Mkuu mbona kisa siku mnaambiwa namna ya kuweka tangazo ili likae kibiashara lakini mnarudia yaleyale!?
Hakuna price, location, contacts, delivery mechanism, yanauzwa kwa kiasi gani ...
Hata hivyo matangazo yana jukwaa lake
Kila la heri

sawa mkuu,namba ya simu ni 0653 685339. Yanapatikana maeneo ya kijichi,ukiwa sehemu inayofikika kiurahisi unaweza ukaletewa.
 
KWA MTU ANAYETAKA INCUBATOR ZA AINA YOYOTE ANAWEZA KUNITAFUTA KWA EMAIL honestaugustine@yahoo.com NITAWEZA KUFANYA MPANGO WA YEYE KUPATA INCUBATOR KUANZIA 8EGGS NA KUENDELEA KWA BEI NZURI KULIKO ZOTE AMBAZO MMESHAWAHI KUSIKIA. HIGH QUALITY UHAKIKA WA KUTOTOA KWA MASHINE 95%. TUWASILIANE KWA QUOTATION ZA BEI. UTATAKIWA KUSUBIRI 1MONTH TU. ASANTENI

hizo incubator zinatotolesha baada ya muda gani.? na ingekuwa vizuri kama ungeorodhesha bei ya incubator na uwezo wake wa kutotolesha. pia ingekuwa vizuri zaidi kama ungeainisha power consumption zake.
 
Hay Gazeti asante sana kwa ushauri wako wa ufugaji wa wakuku wa kienyeji nimefurahishwa na uchanganuzi uliotoa nami napenda sana kufuga kuku nitafuatilia kwa makini njia zote ulizotoa ili niweze kufanikisha azma yangu hii

endapo nitashindwa kufanikisha nitataka ushauri zaidi ili niweze kufanikishajambo hili kwani ni bora kujiajiri kuliko kuendelea kuakaa na vyeti kungoja kuajiriwa hakupo ingawaje nimeshaajiriwa
aksante sana
 
aksante kwa maujuzi mkuu,,,naomba kujua ka haya mayai yanawezwa kuanguliwa na incubators,,,na bei za incubator vipi zinaendaje hasa za kutuimia mafuta ya taa,,,aksante sana
 
Hiki kitu kinawezekana sana kwa watu wenye maono na uvumilivu.
Nakubaliana kabisa tena umenikumbusha mambo meng sana ambayo nilisoma O'level kwenye somo la Kilimo.
Binafsi niko mbioni kufungua kampuni ambayo moja ya malengo yake ni ufugaji wa kuku.
Asante mkuu!
 
Wazo hili nalikubali na naamini litanisaidia sana katika mpango wangu wa kujikwamua na maisha. Hakika wewe ni mtumishi wa Mungu tena mwenye bidii na upendo wa dhati kwa wengine. Tuachane na wanasiasa wanaotupotezea muda wetu.
 
Asante sana mkuu. Naomba msaada kama naweza kupata version ambayo naweza kuprint ili niwatumie vijana kijijini ambako tulianzisha kikundi cha kufuga kuku kwa njia za kisasa naona maelezo yako yatawafaa sana maana kwenye ulezi wa vifaranga ndo kunawasumbua sana hivi nilikuwa najiandaa kumwalika bwana mifiko aende akawape semina lakini kwa vile mi niko dar na wao wako mkoani logistics zinasumbua sana. Tafadhari mkuu nisaidie kwa hilo
 
Hapa naomba msaada wana jamii mie mradi huu ninao lakini utunzaji wa kumbukumbu zake ndio unanipa shida, maana nafuga broilers na hawa wa kienyeji pia sasa ninapoanza hawa broilers kila nikiweka kumbukumbu za matumizi ya kila batch unakuta baadaye haya matumizi yanaingiliana kwa kuwa kuku wa batch hii wanajikuta wanatumia chakula na madawa ya hawa wengine kwa hiyo kutenganisha inakuwa vigumu kama kuna aliye na idea ya kuweka hizi kumbukumbu naomba msaada maana napenda njiue ni batch ipi imefanya vizuri na ipi haikufanya vizuri.
Nawasilisha!
 
mkuu nashukuru sana kwa mchanganuo kwa ni mradi mzuri na wenye tija. Mungu akubariki kwa kuto kuwa mchoyo wa mawazo mazuri na yenye faida kwa watanzania wote wasio kuwa wavivu...
 
Elimu nzuri..Ila kama mtu anakosa jiko la mkaa n.k,unaweza kutumia dumu: chemsha maji halafu chukua dumu la lita 20 na yaweke humo halafu funga kabisa liweke juu ya tofari ili vifaranga wasiungue,kwa kawaida dumu litatoa joto ambalo linawafaa sana vifaranga

Wakisogea karibu sana na dumu ujue joto halitoshi kwa hiyo maji hayakuchemshwa vizuri na wakikaa mbali sana na dumu ujue joto ni kali,ongeza tofali likae juu kidogo.

La msingi kuhusu banda ni vizuri kama una eneo la kutosha fuga nusu huria: jenga banda ambalo kuku watalala usiku halafu mchana wanakaa ndani ya uzio na hiyo itapunguza gharama za usafi na pia kuku watapata mazoezi.Zingatia pia kwamba hawa ni kuku wa kienyeji kwa hiyo unaweza kuwaachia wakatoka nje kabisa ya uzio ili wapate chakula kama wadudu wanaoruka na wanaotambaa.

Nitarudi baadae.........

Umeniongezea kitu mkuu sikuwa nalijua hili la dumu. Big up
 
Snochet,

Ahsante sana, hii ni mada nzuri sana, na nakupa hongera.

Naomba mwenye utaalaam wa ufugaji wa samaki atuwekee ujuzi hapa.
 
tafadhali mwunwana mmoja ajitolee kunifundisha kutengeneza 'chick starter' na vyakula vingine ili nipunguze gharama za uendeshaji wa mradi wangu
 
Jamani ndugu zangu wa JF nina hitaji mtu anayetotolesha mayai ya kuku wa kienyeji kwa bei ngapi na all information nahitaji kufuga kukuwengi iwezekanavyo
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom