DOKEZO UBORA WA ELIMU inayotolewa Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA) unatia shaka

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
A

Anonymous

Guest
Wakuu, Heri ya mwaka mpya 2024.

Barua hii ni taarifa kuhusu ubora wa elimu inayotolewa katika Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA) kwa ufundishaji na utoaji wa masomo ya Shahada za elimu zenye masomo ya Fizikia yaani, BSc. Education (Physics and Chemistry), BSc. Education (Physics and Mathematics), BSc. Education (Physics and ICT) na BSc. Education (Physics and Geography).

Waraka huu ni mahsusi kwa wafuatao;
  1. Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mh. Prof Adolf Mkenda,
  2. Naibu Waziri, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia,. Prof. Omary Kipanga,
  3. Katibu Mkuu, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Carolyne Nombo,
  4. Naibu Katibu Mkuu, Sayansi, Prof. James Mdoe,
  5. Naibu Katibu Mkuu, Dkt. Franklin Rwezimula,
  6. Katibu Mkuu,Tume ya Vyuo Vikuu, TCU, Prof. Charles Kihampa,
  7. Makamu mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine (SUA), Prof. Raphael Chibunda,
  8. Naibu Makamu Mkuu wa Chuo (SUA), Taaluma, Prof. Maulid Mwatawala,
  9. Watanzania wote wenye mapenzi mema na elimu na maendeleo ya nchi yetu.
Wasalaam!.

Kwanza napenda kutoa preamble kuwa sitoi taarifa hii kwa umma kwa lengo la kuichafua SUA, au uongozi wake, bali kuipa serikali taarifa muhimu kwa kuwa Chuo Kikuu ndiyo mahali panapotoa watalaamu mbalimbali kwa maendeleo ya Taifa.

Nimeandika haya mambo kuhusu elimu ya shahada za fizikia zinatolewa SUA, baada ya kufanya uchunguzi wa kutosha na kubaini uhujumu katika elimu inayotokewa kwa wanafunzi hao ambao baada ya kuhitimu watakuwa waalimu katika Shule zetu za Serikali na binafsi.

Haya ni maandiko yangu mwenyewe na ndani yake kuna taarifa nimeziandika kama niivyopokea kutoka kwa mwanafunzi aliyeko SUA akisoma kozi husika.

Shahada ya Elimu kwa masomo ya Fizikia ilianza kutolewa na SUA mwaka 2020, kipindi hicho SUA ikiwa na Wakufunzi wawili tu, huku wanafunzi wakiwa takribani 75 wa mwaka wa kwanza.

Katika kufuatilia Chuo kikuu kiliwezaje kudahili wanafunzi huku kikiwa hakikidhi matakwa na tume ya vyuo vikuu kama angalau wawe na PhD holder mmoja wa kozi husika, Maabara, Vifaa vya maabara, N.K., nikagundua kuwa baadhi ya viongozi wakati huo walikuwa wakidanganya TCU kuwa wana rasilimaliwatu wa kutosha kuweza kufundisha kozi husika wakati siyo ukweli.

Katika miaka mitatu tokea 2020 hadi 2023, Chuo kimekuwa kikitegema wakufunzi wa kuazima(Majina ya wakufunzi husika ninayo) kutoka Chuo cha Kiislamu Morogoro, (MUM) na UDSM. Hii imepelekea wanafunzi kupata elimu chini ya kiwango kwa kuwa wale wakufunzi wawlli waajiriwa wa SUA na hawa wa kuazimwa kwa muda wawili bado hawakukidhi idadi ya wanafunzi muda huo wakiwa wamedahili mara tatu

Baada ya kuona hakuna mwelekeo wa uendelevu wa kozi hii huku wakiwa wanafundisha kama sekondari kwa kuwa hata maabara ya Fizikia haikidhi kuitwa ya kiwango cha Chuo kikuu. Wale wakufunzi wawili walihama mmoja akaenda UDOM (huyu hakuwa na mahusiano mazuri na mkuu wa idara wakati huo, hii ni habari ndefu sana) hii ikiwa ni mwanzo wa mwaka huu 2023, mwingine akaenda chuo cha maji Dar es Salaam (huyu habari yake ni ndefu kidogo sababu ya kuhama SUA) mwezi May mwaka huu.

Shida kubwa ilitokea baada ya hao waalimu wawili waajiriwa wa SUA kuhamia vyuo na taasisi zingine, maana walibaki wale wakufunzi wawili wa kuazima (part timers) tu huku idadi ya wanafunzi ikiwa zaidi ya 250. Hali hii ilipelekea muhula wa pili wa mwaka 2023 kumalizwa kuwa kuunga unga, huku pia ikipelekea uongozi wa Chuo ukiacha kufanya udahili wa kozi husika kwa mwaka 2023- 2024.

KWANINI NAANDIKA WARAKA HUU KUHUSU UBORA WA ELIMU INAYOTOLEWA SUA?

(i) Kwa sasa kuna kozi ya fizikia inafundishwa na mtu asiye na taaluma ya fizikia kabisa, kozi hiyo inafundishwa na mtu mwenye PhD ya chemistry huku akiwa hana uwezo wa kufundisha fizikia. Hii imepelekea kuamini kuwa hata mkuu wa Idara ya Kemia na Fizikia anahusika na uhujumu huu wa elimu kwetu wanafunzi, kwa kuwa mwalimu huyu hana vigezo wala uwezo wa kuweza kufundisha kozi hii. Nimefatilia na kujiridhisha kuwa mtu huyo hata masters hakusoma Fizikia bali Kemia MBAYA ZAIDI PhD yake ni Kemia pia.

Tunaomba mamlaka zifatilie ni sifa gani zimetumika mtu huyu kupewa vipindi vya masomo asiyohusika nayo kitaaluma.

Pia ijulikane ni kwa vigezo gani anafundisha kozi za fizikia?

Kama hiyo haitoshi, mtu huyu huyu pia anahusika na kozi za maabara za physics huku hata mwenyewe akiwa anaongea imeonyesha kuwa alisoma fizikia zamani sana na kwa sasa amewekeza nguvu kwenye kemia ndiyo maana alisoma PhD ya medicinal plants hapahapa SUA, idara hiihii anayofanyia kazi.

Hivyo, tunapata shida sana kuelewa ni nani ameamua kutufanyia hivi sisi watanzania kwa kutoa elimu chini ya kiwango kwa level ya degree? Naamini uongozi wote wa kitaaluma unajua jambo hili kuwa Chuo hakikidhi vigezo kutoa kozi hii sasa kwanini wasihamishe wanafunzi vyuo vingine?.

Mbona St. Joseph Songea ilifungiwa 2016 na wanafunzi wake wakasambazwa vyuo vingine na wamemaliza?. Sababu zote za kufungiwa vyuo vile kipindi kile kwa sasa zipo SUA na zimezidi viwango.

(ii) Tunafundishwa practical za fizikia chini kabisa ya kiwango, hasa baada ya wakufunzi wale wawili kuondoka hali imekua mbaya kwa wanafunzi wote, sawa tutafaulu (KWA KUWA INAJULIKANA SISI MATOKEO HAYA HUWA SI YETU, NI KUPANGWA TU HUKO IDARANI) lakini tutakuwa hatuna ujuzi wowote wa kumfundisha mtu ili aelewe fizikia ikoje. Hii inatokana na uwezo mdogo wa wahusika wa masomo ya maabara.

Tunachokumbuka ni mkufunzi mmoja alikuwa anapenda sana kazi za practical, sasa huyo kabla hajahamia UDOM, mambo ya maabara yalikuwa mazuri sana, na hata wenzetu wa mwaka wa tatu (alikuwa anaafundisha wao kipindi hajaondoka) wanatusimulia kila siku kuwa yule angekuwepo tungekuwa tunapata kitu maabara ila kwa sasa hakuna tunachopata wala kuelewa tofauti na kuandika report za vitu tusivyoelewa ili semester iishe.

Hawa waalimu na mkuu wa idara husika, Principal wa College, Naibu Makamu Mkuu wa Chuo (Taaluma) ni wahusika wakubwa katika kuhujumu elimu yetu, huku wakiwa na uhakika kuwa watoto wao hawasomi na sisi hapa kwa kiwango hiki kibaya, huku wakisahau kuwa wanatuandaa kuwa waalimu na huenda huko tutafundisha watoto au wajukuu zao wakati sisi wametupatia elimu mbovu isiyokuwa na ujuzi wowote.

(iii) Kuna wenzetu walisimamisha masomo mwaka wa kwanza kwa sababu mbalimbali, hawa waliporudi ili waendelee na masomo yao ya mwaka wa kwanza wakaambiwa waalimu wa kozi hizo hawapo, hivyo ikawalazimu wahamie kozi zingine wasizokuwa na malengo nazo tena kwa kulazimishwa na kupangiwa kozi ya kusoma.

Hali hii ilitokana na ukweli kuwa, Uongozi ulipoacha kufanya udahili wa mwaka wa kwanza mwaka huu, kozi za mwaka huo haziwezi kufundishwa tena, hivyo kama mwaka jana ulihairisha mwaka wa masomo ili uje uanze mwaka huu unakuta program haipo maana tumebaki mwaka wa pili na wa tatu tu.
HUU NI UONEVU MKUBWA KUWAHI KUTOKEA KWENYE ELIMU.

(iv) Matokeo ya wanafunzi kwenye kozi hayana uhalisia na kinachofundishwa, utakuta kuna kozi wanafunzi wamesoma asilimia 20 tu kati ya asilimia 100 ila wanatungiwa mtihani wa mwisho yaani UE na kufanya, kitu hiki kilitokea mwaka jana 2022 na mwaka huu kimeendelea pia, kozi hiyo ipo mwaka wa kwanza muhula wa pili.

Ili kuonyesha kuwa uongozi wa ndaki wala idara haujali wanafunzi hawa, imekuwa ni kawaida kuomba kikao na mkuu wa idara ila hatokei na mara chache akitokea kikaoni anaongea kisiasa tu na kukwepa hoja za msingi ila akishindwa kujibu maswali basi hidanganya anahitajika utawaa mkuu n akuondoka harudi tena.

(v) Kumekuwepo pia na kashfa kadhaa ikiwemo masuala ya rushwa kati ya baadhi ya waalimu yanayokwamisha ubora wa elimu SUA.

Mfano, kuna binti amekuwa best student miaka mitatu yote ya masomo yake, lakini ukweli ni kwamba binti huyo ana uhusiano na mmoja wa waalimu hapa idarani na uwezekano wa kuwa anapewa mitihani ni mkubwa sana.
Hii iitokea kwa binti mwingine pia, yeye alimaliza 2021 alikuwa na uhusiano na mwakimu wake wa kozi mojawapo ya hesabu, hata project ni mwalimu huyo alijitahidi mwanfunzi apate A na alipata, anaendelea na masomo yake ya masters lakini michezo yao yote inajulikana na uongozi wa idara husika ila hatua hazichukuliwi.

MAPENDEKEZO
Tunaomba Uongozi wa Chuo na wizaya ya elimu, sayasi na teknolojia kutuhamishia vyuo vingine kama UDSM au UDOM, ambako tuna uhakika na elimu yao kuliko hapa SUA.

Ni mimi,
MTANZANIA MPENDA NCHI YANGU.
KWA SASA MOROGORO.
 
Yani umemaliza kidato Cha sita ukafaulu vizuri, eti uje ushindwe kufundisha secondary.

Anyway, TCU fuatilieni elimu inayotolewa vyuo vikuu vyote.
Usiangalie hapa TU inua macho tazama mbali watu wengine Wanataka kufika mbali wawe na ma masters na kuendelea huko itakuwaje kama Kuna vitu basic wamevikosa hapo kwenye degree hizo
 
Wakuu,Heri ya mwaka mpya 2024.

Barua hii ni taarifa kuhusu ubora wa elimu inayotolewa katika Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA) kwa ufundishaji na utoaji wa masomo ya Shahada za elimu zenye masomo ya Fizikia yaani, BSc. Education (Physics and Chemistry), BSc. Education (Physics and Mathematics), BSc. Education (Physics and ICT) na BSc. Education (Physics and Geography).
Waraka huu ni mahsusi kwa wafuatao;
  1. Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mh. Prof Adolf Mkenda,​
  2. Naibu Waziri, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia,. Prof. Omary Kipanga,​
  3. Katibu Mkuu, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Carolyne Nombo,​
  4. Naibu Katibu Mkuu, Sayansi, Prof. James Mdoe,​
  5. Naibu Katibu Mkuu, Dkt. Franklin Rwezimula,​
  6. Katibu Mkuu,Tume ya Vyuo Vikuu, TCU, Prof. Charles Kihampa,​
  7. Makamu mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine (SUA), Prof. Raphael Chibunda,​
  8. Naibu Makamu Mkuu wa Chuo (SUA), Taaluma, Prof. Maulid Mwatawala,​
  9. Watanzania wote wenye mapenzi mema na elimu na maendeleo ya nchi yetu.​
Wasalaam!.

Kwanza napenda kutoa preamble kuwa sitoi taarifa hii kwa umma kwa lengo la kuiochafua SUA, au uongozi wake, bali kuipa serikali taarifa muhimu kwa kuwa Chuo Kikuu ndiyo mahali panapotoa watalaamu mbalimbali kwa maendeleo ya Taifa.

Nimeandika haya mambo kuhusu elimu ya shahada za fizikia zinatolewa SUA, baada ya kufanya uchunguzi wa kutosha na kubaini uhujumu katika elimu inayotokewa kwa wanafunzi haoa ambao baada ya kuhitimu watakuwa waalimu katika Shule zetu za Serikali na binafsi.

Haya ni maandiko yangu mwenyewe na ndani yake kuna taarifa nimeziandika kama niivyopokea kutoka kwa mwanafunzi aliyeko SUA akisoma kozi husika.

Shahada ya Elimu kwa masomo ya Fizikia ilianza kutolewa na SUA mwaka 2020, kipindi hicho SUA ikiwa na Wakufunzi wawili tu, huku wanafunzi wakiwa takribani 75 wa mwaka wa kwanza.

Katika kufuatilia Chuo kikuu kiliwezaje kudahili wanafunzi huku kikiwa hakikidhi matakwa na tume ya vyuo vikuu kama angalau wawe na PhD holder mmoja wa kozi husika, Maabara, Vifaa vya maabara, N.K., nikagundua kuwa baadhi ya viongozi wakati huo walikuwa wakidanganya TCU kuwa wana rasilimaliwatu wa kutosha kuweza kufundisha kozi husika wakati siyo ukweli.

Katika miaka mitatu tokea 2020 hadi 2023, Chuo kimekuwa kikitegema wakufunzi wa kuazima(Majina ya wakufunzi husika ninayo) kutoka Chuo cha Kiislamu Morogoro, (MUM) na UDSM. Hii imepelekea wanafunzi kupata elimu chini ya kiwango kwa kuwa wale wakufunzi wawlli waajiriwa wa SUA na hawa wa kuazimwa kwa muda wawili bado hawakukidhi idadi ya wanafunzi muda huo wakiwa wamedahili mara tatu

Baada ya kuona hakuna mwelekeo wa uendelevu wa kozi hii huku wakiwa wanafundisha kama sekondari kwa kuwa hata maabara ya Fizikia haikidhi kuitwa ya kiwango cha Chuo kikuu. Wale wakufunzi wawili walihama mmoja akaenda UDOM (huyu hakuwa na mahusiano mazuri na mkuu wa idara wakati huo, hii ni habari ndefu sana) hii ikiwa ni mwanzo wa mwaka huu 2023 ,mwingine akaenda chuo cha maji dar es salaam (huyu habari yake ni ndefu kidogo sababu ya kuhama SUA) mwezi may mwaka huu.

Shida kubwa ilitokea baada ya hao waalimu wawili waajiriwa wa SUA kuhamia vyuo na taasisi zingine, maana walibaki wale wakufunzi wawili wa kuazima (part timers) tu huku idadi ya wanafunzi ikiwa zaidi ya 250. Hali hii ilipelekea muhula wa pili wa mwaka 2023 kumalizwa kuwa kuunga unga, huku pia ikipelekea uongozi wa Chuo ukiacha kufanya udahili wa kozi husika kwa mwaka 2023- 2024.

KWANINI NAANDIKA WARAKA HUU KUHUSU UBORA WA ELIMU INAYOTOLEWA SUA?

(i) Kwa sasa kuna kozi ya fizikia inafundishwa na mtu asiye na taaluma ya fizikia kabisa,kozi hiyo inafundishwa na mtu mwenye PhD ya chemistry huku akiwa hana uwezo wa kufundisha fizikia. Hii imepelekea kuamini kuwa hata mkuu wa Idara ya Kemia na Fizikia anahusika na uhujumu huu wa elimu kwetu wanafunzi, kwa kuwa mwalimu huyu hana vigezo wala uwezo wa kuweza kufundisha kozi hii. Nimefatilia na kujiridhisha kuwa mtu huyo hata masters hakusoma Fizikia bali Kemia MBAYA ZAIDI PhD yake ni Kemia pia.

Tunaomba mamlaka zifatilie ni sifa gani zimetumika mtu huyu kupewa vipindi vya masomo asiyohusika nayo kitaaluma.

Pia ijulikane ni kwa vigezo gani anafundisha kozi za fizikia?

Kama hiyo haitoshi, mtu huyu huyu pia anahusika na kozi za maabara za physics huku hata mwenyewe akiwa anaongea imeonyesha kuwa alisoma fizikia zamani sana na kwa sasa amewekeza nguvu kwenye kemia ndiyo maana alisoma PhD ya medicinal plants hapahapa SUA, idara hiihii anayofanyia kazi.

Hivyo, tunapata shida sana kuelewa ni nani ameamua kutufanyia hivi sisi watanzania kwa kutoa elimu chini ya kiwango kwa level ya degree?,Naamini uongozi wote wa kitaaluma unajua jambo hili kuwa Chuo hakikidhi vigezo kutoa kozi hii sasa kwanini wasihamishe wanafunzi vyuo vingine?.

Mbona St. Joseph Songea ilifungiwa 2016 na wanafunzi wake wakasambazwa vyuo vingine na wamemaliza?. Sababu zote za kufungiwa vyuo vile kipindi kile kwa sasa zipo SUA na zimezidi viwango.

(ii) Tunafundishwa practical za fizikia chini kabisa ya kiwango, hasa baada ya wakufunzi wale wawili kuondoka hali imekua mbaya kwa wanafunzi wote, sawa tutafaulu (KWA KUWA INAJULIKANA SISI MATOKEO HAYA HUWA SI YETU,MI KUPANGWA TU HUKO IDARANI) lakini tutakuwa hatuna ujuzi wowote wa kumfundisha mtu ili aelewe fizikia ikoje.,Hii inatokana na uwezo mdogo wa wahusika wa masomo ya maabara.

Tunachokumbuka ni mkufunzi mmoja alikuwa anapenda sana kazi za practical, sasa huyo kabla hajahamia UDOM, mambo ya maabara yalikuwa mazuri sana, na hata wenzetu wa mwaka wa tatu (alikuwa anaafundisha wao kipindi hajaondoka) wanatusimulia kila siku kuwa yule angekuwepo tungekuwa tunapata kitu maabara ila kwa sasa hakuna tunachopata wala kuelewa tofauti na kuandika report za vitu tusivyoelewa ili semester iishe.

Hawa waalimu na mkuu wa idara husika, Principal wa College, Naibu Makamu Mkuu wa Chuo (Taaluma) ni wahusika wakubwa katika kuhujumu elimu yetu, huku wakiwa na uhakika kuwa watoto wao hawasomi na sisi hapa kwa kiwango hiki kibaya, huku wakisahau kuwa wanatuandaa kuwa waalimu na huenda huko tutafundisha watoto au wajukuu zao wakati sisi wametupatia elimu mbovu isiyokuwa na ujuzi wowote.

(iii) Kuna wenzetu walisimamisha masomo mwaka wa kwanza kwa sababu mbalimbali, hawa waliporudi ili waendelee na masomo yao ya mwaka wa kwanza wakaambiwa waalimu wa kozi hizo hawapo, hivyo ikawalazimu wahamie kozi zingine wasizokuwa na malengo nazo tena kwa kulazimishwa na kupangiwa kozi ya kusoma.
Hali hii ilitokana na ukweli kuwa, Uongozi ulipoacha kufanya udahili wa mwaka wa kwanza mwaka huu, kozi za mwaka huo haziwezi kufundishwa tena, hivyo kama mwaka jana ulihairisha mwaka wa masomo ili uje uanze mwaka huu unakuta program haipo maana tumebaki mwaka wa pili na wa tatu tu.
HUU NI UONEVU MKUBWA KUWAHI KUTOKEA KWENYE ELIMU.

(iv) Matokeo ya wanafunzi kwenye kozi hayana uhalisia na kinachofundishwa, utakuta kuna kozi wanafunzi wamesoma asilimia 20 tu kati ya asilimia 100 ila wanatungiwa mtihani wa mwisho yaani UE na kufanya, kitu hiki kilitokea mwaka jana 2022 na mwaka huu kimeendelea pia, kozi hiyo ipo mwaka wa kwanza muhula wa pili.

Ili kuonyesha kuwa uongozi wa ndaki wala idara haujali wanafunzi hawa, imekuwa ni kawaida kuomba kikao na mkuu wa idara ila hatokei na mara chache akitokea kikaoni anaongea kisiasa tu na kukwepa hoja za msingi ila akishindwa kujibu maswali basi hidanganya anahitajika utawaa mkuu n akuondoka harudi tena.

(v) Kumekuwepo pia na kashfa kadhaa ikiwemo masuala ya rushwa kati ya baadhi ya waalimu yanayokwamisha ubora wa elimu SUA.
Mfano, kuna binti amekuwa best student miaka mitatu yote ya masomo yake, lakini ukweli ni kwamba binti huyo ana uhusiano na mmoja wa waalimu hapa idarani na uwezekano wa kuwa anapewa mitihani ni mkubwa sana.
Hii iitokea kwa binti mwingine pia, yeye alimaliza 2021 alikuwa na uhusiano na mwakimu wake wa kozi mojawapo ya hesabu, hata project ni mwalimu huyo alijitahidi mwanfunzi apate A na alipata, anaendelea na masomo yake ya masters lakini michezo yao yote inajulikana na uongozi wa idara husika ila hatua hazichukuliwi.

MAPENDEKEZO
Tunaomba Uongozi wa Chuo na wizaya ya elimu, sayasi na teknolojia kutuhamishia vyuo vingine kama UDSM au UDOM, ambako tuna uhakika na elimu yao kuliko hapa SUA.

Ni mimi,
MTANZANIA MPENDA NCHI YANGU.
KWA SASA MOROGORO.
Duh,
Hatari sana hii
 
Yote uliyoandika ni kweli.

SUA ni chuo kilichoamua kuuma elimu.

Wewe unampa mtu ana masters na phd ya chemistry kufundisha physics of the atom kweli?

Mwankuna unapoteza credibility,wewe ni wa kushindwa kuandaa japo slides umegawa badala yake umegawa wanafunzi kwenye groups ili wafanye presentation course nzima kweli?

Hii habari kwa sasa inaenda kwa Mkenda.
 
Mmemsikia gwajimaa baada ya miaka mitatu... Kiufupi elimu ya tanzania haina msaada haitakuwa na msaada ni kupotezeana muda kama tunashindwa kuandaa watoto na wakati ujao... Na tumebaki na siasa ngoja dunia ije itubadilishe
 
Kozi za phy si zimefutwa mwaka Jana
Hayo unayouliza mtoa dokezo amesema kwenye andiko lake.

Kwanza kitendo cha kufuta kozi si sawa,kama chuo kikuu wamejiaibisha,

Pili hawajafuta kozi,wameacha kudahili mwaka wa masomo 2023/24,wale wanafunzi waliobaki ndiyo wako wanapigwa brush kiakademia.
 
Mada ni nzuri iliyojaa facts ILA sio ya kushangaa sana,tatizo sisi middle class tunajifanya hatujui yaliyo na uhalisi kuhusu maisha ya lower class, tunaongea yanapotugusa sisi kwa sababu tuna uwezo huo, royal families watoto wao hadi vitukuu vyao havisomi hapa nchini, maana baba/mama zao wameua ubora wa elimu hapa nchini kwa makusudi mazima,ili wao wasomeshe watoto wao nje ya nchi (yenye ubora),ili status ago iendelee hapa nchini, tujiulize why waliua zile FTCs zilizokua zinatupatia elimu bora mno ya wataalamu wa ufundi?,hivi FTC ya Dar Tech na degree ya sasa pale pale chuoni ipi ni bora zaidi?,why waliua zile Teaching Diplomas kutoka Mkwawa CNE ambazo zilitupatia super teacher's wa science kwa level ya sekondari?ona sasa utopolo uliopo pale Mkwawa, why tuliua zile technical secondary school kama Moshi Tech,I Ifunda Tech?,tuangalie tuliko jikwaa sio kuangukia
 
Degree haina maana kwakweli vyuo vya kati ni muhimu zaidi, Arusha na must zilipokuwa zinatoa diploma tu ni tofauti na sasa zinapojitafuta kutoa kozi za degree yan ni bora elimu
 
Mada ni nzuri iliyojaa facts ILA sio ya kushangaa sana,tatizo sisi middle class tunajifanya hatujui yaliyo na uhalisi kuhusu maisha ya lower class, tunaongea yanapotugusa sisi kwa sababu tuna uwezo huo, royal families watoto wao hadi vitukuu vyao havisomi hapa nchini, maana baba/mama zao wameua ubora wa elimu hapa nchini kwa makusudi mazima,ili wao wasomeshe watoto wao nje ya nchi (yenye ubora),ili status ago iendelee hapa nchini, tujiulize why waliua zile FTCs zilizokua zinatupatia elimu bora mno ya wataalamu wa ufundi?,hivi FTC ya Dar Tech na degree ya sasa pale pale chuoni ipi ni bora zaidi?,why waliua zile Teaching Diplomas kutoka Mkwawa CNE ambazo zilitupatia super teacher's wa science kwa level ya sekondari?ona sasa utopolo uliopo pale Mkwawa, why tuliua zile technical secondary school kama Moshi Tech,I Ifunda Tech?,tuangalie tuliko jikwaa sio kuangukia
Mkuu kwa uongozi huu wa SUA,hakika wana dhamira mbaya kuhusu elimu ya hawa madogo.

Mimi niko SUA hapa,aliyosema mtoa mada ni kweli 100%.

Na mengine mabaya zaidi yapo.
 
Hayo unayouliza mtoa dokezo amesema kwenye andiko lake.

Kwanza kitendo cha kufuta kozi si sawa,kama chuo kikuu wamejiaibisha,

Pili hawajafuta kozi,wameacha kudahili mwaka wa masomo 2023/24,wale wanafunzi waliobaki ndiyo wako wanapigwa brush kiakademia.
Doooo pole kwao elimu ya Tanzania hasa vyuo vikuuu imekuwa ya ajabu sana, ahina standards wala framework ya standardisation yenye enforcement ya kutosha how come chuo kikuuu kilichoanzishwa mwaka 84 kianzishe kozi TCU wapitishe na hakuna walimu wala vifaa toshelevu? Tcu wako wapi
 
Mkuu kwa uongozi huu wa SUA,hakika wana dhamira mbaya kuhusu elimu ya hawa madogo.

Mimi niko SUA hapa,aliyosema mtoa mada ni kweli 100%.

Na mengine mabaya zaidi yapo.
Kwanini uongozi auna masikio? Wizara inaweza kufikiwa madogo wajitoe kwa ajili ya kesho yao kupiga kelelee kwa waziri wa elimu, undergraduate ndio msingi kama unataka kwenda elimu ya juu zaidi
 
Back
Top Bottom