Ukitaka kwenda kuishi Marekani inabidi ujipange

Ukitaka kwenda kuishi Marekani inabidi ujipange

Binafsi nipo USA miaka 20 sasa. Mwanzo ilikuwa changamoto sana.. hasa kupata green card. Kweli maisha yalibadilika nilipoipata. Bila ya hio green card au uraia full.. USA mtu utateseka sana. Ukiwa na green card lakini...
1. unasoma bure degree ya kwanza... na nyingine scholarships kibao..
2. ukishasoma kama ulivyosema ndio unapata kazi nzuri..
3. ukiugua.. unapata asilimia kubwa tu mshahara wako vizuri..
4. ukipoteza kazi.. unalipwa pia fidia nzuri tu kila mwezi.. nk.
5. Unasafiri kwenda bongo bila kikwazo... nk.

Binafsi huku matumizi nimeweka chini. Upuuzi wa kushindana na WaTz wengine kununua nyumba na kubadili magari kila siku sifanyi. Investments zangu ni Tz. Na hazijaniangusha kamwe.
Hongera Mkuu, ulipata Green Card kupitia D.V lottery, Ndoa or...?
 
Miaka flani Niko bongo sielewi mambo hayaeleweki Nina sista angu Yuko u.s nongea nae kuhusu mikwenda huko marekani kujaribu maisha anakubali mipango inakamilika kijana natua Jackson heartsfield Atlanta lengo kubwa la kwenda marekani ni kupata exposure

Harakati zinazofuata ni mim kutafuta kazi marekani kazi zipo Ila Sasa kule ukisikia kazin kazini kweli full supervision unafanya kazi masa 10 mpaka 12 hiyo ni uongeze kipato ukizingatia kazi zenyenyewe unalipwa kwa masaa kwa hiyo lazima ukomaee Ila kazi tu zipo, baada ya mda kudunduliza ela nahama kwenye basement nyumbani kwa sister nahamia kwenye kichumba kimoja sehemu moja hivi inaitwa sandy springs

Tatizo la marekani maisha expensive kipato cha kawaida ukizingatia nilienda kama mtu wa Kawaida kila kitu ni ela yaan ukisikia capitalism kule ndo inakua practice 💯 swala la kuwa na depression, loneliness ni moja ya vitu lazima ukumbane navyo usipokua makini lazima uingie kwenye matumizi ya madawa ya kulevya

Ukikaa marekani kitu unachoombea kila siku ni usiumwe sababu ni balaa, kuhusu starehe nayo pia ni mtihan kwa mtu mwenye kipato Cha kawaida, wanawake wengi wa Atlanta ni materials things inabidi kuwapata ni gharama wako after money

Kwa sasa hivi nilisharudi tz sababu za kifamili na maisha ya marekani ili yakuendee vizuri uwe na professional means at least umesomea master kule kama hujasoma bachelor kwenye fani za science, au unakipaji kitu ambacho kwa watanzania wengi mpaka wanakua hawajui vipaji vyao, kwenda marekani hivi hivi ni kugumu sana kwa sababu kwa maisha utajikuta unapata ela ya kawaida alafu unaishi kwa mawazo sana in short unataka kwenda marekani kutafuta maisha jipange na uwe mtu wa kujiongeza sana na uwe competent hivi hivi sikushauri hata kidogo

Vitu nilivuomiss marekani ni exposure Ila mwaka ntarudi nikiwa nimejipanga zaidi
Vijana wa kitanzania,kwa kweli mnatushangaza Sana .Kabla sijakuchambua vizuri kuhusu mada yako,hivi kweli huu ndio mwandiko usio na nukta wa aya?Mm nitaamini vipi mada yako,kama hata kuandika Ni shida?
 
Nimekaa US mwaka wa 12 nikiwa na green card, sijawahi kujutia kuja. Nilijaribu kurudi nyumbani nikapata frustration za kutosha na kuona bora nirudi. Marekani ili uishi unatakiwa kufanya kazi, uwe na Green card au citizenship. Unatakiwa uwe na profession ikiwa umekuja nayo au umeipata huku yote sawa. Uchumi wa hapa ni capitalistic so hamna shortcut, ukifanya ujanja ujanja utaadhirika tu. Ukiwa professional hutajuta, hamna nyumba ya $400 lbd huko kusiko na usalama lkn nilipo mie nalipa $2000 kwa 2 bedroom lkn natengeneza sio chini ya $8000 kwa mwezi naweza kuishi dream life na pia nawekeza nyumbani bila kujali kuna challenge nyingi sana. Marekani ni ngumu lakini Tanzania is far from ugumu. Ndo mawazo yangu
Uliingia kwa Visa gani?, na sasa una aina gani ya Geeen Card?
 
Kuna kampuni ilinisaidia kunifanyia petition my good brother. Ndoa nilijaribu aisee iligonga mwamba vibaya kidogo nirudishwe bongo 😂😂😂
Hatari sana.., inamaana wakati huo visa yako ilikuwa inakaribia ku expire..? Au ulikuwa bafo On job Training?
 
Nyie mlokaa mambele miaka 12 sijui 20 toweni ma koneksheni basi
Halafu sasa kwakuwa ushaaga home huko Kibondo ama Sumbawanga na wanajua upo majuu, basi wanategemea kuwa ushatoboa maisha na ukipita mchango tu wa ndugu wanategemea utoe pesa ndefu. Kumbe choka mbaya tu na wewe, utaishia kupata depression bure. Ndio maana watu huwa wanaogopa kurudi home, kila mwaka anapiga chengachenga tu. Kiufupi kutoboa ukienda ughaibuni ni bahati tu sawa na ilivyo bahati kutoboa ukiwa bongo hata kama una mtaji wa biashara maana unaweza usitoboea na wanaofanikiwa ni wachache sana.
Kiukweli kitu nimejifunza ni kwamba mtu wa kufanikiwa.. atafanikiwa tu. Iwe ni Tz au USA. Japo kwa mtu kama mimi niliyezaliwa familia ambapo ndugu wote ni maskini.. naamini investments nilizoweka Tz nisingeweza kufanya hivyo kama nisingekuja USA. Na sasa hivi mimi ndio Fogo kupita wote kwa ukoo mzima.

USA mshahara ni mkubwa.. na binafsi matumizi huku nimeyafanya madogo sana sana. Naweza tengeneza usd $12000 kwa mwezi baada ya kulipa taxes.. na nika-save $10000 manake kila mwezi na-save 23million tshs. Sina watoto na sina mke. Main investments ni Tz..

Nilioa mke USA karibu aniue.. na bahati nzuri sikuzaa naye watoto.

USA ni nzuri kuliko Tz ukijielewa, usipoharakisha kuoa au kuzaa sababu watoto USA wana gharama zaidi ya Tz. All in all ni kucheza karata zako tu vizuri. Lakini kama ww hauna mipango, unakata tamaa, ni mvivu na hauwezi ku-sacrifice.. bora ungebakia bongo.. ngoma la huku hadi maisha yakae mkao.. sio mchezo.. ila yakikaa .. una-enjoy.
 
Hatari sana.., inamaana wakati huo visa yako ilikuwa inakaribia ku expire..? Au ulikuwa bafo On job Training?
Nilikuja na student visa F1. Niliweza fanya kazi nikiwa nayo tena vizuri tu. Nikataka kupanda level ya immigration status. Nikajichanganya na manzi flani. Ukioa tu, hapo hapo unaweza omba PR (Permanent residence/ green card). Basi nikafanya hivyo. Unapewa lakini ina limitations manake ndoa iki-survive for 2 years unarudi naye ndio wanakupa Yenyewe sasa ya kudumu. Kwa wote ninaowajua.. hio miaka miwili kwani ndoa inakuwa poa? Na unakuta uliingia kwa ndoa in good faith ukitaka kuanza maisha na demu.. ila yeye anawaza tu kwamba ww hauna mpango naye na ulimwoa ili kupata uraia. Na matatizo madogo madogo kwenye ndoa, basi wanaanza kuleta vurumai. Asilimia kubwa watu hawapatagi.

Hatari sana.., inamaana wakati huo visa yako ilikuwa inakaribia ku expire..? Au ulikuwa bafo On job Training?
Visa ilikuwa sawa tu. Ila nilitaka kupanda daraja. 😂😂😂. Student visa ina faida zaidi ya visitor.. lakini ni cha mtoto sifuri kabisa kulinganisha na green card. Mie nilitaka mzee mwenyewe green card.
 
Kiukweli kitu nimejifunza ni kwamba mtu wa kufanikiwa.. atafanikiwa tu. Iwe ni Tz au USA. Japo kwa mtu kama mimi niliyezaliwa familia ambapo ndugu wote ni maskini.. naamini investments nilizoweka Tz nisingeweza kufanya hivyo kama nisingekuja USA. Na sasa hivi mimi ndio Fogo kupita wote kwa ukoo mzima.

USA mshahara ni mkubwa.. na binafsi matumizi huku nimeyafanya madogo sana sana. Naweza tengeneza usd $12000 kwa mwezi baada ya kulipa taxes.. na nika-save $10000 manake kila mwezi na-save 23million tshs. Sina watoto na sina mke. Main investments ni Tz.. mai???

Nilioa mke USA karibu aniue.. na bahati nzuri sikuzaa naye watoto.

USA ni nzuri kuliko Tz ukijielewa, usipoharakisha kuoa au kuzaa sababu watoto USA wana gharama zaidi ya Tz. All in all ni kucheza karata zako tu vizuri. Lakini kama ww hauna mipango, unakata tamaa, ni mvivu na hauwezi ku-sacrifice.. bora ungebakia bongo.. ngoma la huku hadi maisha yakae mkao.. sio mchezo.. ila yakikaa .. una-enjoy.
Wabongo wengi (sio wote) hua wanafeli coz hata nchi za watu atataka aishi kama Bongo,ujanja ujanja na short cut kwenye kibarua chake,uvivu,kutaka kuishi kama wenyeji na hukata tamaa mapema,

Nimeshuhudia wengi wakipitia hayo.
 
Ndio hivyo mkuu mpo wachache mnaofanikiwa kwa kutengeneza hata hiyo faida ya 2.3M kwa mwezi. Watu wengi unakuta wanateseka haswa kutengeneza hiyo pesa, hasa watu wa vibarua vibarua. Halafu uwe na bahati kwamba uwe na BIMA ya afya inayoeleweka. Zaidi ya yote mkuu, nadhani imekuchukuwa muda huenda si chini ya 5 years kupata cash flow kama hiyo. Sasa shida inakuja kama umetokea familia maskini na ni extended, wao wanaamini ushatoboa. Unajikuta kwa mwezi unabakiwa na 1M tu, pesa ambayo ni ya kawaida ukilinganisha na expectations za watu wengi.
 
Well said brother 👏👏👏
 
Ni 23 million mkuu wangu. Million 23. Binafsi nafanya kazi za travel RN wanalipa vizuri sana.. Ndugu niliwafyekelea mbali. Tena walinifanyia unyama sana wakati sina $$. Kwa hio sasa ivi nasaidia wagonjwa na misiba.. tena kwa limits.. manake wema usizidi uwezo.

Wanalipa kuanzia $100 kwa saa na kuendelea.. unaweza piga masaa hata 80 kwa wiki ukitaka.. manake ukiamua unaweza pata $8000 kwa wiki. Wakitoa taxes.. unabakiwa na $6000 mfukoni sawa na karibia 14 million tshs. Binafsi nina investment programs nyingine, kwa hio sifanyi kazi hivyo. Lakini $12000 to $15000 per month unaipata kirahisi sana tu pia as a travel RN.
 
Back
Top Bottom