Wanafunzi 34 wa Udaktari walioondolewa chuo (UDSM-MCHAS) waililia Wizara ya Elimu iwasaidie

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,308
5,460
Mwaka 2018 wakati Tume ya Taifa ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) ilipokuwa katika utaratibu wake wa ukaguzi wa vyuo vikuu Nchini ilibainika kuna vyuo ambavyo ama havikidhi vigezo au mazingira yake si salama kimasomo.

Uamuzi uliochukuliwa baada ya kubainika kutokidhi vigezo ilikuwa ni vyuo kufungwa, masomo kusimamishwa kwa muda au mabadiliko mengine kadhaa.

Sehemu ya waathirika wa ukaguzi huo ni waliokuwa wanasomea Udaktari wa “Doctor of Medicine” katika Chuo cha The Archbishop James University College (AJUCO) kilichopo Songea ambacho ni tawi la Chuo cha St. Augustine University of Tanzania (SAUT) cha Mwanza.

Baada ya ukaguzi, Wanafunzi wa AJUCO wanaosomea udaktari wakapewa nafasi ya kuchagua vyuo tofauti chuo husika hakikukidhi vigezo vya kuendelea kutoa elimu hiyo, wakatakiwa kuchagua kwenda Bugando (Mwanza) au Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).
dei.jpg

The Archbishop James University College (A JUCO)

ADA IKAWAPELEKA UDSM
Wengi wao waliamua kuchagua kuhamia UDSM ikidiwa kuwa waliangalia mazingira ya ada kwa wakati huo.

Inaelezwa kuwa Bugando ada ilikuwa Tsh. Milioni 4.5 wakati AJUCO ada ilikuwa Tsh. Milioni 3.1 huku UDSM ambacho ni chuo cha Serikali ada yake ilikuwa Tsh. Milioni 1.8.

Hivyo, wanafunzi wa AJUCO wakahamia UDSM lakini katika tawi la Mbeya linalotambulika kwa jina la The University of Dar es Salaam Mbeya College of Health and Allied Sciences (UDSM-MCHAS).

Baada ya kufika UDSM- MCHAS, wale wanafunzi wa Mwaka wa Tatu ambao walianza chuo Mwaka 2015, wakatakiwa kupitishwa katika ‘crash program’ ili kufikia viwango ambavyo UDSM walihitaji kwa sababu kila chuo huwa kinakuwa na vigezo na viwango vyake.

Wanafunzi hao wakaambiwa watapita katika program hiyo kwa muda wa miezi mitatu, lakini haikuwa hivyo, badala yake wakaendelea kusoma kwa takribani mwaka mmoja zaidi ya ilivyopangwa awali.

Baada ya takribani miezi kadhaa wakarejeshwa darasani lakini wakarudishwa kusoma Mwaka wa Tatu badala ya kuendelea na Mwaka wa Nne.

Hali hiyo inadaiwa ikawarudisha nyuma kimasomo kwa asilimia kubwa japokuwa wapo ambao waliamua kupambana katika mazingira hayohayo kuendelea kusoma masomo ya mbele huku wengine wakibaki nyuma.
Mbeya11.JPG

The University of Dar es Salaam Mbeya College of Health and Allied Sciences (UDSM-MCHAS)

BARUA ZATOLEWA
Kutokana na ratiba kuonesha kuwa muda ambao Mwanafunzi anatakiwa kusoma Doctor of Medicine kuwa ni miaka mitano na ikizidi anaongezwa miwili hivyo jumla kuwa 7, kufikia Desemba 2022 wakawa wamefikia ukomo wa muda wa wao kuendelea kuwa chuoni.

Ndipo zikaandaliwa barua za kuonesha kuondolewa chuoni na zikafikishwa chuoni Desemba 2022 na ilipofika Januari 2023 wanafunzi hao wakakabidhiwa barua zao za kuondolewa chuoni kigezo kikiwa ni muda kufika ukomo (time barred).

WAKATA RUFAA
Baada ya kukabidhiwa barua zao, Wanafunzi wakakata rufaa chuoni kupinga wao kuondolewa chuoni, lakini majibu yaliyotoka msimamo ukawa ni uleule.

WANAFUNZI WENGINE WAMETOBOA
Inaelezwa kuwa wanafunzi wa Doctor of Medicine wa mwaka husika ambao wanalalamika walikuwa zaidi ya 250, lakini ambao wamefukuzwa chuo kutokana na kigezo cha muda ni 34.

Wanafunzi wengine walifanikiwa kuhitimu masomo yao Mwaka 2021 na wengine 2022 kwa kuwa walilazimika kwenda na kasi ya ziada wakati wakiwa chuoni hapo, kwamba walitumia muda wao wa ziada kusoma na kufanya mitihani bila kwenda na ratiba ambayo ilikuwepo wakati huo.

Hivyo, hao 34 walioondolewa chuo wao wanadai wamekuwa nyuma kutokana na changamoto kadhaa, wanazitaja changamoto kuwa ni;

Matokeo kutoka kuchelewa kutoka, wanadai hali hiyo ilikuwa ikiwarudisha nyuma na kushindwa kuendelea na masomo ya mbele.

Mafunzo katika vituo visivyo na vigezo, wanadai kuwa walipelekwa katika vituo vya afya ambavyo hazikidhi vigezo kwa mwanafunzi wa shahada kujifunza.

Idadi ya Wanafunzi kuwa wengi, wanaeleza kuwa hiyo ilisababisha wengi wao kutojifunza vema hasa masomo ya vitendo…

Kutokana na hali hiyo maombi yao kwa Wizara ya Elimu ni kuwasaidia kupewa muda wa ziada kumalizia masomo yao kwa kuwa muda walioupoteza hapo kati ndio umesababisha changamoto inayoendelea.

Wanadai kuwa mamlaka zinafahamu kilichotokea na walishazungumza na uongozi wa chuo chao kuhusu muda wao kupotezwa, wakaahidiwa watapewa nafasi lakini wanashangaa mamlaka zimewageuka licha ya kutambua changamoto iliyowatokea hapo kati.

TAMKO LA CHUO (MCHAS)
Mkuu wa Chuo cha MCHAS, Prof. Projestine Selestine Muganyizi anatoa ufafanuzi kwa kusema:

“Ninachofahamu ni kuwa chuo kina taratibu zake ambazo zinatumika kuwawezesha wanafunzi kusoma na kutimiza majukumu yao, ikiwemo hilo suala la muda, yote hayo yapo katika maandishi.

“Lakini pia hata kama mwanafunzi ana supplementary, hata anapofanya mara kadhaa akashindwa haimaanishi muda unasimama kumfidia yeye, hata hao wanafunzi wametolewa kwa mujibu wa taratibu za chuo.

“Kuhusu crash programs, sikuwepo wakati huo lakini ninavyoelewa unapokuwa katika utaratibu huo haikuzuii wewe kuendelea kusoma masomo yako mengine.

“Tuliwapokea wanafunzi zaidi ya 600, wengine wamehitimu na wengine bado wapo, kwa nini iwe wao tu hao 34, unatakiwa kujiuliza kuna jambo gani tofauti kuhusu wao?”
 
Mwaka 2018 wakati Tume ya Taifa ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) ilipokuwa katika utaratibu wake wa ukaguzi wa vyuo vikuu Nchini ilibainika kuna vyuo ambavyo ama havikidhi vigezo au mazingira yake si salama kimasomo.

Uamuzi uliochukuliwa baada ya kubainika kutokidhi vigezo ilikuwa ni vyuo kufungwa, masomo kusimamishwa kwa muda au mabadiliko mengine kadhaa.

Sehemu ya waathirika wa ukaguzi huo ni waliokuwa wanasomea Udaktari wa “Doctor of Medicine” katika Chuo cha The Archbishop James University College (AJUCO) kilichopo Songea ambacho ni tawi la Chuo cha St. Augustine University of Tanzania (SAUT) cha Mwanza.

Baada ya ukaguzi, Wanafunzi wa AJUCO wanaosomea udaktari wakapewa nafasi ya kuchagua vyuo tofauti chuo husika hakikukidhi vigezo vya kuendelea kutoa elimu hiyo, wakatakiwa kuchagua kwenda Bugando (Mwanza) au Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).
View attachment 2559137
The Archbishop James University College (A JUCO)

ADA IKAWAPELEKA UDSM
Wengi wao waliamua kuchagua kuhamia UDSM ikidiwa kuwa waliangalia mazingira ya ada kwa wakati huo.

Inaelezwa kuwa Bugando ada ilikuwa Tsh. Milioni 4.5 wakati AJUCO ada ilikuwa Tsh. Milioni 3.1 huku UDSM ambacho ni chuo cha Serikali ada yake ilikuwa Tsh. Milioni 1.8.

Hivyo, wanafunzi wa AJUCO wakahamia UDSM lakini katika tawi la Mbeya linalotambulika kwa jina la The University of Dar es Salaam Mbeya College of Health and Allied Sciences (UDSM-MCHAS).

Baada ya kufika UDSM- MCHAS, wale wanafunzi wa Mwaka wa Tatu ambao walianza chuo Mwaka 2015, wakatakiwa kupitishwa katika ‘crash program’ ili kufikia viwango ambavyo UDSM walihitaji kwa sababu kila chuo huwa kinakuwa na vigezo na viwango vyake.

Wanafunzi hao wakaambiwa watapita katika program hiyo kwa muda wa miezi mitatu, lakini haikuwa hivyo, badala yake wakaendelea kusoma kwa miezi kadhaa zaidi ya ilivyopangwa awali.

Baada ya takribani miezi kadhaa wakarejeshwa darasani lakini wakarudishwa kusoma Mwaka wa Tatu badala ya kuendelea na Mwaka wa Nne.

Hali hiyo inadaiwa ikawarudisha nyuma kimasomo kwa asilimia kubwa japokuwa wapo ambao waliamua kupambana katika mazingira hayohayo kuendelea kusoma masomo ya mbele huku wengine wakibaki nyuma.
View attachment 2559138
The University of Dar es Salaam Mbeya College of Health and Allied Sciences (UDSM-MCHAS)

BARUA ZATOLEWA
Kutokana na ratiba kuonesha kuwa muda ambao Mwanafunzi anatakiwa kusoma Doctor of Medicine kuwa ni miaka mitano na ikizidi anaongezwa miwili hivyo jumla kuwa 7, kufikia Desemba 2022 wakawa wamefikia ukomo wa muda wa wao kuendelea kuwa chuoni.

Ndipo zikaandaliwa barua za kuonesha kuondolewa chuoni na zikafikishwa chuoni Desemba 2022 na ilipofika Januari 2023 wanafunzi hao wakakabidhiwa barua zao za kuondolewa chuoni kigezo kikiwa ni muda kufika ukomo (time barred).

WAKATA RUFAA
Baada ya kukabidhiwa barua zao, Wanafunzi wakakata rufaa chuoni kupinga wao kuondolewa chuoni, lakini majibu yaliyotoka msimamo ukawa ni uleule.

WANAFUNZI WENGINE WAMETOBOA
Inaelezwa kuwa wanafunzi wa Doctor of Medicine wa mwaka husika ambao wanalalamika walikuwa zaidi ya 250, lakini ambao wamefukuzwa chuo kutokana na kigezo cha muda ni 34.

Wanafunzi wengine walifanikiwa kuhitimu masomo yao Mwaka 2021 na wengine 2022 kwa kuwa walilazimika kwenda na kasi ya ziada wakati wakiwa chuoni hapo, kwamba walitumia muda wao wa ziada kusoma na kufanya mitihani bila kwenda na ratiba ambayo ilikuwepo wakati huo.

Hivyo, hao 34 walioondolewa chuo wao wanadai wamekuwa nyuma kutokana na changamoto kadhaa, wanazitaja changamoto kuwa ni;

Matokeo kutoka kuchelewa kutoka, wanadai hali hiyo ilikuwa ikiwarudisha nyuma na kushindwa kuendelea na masomo ya mbele.

Mafunzo katika vituo visivyo na vigezo, wanadai kuwa walipelekwa katika vituo vya afya ambavyo hazikidhi vigezo kwa mwanafunzi wa shahada kujifunza.

Idadi ya Wanafunzi kuwa wengi, wanaeleza kuwa hiyo ilisababisha wengi wao kutojifunza vema hasa masomo ya vitendo…

Kutokana na hali hiyo maombi yao kwa Wizara ya Elimu ni kuwasaidia kupewa muda wa ziada kumalizia masomo yao kwa kuwa muda walioupoteza hapo kati ndio umesababisha changamoto inayoendelea.

Wanadai kuwa mamlaka zinafahamu kilichotokea na walishazungumza na uongozi wa chuo chao kuhusu muda wao kupotezwa, wakaahidiwa watapewa nafasi lakini wanashangaa mamlaka zimewageuka licha ya kutambua changamoto iliyowatokea hapo kati.

TAMKO LA CHUO (MCHAS)
Mkuu wa Chuo cha MCHAS, Prof. Projestine Selestine Muganyizi anatoa ufafanuzi kwa kusema:

“Ninachofahamu ni kuwa chuo kina taratibu zake ambazo zinatumika kuwawezesha wanafunzi kusoma na kutimiza majukumu yao, ikiwemo hilo suala la muda, yote hayo yapo katika maandishi.

“Lakini pia hata kama mwanafunzi ana supplementary, hata anapofanya mara kadhaa akashindwa haimaanishi muda unasimama kumfidia yeye, hata hao wanafunzi wametolewa kwa mujibu wa taratibu za chuo.

“Kuhusu crash programs, sikuwepo wakati huo lakini ninavyoelewa unapokuwa katika utaratibu huo haikuzuii wewe kuendelea kusoma masomo yako mengine.

“Tuliwapokea wanafunzi zaidi ya 600, wengine wamehitimu na wengine bado wapo, kwa nini iwe wao tu hao 34, unatakiwa kujiuliza kuna jambo gani tofauti kuhusu wao?”
Nasubiri wenye mamlaka wajibu, tatizo ni wanafunzi ndio vilaza au chuo kimezingua?
 
kabla ya yote vigezo vya hao wanafunzi kwenda kusoma Ajauco vilikuwaje huenda walikuwa wanaandaa waacha mikasi tumbon , naua waswahili weng wataweka huruma ila hawajui athari za kumruhusu mediocre kuingia mtaani hasa kwa kada ya afya , HURUMA ISIWE KIPAUMBELE KWENYE HILI
 
Nasubiri wenye mamlaka wajibu, tatizo ni wanafunzi ndio vilaza au chuo kimezingua?
“Tuliwapokea wanafunzi zaidi ya 600, wengine wamehitimu na wengine bado wapo, kwa nini iwe wao tu hao 34, unatakiwa kujiuliza kuna jambo gani tofauti kuhusu wao?”
 
Nasubiri wenye mamlaka wajibu, tatizo ni wanafunzi ndio vilaza au chuo kimezingua?
Kimsingi, UDSM wamejitahidi sana kuwaabeebaa hao 34. Nadhani km wangekuwa na sifa hapo awali wangeenda UDSM, Bugando au Kairuki... Hivyo, UDSM kuwapokea na kuwapika hadi kuondoa hawa 34 walifanya kazi kubwa sana. Nijuavyo, UDSM hawafanyi biashara ya kumbembeleza mwanafuzi; ukizubaa Guidelines zinakutema. Wengi wa hawa wanafunzi 34, usishangae wametokea English medium ambapo ubembelezwa ili washinde. Tusubiri cha Zaidi.
 
kuna mkeka niliuona juzi kati wa wanafunzi wa UDSM MCHAS ambao walikuwa discontinued kutokana na ufaulu kutokuwa mzuri sijajua ndio hawa ama la, ila kama ndio hawa basi ufaulu haukuwa mzuri

na degree za medicine huwa hawana mba mba mba, nenda muhimbili etc. raia wana-leftishwa kila hatua mdogo mdogo kama Squid game😂
 
Mbona barua maelezo yanajitosheleza,yaani wengine waendelee alafu useme mie sikufaulu kwa sababu ya changamoto fulani?ni sawa na kusema nilifeli shule sababu ya mazingira magumu hamna mwenye habari na wewe
 
Kwenye udaktari kunahitaji uzoefu zaidi . Kipindi cha Corona madaktari wengi waliokazini walionekana vilaza kwa sababu ugonjwa wa Corona walikuwa hawana uzoefu nao . Hao wanafunzi wa Udsm-mchas kama walikuwa wamefika mwaka wa tano serikali iingilie kati iwarudishe wawe madaktari . Mwanafunzi wa udaktari aliyefika mwaka wa tano , akienda intern ya mwaka mmoja kupata uzoefu wa kazini anaweza kuwa daktari mzuri . Udaktari unahitaji uzoefu zaidi . Kipindi cha Corona tuliona jinsi madaktari walivyoonekana vilaza japo kwenye vyeti vyao wana A's tupu . Kama wanafunzi hao wamefika mwaka wa tano , serikali iwarudishe . Wakipata uzoefu wanaweza kuwa madaktari wazuri . Kukomoana ilikuwa enzi za zamani .
Mkuu mwanafunzi kufanya vizuri na kufaulu mitihani ni jambo la msingi na haliingiliani kabisa na uzoefu. Uzoefu yes, lakini hii haiondoi ama haiwi sababu kwamba hata waliofeli wanaweza kuwa madaktari wazuri kwa kigezo cha kwamba watapata uzoefu tu
 
kuna mkeka niliuona juzi kati wa wanafunzi wa UDSM MCHAS ambao walikuwa discontinued kutokana na ufaulu kutokuwa mzuri sijajua ndio hawa ama la, ila kama ndio hawa basi ufaulu haukuwa mzuri

na degree za medicine huwa hawana mba mba mba, nenda muhimbili etc. raia wana-leftishwa kila hatua mdogo mdogo kama Squid game😂
Ebu huo mkeka utume tuthibitishe madai
 
Hao 34 wana nn, ikiwa wenzao zaid ya 200 wamemaliza? Hii ni sekta ambao haitaji huruma yoyote, kama wame fail haina haja ya kuendelea na masomo wala kuwaonea huruma, wenyewe wameshindwa kufuata utaratibu wasiwalazimishe na wengine wasifuate utaratibu
 
Inaonesha hao wanafunzi 34 walifeli ingawa mleta mada umeiweka kiufiche sana.

Nilitegemea kama ni kuondolewa wangeondolewa cohort nzima.
Hawa wazee wa carry over ...
Walirudia mara kibao, haiitaji akili nyingi kujua tatizo siyo chuo au mamlaka.
Watu 34 kati ya 600 ndiyo muda ulikuwa tatizo?
 
Back
Top Bottom