FORMULA 100Kgs za Chakula cha Kuku
  1. Mahindi yaliyoparazwa 25Kgs.
  2. Pumba za Mahindi 25Kgs.
  3. Dagaa/Uduvi 10Kgs.
  4. Unga wa Mifupa/Bionemeal 5Kgs.
  5. Chokaa/Limestone 5Kgs.
  6. Mashudu ya Alizeti 5kgs.
  7. Mashudu ya Pamba 10kgs.
  8. Ngando ndogondogo 5kgs.
  9. Machicha ya ngano/Wheat Brand 10kgs.
Hapo namba 8 ngando ndogondogo ndiyo kitu gani?
 
Wakuu habari Nina Kuku wangu wawili Yani imewachukua miezi 2 na nusu hawajaangua vifaranga na mayai kwa ndani ukiyatikisa yanaonekana yana maji kwa ndani na yapo mayai 35 Ni nn kinasababisha kuku kutoangua hayo mayai na imebidi niwatoe hayo mayai ili waanze upya kutaga.
 
Pole sana. Bila shaka yatakuwa yameshaharibika kama kuku kalalia siku zote hizo. Inawezekana hayakuwa na jogoo ndio maana wanashauri kuku akilalia au ukitumia mashine uwe unayafuatilia kwa ile torch ili kujua kama yaendelee kuhatamiwa au yageuzwe chakula. Wataalamu wanasema siku ya 7 au 8 utakuwa ushajua kama ule au yahatamiwe.

Test kupasua hata 1 uone kama yashakuwa takataka.
 
Unapimaje kwa mwanga?
 
Jamani nina Bata wangu 2 majike wanataga mayai mengi lakini bado akilalia wanayala yote Kama yakibaki basi mayai 3au 2.
Swali langu Kwanini wanakula mayai?
Na niwafanyaje ili wasiyale?
 
Habari zenu wakuu naomba mwenye elimu zaid juu ya ujenz wa banda la kufugia kuku liweje anipe abc, kiu yangu nifuge nusu huria.
Pia kama kuna mchoro wa banda anitumie ninataka kujenga kwa kutumia tofali za udongo
 
View attachment 1489822

Nimeanza ufugaji wa kuku wa kienyeji, bado sija survey soko la kuku wa kienyeji likoje.
Kama kuna mtu mwenye uzoefu na hili anishauri, pros and cons etc.

By the way, nimeanza na Jogoo mmoja, ila natarajia kuongeza kuku within a week, projections ni kuwa na kuku 1,000, hapo ndio nianze kuuza, matarajio yangu ni kuuza via interent - hapa nalenga watu wa DAR, ambao wako bize, I can do delivery maofisini within city center, na baadae kuweka vituo vya kufanya pickup wakati watu wanarudi home jioni, e.g Mwenge Junction, Morocco Petrol Station, etc. Malipo via M-Pesa, SMS banking pia na mahoteli.

Sitarajii faida ya haraka, naomba ushauri kwa wale walifanya biashara hii, au wanajua mtu wa karibu aliyeifanya.
Ni marajio yangu na mimi pia nitafaidika

Sent from my itel A11 using JamiiForums mobile app
 
Naomba kupatiwa sehemu nayoweza kupata kuku wakienyeji 5000 vifaranga wakubwa
Nunua majike 20 na jogoo 3, hao vifaranga 5,000 utawapata chini ya mwaka mmoja.

Andaa sehemu zao za kutagia,

Vifaranga vikianguliwa andaa nursery, uwatenge na mama zao ndani ya wiki mbili.
 
Hakuna yai asili la kuku wa kienyeji dar! Yai asili linatokana na kuku huria, hao wa dar ni zero glaze, formula meal, mayai ndani kiini cha njano hakuna.
Kiini cha njano hakina uhusiano wa moja kwa moja na uzururaji wa kuku bali hutokana na majani au mbogamboga (za kijani) anazokula kuku. Unaweza kumfuga kuku "zero grazing" na akawa na mayai ya njano na matamu kuliko huyo anayezurura.

Mradi wangu kwa mfano, kuku wanafugwa ndani ila kuna bustani maalum kwa ajili yao. Hayo mayai ukianza tu kutumia hautoki!
IMG_20201220_154318_271.jpg
IMG_20201219_122632_798.jpg
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom