Ukitaka kwenda kuishi Marekani inabidi ujipange

Nilikuja na student visa F1. Niliweza fanya kazi nikiwa nayo tena vizuri tu. Nikataka kupanda level ya immigration status. Nikajichanganya na manzi flani. Ukioa tu, hapo hapo unaweza omba PR (Permanent residence/ green card). Basi nikafanya hivyo. Unapewa lakini ina limitations manake ndoa iki-survive for 2 years unarudi naye ndio wanakupa Yenyewe sasa ya kudumu. Kwa wote ninaowajua.. hio miaka miwili kwani ndoa inakuwa poa? Na unakuta uliingia kwa ndoa in good faith ukitaka kuanza maisha na demu.. ila yeye anawaza tu kwamba ww hauna mpango naye na ulimwoa ili kupata uraia. Na matatizo madogo madogo kwenye ndoa, basi wanaanza kuleta vurumai. Asilimia kubwa watu hawapatagi.

Au wee ndio yule mjomba wangu nn loiruki labda Ni wee aise
 
Wafanyakazi wa McDonalds na Walmart wamepata fursa kujisifu wanaishi Marekani.

Wanaume wazima wameamua kusomea unesi maana kila kona wamebanwa hawapati kazi. Their feminine side ultimately takes control of their lives out of a sheer desperation to survive in a iredeemiably racist, capitalist society.

Hao wanaume wangekuwa TZ wasingefikiria hiyo kazi ya kike hata siku moko.

Dume zima anajisifia yeye registered nurse?!!
Sijawahi kukutana na ufala, ujinga uliokithiri kama huu, [emoji1785] embu futa haya matapishi yako,

Jitu Zima lina dikiri kusema Kuna kazi za kike na kiume. Subiria uumwe uje uuguzwe na Nesi mwanaume alafu urudie kusema haya unayo Nena.

Sasa mbaguzi hapo ni nani kati ya hao unao waita wa baguzi na wewe. Maana ubaguzi sio mpaka uwe wa rangi ya mtu.

Ovyoooo mxiuuuuuuuuuu
 
Kwa nn wanagoma je mm ambae nimesoma account Kaz ganj naweza pata au science sna ndio zinaitajiak
Kama umesoma account, kuna exams za accountant, utasoma utapata certification... then utatafuta internship..then kazi hauwezi kukosa kamwe...
That's the easy part ..

**Naona wengi wanauliza wakienda sijui itakuwaje, hivi au vile..?

**Swali la kujiuliza utapataje VISA????

ishu ipo kwenye KUAPATA HIVI VITU...

VISA
PERMANENT RESIDENT
SOCIAL SECURITY NUMBERS
WORK PERMIT
 
Wafanyakazi wa McDonalds na Walmart wamepata fursa kujisifu wanaishi Marekani.

Wanaume wazima wameamua kusomea unesi maana kila kona wamebanwa hawapati kazi. Their feminine side ultimately takes control of their lives out of a sheer desperation to survive in a iredeemiably racist, capitalist society.

Hao wanaume wangekuwa TZ wasingefikiria hiyo kazi ya kike hata siku moko.

Dume zima anajisifia yeye registered nurse?!!
Goldschmidt: Sijakuelewa, ni chuki yako dhidi ya capitalist society au una mengine! Naona umeandikia hasira sana! Je wanaofanya kazi za nursing ni wanaume kutoka Tanzania tu? Elewa hiyo dhana ya kazi za kike na kiume ndio inarudisha nyuma maendeleo ya watu wengi dunia ya tatu! Hebu turudi nyumbani tu kama wanawake wangeamua kujifunza kuwa madereva, mafundi wa magari, ujenzi, umeme jamii ingekuwa wapi leo! Huo mfumo wa kufikiri kijima ni sababu mojawapo bado imetufunga katika lindi la umaskini katika nchi yetu ya Tanzania!

Tusadie kutupa lists za kazi za kiume na kike basi! Mwisho wa siku kazi ni le ambayo inaweza kukimu na kumudu maisha ! au ambayo unaona inaendana na interests zako!
 
Marekani sio nchi ya kuishi. Kuzamia US ni kuweka maisha rehani. Uzi umegusia moja ya viwili nyeti huduma ya afya, na kingne ni hali ya usalama binafsi. Kimsingi kuna nchi nyingi zilizoendelea za kwenda kutafuta maisha bora. US inatrend na kuonekana sana lakini maendeleo ni ziro. Kazi iendelee.
Masdinero: Hivi majuzi nimehudhuria sherehe kama mbili za watu ambaao wanaapishwa kuwa raia wa Marekani, ofisi zilifunguliwa saa moja asubuhi hadi saa kumi na mbili jioni, Huo umati ambao niliuona kutoka mataifa mbali mbali ulinishangaza, kama maendeleo na uchumi wa marekanii ambao umeuita ziro sidhani ingekuwa hivyo! Niliona Waarabu, Wachina, Scandanavians, Filipino, Japanese, Cuba nk. Kwa kifupi waaafrika walikua ni wachache mno!

Nilijiuliza maswali hayo hayo, Kama US ni mbaya, hali ya usalama binafi haipo, ni nini hasa kinachofanya au kinachovuta watu kuja au kukimbilia katika katika nchi hii! Kwa nini hata wailio na uweza duniani wanataka kuwekeza Marekani! Karibu gas stations nyingi hapa Texas nilipo ni mali ya wahindi! Hoteli za hali ya kati pia! Nimeshangaa kusoma leo hao matajiri wa Kirusi kama kina Roman Abramovic na wengine wanavyomiliki mali Marekani! Kama maendeleo ya US yangekua ziro kama unavyosema wewe, jamaa hawa wengewekeza US ? Je Wao ni wapumbavu!

Kwa kifupi Masdinero, Marekani ina mapungufu mengi kama mataifa mengine lakin ni nchi ambayo bado inatoa opportunities kwa mtu wa KUJA asiwe mzawa wa hapa kufanikiwa kimaisha kuliko nchi nyingi zilizoendelea, huo ndio ukweli, ni vigumu sana kwa mtu wa kuja kutengeneza opportunites kama hizo kirahisi kama akienda Japan, German hata Urusi au nchi tajiri za Kiarabu!
Kuna nchi kama Japan sidhani hata zinatoa uraia na kuwa Mjapan hata ukifuata taratibu zote! Utapayta vibali tu! Marekani haikupi Kibali tu, inakupa uwezo wa kukufanya raia na kuwa na haki sawa na mzawa wa hapa!

Masdinero namalizia kwa mfano binafsi, nimeingia Marekani na watoto watatu, simjui mtu serikalini wala popote pale, wanangu wamemaliza degree zao pasipo kutoa senti yangu mfukoni, mmojawapo kapata kazi kwenye taasisi kubwa ya fedha kama Internal auditor na weusi wake kama mpingo pasipo kuhonga! wala kuwa na connection na mtu yoyote! Je unataka nisemeje kuhusu Marekani? Mimi ni mfano tu wa baadhi ya watu ambayo tunaamini nchi hii ukifuata taratibu bado ina oppotunites kwa mtu wa kuja asiwe mzawa tofauti na nchi nyingine nyingi.
 
Masdinero,

Hii ni idadi ya watu walioomba uraia 2021

How many new citizens were there in 2021?

855,000 new

Promoting Naturalization: During FY 2021, USCIS welcomed 855,000 new U.S. citizens, including derivative citizens.Dec 16, 2021.
 
Umepishana na pointi zangu kabisa. Sikutoa tamko kwamba US ni ya mwisho duniani! Hoja yangu kuu ni kwamba sio namba 1 kama unaweza kuchagua sehemu ingine. Maendeleo sio fursa za kiuchumi tu! Pia mstari wa masharti uko chini kuingia US ukilingajisha na nchi zingne. Kiufupi US inapenda immigrants, au niseme tabaka la juu-the 1%-kwa manufaa ya kunyonya nguvu kazi. Ukiachilia vitega uchumi vidogo vya mitaani wengi wanaohamia huishia kutumika tu! Hakuna pepo duniani, kuna nchi ni pepo ukilinganisha na US. Mfano NewZealand, Iceland, Ukanda wa Scandinavia.

Hata jamii ya US inashida nyingi. Kuna majimbo yanaingilia mpaka uhuru binafsi wa mtu mmojammoja(hapa kuna hoja nyingi sina stamina ya kutype nisamehe tu), achilia mbali shida za usalama(hasa gun and knife violence), huduma mbovu na ghali za afya, ubaguzi... kama unauwezo wa kwenda kwingne dunian badala ya US ni bora! Kama huwezi tulia pambana na hali yako ulipo.
 
Nchi zenye maendeleo ya hasa huwezi kwenda kirahisi kama US... pitia immigration agencies za nchi zilizozendelea zaidi ya US utaona. Hizo namba zipe context. Hali ya US kwa ukubwa na uhitaji wa wahamiaji wa kwenda kuhenya ni tofauti na nchi kama Finland! Dadavua taarifa usichukue wingi wa watu kama ni kwamba US ni nzuri... kwa wengi ni kimbilio la unafuu kutoka huko watokako. Mfano raia weng wa Mexico wanavuka boda kila siku kuja kulima, ishu ni uchumi. Wachina wanahamia kusoma, kukimbia ukandamizaji, kufungua matawi ya kampuni za kichina n.k. nao ishu ni uchumi, warusi wanakimbia ubanaji wa govt huko kwao, el salvador, guatemala, waafrika wanakimbia vita, njaa, siasa na shida makwao.. wap rahisi kuingia na kupata fursa(za kuhenya)? US.... kuna watu wanafanya kazi kwenye depot za Amazon wanakamuliwa mzigp hadi wanakosa muda kukojoa wanajisaidia kwenye makopo, US ni pazuri kama una shida zako njoo... unyonyaji na shida ambazo kuna nchi zaidi ya 30 zilizoendelea hutosikia! Ni vile trade unions zinapigwa vita huku shida hazipati airtime. Utu hamna huku! Unless kwenye sekta fulani chache keki ya raha US utaiona kwenye matangazo tu!

Chukua hizo namba za idadi ya watu jiulize sababu zaidi ni mvuto wa US au ni msukumo wa huko watokako.
 
Masdinero: Hivi majuzi nimehudhuria sherehe kama mbili za watu ambaao wanaapishwa kuwa raia wa Marekani, ofisi zilifunguliwa saa moja asubuhi hadi saa kumi na mbili jioni, Huo umati ambao niliuona kutoka mataifa mbali mbali ulinishangaza, kama maendeleo na uchumi wa marekanii ambao umeuita ziro sidhani ingekuwa hivyo! Niliona Waarabu, Wachina, Scandanavians, Filipino, Japanese, Cuba nk. Kwa kifupi waaafrika walikua ni wachache mno!

Nilijiuliza maswali hayo hayo, Kama US ni mbaya, hali ya usalama binafi haipo, ni nini hasa kinachofanya au kinachovuta watu kuja au kukimbilia katika katika nchi hii! Kwa nini hata wailio na uweza duniani wanataka kuwekeza Marekani! Karibu gas stations nyingi hapa Texas nilipo ni mali ya wahindi! Hoteli za hali ya kati pia! Nimeshangaa kusoma leo hao matajiri wa Kirusi kama kina Roman Abramovic na wengine wanavyomiliki mali Marekani! Kama maendeleo ya US yangekua ziro kama unavyosema wewe, jamaa hawa wengewekeza US ? Je Wao ni wapumbavu!

Kwa kifupi Masdinero, Marekani ina mapungufu mengi kama mataifa mengine lakin ni nchi ambayo bado inatoa opportunities kwa mtu wa KUJA asiwe mzawa wa hapa kufanikiwa kimaisha kuliko nchi nyingi zilizoendelea, huo ndio ukweli, ni vigumu sana kwa mtu wa kuja kutengeneza opportunites kama hizo kirahisi kama akienda Japan, German hata Urusi au nchi tajiri za Kiarabu!
Kuna nchi kama Japan sidhani hata zinatoa uraia na kuwa Mjapan hata ukifuata taratibu zote! Utapayta vibali tu! Marekani haikupi Kibali tu, inakupa uwezo wa kukufanya raia na kuwa na haki sawa na mzawa wa hapa!

Masdinero namalizia kwa mfano binafsi, nimeingia Marekani na watoto watatu, simjui mtu serikalini wala popote pale, wanangu wamemaliza degree zao pasipo kutoa senti yangu mfukoni, mmojawapo kapata kazi kwenye taasisi kubwa ya fedha kama Internal auditor na weusi wake kama mpingo pasipo kuhonga! wala kuwa na connection na mtu yoyote! Je unataka nisemeje kuhusu Marekani? Mimi ni mfano tu wa baadhi ya watu ambayo tunaamini nchi hii ukifuata taratibu bado ina oppotunites kwa mtu wa kuja asiwe mzawa tofauti na nchi nyingine nyingi.
Boss samahani una umri gani kwa sasa na umeingia USA 12 years ago ukiwa na umri gani ?

Sent from my SM-J610F using JamiiForums mobile app
 
Anayekupenda kwa dhati.. mtazaa watoto mapema. then gharama za kulea ni kubwa sana. Investments tanzania zinashindwa. Hio ndio nimeona kwa immigrants wengi.
Hakuna namna ya kutokuzaa nae kama hutaki upate mtoto ili kukimbia hayo matatizo ya gharama mfano kupigia nje[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] au njia yoyote tu ili usimkasirishe manzi ikawa shida zaidi?
 
Boss samahani una umri gani kwa sasa na umeingia USA 12 years ago ukiwa na umri gani ?

Sent from my SM-J610F using JamiiForums mobile app
Fentfold: Nimeingia mtu mzima kabisa na watoto teenagers, Kitu ambacho sishauri kabisa kwa mtu yoyote kufanya, ukiingia Marekani ukiwa kijana una flexibility nyingi mno kuliko umri ukiwa umekwenda.Sikuuingia actually kutafuta maisha, tayari maisha nilikuwa nimeisha yajenga Tanzania na kuwa na vitu vya msingi tayari.Nilikuja kusoma na kuwapa watoto wangu mwelekeo mwingine wa maisha plus adventure, na kupata Green Card kirahisi kulinichochea kupiga kambi Marekani.

Bado nashauri sana kuja ukiwa kijana una flexbility kubwa mno wa kukipata unacho kitafuta kwa urahisi, faida ya umri mkubwa na kama nyumba una chochote, na maana biashara na funds, ukikwama Marekani unaweza kutumia funds zako za huko kukusaidia Marekani tofauti na ukiwa kijana kama hauna familia yenye uwezo nyumbani kukupa push ya aina yoyote.
 
Fentfod: Labda kwa kuongezea tu, hasa kwa wale wanaotaka kuja US ni kujiuliza unataka kuja kufanya nini? Je milango ya kufanikiwa nyumbani imefungwa? Kama kweli imefungwa Marekani inaweza kabisa kukusaidia ukiwa na vibali, lakini kama ni kula bata kama wengi wanavyoona kwenye movies utapotea!

Kwangu mimi nashauri njia rahisi ya kuanzia kuja huku ni kutafuta chuo, huo ni mlango rahisi hata kabla ya kuanza kuitafuta Greencard, na mengi yatafuata.Ningependa sana vijana waliokata tamaa na kuona milango imefungwa nyumbani kujaribu nje ya nchi! Nimeona sana kwa Nigerians na Kenyans, na lengo lao sasa hivi si kuishi hasa US, ni kuitumia kama ngazi tu ya kutimiza malengo yao! Nilisoma article mahali fulani kuwa Marekani ya sasa hivi si mahali pa kuishi, bali ni kuitumia kama ngazi tu ya kufikisha ndoto zako ulikotoka.Wachina wanafanya hivo sana, Waraabu pia, maana best colleges Marekani bado Wachina na waarabu ndio wengi.

Lakini pia kwangu mimi Marekani bado ina offer maisha ya kila aina wewe mwenyewe unayoyatafuta! Ukitaka kukaa shamba au vijijini kwenye utulivu unaweza! Hata kufuga mbuzi na na kupanda mchicha kujilisha! Inategemea wewe mwenyewe unataka maisha ya namna gani.Achana na media ambayo zinatoa biased news kwa nchi yoyote ile, ambayo hata Marekani imekuwa biased kwa wengi kutokana na media hizo. Unaweza kudhani Marekani ni nchi imejaa wasenge na mashoga tu, si kweli! Unaweza kudhani Marekani imejaa ubaguzi, kila mweusi anakandamizwa au ni shida sana ukiwa black, si kweli! Unaweza kudhani Marekani haina watu wenye imani za dini na nidhamu ya maisha, si kweli kabisa, bado kuna Makanisa na misikiti inajaa watu! Nakaa nje mji mkubwa, ambako ni predominantly whites, juzi nimeona Msikiti umeanzishwa, na napopita hapo Ijumaa naona Ibada zinafanyika. Bado naheshimu sana uhuru ambao katika ya Marekani imewapa watu wake! ndio una mapungufu lakini bado kuna uhuru wa aina ya maisha ambayo wewe binafsi unayatafuta.
 
Umepishana na pointi zangu kabisa. Sikutoa tamko kwamba US ni ya mwisho duniani! Hoja yangu kuu ni kwamba sio namba 1 kama unaweza kuchagua sehemu ingine. Maendeleo sio fursa za kiuchumi tu! Pia mstari wa masharti uko chini kuingia US ukilingajisha na nchi zingne. Kiufupi US inapenda immigrants, au niseme tabaka la juu-the 1%-kwa manufaa ya kunyonya nguvu kazi. Ukiachilia vitega uchumi vidogo vya mitaani wengi wanaohamia huishia kutumika tu! Hakuna pepo duniani, kuna nchi ni pepo ukilinganisha na US. Mfano NewZealand, Iceland, Ukanda wa Scandinavia.

Hata jamii ya US inashida nyingi. Kuna majimbo yanaingilia mpaka uhuru binafsi wa mtu mmojammoja(hapa kuna hoja nyingi sina stamina ya kutype nisamehe tu), achilia mbali shida za usalama(hasa gun and knife violence), huduma mbovu na ghali za afya, ubaguzi... kama unauwezo wa kwenda kwingne dunian badala ya US ni bora! Kama huwezi tulia pambana na hali yako ulipo.
Labda sikukuelewa jamaa yangu, na pia kwa lugha uliyotumia! Kwanza Hakuna jamii isiyo na shida ulimwenguni! Kitabu cha dini ya Kikristo kinasema katika aya fulani, maskini mnao siku zote ulimwenguni! Ndio maana hata sera za Ujamaa zenye kutaka kuondoa Umaskini kwa huwa zinashindwa! Marekani inaweza kuwa na 1% inayomiliki uchumi, Je nchi nyingine huwa na nini? Ni jamii gani isiyo na tabaka la Juu! Umeeleeza ju ya Scandnavia countries, nadhani uko informed juu ya mabadiliko mengi kuhusu wageni katika nchi hizo, Scandnavia countries za miaka ya nyuma kuingia, kupata kazi na maisha hata kwa wakimbizi tu si rahisi tena! Hapa tunazumgumzia mtu wa KUJA anayetafuta maisha ugenini! Jinsi ya kuingia na kupata au kutengeza maisha yake ukilinganisha na alikotoka! Sidhani kama tunalinganisha quality of life! Hicho ni kitu kingine kabisa.

Umeeleza mambo mengi yenye negative kama shida za usalama, niko Marekani na Marekani ni kubwa sana, hivyo unapozungumizia violence uwe makini sana, sio kama unavyoona kwenye Media! Labda hofu yangu ya maisha Marekani niliyopo ni kufa kwa ajali barabarani sio risasi! Maana licha ya bararabara kuwa kubwa tunaendesha kwa kasi sana hasa huku Texas! Siogopi hata kidogo kupoteza maisha kwa bunduki!

Kuhusu ubaguzi, nayo pia unahitaji kuwa naungalifu, Nimekamatwa sio mara moja na polisi kwa kuvunja sheria za barabarani, sikubaguliwa, sikuonewa na wala kudhalilishwa! Nilionyeshwa makosa yangu na kuambiwa nilipe faini! Actually nimewahi kukamatwa nikiwa na arrest warrant, yaani kesi yangi imesomwa Mahakamani sikutokea, kwa makosa ya barabarani, Polisi mweupe aliniambia kwa nini nisilipe faini kuliko kunipeleka Jela! Nilifanya hivyo mambo yakaisha! Watoto wangu ni vijana, wanatoka usiku, wanaenda viwanja hawajawahi hata kidogo kusimamishwa na polisi sababu n iweusi! Sio kwamba wana bahati, bali wanafuata sheria! Ni vigumu kwa mtazamo wangu Polisi kukuamkia tu mahali kwa sababu ni mweusi, inategemea wapi au maeneo gani! Na kipi hasa kimemfanya Polisi akufuate wewe! Hiyo knife violence mkuu ipo kila mahali!
Kuhusu bima za Afya nakubali ni ghali ukilinganishwa na nchi nyingine, napenda kutumia mfano wangu, mimi ni kama mtu kawaida, I dont think I'm really middle class American, napiga kazi Kiwandani, nina Medical Insurance mbili ya Kawaida na meno, nalipa roughly $400 kwa mwezi, napata matibabu mazuri na pia Kiwanda nachopiga mzigo naweza kwenda wakati wowote kupata matinabu kwa $40 kwa mwezi. Sasa unataka niseme Huduma za Afya Mbovu? Unalinganisha na wapi hasa? Hasa kwa mimi mtu wa KUJA toka bongo!
Nasema tena Marekani sio Paradiso, kila Nchi ina upper class! kumbuka hiyo 1% unayoizungumza hai control Marekani peke yake, ina control ulimwenguni kote, hata wewe uliko pengine kwa sehemu inakukaba pasipo kujitambua!

Hivyo kama Scandanavia, New Zealand ni rahisi kuishi, wasaidie vijana wa kibongo watafute fursa huko! Kwangu Marekani from my own practical experience ni rahisi kuingia na ku establish maisha kuliko hizo sehemu ulizo zitaja.
 
Masdnero,

Naishi Texas , sijwahi kukoswa na risasi, wa kutishiwa tu na Bunduki, Texas ina uhuru mno wa kumiliki silaha! Bali sheria zake ni kali sana kwa muuaji wa aina yoyote ile! Hali sio ya kutisha kama Media zinazosema!

Gun Ownership in Texas
In 2019, it is estimated that at least 36% of Texans own guns and there are more than 29 million guns owned in Texas. 725,368 guns are registered in Texas, the most of any state and 67% more registered guns than second-place Flor
ida.

Hivyo huko Tanzania kila Albino yuko mashakani kuuawa ?! Jibu ni Hapana, lakini ukisoma media hata huku naulizwa nchi yenu ndio inayoua Albino? Media inatoa picha tofauti kabisa na hali halisi! Marekani ina guns violence, lakini ukubwa wa nchi na mahali zinapotokea na wingi wa Bunduki mikononi mwa watu, hilo sio tatizo katika maisha ya kawaida.

Huwa nafikiria Tanzania, kama tu 36% ya Watanzania wengekuwa na bunduki, nini kingetokea!
 
Masdinero: Hivi majuzi nimehudhuria sherehe kama mbili za watu ambaao wanaapishwa kuwa raia wa Marekani, ofisi zilifunguliwa saa moja asubuhi hadi saa kumi na mbili jioni, Huo umati ambao niliuona kutoka mataifa mbali mbali ulinishangaza, kama maendeleo na uchumi wa marekanii ambao umeuita ziro sidhani ingekuwa hivyo! Niliona Waarabu, Wachina, Scandanavians, Filipino, Japanese, Cuba nk. Kwa kifupi waaafrika walikua ni wachache mno!

Nilijiuliza maswali hayo hayo, Kama US ni mbaya, hali ya usalama binafi haipo, ni nini hasa kinachofanya au kinachovuta watu kuja au kukimbilia katika katika nchi hii! Kwa nini hata wailio na uweza duniani wanataka kuwekeza Marekani! Karibu gas stations nyingi hapa Texas nilipo ni mali ya wahindi! Hoteli za hali ya kati pia! Nimeshangaa kusoma leo hao matajiri wa Kirusi kama kina Roman Abramovic na wengine wanavyomiliki mali Marekani! Kama maendeleo ya US yangekua ziro kama unavyosema wewe, jamaa hawa wengewekeza US ? Je Wao ni wapumbavu!

Kwa kifupi Masdinero, Marekani ina mapungufu mengi kama mataifa mengine lakin ni nchi ambayo bado inatoa opportunities kwa mtu wa KUJA asiwe mzawa wa hapa kufanikiwa kimaisha kuliko nchi nyingi zilizoendelea, huo ndio ukweli, ni vigumu sana kwa mtu wa kuja kutengeneza opportunites kama hizo kirahisi kama akienda Japan, German hata Urusi au nchi tajiri za Kiarabu!
Kuna nchi kama Japan sidhani hata zinatoa uraia na kuwa Mjapan hata ukifuata taratibu zote! Utapayta vibali tu! Marekani haikupi Kibali tu, inakupa uwezo wa kukufanya raia na kuwa na haki sawa na mzawa wa hapa!

Masdinero namalizia kwa mfano binafsi, nimeingia Marekani na watoto watatu, simjui mtu serikalini wala popote pale, wanangu wamemaliza degree zao pasipo kutoa senti yangu mfukoni, mmojawapo kapata kazi kwenye taasisi kubwa ya fedha kama Internal auditor na weusi wake kama mpingo pasipo kuhonga! wala kuwa na connection na mtu yoyote! Je unataka nisemeje kuhusu Marekani? Mimi ni mfano tu wa baadhi ya watu ambayo tunaamini nchi hii ukifuata taratibu bado ina oppotunites kwa mtu wa kuja asiwe mzawa tofauti na nchi nyingine nyingi.
Hongera bro umeandika vzr na nimekuelewa sana!inspiring hawaangalia una nani Bali una nini!!afadhali wenzetu wameweza

Sent from my Infinix X559C using JamiiForums mobile app
 
penye nia pana njia..
Wapo walioenda hawana elimu na sasa wamepiga kazi vya kutosha now wanamiliki gyms / local shops etc.

Na hizo Degree kwa karne ya sasa au Generation ya sasa huko U.S hazimati sana fanya uchunguzi utajua..
Huko huko U.S wapo wazungu unakuta mtu ana Degree ya mambo fulani .. lakin ameachana nazo anapiga kazi za photography au film maker
Ni kweli mkuu
 
Masdinero: Hivi majuzi nimehudhuria sherehe kama mbili za watu ambaao wanaapishwa kuwa raia wa Marekani, ofisi zilifunguliwa saa moja asubuhi hadi saa kumi na mbili jioni, Huo umati ambao niliuona kutoka mataifa mbali mbali ulinishangaza, kama maendeleo na uchumi wa marekanii ambao umeuita ziro sidhani ingekuwa hivyo! Niliona Waarabu, Wachina, Scandanavians, Filipino, Japanese, Cuba nk. Kwa kifupi waaafrika walikua ni wachache mno!

Nilijiuliza maswali hayo hayo, Kama US ni mbaya, hali ya usalama binafi haipo, ni nini hasa kinachofanya au kinachovuta watu kuja au kukimbilia katika katika nchi hii! Kwa nini hata wailio na uweza duniani wanataka kuwekeza Marekani! Karibu gas stations nyingi hapa Texas nilipo ni mali ya wahindi! Hoteli za hali ya kati pia! Nimeshangaa kusoma leo hao matajiri wa Kirusi kama kina Roman Abramovic na wengine wanavyomiliki mali Marekani! Kama maendeleo ya US yangekua ziro kama unavyosema wewe, jamaa hawa wengewekeza US ? Je Wao ni wapumbavu!

Kwa kifupi Masdinero, Marekani ina mapungufu mengi kama mataifa mengine lakin ni nchi ambayo bado inatoa opportunities kwa mtu wa KUJA asiwe mzawa wa hapa kufanikiwa kimaisha kuliko nchi nyingi zilizoendelea, huo ndio ukweli, ni vigumu sana kwa mtu wa kuja kutengeneza opportunites kama hizo kirahisi kama akienda Japan, German hata Urusi au nchi tajiri za Kiarabu!
Kuna nchi kama Japan sidhani hata zinatoa uraia na kuwa Mjapan hata ukifuata taratibu zote! Utapayta vibali tu! Marekani haikupi Kibali tu, inakupa uwezo wa kukufanya raia na kuwa na haki sawa na mzawa wa hapa!

Masdinero namalizia kwa mfano binafsi, nimeingia Marekani na watoto watatu, simjui mtu serikalini wala popote pale, wanangu wamemaliza degree zao pasipo kutoa senti yangu mfukoni, mmojawapo kapata kazi kwenye taasisi kubwa ya fedha kama Internal auditor na weusi wake kama mpingo pasipo kuhonga! wala kuwa na connection na mtu yoyote! Je unataka nisemeje kuhusu Marekani? Mimi ni mfano tu wa baadhi ya watu ambayo tunaamini nchi hii ukifuata taratibu bado ina oppotunites kwa mtu wa kuja asiwe mzawa tofauti na nchi nyingine nyingi.
Umenena vema

Mueleze kuhusu mtu kama Arnold Schwarzenegger. Kaja marekani ukubwani mpaka kawa governor wa state kubwa kama California halafu mtu anakuja kusema Marekani ni nchi ya hovyo?

Kuna kitabu kinaitwa "Out of Many, One" kimeandikwa na George w Bush. Humo ukisoma stori za watu waliotokea mataifa mengine wakiwa ni wa kudharauliwa walivyopokelewa vizuri marekani na kuja kufanikiwa maishani unaweza kulia
 
Back
Top Bottom