Jamani kifaranga changu sijui kimefanyaje naona anachechemea mguu mmoja haugusi chini ,sijui nifanyaje
Hongera sana sana hata mimi nimeamua kuwekeza kwenye Ufugaji wa Kuku wa kienyeji, nimejaribu kufuatilia nikakuta kuna soko zuri kama utachangamka! Nimejenga banda la ukubwa wa Mita 26 kwa upana wa nne, plan yangu ni kufuga kuku kama 2000 hivi, na mimi pia nimejifunza mengi ya ufugaji hapa hapa jukwaani, nikaona kumbe kuna utajiri upo tuna ukalia tu. Na mimi naahidi kuwaletea updates. kwa sasa banda limekamilika
Congraturation kwa hatua uliyo fikia mimi pia ni mfugaji" kuhusu hayo matandiko ya kwenye banda nakushauri usipendelee kutumia maranda ya mbao ni vizuri ukatumia yale ya mchele maana nasikia kuna jinsi yanavyo athiri kwenye mfumo wa upumuaji wa kuku. Na kuhusu muda wa kuyatoa inategemea mi huwa natoa baada ya wiki baada ya kuona yamesha chafuka kiasi. Nakutakia kila lakheri mkuu.
Mkuukuku wako ni wa malawi??Naomba nianze kwa kushukuru sana JF kwa posts nyingi zinazohusu mambo ya ujasiriamali na hususan ufugaji. Nimejifunza mengi sana hapa. Pia nashukuru mitandao mingine kama vile Mkulima Young na Kilimo ni ujuzi (hivi ni vya Kenya). Baada ya kutafakari watu wanavyotengeneza hela kupitia ujasiriamali, na mimi nimeanza.
Kwa kuanza, nimeanza na vifaranga vya mwezi mmoja 50. Nimeamua kuchagua umri huu kwa sababu ni rahisi kuchagua kati ya tetea na jogoo. Hivyo mimi nimeweka ratio ya jogoo 1 kwa tetea 7. Nimechukua mbegu ya kienyeji ambayo imekuwa crossed (chotara) kwa maana ya mchanganyiko wa kienyeji ya hapa kwetu na wale wa Malawi na wale wa Afrika kusini). Nilivutiwa sana baada ya kuangalia kuku wakubwa kwa huyu jamaa ambaye nimenunua kutoka kwake, yaani utapenda.
Mwisho wa mwezi ujao natarajia kuongeza tena vifaranga vyenye umri wa mwezi mmoja kama nilivyofanya mwezi huu.
Kusema ukweli sina uzoefu mimi binafsi katika kazi hii, lakini nimesoma mengi kuhusu ufugaji wa kuku.
Naombeni uzoefu wenu wapendwa, kwa sasa mambo mengine nafanya kwa kuuliza kwa wazoefu. Ila baada ya miezi michache nitakuwa na uzoefu pia. Nina swali;
- Hivi zile randa tunazotandaza sakafuni inatakiwa ikae muda gani ndo nibadilishe niweke nyingine? Je ni kila siku au baada ya siku ngapi? Kwa sasa mimi natumia tuu uzoefu naangalia zikianza kuchafuka ndo nabadilisha (kwa hiyo yaweza kukaa siku tatu, nne au tano.
- Maswali mengine nitauliza kadiri nitakavyokutana na changamoto
Uko mkoa gani?
Nahitaji nami nipate hivyo vifaranga chotara huko ulikonunua
Waliopo dar mjooni tegeta kibaoni kona ya nyuki kuna mtaalm