Simu inavyoweza kusababisha ukapata Ugonjwa wa Bawasiri (kuvimba njia ya haja kubwa)

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,267
5,367
Baadhi ya watu watabia ya kuongea na simu na wapendwa wao kwa muda mrefu. Licha ya kupata maumivu ya masikio, kichwa na matatizo ya macho, wataalamu pia wamebainisha madhara makubwa yanayoweza kutokea kupitia simu yako ya mkononi.

Shinikizo la damu
Ripoti iliyotolewa na watafiti kutoka Nchini Italia inasema baada ya kuchunguza wagonjwa 94 wenye shinikizo la juu la damu, waligundua kuongea kupitia simu ya mkononi kunaweza kuongeza shinikizo la damu.

Kwenye jaribio la kutafuta uhusiano kati ya simu ya mkononi na shinikizo la damu, watafiti waliwafanyia majaribio wagonjwa wenye shinikizo la damu na matokeo ya jaribio hilo yalionesha wagonjwa hao wanapoongea kupitia simu za mkononi, shinikizo la damu lao huwa juu kuliko wakati ambao hawaongei kupitia simu za mkononi.

Hivyo, watafiti wameshauri watu wenye shinikizo la damu la juu wanapopimwa shinikizo hilo, wasitumie simu za mkononi, ili kuhakikisha usahihi wa matokeo ya upimaji.

Bawasiri
Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na Daktari Bingwa, Sarah Jarvis kutoka Uingereza, umeonesha watu wengi wanaoingia na simu chooni na kuanza kuzitumia wamepatwa na Bawasiri

Bawasiri ni kuvimba kwa mishipa ya damu iliyopo ndani ya au katika eneo linalozunguka njia ya haja kubwa. Ni hali ambayo inaweza kusababisha nyama kujitokeza nje. Hivyo Bawasiri inaweza kuwa bawasiri ya ndani au bawasiri ya nje.

Daktari huyo amesema kuwa kitaalamu, chooni unatakiwa ujisaidie ndani ya dakika 5 na watu wengi wanaoingia na simu vyooni hutumia zaidi ya dakika 5 kujisaidia.

Sarah amesema kitendo cha kukaa muda mrefu ukiwa unajisaidia haja kubwa husaidia bakteria kuzaliana na kuingia mwilini kwa urahisi.

Kwenye tafiti hiyo, Sarah amesema kati ya watu 500 wanaotumia vyoo vya kukaa, alikuta 10 wamepatwa na Bawasiri na walikiri kutumia simu wanapokuwa maliwatoni.
 
Na mimi utafiti wangu unasema kula vyakula laini visivyokuwa na nyuzinyuzi (fibres) hudhoofisha mishipa ya "matokeo". Kula Dona iliyochanganywa na mtama kidogo au ulezi na mhogo kiasi ili ukate gogo lililoungana. Pia vyoo vya kuchuchumaa vinaimarisha mishipa ya "matoleo". Ni hayo Tu.
 
Namm ntafanya research kuwa wenye stress na depression hupatwa na bawasiri, sababu wakiingia chooni wanakaa muda mrefu zaidi ya dk 5.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom