seattle lakini wenzangu wa DC walijeruiwa vbaya.
Ubaguzi unaosema hujapata kuupitia shukuru sana, wewe ni exception sio the norm. Usipake rangi picha kama huku ukizamia basi itakuwa mserereko tu... wengi sana wamefeli kuliko waliofaulu. Amerika ni foxhole, lugha yetu inakosa maneno ya kutafsiri napata shida. Yaani jitihada na ubunifu ambayo mtu atakuja kuutumia huku akiwekeza nyumbani atapata zaidi maishani kuliko anavyodhani.
Huku maisha ni vita sio rahisi.