Baridi yabisi (Arthritis): Ugonjwa wenye tiba maelfu

Baba Vladmir

JF-Expert Member
Aug 31, 2021
300
490
UGONJWA WA BARIDI YABISI NI NINI?
Baridi yabisi ni neno la jumla kwa magonjwa au michakato mingine isiyo ya kawaida itokeayo kwenye viungo. Mamilioni ya watu ulimwenguni kote wanaugua aina fulani ya baridi yabisi.

Viungo vyetu na mishipa yetu, kama ilivyo misuli yetu, hudhoofika kadiri vinapotumika na huhitaji kurekebishwa daima, mchakato ambao mara kwa mara hutokea wakati wa kulala. Urekebishaji wa kiungo chochote cha mwili huhitaji upatikanaji wa oksijeni na viinilishe vingine. Mzunguko wa damu unapopungua, mishipahl hudhoofika, majimaji kwenye maungio hupungua na tishu hulika.

AINA GANI YA BARIDI YABISI HUKULIKANA SANA?
Kusagika viungio ni aina ya baridi yabisi inayojulikana sana na hupatikana zaidi kwa watu wenye umri mkubwa. Pia inaweza kutokea wakati wowote baada ya jeraha au kwa kukifanyisha kazi kiungio fulani kupita kiasi, kama inavyotokea kwenye uzito kupita kiasi au katika michezo.

Baridi yabisi ya kulika/kusagika viungio mara nyingi hutokea wakati usambazaji wa damu kwenye kiungio unapokuwa hautoshi kwa ajili ya matumizi. Kama ambavyo moyo hudhoofika na hatimaye kushindwa kufanya kazi wakati ateri za moyo zinapoziba kwa utando, ndivyo ambavyo viungio husagika pindi ateri zinazosafirisha damu zinaposinyaa au kuziba.

Kwa sababu hii watu wengi sana wenye baridi yabisi ya kwenye viungio hupona kwa kufanya shughuli zinazoboresha mzunguko wa damu, kama vile kupunguza kiasi cha mafuta kwenye mfumo wa damu, mazoezi ya mara kwa mara na tiba kwa njia ya maji.

Baridi yabisi ya kwenye viungio vinavyobeba uzito, kama vile mifupa ya uti wa mgongo, magoti na kiuno huzidiwa uzito kwa sababu ya uzito kupita kiasi.

Dalili zijulikanazo mara kwa mara za baridi yabisi ni maumivu na kukakamaa, hali inayozidi kupungua wakati kiungo kinaposhughulishwa kwenye mazoezi.

JE, MAUMIVU YA MGONGO HUSABABISHWA NA BARIDI YABISI?
Maumivu ya mgongo ni tatizo lililoenea ulimwenguni kote. Watu wanne kati ya watano wanaugua ugonjwa huu katika kipindi fulani cha maisha yao.

Jambo la kushangaza, asilimia kubwa ya wagonjwa wenye maumivu katika upande wa chini wa mgongo ni wahanga wa kufanya kazi kupita kiasi au misuli ambayo haikufanywishwa mazoezi ya kiwango cha chini. Msuli ulioteguka kwa ghafla unaweza kukaza kwa kipindi kirefu au kushtuka na kusababisha maumivu makali.

Asilimia ndogo ya matatizo ya mgongo huweza kusababishwa na baridi yabisi kwenye viungio au tatizo la kisahani (gegedu). Ni wachache tu wanaougua maumivu ya mgongo wana majeraha mabaya.

Kunapokuwa na maumivu ya mgongo, ni mhimu kujua ikiwa kulikuwa na jeraha kabla ya jambo lingine lolote kufanyika. Bila jeraha linalojulikana, jambo lingine mhimu si kufanya kile unachohisi kufanya (kwenda kulala na kubaki hapo). Unaweza kupumzika siku moja baada ya jeraha au kutokea kwa maumivu au siku mbili na si zaidi ya hapo. Usiendelee kupumzika tu.

Katika hatua hii, kukanda barafu kwenye eneo lenye maumivu inaweza kusaidia. Halafu ni wakati wa kusimama na kuanza kutembea. Tembe hadi maumivu yatakapopungua. Kulala sana kitandani kutasababisha madhara makubwa kuliko manufaa, kwa sababu kulala husababisha misuli ya mgongo kudhoofika kwa haraka.

Badala ya kuimarika unakuwa dhaifu. Baada ya muda fulani, hata shughuli rahisi inaweza kutengua au kukakamaza misuli ya mtu fulani asiyefanya mazoezi.

Kwa bahati njema sehemu kubwa ya matatizo ya mgongo hutibika yenyewe kwa kipindi cha majuma 4 hadi 12. Unaweza kuzuia kujirudia au kuzuia maumivu ya mgongo kabisa kwa kufanya yafuatayo;

1. Punguza uzito wako; hii ni fadhila kubwa kabisa unayoweza kuufanyia mgongo wako.

2. Epuka viatu vyenye kisigino kirefu. Huinamisha fupanyonga na husogeza mgongo kutoka kwenyw mkao wake mzuri. Hivyo husababisha matatizo mengi ya kiafya.

3. Imarisha mgongo na misuli yako ya kwenye tumbo kwa mazoezi maalum. Tembea, ogelea au kimbia kwa dakika angalau 20 mara tano kwa juma.

4. Kula mlo wenye kiasi kidogo cha mafuta na wenye nyuzinyuzi nyingi ili kuimarisha mzunguko wa damu, ukiruhusu vyema damu kusafirisha oksijeni na viinilishe vya ziada kwenda kwenye maeneo yenye kasoro.
Hatua hizi ni mhimu kwa aina zote za baridi yabisi pamoja na maumivu ya mgongo.

VIPI KUHUSU VIUNGIO VYEKUNDU KWA SABABU YA UVIMBE?
Huenda unafikria kuhusu baridi yabisi inayosababisha maumivu kwenye viungio na kusababisha ulemavu na kupoteza uwezo wa kujongea hasa kwenye vidole, kifundo cha mkono, miguu na magoti. Ugonjwa huu ni tofauti na baridi yabisi ya kulika kwa tishu na mifupa kwa maana kuwa inatokana na uvimbe chungu wa viungio vyenye wekundu, uvimbe, maumivu na homa badala ya kutokana na majeraha au kusagika kutokana na kufanywisha kazi.

Baridi yabisi ya ulemavu wa viungio ni ugonjwa utokanao na mfumo wa kinga kutofanya kazi vizuri. Mashambulizi makali huwa na mwelekeo wa kujirudia baada ya miaka, ikizalisha vifundo na hatimaye hukakamaza na kupoteza umbo la kiungio, hasa hutokea kwenye kifundo cha mkono na viungio vya vidole.

UPONYAJI HUFANYIKA KWA VIUNGIO VINAVYOUMA
Pamoja na aina tofauti za baridi yabisi, hizi ni kanuni za jumla ambazo zina ufanisi;

1. Sawazisha uzito wako: Kila kilogram ya ziada huongeza msuguano na kulika kwa viungio vya kubeba uzito kama vile kiuno, magoti na uti wa mgongo.

2. Rahisisha mlo wako. Milo yenye kiwango kidogo cha mafuta na kiwango kikubwa cha nyuzinyuzi, huimarisha mzunguko wa damu katika viungio. Baada ya muda fulani, aina hii ya chakula inaweza pia kusaidia kufungua baadhi ya ateri zilizosinyaa. Ondoa vyakula vyote vya maziwa na nyama kwa muda wa majuma matatu na tathmini mwelekeo wako.

3. Fanya mazoezi kila siku ili kuimarisha misuli. Misuli iliyodhoofika hailindi viungio kwa ukamilifu. Wakati viungio vinapouma, kuogelea na kufanya mazoezi majini hufaa zaidi.

4. Fanyia kazi viungio vilivyoathirika ndani ya uwezo wao wa kupata damu.Kupumzika wakati wa maumivu, halafu kurejea kwenye utendaji kwa haraka ni mhimu katika kuzuia ulemavu wa kudumu

5. Tumia madawa kwa tahadhari. Vituliza maumivu na vilegeza misuli, madawa yasiyokuwa na steroid ambayo hupunguza uvimbe chungu huweza kusaidia, hasa hasa katika hatua mbaya ya ugonjwa. Tiba kwa njia ya steroid inaweza kusababisha mabadiliko makubwa sana; lakini inapotumika kwa muda mrefu mara nyingi huleta athari zaidi kuliko faida.

Kama unaweza kutengeza madawa kwa kutumia mimea tiba ni jambo jema zaidi maana utapata faida mara mbili, moja utajiponya na ugonjwa na pili utarudisha na kuimarisha mfumo wako wa viungo zaidi kama awali kwa njia ya asili, lakini pia hakuna kemikali au madhara yanayoachwa na mimea mwilini.

NOTE: Pigania afya yako. Jishughulishe. Watu wanaorejea katika afya bora ni wale wanaofanya juhudi za dhati katika kuleta mabadiliko chanya na ya kudumu katika mitindo yao ya maisha.

Kama una swali lolote juu ya magonjwa yasiyoambukiza au magonjwa yasababishwayo na mtindo wa maisha, usisite! Unaweza kuuliza hapa na ukapata majibu na kanuni nzuri ya kujiepusha.
 
Pigania afya yako, jishughulishe..... mwili wako ndo kitu pekee utazikwa nacho.
 
UGONJWA WA BARIDI YABISI NI NINI?
Baridi yabisi ni neno la jumla kwa magonjwa au michakato mingine isiyo ya kawaida itokeayo kwenye viungo. Mamilioni ya watu ulimwenguni kote wanaugua aina fulani ya baridi yabisi.

Viungo vyetu na mishipa yetu, kama ilivyo misuli yetu, hudhoofika kadiri vinapotumika na huhitaji kurekebishwa daima, mchakato ambao mara kwa mara hutokea wakati wa kulala. Urekebishaji wa kiungo chochote cha mwili huhitaji upatikanaji wa oksijeni na viinilishe vingine. Mzunguko wa damu unapopungua, mishipa hudhoofika, majimaji kwenye maungio hupungua na tishu hulika.

AINA GANI YA BARIDI YABISI HUJULIKANA SANA?

Back
Top Bottom