ni kweli watu tunakimbia kuku wanaouzwa masokoni sababu mtu akiona wagonjwa anaamua kuuza. Pia wengi hawapatiwi chanjo ikitokea wamesafirishwa toka mbali wanafika wanaanza kuumwa aidha kudhoofu na hali ya hewa au kuambukizwa njiani. Tunategemea hapa JF itakuwa gulio la wasomi kutokana na darasa zinazotolewa hapa na kupigiwa mfano.

'kabisa kabisa,ni bora akafanya hivyo ila mi sidhani kama atakuwa serious kwa kweli coz jamaa tangu aweke hili bandiko hapa hajajibu hayo maswali yenu,hajaweka comment yoyote,hajatoa hata namba ya simu na tangazo hajaweka jana wala juzi na pia wala halipii lakini haonekani kabisa au alishaku-check kwa PM pengine labda'
 
Elezea vzr mkuu wanapatikana wapi na kwa bei gani? Na kama wamepata chanjo

Sent from my BlackBerry 9790 using JamiiForums

'hivi wasipokuwa na chanjo na wanapokuwa na chanjo kuna vitu gani vinakuthibitishia kuwa huyu ana chanjo na huyu hana chanjo mkuu unaomva utujulishe kdg kwa faida ya wote ndugu'
 
Wakuu badala ya kujikita kwenye kilimo na biashara ya mazao tuu ambavyo vimenipa faida, nimeamua kuanza ufugaji wa kuku wa kienyeji hybrid kuanzia mwakani january hapa Dar es salaam Kwa ajili ya nyama na mayai. Nina mpango wa kufanya processing mwenyewe yaani kuchinja na kuuza kidogo kidogo nyama mwenyewe. Tayari nina banda kubwa. NInatarajia kuanza na kuku (HYBRID) 11 na ninatarajia kuwa na kuku mia tatu mpaka mwishoni mwa mwaka 2014. Kuhusu malighafi kama mashudu na mahindi si tatizo ,nina mashudu na mahindi ya kutosha huko mkoani. Pamoja na kwamba nimepitia thread kadhaa papa jf , bado sijapapa maelezo yakutosha kuhusu hawa hybrid hasa ktk mambo yafuatayo.
Ninaomba mnisaidie.

1.Ni aina gani ya hydrid inafaa zaidi?

2.Mchanganuo wa kiasi na gharama ya chakula kwa hawa hybrid, yaani kuku 100?

3. Wanachukua miezi mingapi hadi kufikia wezo wa kutaga mayai au kuuza/kuchinja kwa ajili ya nyama ?
 
Ufugaji wa kuku wa kienyeji ni mzuri na wenye manufaa sana. Unauwezo wa kumnyanyua mtu mwenye kipato cha kuanzia Tsh. 6,000 hadi10,000/= (nunua kuku mmoja) na kuwa milionea. Ni kuwa serious, determined, mvumilivu na mwenye kutumia ufugaji wa kisasa. Tatizo la wengi vijijini they don't take it seriously, wanafuga tu kimtindo kama supplement ya kazi zao za mashambani au ufugaji wa ng'ombe. Tatizo lingine kubwa kwao ni Kideri/mdondo (New castle disease), hawachanji kuku dhidi ya gonjwa hili plus magonjwa mengine. Serikali ingewasadia kuchanja kuku dhidi ya kideri ingewasaidia sana. Dawa yenyewe ni cheap sana, by 2012 tube ya kuchanja kuku 400 ilikuwa Tsh. 5,000. Ukiwa kasehemu kakuwafanya wawe huru kidogo hata mijini au pembezoni mwa miji unaweza wafuga. Lakini siku hizi kuna watu wanawafungia ndani kama wa kisasa either kwa kukosa enough space au ili kufuga wengi zaidi kibiashara.

Nimekusoma; ukiwa na kuku zaidi ya 100 ukiwaacha huru ni kero kwa majirani. Pia wanapata magonjwa mengine kutoka kwa kuku wa jirani ambao hawachanji kuku wao.

Hilo limeisha.

Tatizo langu kwa leo;
nimepata taarifa toka kwa mama watoto kwamba tayari kuku wanne wamedondoka na dalili kashindwa kujua ni gonja lipi? wanaanza kwa kutetemeka then chali; mwenye kujua ni kitu gani hicho tafadhali anijuze.
 
Samahani wa jamii, baada ya kupiga misele na bahasha ya khiki kwa bila mafanikio, kwasasa nataka nijiajili, nataka kufuga kuku wa kienyeji kibiashara zaidi. Naomba ushauri kwa mwenye idea juu ya ufugaji ya hawa kuku wa kienyeji.
 
Samahani wa jamii, baada ya kupiga misele na bahasha ya khiki kwa bila mafanikio, kwasasa nataka nijiajili, nataka kufuga kuku wa kienyeji kibiashara zaidi. Naomba ushauri kwa mwenye idea juu ya ufugaji ya hawa kuku wa kienyeji.

Hongera kwa uamuzi huo, Nashauri ufatilie post za ufugaji kuku wa kienyeji humu jamvini zipo nyingi. Naamini utapata mwongozo mzuri.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom