Katavi: Dereva aliyetoa taarifa ya Basi lake analoendesha kuwa bovu afukuzwa kazi

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,812
11,989
Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani kimechukizwa na kitendo cha baadhi ya wamiliki wa mabasi kuwafukuza madereva kwa kudaiwa kutoa taarifa kwa mabasi mabovu kwa Vyombo vya Usalama Barabarani ambapo limesisitiza sheria kali kuchukuliwa dhidi ya mmiliki atakaye mfukuza dereva.

Deus Sokoni ni Mrakibu Mwandamizi kutoka Kikosi cha Usalama Barabarani Makao Makuu ameyasema hayo wakati akiongoza Makamanda wa Jeshi hilo katika ukaguzi wa mabasi katika Stendi Kuu ya Mabasi ya Mizengo Pinda Mkoani Katavi ambapo amechukizwa na kitendo cha dereva kufukuzwa kazi baada ya kutoa taarifa ya basi bovu kwa vyombo vya usalama barabarani ambapo amesisitiza Sheria kali kuchukulia dhidi yake huku Faustina Ndunguru Mkaguzi Msaidizi akiwakumbusha madereva kuzingatia na kutii viashiria hatarishi vya ajali.

Leopord Fungu ni Mkuu wa Usalama Barabarani Mkoa wa Katavi amewaonya madereva kutotumia kilevi aina yoyote wakati wanaendesha vyombo vya moto ambapo Afisa Mfawidhi kutoka Mamlaka ya Usafirishaji Ardhini (LATRA), Alen Mwanri akitoa onyo kali kwa yeyote atakaye chezea mfumo wa usalama katika basi lake.
 
Michongo mingi sana Huwa inaanzia kwa watu wa karibu Sanaa ata nduguyo, .....etc
 
Back
Top Bottom