UDSM: Tunaomba msaada wenu JF!

nimesoma nadhani siajelewa huo msaada wanaoutaka ndio maana nimeomba ayaweke in one post sound and clear (agenda kubwa ni kuzuia kugoma au kufukuzwa viongozi wao, au kuzuiwa kufanya uchanguzi)

yote kwa pamoja ... kikubwa ikiwa suala la uongozi wa chuo la kutaka kuwaamulia nani awe kiongozi wao.
 
Ninapata habari hapa kwamba wanafunzi wamezingira Utawala na hakuna kutoka wala kuingia .Je wewe unapata haya haya ninayo yapata ?
 
Wanafunzi Chuo Kikuu Dar waanza mgomo ili kurejeshwa Waziri Mkuu wao
Jackson Odoyo na Joymertha Ishengoma (www.mwananchi.co.tz)

WANAFUNZI wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) wameanza mgomo wa siku mbili kushinikiza uongozi wa chuo hicho umrudishe Waziri Mkuu wa Serikali ya Wanafunzi (Daruso), Julius Mtatiro na wanafunzi 19 waliosimamishwa masomo kwa makosa mbalimbali.

Mgomo wa wanafunzi hao ulianza rasmi jana majira ya saa 5:30 asubuhi,ambapo waliandama kutoka hosteli namba saba hadi Ukumbi wa Nkrumah na kuwatoa nje wanafunzi wote waliokuwa wanaendelea na masomo.

Wanafunzi hao waliendelea na utaratibu huo wa kuzunguka katika madarasa mbalimbali ya chuo hicho kwa lengo la kuwatafuta wanzao waliokuwa wanaenandelea na masomo kwa lengo la kuwatoa nje .

Mgomo huo uliambatana na maandamano ya kuzunguka chuo hicho huku wakiimba nyimbo mbalimbali zilizoashiria amani na mshikamano zikiwemo za "Mungu ibariki Tanzania, Tusipowatetea sisi ninani atakaye watetea na wasiporudishwa na sisi tufukuzwe".

Akizungumza na waandishi wa gazeti hili, mmoja wa wanafunzi hao, Joseph Emmanuel alisema uongozi wa chuo hicho unalengo la kuwanyima wenzao haki ya kusoma, kwa sababu hawawezi kuwachunguza wanafunzi hao wakiwa nje ya chuo.

Alisema mbali na kuwa nje ya chuo wanafunzi hao pia majina yao yameshapelekwa kituo cha polisi kwa ajiri ya kupelekwa mahakamani.

"Huu ni uonevu, haiwezekani waseme kuwa wanafunzi hao wanachunguzwa wakati huo huo majina yao yamepelekwa polisi tayari kwenda mahakamani," alisema Emmanuel.

Mwanafunzi mwingine, Sylvia Eric alisema uongozi wa chuo umeshindwa kuongoza kwa kutumia kanunu na utaratibu, badala yake wanatumia mabavu na kwamba kuna mambo mengi yanafanywa chuoni hapo yasiyofuata haki za binadamu.

Naye Rais wa Daruso, Deo Daudi alisema ingawa wanafunzi hao wamesimamishwa masomo, Bunge la Wanafunzi bado jakaa na kufikia mwafaka wa kufanyika kwa mgomo huo bali umeitishwa na wanafunzi wenyewe.

Naye Mkurugenzi wa Masomo ya Shahada ya Kwanza chuoni hapo, Profesa Florens Luoga alisema baadhi ya wanafunzi walisimamishwa kwa masomo kwa sababu ya makosa mbalimbali yakiwemo ya ubakaji.

Alisema kutokana na makosa hao, mgomo na maandamano hayo haviwezi kuushinikiza uongozi wa chuo kuwarudisha kabla ya sheria na utaratibu kufuata mkondo wake.
 
Nyie wana UDSM kwanza nina ushauri mmoja mkubwa"mwache nidhamu ya woga"FDR alisema "the only thing to fear is fear itself"Koba amesema mliandamana kusapoti ufisadi!sasa kweli ni kivipi wana jf wataweza kuwapa ushauri na mnajua jf ni anti fisadis?Mko wapi kwenye vilio vya mabadiliko ya katiba na nyie ndo wasomi tunaowategemea?Kwani hujui faculty inawakilisha serikali na propaganda zake?Hizi issue ziko mpaka kwenye shule za sekondari ambapo mafisadi wakuu wa shule wanazificha ratiba za mlo kutoka wizarani na kuwalisha wanafunzi maharagwe ya wadudu na mlo mbovu?Wakuu wa shule wanaweka pesa mfukoni na kuificha ratiba ya mlo kutoka wizarani zinazoonyesha kuwa wizara inatoa pesa za kutosha kuwalisha wanafunzi milo ya tofauti pamoja na matunda hapa na pale!Tunajua hayo kuanzia Same sekondari mpaka Lyamungo!Madai yenu hayatofautiani sana!Ni mikwaruzo ya ki haki dhidi ya utawala uanosimamia sera za serikali na chama tawala!Mpiganie nchi huru itakayotokana na katiba mpya!Inayojali haki na maslahi ya kila mwananchi bila ya vitisho na unyanyasajiHuo ni ushauri wangu tuu!
 
Wanafunzi Chuo Kikuu Dar waanza mgomo ili kurejeshwa Waziri Mkuu wao
Jackson Odoyo na Joymertha Ishengoma (www.mwananchi.co.tz)

WANAFUNZI wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) wameanza mgomo wa siku mbili kushinikiza uongozi wa chuo hicho umrudishe Waziri Mkuu wa Serikali ya Wanafunzi (Daruso), Julius Mtatiro na wanafunzi 19 waliosimamishwa masomo kwa makosa mbalimbali.

Mgomo wa wanafunzi hao ulianza rasmi jana majira ya saa 5:30 asubuhi,ambapo waliandama kutoka hosteli namba saba hadi Ukumbi wa Nkrumah na kuwatoa nje wanafunzi wote waliokuwa wanaendelea na masomo.

Wanafunzi hao waliendelea na utaratibu huo wa kuzunguka katika madarasa mbalimbali ya chuo hicho kwa lengo la kuwatafuta wanzao waliokuwa wanaenandelea na masomo kwa lengo la kuwatoa nje .

Mgomo huo uliambatana na maandamano ya kuzunguka chuo hicho huku wakiimba nyimbo mbalimbali zilizoashiria amani na mshikamano zikiwemo za "Mungu ibariki Tanzania, Tusipowatetea sisi ninani atakaye watetea na wasiporudishwa na sisi tufukuzwe".

Akizungumza na waandishi wa gazeti hili, mmoja wa wanafunzi hao, Joseph Emmanuel alisema uongozi wa chuo hicho unalengo la kuwanyima wenzao haki ya kusoma, kwa sababu hawawezi kuwachunguza wanafunzi hao wakiwa nje ya chuo.

Alisema mbali na kuwa nje ya chuo wanafunzi hao pia majina yao yameshapelekwa kituo cha polisi kwa ajiri ya kupelekwa mahakamani.

"Huu ni uonevu, haiwezekani waseme kuwa wanafunzi hao wanachunguzwa wakati huo huo majina yao yamepelekwa polisi tayari kwenda mahakamani," alisema Emmanuel.

Mwanafunzi mwingine, Sylvia Eric alisema uongozi wa chuo umeshindwa kuongoza kwa kutumia kanunu na utaratibu, badala yake wanatumia mabavu na kwamba kuna mambo mengi yanafanywa chuoni hapo yasiyofuata haki za binadamu.

Naye Rais wa Daruso, Deo Daudi alisema ingawa wanafunzi hao wamesimamishwa masomo, Bunge la Wanafunzi bado jakaa na kufikia mwafaka wa kufanyika kwa mgomo huo bali umeitishwa na wanafunzi wenyewe.

Naye Mkurugenzi wa Masomo ya Shahada ya Kwanza chuoni hapo, Profesa Florens Luoga alisema baadhi ya wanafunzi walisimamishwa kwa masomo kwa sababu ya makosa mbalimbali yakiwemo ya ubakaji.

Alisema kutokana na makosa hao, mgomo na maandamano hayo haviwezi kuushinikiza uongozi wa chuo kuwarudisha kabla ya sheria na utaratibu kufuata mkondo wake.

Yameshatokea!

Nafikiri nguvu iwekwe kuwatetea walioshitakiwa na kusubiri matokeo ya mgomo. Lakini wana-UDSM wanatakiwa wawe tayari muda wowote kutetea maslahi yao sio kuwa-suprised na matokeo! Hiyo (chuo) ni moja ya maeneo ambayo CCM inaiangalia kwa macho yote hivyo kujipanga vilivyo!
 
kabla hawajashinda kwenye uwanja wa kuzunguka majengo ni lazima washinde kwenye fikra. Ni lazima kama wasomi waoneshe wanachotaka nini na kwanini; they have to make a plausible and rational argument why the community should support them. To demand the reinstatement of their leader merely kama matakwa tu haitoshi; they have to have a rational basis for demanding such an action.

It is rather pathetic when educated (or soon to be educated) people use emotional response to rational problems.

Fanyeni kama walivyofanya wenzenu ATC, Posta, Mafisadi n.k they made their case, with names, figures, and numbers.. Ushauri wangu:

a. Chagueni watu watatu au wanne kati yenu ambao wanaweza kujenga hoja na kuziandika kiufasaha.

b. Waandike hoja za kujaza kurasa zisizozidi mbili.

c. Waelewe introduction ya mgogoro wa sasa wa Chuo Kikuu kwa kadiri wanavyouona wao.

d. Wafafanue kiini hasa cha mgogoro huo na kanuni au taratibu zilizokiukwa.

e. waeleze ni jinsi gani wamejaribu kutumia njia nyingine zote za kutatua mgogoro huo na zimeshindikana.

f. Na waelewe kwanini wameamua kuresort to demonstrations (ambayo ni haki yao).

g. Wasema ni nini wanachohitaji ni kitu gani.

Binafsi sijali sana ni idadi gani ya watu wanahusika. Hata kama wanafunzi 9990 watakuwa hawajali kinachoendelea na wakaendelea na masomo yao na wanafunzi 10 wakajitokeza kusema "this is not right" basi hawa kumi lazima wapewe nafasi ya kujenga hoja kuwashawishi wale 9990 waone kosa la wao kuendelea na status quo.

I believe it is only justice to give the minority a chance to air their grievances and concern as well as an opportunity to convince the majority why certain actions should be rescinded. Ni lazima waweze kujenga hoja yenye kuweza kushawishi.

Ni pale tu wanapoona hawapati nafasi ya kusikilizwa au kupewa nafasi ya kutoa concerns zao through regular and acceptable channels ndipo njia za civil disobedience zinapoanza kuingia ikiwemo demonstrations, sit-ins etc.

Na njia hizo zinapofeli, na ile injustice continues then measured and targeted violence is warranted.
 
CCM ni lazima wawe makini na UDSM!Hapo ndio chimbuko la mabadiliko halisi ya nchi pamoja na uwezekano wa kuwa ngome madhubuti dhidi ya ufisadi!Sasa ni vizuri tuhakikishe kuwa vijana wanarudi shule..na pia muwe chachu ya haki za binadamu!Muibebe katiba ya nchi na kuinyenyua juu popote pale mtakapokuwa mnanyanyaswa..katiba ndio mwongozo!Mahakamani,polisi,mbele za huyo professa..nyeyua katiba juu na muwasomee haki zenu!Na kama ina mapungufu muibadilishe!Sasa kama UDSM hawana namna ya kuipigia kelele serikali badala yake na wao ni victims licha ya usomi wao..vipi kuhusu mwanakijiji asiyejua lolote?Nani anasimamia haki zao?Nyie muonde vijijini mukaibadilishe nchi from the bottom up!na sio kukalia nidhamu ya woga na maslahi binafsi yanayotugawanya!
 
Kwenye msafara wa Mamba sio kenge tu waliopo hata na mijusi pia hujiunga. Tusiwalauma WaUDSM wote kwa sababu ya wachache waliosapoti ufisadi na wanaoenda kupewa 5000 na Makamba ili wamwimbie Diamond
 
Wanafunzi wa chuo kikuu wana utoto sana. Tanzania sasa ina vyuo vingi je ni kwanini UDS pekee ndiyo inamatatizo kila siku???.Wanafunzi acheni siasa na shukuru mungu kupata nafasi na soma bila elimu madogo mtadata na mko bongo. Vumilieni na someni ni miaka mitatu au minne tu hiyo miaka ni ya muhimu kuliko elimu yako ya miaka kumi iliyopita.Haya mambo ya siasa tuachieni sisi wengi tuko nje, wasomi na tunafanya vizuri. elimu ni ngumu na sisi wa nje tumesoma kwa shida sana na ningewashauri mpunguze siasa na muombe haki zenu kisomi na kwa hoja.
 
So what Mr Ant Ufisadi?
 
kabla hawajashinda kwenye uwanja wa kuzunguka majengo ni lazima washinde kwenye fikra. Ni lazima kama wasomi waoneshe wanachotaka nini na kwanini; they have to make a plausible and rational argument why the community should support them. To demand the reinstatement of their leader merely kama matakwa tu haitoshi; they have to have a rational basis for demanding such an action.

It is rather pathetic when educated (or soon to be educated) people use emotional response to rational problems.

Fanyeni kama walivyofanya wenzenu ATC, Posta, Mafisadi n.k they made their case, with names, figures, and numbers.. Ushauri wangu:

a. Chagueni watu watatu au wanne kati yenu ambao wanaweza kujenga hoja na kuziandika kiufasaha.

b. Waandike hoja za kujaza kurasa zisizozidi mbili.

c. Waelewe introduction ya mgogoro wa sasa wa Chuo Kikuu kwa kadiri wanavyouona wao.

d. Wafafanue kiini hasa cha mgogoro huo na kanuni au taratibu zilizokiukwa.

e. waeleze ni jinsi gani wamejaribu kutumia njia nyingine zote za kutatua mgogoro huo na zimeshindikana.

f. Na waelewe kwanini wameamua kuresort to demonstrations (ambayo ni haki yao).

g. Wasema ni nini wanachohitaji ni kitu gani.

Binafsi sijali sana ni idadi gani ya watu wanahusika. Hata kama wanafunzi 9990 watakuwa hawajali kinachoendelea na wakaendelea na masomo yao na wanafunzi 10 wakajitokeza kusema "this is not right" basi hawa kumi lazima wapewe nafasi ya kujenga hoja kuwashawishi wale 9990 waone kosa la wao kuendelea na status quo.

I believe it is only justice to give the minority a chance to air their grievances and concern as well as an opportunity to convince the majority why certain actions should be rescinded. Ni lazima waweze kujenga hoja yenye kuweza kushawishi.

Ni pale tu wanapoona hawapati nafasi ya kusikilizwa au kupewa nafasi ya kutoa concerns zao through regular and acceptable channels ndipo njia za civil disobedience zinapoanza kuingia ikiwemo demonstrations, sit-ins etc.

Na njia hizo zinapofeli, na ile injustice continues then measured and targeted violence is warranted.

mwanajj, you said it!!!!

Toka mwanzo nasoma haya mambo ya wanafunzi wa UDSM............ Ninaona they are defeated by purpose! Wanatakiwa kutueleza mwanzo hadi mwisho tuelewe ili tuwape support inayoeleweka. Mwenye kuweka thread naona hayupo tena.

Otherwise wakasome, they are burning my P.A.Y.E.
 
Wanafunzi wa chuo kikuu wana utoto sana. Tanzania sasa ina vyuo vingi je ni kwanini UDS pekee ndiyo inamatatizo kila siku???.Wanafunzi acheni siasa na shukuru mungu kupata nafasi na soma bila elimu madogo mtadata na mko bongo. Vumilieni na someni ni miaka mitatu au minne tu hiyo miaka ni ya muhimu kuliko elimu yako ya miaka kumi iliyopita.Haya mambo ya siasa tuachieni sisi wengi tuko nje, wasomi na tunafanya vizuri. elimu ni ngumu na sisi wa nje tumesoma kwa shida sana na ningewashauri mpunguze siasa na muombe haki zenu kisomi na kwa hoja.

kamundu,

Hii attitude ya kuvumilia tu yapite ndiyo inasababisha mafisadi wanafanya ufisadi kwa sababu wanajua kuwa watanzania kama ilivyo kawaida yao watavumilia tu.

Wanafunzi wa UD lazima wajifunze kutetea haki zao kabla ya kutoka chuoni ili wapambane na kina Rostam Azizi huko mitaani
 
Back
Top Bottom