Ongezeko la BODABODA kujichukulia sheria mikononi vyombo vya usalama hamlioni hili?

Mr Nyau

JF-Expert Member
Oct 18, 2018
1,128
2,337
Ongezeko la BODABODA kujichukulia sheria mikononi vyombo vya usalama hamlioni hili?

Iwe kwenye mataa, taa ya rangi ya RED imewashwa bodaboda unawaona wanapita

Iwe kwenye pundamilia magari mengine yamesimama watu wapite bodaboda unawaona wanapita unaogopa kuvuka barabara hata kama magari yamesimama kuhofia bodaboda anaweza pita

- Majibu mabovu na matusi bodaboda

- utekaji na unyang'anyi wa vitu bodaboda

- Kuchoresha mipango yako kwa vibaka wa mji bodaboda

- Ajali nyingi barabarani mara nyingi bodaboda ni chanzo anaingia katikati kujipenyeza

- Ajali ikitokea wao ndio wa kwanza kushambulia huu ujasiri wa hadi kuchoma Bus unatoka wapi? Mambo huwa yanaanza mdogo mdogo ipo siku watavamia msafara wa kiongozi na kuchoma ipo hii tabia haivumiliki tunaongoza taifa la namna gani ? Ni Bangi au madawa ya kulevya ? Ulevi au kitu gani?

Bodaboda popote walipo wanazidi wafahamike wapimwe utimamu wa akili wapewe mafunzo ya usalama barabaranj wanaokizi vigezo waruhusiwe..


Askari na vyombo vingine vya usafiri mambo haya mmeyabariki?.. haya sio ya kupuuzwa.
 
'Ajari' ndo nini?

Mtu akiandika tu hivi naishia njiani kusoma maana kama kuandika tu tabu vipi anaweza kuleta habari yenye kueleweka?
 
Siyo bodaboda pekee; taifa letu lina watu wengi sana wenye matatizo ya akili.
 
'Ajari' ndo nini?

Mtu akiandika tu hivi naishia njiani kusoma maana kama kuandika tu tabu vipi anaweza kuleta habari yenye kueleweka?
Unaonekana una gubu sana,sometimes kuna age ukifika haya mambo ya spelling yanatokea na sio kwamba hafaham,ila kichwa kikiwa na mambo meng ni vigumu kuconcetrate
 
CCM ilishatangaza Bodaboda ni "kundi maalumu" hivyo hawatakiwi kusemwasemwa kwa lolote wanalofanya
 
Siyo kwamba nadharau kazi ya bodaboda hapana.Kwanza kundi hili kama lingekuwa halijajiajiri kufanya kazi hii mitaani sijuwi hali ingekuwaje.
Ukifatilia kiundani kabisa kundi hili la vijana,na watu wazima wanaofanya kazi hii wengi wao siyo wote,ni kundi la vijana walioacha ama kufeli shule ya msingi na kundi lingine ni walio acha au kufeli kidato cha nne hivyo chaguo la mwisho la kazi kwasababu hawana taaluma yoyote wengi wao wamechagua boda boda.
Ni watu ambao ni kama wamekata tamaa ya maisha ndiyo maana hawajali chochote wanapokuwa barabarani.
Serikali inabidi kuwa na usimazi na ufuatiliaji ili kundi hili la vijana wajuwe sheria za nchi na kuziheshimu.
 
Huwa wanajifanya wana umoja sana hawa viumbe. Yaani kama vile ni watoto wa baba na mama mmoja.
 
Nadhani ifike muda hizi piki piki Pendwa zinazotumika kwa bodaboda ziongezewe kodi maradufu ili ziwe ghali kupatikana ili kupunguza hawa bodaboda wasiojipenda wala kupenda wengine. Warudi kijijini wakalime na kufanya kazi nyingine. Pia wapungue kupata ulemavu wa kudumu na kupoteza mali na maisha
 
Hawa dawa yao unawarekodi kisha unaanza wadondosha mmoja mmoja
 
Back
Top Bottom