Ukitaka kwenda kuishi Marekani inabidi ujipange

Ukitaka kwenda kuishi Marekani inabidi ujipange

Wanaija wana miaka kadha hawaruhusiwi kucheza, sababu ya idadi yao kwa kipindi cha miaka kadhaa mfululizo ilizidi ile asilimia inayotakiwa , so waliswastopisha, maybe kuanzia mwakani wanaweza ruhusiwa kucheza tena baada ya muda mrefu..

Walifanya hivyo ili na watu wa mataifa mengine wapate chance na ndio maana zikaitwa diversity .

Yes wabongo wengi hawana taaarifa..

Wengne ni zile mentality za umasikini jeuri "bongo ndio kila kitu"
Mkuu nipe tips muhimu ambazo zinaweza kunifanya nkashinda hii lottery ..Tafadhali
 
Mkuu umesema mademu wa hapo Atlanta wanataka $$$ na sio longolongo kwahiyo ulifanyafanyaje kuhusu sex halafu huo ugumu wa maisha ndio chanzo cha kuwa na mashoga wengi huko US au kuna sababu nyingine
 
Miaka flani Niko bongo sielewi mambo hayaeleweki, nina sista angu yuko U.S nkaongea nae kuhusu mi kwenda Marekani kujaribu maisha anakubali, mipango inakamilika kijana nkatua Jackson heartsfield Atlanta lengo kubwa la kwenda Marekani ni kupata exposure na kutafuta maisha.

Harakati zinazofuata ni mim kutafuta kazi, Marekani kazi zipo Ila sasa kule ukisikia kazin kazini kweli full supervision unafanya kazi masaa 10 mpaka 12 hiyo ni uongeze kipato ukizingatia kazi zenyenyewe unalipwa kwa masaa, kwa hiyo lazima ukomaee Ila kazi tu zipo, baada ya mda kudunduliza ela nahama kwenye basement nikahamia kwenye chumba kimoja sehemu moja hivi inaitwa sandy springs.

Tatizo la Marekani maisha expensive kipato cha kawaida ukizingatia nilienda kama mtu wa Kawaida, kila kitu ni ela yaan ukisikia capitalism kule ndo inakua practice [emoji817] swala la kuwa na depression, loneliness ni moja ya vitu lazima ukumbane navyo usipokua makini lazima uingie kwenye matumizi ya madawa ya kulevya.

Ukikaa Marekani kitu unachoombea kila siku ni usiumwe sababu ni balaa, kuhusu starehe nayo pia ni mtihan kwa mtu mwenye kipato cha kawaida, wanawake wengi wa Atlanta ni materials things inabidi kuwapata ni gharama wako after money.

Kwa sasa hivi nilisharudi tz sababu za kifamili, na maisha ya marekani ili yakuendee vizuri uwe na professional means at least umesomea master kule kama hujasoma bachelor kwenye fani za science, au unakipaji kitu ambacho kwa watanzania wengi mpaka wanakua hawajui vipaji vyao, kwenda marekani hivi hivi ni kugumu sana kwa sababu kwa maisha utajikuta unapata ela ya kawaida alafu unaishi kwa mawazo sana in short unataka kwenda marekani kutafuta maisha jipange na uwe mtu wa kujiongeza sana, na uwe competent hivi hivi sikushauri hata kidogo.

California, new York, Illinois, Massachusetts, na Washington state hayo ni majimbo ya kuyaepuka Kodi na gharama za maisha ziko juu. Ila Texas, Florida, Georgia, na north Carolina haya majimbo maisha yako cheap.

Vitu nilivuomiss marekani ni exposure Ila mwaka huu ntarudi nikiwa nimejipanga zaidi, kunakikampuni ntaenda kukifungua deleware kama domestic company, alafu baadae Virginia na Texas kama foreign company.
Oyaa, kama mimi ni dereva wa mashirika naweza kutimba USA? [emoji20]
 
Mkuu nipe tips muhimu ambazo zinaweza kunifanya nkashinda hii lottery ..Tafadhali
Kila mwaka October, application zinaanza, ni free kuapply .

Mambo yakuzingatia wakati unajaza form..

*Usikosee PASSPORT number yako...

*Marital status - usiongope/ toa taarifa ambazo hazitaleta mkanganyiko baadae..

*Number of children: ukijaza huna ,ikagundulika unao /au baada ya kuwa selected ndio udai ooh nilisahau kujaza... utanyimwa visa
 
Wachaga wa aina gani hao, maana kijijini kwetu kwetu walioenda kule wametoboa sana kimaisha na wanaendeleza kijiji kama vile kusaidia ujenzi wa shule, hosp.
Watoto shule nk.
Sasa hao ndugu zako ni wachaga wa aina gani?
Yaani hpo shida ni yeye kukutajia kabila, angekutajia kabila jingine ungekuja na ngonjera tofauti

Sent from my SM-A013G using JamiiForums mobile app
 
Oyaa, kama mimi ni dereva wa mashirika naweza kutimba USA? [emoji20]
Kama hilo shirika lipo Canada , hii itakuwa fursa kwako .. kwani sasa hivi ili kujaza uhaba wa wafanyakazi ...
Canada wameanzisha hizpo program za kutransfer watu , mfano kutoka kampuni ya tz kwenda kampuni ya Canada ..as long as hiyo kampuni inuahitaji wa position unayoiomba
 
Huo uandishi tu kwanza!! Unajua kabisa hii njemba ni ya hapo ulongoni hapo,akienda mbali sana kariakoo
Ndoano imerushwa mkuu, kuna mtu atapigwa hapa hapa kabla jogoo hajawika mara tatu!
 
Wafanyakazi wa McDonalds na Walmart wamepata fursa kujisifu wanaishi Marekani.

Wanaume wazima wameamua kusomea unesi maana kila kona wamebanwa hawapati kazi. Their feminine side ultimately takes control of their lives out of a sheer desperation to survive in a iredeemiably racist, capitalist society.

Hao wanaume wangekuwa TZ wasingefikiria hiyo kazi ya kike hata siku moko.

Dume zima anajisifia yeye registered nurse?!!
 
Kuna ndugu zangu mtu na Dada yeke walifight sana wakenda state baada ya kumaliza A level Miaka ya 90, mpaka leo hawajatoboa Dada mtu alipata tatizo la akili kwasababu ya sonoma , wakamrudisha TZ mpaka leo hayupo sawa, Kaka mtu alishindwa kurudi kwenye msiba wa mama yake kwa wakati ila yeye aliamua kuoa Mke wa Kizungu

Ndugu yangu nwingine alienda Uingereza yeye aliambulia kurudi na tv kubwa sana sijui nchi 80 ile, na kuwa mraibu wa ulevi
Lucky and Risk are siblings
 
Bora niendelee kukaa hapahapa Nanjilinji kuliko kwenda mbele kubeba box afu hata ganji ya kunywea balimi sina
Majuu, namaanisha Marekani, Canada, Ulaya Magharibi na nchi za Asia zilizoendelea kama Japan na South Korea maisha ni kama yako sawa. Ukiwa kule kama unafanya kazi ya masaa nane kwa siku huwezi kushindwa kula vizuri, kuvaa vizuri na kusafiri. Kwa ujumla utaishi maisha ya standard nzuri tu kuliko Tanzania. Tatizo linakuwa ni kwamba mtanzania anataka akiwa majuu aishi maisha mazuri huku akikidhi mahitaji mengine ya Bongo kama kusaidia ndugu, kujenga, kufungua biashara na ku-save fedha ya kuendeleza maisha atakaporudi mazima. Hapo ni lazima utaona maisha magumu. Unakuta wengine tena wana zile mind-set za kibongo bongo za kufanya kazi kidogo na kutumia sana...
 
Wafanyakazi wa McDonalds na Walmart wamepata fursa kujisifu wanaishi Marekani.

Wanaume wazima wameamua kusomea unesi maana kila kona wamebanwa hawapati kazi. Their feminine side ultimately takes control of their lives out of a sheer desperation to survive in a iredeemiably racist, capitalist society.

Hao wanaume wangekuwa TZ wasingefikiria hiyo kazi ya kike hata siku moko.

Dume zima anajisifia yeye registered nurse?!!
Du bado una mawazo ya kizamani namna hii? U-nurse una tatizo gani kwa mwanaume? Hao wote analipwa vizuri na wangekaa Tanzania wangekuwa na maisha mabaya sana.
 
Wafanyakazi wa McDonalds na Walmart wamepata fursa kujisifu wanaishi Marekani.

Wanaume wazima wameamua kusomea unesi maana kila kona wamebanwa hawapati kazi. Their feminine side ultimately takes control of their lives out of a sheer desperation to survive in a iredeemiably racist, capitalist society.

Hao wanaume wangekuwa TZ wasingefikiria hiyo kazi ya kike hata siku moko.

Dume zima anajisifia yeye registered nurse?!!
Pamoja na hayo,
Hela anayopata hata mbunge wako hawezi pata
 
Nchi zilizoendelea si mchezo hakuna hela ya pembeni kila kitu kimenyooka...dawa ni kupunguz matumizi tuu sio kama bongo utampiga mzinga mtu? Au utapiga udalali sehemu...
Nakubaliana na wewe. Kinachofanya wabongo wengi walalamikie maisha ya majuu ni yale mazoea ya kuishi kwa ujanja ujanja. Ngoja nikupe mfano. Le Mutuz aliishi USA karibia miaka 30 lakini alishindwa kufanya kitu chochote cha maana, lakini baada ya kurudi Bongo eti na yeye ni ma-super stars wenye maisha mazuri. Ukiambiwa uelezee anafanya kazi gani Bongo unaijua? Jibu ni kuishi kwa ujanja ujanja. Majuu ni kuwa hakuna short-cut na kila mtu anakula kuendana na jasho lake. Siyo Bongo unaweza kuingia kuishi kwa ujanja ujanja kama kina Steve Nyerere.
 
Du bado una mawazo ya kizamani namna hii? U-nurse una tatizo gani kwa mwanaume? Hao wote analipwa vizuri na wangekaa Tanzania wangekuwa na maisha mabaya sana.
Acha hizo. Fikiria motivation za Wanaume wa kiafrika kuukumbatia unesi Marekani. Ni kwa vile wanabaguliwa kwenye kazi nyingine ambazo Wanaume wa Kimarekani wametawala. Wanaenda kushindana na Wanawake.
 
Back
Top Bottom