SoC02 Ukaidi wa sheria kutoka kwa madereva na wamiliki vyombo vya usafiri maarufu kama bodaboda

Stories of Change - 2022 Competition

0743919950

Member
Sep 20, 2021
7
0
Katika nyakati hizi tofauti na nyakati za nyuma kidogo, dunia imejaliwa kufanya gunduzi mbalimbali za sayansi na tekinolojia ikiwemo gunduzi bora kabisa za vyombo mbalimbali vya usafiri ikiwemo pikipiki. Vivyo hivyo kwa Tanzania usafiri huu wa pikipiki maarufu kama boda boda umeleta ufanisi mkubwa kwa wakazi wengi katika shughuli zao za kila siku ikiwemo za kiuchumi, kijamii na kisiasa.

Na pia mwanzoni usafiri wa aina hii ulikithiri sana maeneo ya mjini lakini kwa sasa usafiri wa aina hii umefika mpaka maeneo ya ndani kabisa ya Nchi ikiwemo vijijini nahii imetokana na muingiliano mkubwa wa watu, maendeleo ya upatikanaji wa habari lakini pia uboreshwaji wa miundo mbinu mpaka maeneo ya vijijini au pembezoni mwa Tanzania.

Kinyume na matarajio ya wengi juu ya ujio wa usafiri huu, usafiri huu umeleta madhara makubwa sana kama vile vifo, ulemavu wa kudumu na usio wa kudumu, idadi kubwa ya wategemezi ikiwemo mayatima na upungufu wa nguvu kazi ya taifa kutokana na wamiliki wake ikiwemo madereva kukaidi sheria za barabarani ikiwemo pia kuendesha kihorela katika mitaa mbalimbali.Na tatizo hili limetawala sana maeneo ya vijijini ambapo madereva na wamiliki wengi hawana ujuzi na elimu ya kutosha kuhusiana na umiliki wa vyombo hivyo.Lakini sio tu elimu ya kutosha wengine elimu wanazo lakini wanakaidi kuzitumia elimu hizo katika kuvisimamia na kuvitumia vyombo hivyo.

Kuhusiana na wamiliki kutokuwa na elimu ya kutosha swala hili linaweza kuelezewa katika maeneo kadhaa ikiwemo swala la kutovifanyia usajiri wa kisheria vyombo vyao na hivyo kuikosesha serikali kukusanya mapato yake stahiki, lakini pia kutokufanya makubariano ya kisheria na wale ambao huwaachia vyombo hivyo kwa ajiri ya kuvifanyia biashara na lingine kubwa kuliko ni kutochunguza sifa na viwango vya madereva hao ikiwemo swala la mfunzo ya kuendesha vyombo vya moto.Hivyo basi wadau wanaomiliki vyombo hivi vya usafiri maarufu kama boda wanaaswa kuvifanyia usajiri vyombo hivyo ili viweze kutambulika kisheria hasa maeneo ya vijijini, pili kwa wale wamiliki wanao wapa wafanyakazi wao vyombo hivyo vya usafiri wawe makini katika kuchunguza viwango vyao vya mafunzo pamoja na tabia zao.

Kuhusiana na waendeshiji wa vyombo hivi vya usafiri maarufu kama boda, wanapaswa kuzingatia sheria zote za usalama barabarani ikiwemo kuendesha vyombo vyao kwa mwendo uliowekwa kisheria au chini ya hapo na sio Zaidi, kuheshimu njia za watembea kwa miguu pembezoni mwa barabara, kuheshimu vivuko maalumu vya waenda kwa miguu maarufu kama zebra na pia kupitia mafunzo maarumu ya kuendesha vyombo hivyo na hivyo kujipatia lesseni maarumu kwaajili ya kazi hiyo.

Lakini hiyo imekaidiwa na madereva walio wengi wa vyombo hivyo ambao wanafanya kazi hiyo bila kibali maarumu hasa maeneo ya vijijini.Kwa wale ambao wamekaa vivjijini kwa muda mrefu ni dhahiri wataungana na mimi kwamba kutokana na upungufu wa vyombo vya usalama, elimu isiyo ya kutosha na sababu nyingine nyingi kila kukicha ajari zimekuwa ni jambo la kawaida na sio stori tena.Na si hivyo tu madereva weni wamekua wakiacha njia kuu na kufuata njia za waenda kwa miguu na kuwasababishia madhara mbalimbali ikiwemo kuwatolea maneno machafu ya lugha ya matusi.

Katika kuhakikisha swala hili linakwenda vizuri na kwa mujibu wa sheria, Serikali ambacho ni chombo kinachosimamia sheria hizo kinapaswa kutunga sera maalumu kwaajiri ya uhamasishaji wa kutii sheria bila shuruti kwa madereva na wamiliki wa vyombo vya usafiri ikiwemo bodaboda, kutoa adhabu kali kwa watakao kaidi maagizo yake ikiwemo madereva na wamiliki wa vyombo hivyo na pia adhabu hizo kutambulika kisheria, na pia elimu ya kutosha kuhusu maswala ya usafirishaji na vyombo vya usafiri inapaswa kutolewa kwa wadauwa sekta hii nyeti Nchini.

Lakini pia katika kuhamasisha swala la kufuata sheria bila shuruti serikali inashauriwa kufanya makongamano mbalimbali yatakayoambatana na burudani mbalimbali kwaajili ya kuvutia watu wengi na hivyo kusambaza elimu kwa watu wengi juu ya suala la usalama barabarani.Lakini pia serikali inawajibika kuboresha alama za barabarani hasa maeneo ya vijijini ambapo ajari zimekuwa nyingi sana kwasababu ya uelewa mdogo wa wananchi na kutokuwepo kwa alama stahiki za barabarani.

Lakini pia serikali kwa nafasi yake inawajibiki kuzuia vitendo viovu ikiwemo rushwa kwa baadhi ya madereva na wasimamizi wengi wa sheria za barabarani wajulikanao kam “traffic”.Hivyo basi hatua za kisheria zinapaswa kuchukuliwa haraka sana inapotokea kuna dalili zozote za uwepo wa rushwa katika eneo husika ikihusisha maofisa wa sehemu hiyo pamoja na madereva.

Kwa wananchi wa kawaida, wanawajibika katika maswala tofauti ikiwemo kutoa taarifa za uvunjifu wa sheria kwa wakati katika vyombo vya ulinzi na usalama katika maeneo yao. Sio hivyo tu wananchi wanapaswa pia kuzingatia sheria za usalama barabarani ikiwemo kuheshimu taa za mwongozo, kuvuka barabara katika sehemu sahihi na tengefu.

Na sio hivyo tu raia wa kawaida wanatakiwa kufungua mashtaka dhidi ya vitendo vya kiharifu vya uvunjaji wa sheria za barabarani na kufwatilia mashauri yao mpka yanapokwisha na sio kukaa kimya na kuyafumbia macho na kuamalizia katika ngazi ya familia.

Watu wengi wamekua wakiwafumbia macho madereva wa pikipiki kutokana na kwamba wengi ni sehemu ya jamii yao na kusahau ya kwamba athari zinazotokana na kuficha uharifu huo ni nyingi na ni kubwa sana.

Namaliza kwa kutoa ombi kwa wadau wote wanaohusika kwa namna yoyote na usafiri wa aina hii, kuzingatia sheria za barabarani kama ilivyo ainishwa katika sheria zetu za nchi.Hii itasaidia kuleta maana halisi ya maendeleo ya sayansi na tekinolojia hasa katika swala hili la vyombo vya usafiri.

Na wadau lengwa hapa ni pamoja na wananchi, vyombo vya sheria, wamiliki na madereva wa pikipiki pamoja na serikali kwa ujumla, wahakikishe ya kwamba kila mmoja kwa sehemu yake anaokoa jamii yetu dhidi ya athari zisizo za lazima, zitokanazo na ajari mbalimbali za pikpiki maarufu kama bodaboda.
 
Back
Top Bottom