Ugonjwa wa Kuota Vinyama Sehemu za Siri (Bawasiri/ Hemorrhoids): Chanzo, Dalili, Tiba na Kinga

HESHIMA KWENU WOTE

NAOMBA KUJUA DAWA SAHIHI YA BAWASIRI NA KAMA IPO YA KIENYEJI NI MUHIMU PIA TAFADHALi

Kata kipande kidogo cha gamba la dafu ambacho(kichonge) kiweze kuingia sehemu ya haja kubwa bila kukuchubua,kisha kipashe moto wa kiasi..afu kiingize sehemu hiyo mara 3 hivi...kaka siku tatu utaanza kuona matokeo kama sio kuisha kabisa tatizo...ukifanikiwa ushuhuda p/se..
 
Sijuwi kama hayo majani ya Witch Hazel Leaf yanapatikana hapo bongo?

[SIZE=-1]
hamvir67.jpg
[/SIZE]
[SIZE=-2]Copyright, Mark Brand[/SIZE]

Nakusaidia Dawa ingine Rahisi fanya hivi
CHUKUWA MIZIZI YA MKOMA-MANGA PAMOJA NA UBANI KIASI KIDOGO. CHEMSHA ICHEMKE SAWASAWA. CHUKUWA MAJI YAKE TIA KATIKA CHUPA UWE UNAKUNYWA KIKOMBE CHA KAHAWA MARA TATU KILA SIKU ASUBUHI MCHANA NA USIKU KABLA YA KULA KITU KWA MUDA WA SIKU SABA INSHAALLAH MWENYEZI MUNGU ATAKUPONESHA.

Heshima kwako mkuu mzizimkavu,samahani unaweza ukanitajia miti ya kupanda home yenye manuafaa? Nimepanda mipera,mzambarau,mfenesi na mikomamanga,je unaweza ukanisaidia faida za hio miti
 
Heshima kwako mkuu mzizimkavu,samahani unaweza ukanitajia miti ya kupanda home yenye manuafaa? Nimepanda mipera,mzambarau,mfenesi na mikomamanga,je unaweza ukanisaidia faida za hio miti
Kila Mti uliotaja una faida zake tena nyingi kimatibabu tukianza kueleza hapa nafikiri tutajaza server yote kwa ufupia jaribu kupanda miti mingineyo ya matunda kwa mfano michungwa minanasi,michenja,milimau,midimu,Mkunazi,mibaazi,Mipilipili mboga ,figili Mwarubaini, Mlonge na ipo mingi tu yenye faida nikipata nafasi nitakueleza mmoja baada ya mmoja. kila Mtu ni dawa na una faida yake nyingi tu.
 
Kata kipande kidogo cha gamba la dafu ambacho(kichonge) kiweze kuingia sehemu ya haja kubwa bila kukuchubua,kisha kipashe moto wa kiasi..afu kiingize sehemu hiyo mara 3 hivi...kaka siku tatu utaanza kuona matokeo kama sio kuisha kabisa tatizo...ukifanikiwa ushuhuda p/se..

wewe ulifanikiwa au??
 
Kila Mti uliotaja una faida zake tena nyingi kimatibabu tukianza kueleza hapa nafikiri tutajaza server yote kwa ufupia jaribu kupanda miti mingineyo ya matunda kwa mfano michungwa mananasi,michenja,milimau,midimu,Mkunazi,mibaazi,pilipili mboga ,figili Muarubaini na ipo mingi tu yenye faida nikiapata nafasi nitakueleza mmoja baada ya mmoja. kila Mtu ni dawa na una faida yake nyingi tu.

Mkuu mzizimakavu,nitapataje hilo desa la tiba za hiyo miti niliyoipanda?
 
WAKUU NAOMBA KUULIZA SABABU ZA BAWASIRI KWA WANAUME WA SHOKA SIO WALE MABWABA MAANA NIMEGUNDUA WENGI WaNAOUGUA UGONJWA HUU NI WANAUME WA SHOKA NA SIO MABWABWA

HESHIMA MBELE KWA MADAKTARI SIKU ZOTE
 
Mabwabwa anal sphincter zao tayari zinakuwa stretcked kila anapoingiliwa. Lakini wazee wa shoka wako tight na pale panapotokea end to end anastomosis ya rectal arteries zina pool damu na zinakuwa congested na kusababisha maumivu makali na zikivimba zaidi zaweza ku prolapse nje na hazirudi zenyewe sababu tight anal sphincters haziruhusu. Mpaka zirudishwe kwa vidole.

Tiba mojawapo ya Bawasiri hosp. ni kuzistretch hizo anal sphinters under anaesthesia.
 
Nasikia wanapata watu wanaopata choo kigumu kwa kawaida. Lakini kuna tib mbadala ambayo ni mafuta ya nyonyo sijui au kitu kama hicho ambayo mtu anapaka hadi inarudi ndani
 
Hemorrhoids.png

Bawasiri (Hemorrhoids)

Bawasiri ni mojawapo ya tatizo ambalo mara nyingi

linapotokea
humfanya mtu kuwa na aibu kuelezea au kwenda hospitali ili kupata tiba sahihi. Bawasiri au hemorrhoids husababishwa na kuvimba kwa mishipa ya damu aina ya vena katika eneo la mfereji wa haja

kubwa.Kuna aina mbili za BawasiriNje: Aina hii ya bawasiri hutokea katika eneo la mwisho kabisa la mfereji wa haja kubwa, na huweza kuambatana na maumivu, pamoja na kuwashwa kwa ngozi katika eneo hilo. Mara nyingine mishipa hiyo ya damu (vena) hupasuka na damu huganda na kusababisha aina kitaalamu inaitwa Thrombosed hemorrhoid.Ndani: Aina hii ya bawasiri

hutokea ndani ya mfereji wa haja kubwa. Na huwa haimbatani na maumivu na wengi huwa hawatambui kuwa wanatatizo hili.Aina hii imegawanyika katika mainisho yafuatayo daraja I- Bawasiri kutotoka katika mahali pake pa kawaidaDaraja II-

Bawasiri kutoka wakati wa haja kubwa na kurudi yenyewe baada ya tukio hilo.Daraja III- Bawasiri kutoka wakati wa haja kubwa na mtu kuweza kuirudisha mwenyewe baada ya tukio hilo.Daraja IV- Bawasiri kutoka wakati wa haja kubwa na vigumu mtu kuirudisha baada ya tukio hilo.Je bawasiri husababishwa na nini?Bawasiri husababishwa na;

    • Tatizo sugu la kuharisha
    • Kupata kinyesi kigumu
    • Ujauzito
    • Uzito kupita kiasi (obesity)
    • Kupenda kufanya ngono ya njia ya haja kubwa (anal sex)
    • Kwa ujumla mambo yanayo ongeza shiniko katika tumbo.
    • Umri mkubwa
Dalili za bawasiri

    • Damu kunuka kinyesi wakati wa kujisaidia (hematochezia)
    • Maumivu au usumbufu
    • Kinyesi kuvuja
    • Kijiuvimbe katika eneo la tundu la haja kubwa
    • Ngozi kuwasha katika eneo la tundu la haja kubwa
    • Kujitokeza kwa kinyama (bawasiri) wakati wa haja kubwa
Matatizo yanayoweza kutokana na Bawasiri

    • Upungufu wa damu mwilini (Anemia)
    • Strangulated hemorrhoids
Vipimo na uchunguzi

    • Digital rectal examination
    • Kipimo cha njia ya haja kubwa (Proctoscope)
    • Kipimo cha utumbo mpana (Sigmoidoscope)
MatibabuMatibabu hutegemea na hali na aina ya Bawasiri

    • Rubber band ligation - Hapa mishipa hufungwa na rubber band ili kuzuia damu kwenda kwenye eneo liloathirika, na hutumika kwenye aina ya ndani ya bawasiri.
    • Sclerotherapy- Hapa kemikali huwekwa kwa njia ya sindano
    • Coagulation (infrared, laser and bipolar)
    • Upasuaji;
      • Hemorrhoidectomy
      • Stapled hemorrhoidopexy
Njia za kuzuia Bawasiri

    • High fibre diet, kula mboga za majani, matunda, na nafaka kwa wingi.
    • Kunywa maji mengi kwa siku (glasi sita had nane kwa siku)
    • Punguza kukaa kwa muda mrefu sana hasa ukiwa chooni, kwa sababu unaweza kuongeza shinikizo katika mfereji wa haja kubwa
chanzo. Bawasiri (Hemorrhoids)
 
Habari wadau, mimi ni kijana wa kitanzania, nimeoa mwezi uliopita tu. Mpaka sasa naandika ni kwamba mke wangu ni mja mzito wa miezi miwili kasori. Tatizo ni kuwa mke wangu katika sehemu ya haja kubwa kuna kijinyama kidogo kimejitokeza,hatuna uhakika lakini baada ya kuuliza tukaambiwa inaweza kuwa " bawasiri". Je ni nini tiba yake? Pia kama haijatibiwa inaweza kuleta madhara gani wakati wa kujifungua? Nampenda sana mke wangu and napenda sana kumuona mtoto wangu mtarajiwa. Naombeni maoni na ushauri wenu. Asante
 
Bawasiri inayojulikana ni ile ya tupu ya nyuma, bawasiri huwa ni mfano wa tutu kwa ugumu wake, na udogo wake na mviringo wake au huwa mwekundu huenda ikatoa damu na pengine isitoe damu.

Namna ya kuifanyia dawa:

1. Ipake mafuta ya mbono kwenye hicho kipele cha bawasiri mara nyingi, na baada yake itawezekana kuirudisha ndani.

2. Iponde habbat Sauda kisha changanya na sukari kiasi kama cha habbat Sauda, ule siku moja mara moja kila mara nusu kijiko kisha na unywe maji.

3
dawa ya bawasir ni Mshubiri fresh unakata jani lake na unalimenya kisha unatoa ile nyama ya ndani inayoteleza unajisugulia pahala penye hiyo bawasir na kwa uwezo wake Allah inarudi (inaondoka).

Miiko ya Mgonjwa wa Bawasiri asitumie vitu hivi

Anatakiwa mgonjwa wa bawasili asitumie maharage, Nyama ya ng'ombe, na nyama ya kuku mkongwe sana.
Ni muhimu sana kwa mgonjwa asitumie vitu hivi kwa usalama wake basi nibora ajiekee miko kabisa.

Mwambie shemeji yangu atumie moja kati ya hizo Dawa nilizotaja kisha unipe Feedback.
 
ri wana jf doctor..mimi ni mdada wa 22 years,ninasumbuliwa na tatizola tumbo alafu nikienda chooni kupata haja kubwa natokwana damu sana kama vile nipo katika menstruation cycle...ila hapa umi kabisa,zamani zilikua zikinitoka na ni kidogo sana na palikua panauma sana kwasababu ya mabasili yalikua yakipasuka...ilia sasa moja limepona na moja limebaki na haliumi kabisa... ila damu ndo zimenshtua nisaidieni hili ni tatizo gani pia tumbo la chakula linakua linaongezeka tanu damu zimeanza nitoka
 
Naomba fafanua damu inatoka njia ya haja kubwa au ukeni? Na hicho unachoita mabasili ni kitu gani? naomba ufafanuzi kabla sijachangia.
 
Back
Top Bottom