Majirani zetu Kenya na Uganda wana bodaboda wasiyozingatia Sheria kama Tanzania?

mafutamingi

JF-Expert Member
Feb 14, 2011
2,772
2,171
Wakati mashindano ya AFCON yalipokuwa yanafanyika huko Ivory Coast, nilimsikia mmoja wa wanahabari aliyekuwa huko akituhabarisha kilichokuwa kinaendelea akisema boda boda wa huko wana nidhamu sana.

Wakifika kwenye taa za barabarani wanasimama mpaka pale taa ya kijani itakapowaruhusu kuendelea na safari yao. Hii ni tofauti na hapa kwetu ambapo traffic light haziwahusu. Hapa boda wanaendesha kulia, kushoto na katikati. Hakuna sheria yoyote ya barabarani ambayo inawahusu!

Sasa naomba kuuliza wale ambao wamepata fursa ya kutembelea miji mikubwa ya Kenya na Uganda, hivi boda boda wa nchi hizo ni vichaa kama wa huku kwetu? Au wa huko ni zaid?

Kwa lugha nyingine kati ya nchi hizi tatu ni nchi ipi ambayo boda boda wake wanaendesha hivyo vyombo vya moto kiwendawazimu kuliko wa nchi zingine mbili?
 
Na wa Rwanda nao wana nidhamu ya hali ya juu. Kule Sheria zipo kwa ajili ya kufuatwa.
 
Back
Top Bottom