Mkuu hii sishauri mtu aifuate maana ataumia sana kama anategenea kuku haohao, binafsi nilitenga laki 4 nikanunua kuku wa miezi 2 kwa shs 3500 kijijini walikuwa kama 23 hivi, nikajipanga chakula kizuri plus,chanjo zote maana banda lilikuwepo.

kuku walikufa wengine kwamagonjwa ambayo umewapa chanjo wakabaki 15 hivi ndo walivuka salama wakawa wakubwa wote tetea nikanunua jogoo 1 kwa 15.

hapo kuna vifaranga kufa kutokana na sababu fulani kuna kuku kutolalia vizuri unakuta mayai 12 anatotoa 3.....sema naahukuru kipato ninacho so nawahudumia ila sijapata profit yoyote zaidi ya nyama tu.

Kutotoa wanatotoa ila kunachangamoto sana kuvivusha vifaranga kwenda kwenye stage ya 2.
Kutotoa 3 kati ya 12, na vifaranga kufa ni uamuzi tu wa mfugaji. Mimi nilipoamua kuzifuta hizo changamoto zilifutika. Kuku wangu nawawekeaga mayai 15 na ni wachache sana ambao hubakiza mayai 3. Sehemu kubwa huangua yote au kubakiza moja.

Kulea vifaranga ni kuhusu chakula, vitamin, na chanjo. Mimi huwapa broiler starter kwa mwezi mzima wa kwanza, vitamin na amplolium. Vitamin ninayotumia ni lazima iwe na O.T.C ndani yake. Vifo hutokea kwa vifaranga waliozaliwa dhaifu au walemavu pekee.
 
Hongera mkuu nimejifunza kitu.
 
Naombeni msaada nitumie njia gani kulea vifaranga wangu kwani watotolesha zaidi ya 50 ila hufa zaidi ya 30,nifanyenini hapa wadau?
 
Mimi nnachoweza kukushauri mkuu wanapototoleshwa tumia mfumo wa ndani sio huria kwanza kuwaepusha na maadui kama mwewe kunguru na paka ila pia wasiambukizwe magonjwa na kuku wakubwa .

Hakikisha wanapata joto la kutosha hasa wakati wa usiku (kama umewatenga na mama zao unaweza kutumia taa au yale majiko ya kukuzia vifaranga).

Wapatie chanjo (sana sana kuku wa kienyeji wanasumbiliwa na magnjwa kama kideli na mafua na minyoo ).chanjo ya kideli vifaranga wako wape siku ya saba toka wametotoleshwa baada ya hapo siku ya 21 then mwsho wa mwezi minyoo .

Hakikisha unawafuga katika mazingira safi na mabanda bora wasiwe wasiwe overcrowdng .

Wapatia chakula kwa ratio sahihi ya virutubisho namaanisha hakikisha chakula wanachotumia kina muunganiko wa wanga protini mafuta na vitamin bila kusahau maji ya kutosha .

La kuongeza kwa upande ufagaji wa hawa ndege wakishaanza kuumwa kupona kidogo hua ni mthani kwa hio chanjo ni bora kuliko tiba

Tumia vitu kama OTC na multivitamin ili kuuwa vijidudu nyemelezi na kuwaongezea hamu ya kula mpka watakapofikia stage nzuri ya kuwaachia

Sent from my SM-J200H using JamiiForums mobile app
 
@Joninho Nakushauri pia upitie za post za Kubota kule juu kuhusu uleaji wa vifaranga. Pia ongezea na haya;

1. Joto.

Vifaranga wapewe joto la kutosha mpaka watakapochangamka. Hii haina formula. Yaweza kuwa siku 3, 7, 14, 21, nk kutegemeana na observation juu ya uchangamfu wao. Tumia jiko maalum la kuku ili kupata matokeo mazuri; joto hutolewa taratibu na hivyo kupunguza matumizi ya mkaa na usumbufu wa kuongeza ongeza mkaa. Mie huweka mara moja tu jioni na asubuhi ndiyo unaishia na chumba bado cha moto. Hii ni ikiwa mkaa wako ni mzuri.

2. Chakula

Kwa mujibu wa hii thread (ukiisoma yote), hauwezi kutengeneza chakula cha vifaranga yaani starter. Nishawahi kujaribu kukinzana na huu ukweli nikadondokea pua. Vifaranga wapewe chakula "special" cha kiwandani cha watengenezaji wanaoaminika kama 'Silverlands'.

Kifaranga wa nyama apewe broiler starter na yule wa mayai apewe Layer's starter. Kuepuka risk ya vifo kabla ya kufikisha mwezi mmoja, waweza kuwapa vifaranga wa mayai broiler starter kwa wiki 1, 2, mwisho 3 kabla ya kuwapa layer's starter mpaka watakapotimu wiki 6 ambapo utaanza kuwapa grower feeds.

NB: Ukiona huwezi kununua chakula mfuko mzima kwa wakati mmoja au ikiwa vifaranga ni wachache, nunua katika kilo.

PIA: Vifaranga wanapaswa kupewa chakula masaa 24 siku 7 za wiki ikiwa kweli uko siriaz.

3. Dawa

Pamoja na kwamba starter nzuri ya kiwandani huwa na dawa tayari, ni muhimu kuwapa dawa vifaranga wako kwa utaratibu ufuatao:

Vifaranga wapewe maji ya kunywa muda wote yenye dawa/chanjo zifuatazo;

I. Sukari.

Badala ya kuingia gharama ya kununua glucose, wewe wape ile sukari unayotumiaga mezani. Weka kijiko kimoja cha chakula kwenye maji lita 1. Wape kwa angalau siku 7 mpaka pale utakapoona yafaa, zingatia uchumi pia.

II. Amplolium.

Hii ni dawa na chanjo (vyote kwa mpigo) ya kukinga na kutibu ugonjwa wa coccidiosis. Ule ugonjwa ambao vifaranga au kuku husinzia na kuvaa makoti.

Hii ndiyo muhimu zaidi kwenye huu mchanganyo kwa vifaranga. Ugonjwa husababishwa na unyevu hivyo hakikisha banda ni kavu muda wote.

Amplolium iwekwe kwenye maji kwa angalau siku 7. Kipimo ni gramu 5 sawa na kijiko kimoja (level) cha chai. Yaani kale kakijiko kadogo kawe level kasiwe na mlima kwenye maji lita tano. Mimi huweka na mlima.

III. Vitamins

Vifaranga wapewe maji yenye vitamini kwa mwezi mzima wa kwanza. Ikipungua sana wiki 3. Pendelea zaidi kutumia vitamin zenye O.T.C ndani. Kama vitamini yako haina OTC ndani, nasa
hauri ununue OTC ikiwe uchumi unaruhusu, uchanganye na vitamins.

Hivi vyote viwekwe pamoja kwenye maji ambayo kuku watakunywa muda wote. Siku za chanjo vifaranga wanywe maji plain. Yaani baada ya kuondoa maji ya chanjo husika, wape maji ya kawaida. Kesho yake ndiyo uendelee na ukemia. Hii ni ikiwa unatumia chanjo za kuweka kwenye maji (kwa Newcastle na Gumboro).

4. Chanjo

Wape chanjo 4 zifuatazo ndani ya mwezi wa kwanza:

I. Newcastle.

Siku ya 3, 4, 5, 6 au 7

II. Ndui ya kuku (fowl pox);

Wiki ya 2. Yaani siku ya 14. Usisikilize vitabu vya kibongo utafeli. Chanjo hii yaweza kutolewa hata siku ya kwanza. Tunavuta muda kudogo ili kifaranga kitengeneze bawa litakaloshikika na kuchomeka sindano kirahisi.

Vitabu vyetu vimeandika wape wiki ya 6 hadi 8! Utapotea. Ugonjwa huu umekuwa sugu kwa baadhi ya koo za kuku na huja mapema, mpaka wiki ya 3 hivyo wape mara tu wanapoanza kuota mabawa.

III. Gumboro

Wiki ya 3

IV. Newcastle tena.

Wiki ya 4

Kwa kutumia program hii, siku ya 30 unakuwa na idadi ile ile ya vifaranga ulioanza nao, tena wakiwa na afya tele.

Endelea kusoma zaidi kwenye vyanzo vingine.
 
Wakuu habari ya majukumu, Nina changamoto kwa kuku wangu (kienyeji) naombeni msaada na uzoefu wenu kwenye hili. Nimeanza huu mradi mwezi mmoja sasa.

Kama siku 10 zilizopita nimempoteza kuku mmoja baada ya kuugua ndani ya masaa 24. Alianza kuwa mnyonge, hatoki bandani Wala kula. Akaanza kuonyesha dalili za kupumua kwa shida na kutoa sauti ya kama amekabwa na kitu kooni na anatoa ile sauti ili kuondoa huo mkwamo. Akanyon'gonyea hata kusimama na kutembea ikawa shida anayumba tu, kesho yake naplan kutafuta daktari akafa.

Leo mchana naona mwingine pia ameanza zile dalili, sijui ni kikohozi, anatoa hizo sauti za kukabwa na hana hamu ya kula. Hii shida yaweza kuwa ni nini naombeni msaada tafadhali.
 
Tuma picha ya mmoja wa wagnjwa ili tuwez kukusaidia ushauri mkuu
 
Sijui kama ushapata suluhisho. Hayo maelezo yanaonesha kuku wana kideri au Newcastle.
 
Wakuu habari ya majukumu, Nina changamoto kwa kuku wangu (kienyeji) naombeni msaada na uzoefu wenu kwenye hili. Nimeanza huu mradi mwezi mmoja sasa.

Kama siku 10 zilizopita nimempoteza kuku mmoja baada ya kuugua ndani ya masaa 24. Alianza kuwa mnyonge, hatoki bandani Wala kula. Akaanza kuonyesha dalili za kupumua kwa shida na kutoa sauti ya kama amekabwa na kitu kooni na anatoa ile sauti ili kuondoa huo mkwamo. Akanyon'gonyea hata kusimama na kutembea ikawa shida anayumba tu, kesho yake naplan kutafuta daktari akafa.

Leo mchana naona mwingine pia ameanza zile dalili, sijui ni kikohozi, anatoa hizo sauti za kukabwa na hana hamu ya kula. Hii shida yaweza kuwa ni nini naombeni msaada tafadhali.
Mafua hayo wape dawa ya mafua na uchanganye na ya vitamin na uzidishe kiwango walichokuandikia maana hayo mafua yamezidi na wape kwa siku tatu mfululizo.
 
Hutakosa wateja tena ukitegemea ni kuku wa kienyeji,,,mie nnafanya biashara iyo ila sio Dar.

Nilianza kutafuta wafanyabiashara asa masokoni ili nipate angalizo na soko la jumla au rejareja,pia mahotelini unaweza pitia nk nk. Unajua biashara hii kweli ujue tu kujieleza na ukidhi haja ya wateja kwa uzuri,me ilinsaidia hasa ya masokoni na mnaingia mkataba kabisa.

Pia ukiwa na plani ya biashara (sijui niitaje business plan/profile??) ambayo umeiandika unaweza onyesha wateja asa big customers nk haaa si haba.

Keep it up ndugu
Hii ni nzuri. Natarajia kufuga kuku wa kienyeji tayari kwa kuanza biashara hii. Unaweza kunipa muongozo juu ya hili?
 
Nakushauri ufuge wa kisasa - Layers. wa kienyeji it takes time na faida si kubwa vile unavyodhani - nitafute nikupe ushauri wa bure - meanwhile angalia kazi hii hapa

Hawa wako 900, wanatoa Tray 24 kila siku kila Tray 5000- Chakula chao ni kilo 125 approx Tshs 55,000/-

Mtaji wa kuanzia unahitaji kuwa na not less than 6m before you start production. Kama unataka mchakato mzima sema nitakutumia database yangu.

View attachment 10528nzuri. Naomba unitumie nami nijifunze. alphoambrosi106@gmail.com
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom