UDSM: Tunaomba msaada wenu JF!

Na kwa taarifa tu ni kwamba Mukandara hajawahi kuwa hata head wa department Leo ni VC.

Hii ndio unazidi kuharibu kabisa. Usichojua wewe ni kwamba wana JF kibao hapa ni product ya UDSM na wanakijua chuo chao pengine kuliko nyie.

Sasa wewe unatudanganya mchana kweupe kwamba Mukandara "hajawahi hata kuwa head wa department" halafu unategemea watu wawapeni msaada hapa? Tunajua Mukandara kabla hajawi VC alishashika vyeo kadhaa ikiwemo ukuu wa kitivo na idara. Sasa wewe kwa nini unataka sympathy kwa kutupa habari za uongo? Hapa JF uongo unachukiwa kama unavyochukiwa ufisadi. Sasa hebu rekebisha kwanza hili kabla hatujaendelea.
 
Kwanza Hapa Watu Kuna Makundi Mfano Wale Waliokuwa Wanagoma Waliwarushia Mawe Hawa Wengine Waliokuwa Wanaendelea Na Shuguli Zao , Ni Kundi Dogo Sana Linalotaka Kugoma Kutokana Na Udogo Wao , Hawana Nguvu Za Kutosha Kuweza Kuushawishi Uongozi Wa Chuo Na Viongozi Wao Kukaa Meza Moja Kuongea Kitu Fulani Cha Maana Hata Viongozi Wa Wanafunzi Hawa Wanaogoma Pia Hawaelewani Wenyewe Kwa Wenyewe .

Nimeona Hawa Baadhi Ya Vijana Wakijaribu Kuwashawishi Wadogo Ndugu Na Jamaa Zao Wasiwaunge Mkono Wale Wanaoandamana Na Kudai Haki Zao .

Kwa Maana Hiyo Kuna Tatizo Hapa Na Tatizo Hili Mpaka Sasa Limeshagawa Wanafunzi Hawa
 
Usichojua wewe ni kwamba wana JF kibao hapa ni product ya UDSM na wanakijua chuo chao pengine kuliko nyie.
Wakijua hilo basi itakuwa rahisi wao kujieleza vema. Mkiona hoja yenu inajadilika na kwa kasi ya ajabu mwelewe kila mtu anaguswa na angependa kuona suluhu inapatikana.

Tunakupendeni ila tungefurahi mkija na maelezo ambayo yamenyooka na kwa busara za kisomi.

Karibuni
 
Mwe! Prof. Kithuku hapa umeua kweli kweli.

Dah, ukweli unauma... Labda kuna mwenye kuwa na madai yao kwa mapana yanayoonyesha kuonewa waziwazi.

UDSM Students: JF na wanachama wake hawataweza kuingizwa mkenge bila kujua madai yenu yakoje. Come out clean with your allegations and people will lead you into the right place.

Invisible

Na katika mawazo yote jaribu kutumia usomi wako kuchambua cha kukusaidieni. Connect the dots and you'll succeed. Wajibu wangu ni kukuombeeni kwa wadau wajaribu kuwapa namna mbadala za kupata suluhu ya tatizo lenu.

Great to have both of you here.

Invisible

mkuu hawa jamaa wa UD kama utapeleleza siku zote migomo yao inapokuwa examz inakaribia.mkuu hawa jamaa history yao inasema hujisahau hao chuoni na KUNONGOANA weeee mpaka paper zikwia karibu tena ndio huanza visababu.kwa maana hiyo achana nao mkuu,waache wasubiri after 6wks wapigwe final examz ndio hapo watajua KAMA KITUNGUU MBOGA AU PAMBO LA MCHUUZI.
 
Sasa wewe unatudanganya mchana kweupe kwamba Mukandara "hajawahi hata kuwa head wa department" halafu unategemea watu wawapeni msaada hapa? Tunajua Mukandara kabla hajawi VC alishashika vyeo kadhaa ikiwemo ukuu wa kitivo na idara. Sasa wewe kwa nini unataka sympathy kwa kutupa habari za uongo? Hapa JF uongo unachukiwa kama unavyochukiwa ufisadi. Sasa hebu rekebisha kwanza hili kabla hatujaendelea.

Labda amewahi kuwa dean lakini si UDSM. Idara aliyoiongoza ni REDET ambayo kila mtu anafahamu ipo kwa ajili ya nani. Na kwa taarifa sehemu kubwa ya wanafunzi hawamtaki huyu mtu kwa sababu analeta UCCM hapa chuoni.
 
Mtu Analalamika Bila Kutaja Contact Zake Mimi Niko Udsm Sasa Napenda Kuonana Na Huyo Mtu Anayehitaji Msaada

Udsm Wanaohitaji Msaada Wawasiliane Na Mimi Niko Hewani Hapa Udsm 0784 360204 , 0713620278

Kumbuka Kutaja Jina Lako Halisi Na Ulipo Tutakufuata Tuongee Na Wewe Habari Hizo Zitapelekwa Katika Vyombo Vya Habari Na Waandishi Wa Habari Wengine

Ahsante
 
Mimi Niko Hall 6 Hapa Na Muda Mwingi Niko Hapa Eneo Hili Sasa Uliza Mtu Wowote Aliyekuwa Hapa Au Kule Yombo Atakwambia Wanafunzi Wamefanya Nini Kama Ni Uwongo Hawakujaribu Kuingia Katika Internet Cafe Moja Hapo Hall 6 Na Kurusha Mawe

Sisi Wote Tuko Udsm Sasa Wewe Sema Uko Eneo Gani Au Unaambiwa Tu Unakanusha ??

Heshima kwako mkuu,

Unajua wewe wakati mwimgine nakufananisha na wale vibaraka wa Makaburu enzi zile wasauzi wanapigania uhuru wao kutoka kwa makaburu wale waafrika ndio walikua mstari wa mbele kuwakatisha wenzao tamaa.

Hapo UDSM kuna uonevu wa kutisha na sasa kama ni mabadiliko ya nguvu lazima yaanzie hapo.

Vijana jengeni hoja za nguvu ambazo hata mkiziweka katika jukwaa la kimataifa zitakubalika hata ikiwa worse kufikia hatua za kuandikwa na vyombo vya habari vya kimataifa zionekane logic za kweli.

Kisha watengeni wale ambao wana uchungu wa kudai haki na wale waoga wachache ambo inawezekana uoga wao unatokana na kutokuelewa umuhimu wa mnachofanya.Kisha hilo kundi la ambao wanaogopa kugoma mtafute kijikamati kidogo cha watu wenye ushawishi mkubwa na wanaoweza kusikilizwa na makundi yote ya wanafunzi halafu wawashawishi kwa kukaa upande wao kwanza ili wafanane.Wawaeleze kwanza hasara za kugoma na kisha waombe sapoti ya hilo kundi kwa wale walio katika ari ya kugoma.Tarehe ya kuanza mgomo itangazwe rasmi na taarifa zipelekwe kwenye vyombo vya habari ikiambatana na maandamano ya nguvu lakini ya amani na yenye kila dalili ya kuwa hakuna kulala mpaka kieleweke.Mkishashinda hapa,mtakua mmekomaa kiasi ambacho mtaweza kushinikiza kufanyika kwa mambo makubwa ya kitaifa.

Msiogope polisi hata kidogo.Hata hivyo kama mtu hujui haki yako au kama hujui kwa nini unagoma ni bora usigome.

Tumieni Nguvu ya Umma
 
Labda amewahi kuwa dean lakini si UDSM. Idara aliyoiongoza ni REDET ambayo kila mtu anafahamu ipo kwa ajili ya nani. Na kwa taarifa sehemu kubwa ya wanafunzi hawamtaki huyu mtu kwa sababu analeta UCCM hapa chuoni.

ANTIFISADI UKO MITAA GANI HAPA UDSM ? NAONA MAMBO YA WIRELESS HAYA KATIKA VILAPTOP

TUWASILIANE TUWEZE KUONANA NA KUONGEA KWA MAPANA

+255784 360204
 
Jamani eeh this is too much. Wanafunzi wameenda diamond lakini walioenda hawazidi 1000 na chuo kizima kina watu zaidi ya 10000. Na kwa taarifa na nina uhakikia kila mtu anafahamu kuwa Mukandara amewekwa pale na JK kwa manufaa ya chama kwa sababu wameshaona kuwa UDSM hawapati sapoti wanayoihitaji. Sasa wapo hao wachache ambao hawana tofauti na wote ambao wapo hata JF ambao ni Makada wa CCM. Ila wapo ambao lengo sio tu kuongezea posho bali kuhakikisha Huyo Mukandara anaondoka hapo alipo. Na kwa taarifa tu ni kwamba Mukandara hajawahi kuwa hata head wa department Leo ni VC.

Na hapo ndio tunahitaji msaada. Mahakamani it wont work.

Mwaka jana tulijaribu kusimamisha uchaguzi lakini kesi ikapangwa kuanza kusikilizwa wiki 2 baada ya uchaguzi. Tunajua hawa jamaa wapo everywhere ndio maana tunataka msaada kwa ambao wanauzoefu nao katika kupambana nao.

.......huku kugoma kwenu mbona hakueleweki.........kama moja ya sababu ya kugoma kwenu kunatokana na hilo hapo juu........then hilo rumba inabidi mlicheze wenyewe.......not JF.........hiyo hapo nyekundu INATIA KINYAA hata kwa kuisoma
 
Heshima kwako mkuu,

Unajua wewe wakati mwimgine nakufananisha na wale vibaraka wa Makaburu enzi zile wasauzi wanapigania uhuru wao kutoka kwa makaburu wale waafrika ndio walikua mstari wa mbele kuwakatisha wenzao tamaa.

Hapo UDSM kuna uonevu wa kutisha na sasa kama ni mabadiliko ya nguvu lazima yaanzie hapo.

Vijana jengeni hoja za nguvu ambazo hata mkiziweka katika jukwaa la kimataifa zitakubalika hata ikiwa worse kufikia hatua za kuandikwa na vyombo vya habari vya kimataifa zionekane logic za kweli.

Kisha watengeni wale ambao wana uchungu wa kudai haki na wale waoga wachache ambo inawezekana uoga wao unatokana na kutokuelewa umuhimu wa mnachofanya.Kisha hilo kundi la ambao wanaogopa kugoma mtafute kijikamati kidogo cha watu wenye ushawishi mkubwa na wanaoweza kusikilizwa na makundi yote ya wanafunzi halafu wawashawishi kwa kukaa upande wao kwanza ili wafanane.Wawaeleze kwanza hasara za kugoma na kisha waombe sapoti ya hilo kundi kwa wale walio katika ari ya kugoma.Tarehe ya kuanza mgomo itangazwe rasmi na taarifa zipelekwe kwenye vyombo vya habari ikiambatana na maandamano ya nguvu lakini ya amani na yenye kila dalili ya kuwa hakuna kulala mpaka kieleweke.Mkishashinda hapa,mtakua mmekomaa kiasi ambacho mtaweza kushinikiza kufanyika kwa mambo makubwa ya kitaifa.

Msiogope polisi hata kidogo.Hata hivyo kama mtu hujui haki yako au kama hujui kwa nini unagoma ni bora usigome.

Tumieni Nguvu ya Umma

WANAOFANYA HIZO FUJO NA MIGOMO NI SEHEMU NDOGO SANA YA WANAFUNZI INGAKUWA NI WANANCHI TUNGEWAITA WAASI AU MAJINA MENGINE YANAYOFAA KUWAITA , WATU HAWA HAWANA USHAWISHI WOWOTE HAPA UDSM NDIO MAANA HATA ASKARI WA KUTULIZA GHASIA HAWANA MPANGO NAO WANAWAACHA TU WAWAONE WATAFIKIA WAPI SASA HIVI MPAKA NINAVYORUSHA HABARI HII WAMESHATULIA WATU WAMEENDA VYUMBANI WAO WALE WENYE NJAA WAKO KATIKA KANTINI WANAPATA MILO YAO

NAPENDA KUWASIHI WANAFUNZI WA UDSM AMBAO WENGINE NI WANACHAMA HAPA ,MSIKUBALI KUPELEKESHWA KAMA PUNDA NA WATU WACHACHE AMBAO HAWAWATAKII MAENDELEO YENU YA LEO HATA SIKU NYINGI ZIJAZO MNAPOLALAMIKA HAKIKISHA UNAJUA UNALALAMIKA KUHUSU NINI KAMA UNAONA HUFANYIWI HAKI KUNA NJIA NYINGI UNAWEZA KUANDIKA BARUA KWA UONGOZI WA CHUO , KUONGEA NA VYOMBO VYA HABARI NA MAMBO MENGINE MENGI SANA YA KUFANYA KABLA YA KUFIKIA UAMUZI WA KUGOMA

UKIGOMA MAANA YAKE UMEVUNJA MAADILI NA NIDHAMU YA CHUO PAMOJA NA MENGINE YOTE YALE , WAKATI UNAJIUNGA NAFIKIRI HUKUWAHI KUSOMA SEHEMU YOYOTE ILE KWAMBA MAANDAMANO NDIO NJIA SAHIHI YA KUDAI HAKI ZAO HATA KAMA NI NJIA SAHIHI JE HAYO MAANDAMANO MBONA HAYAUNGWI MKONO NA WATU WENGI ?
 
nimesubiri material fact of the cause of action ili tuwasaidie sijapata. jamani usiogope ilete tuiangalie.
 
Mtu Analalamika Bila Kutaja Contact Zake Mimi Niko Udsm Sasa Napenda Kuonana Na Huyo Mtu Anayehitaji Msaada

Udsm Wanaohitaji Msaada Wawasiliane Na Mimi Niko Hewani Hapa Udsm 0784 360204 , 0713620278

Kumbuka Kutaja Jina Lako Halisi Na Ulipo Tutakufuata Tuongee Na Wewe Habari Hizo Zitapelekwa Katika Vyombo Vya Habari Na Waandishi Wa Habari Wengine

Ahsante

Mimi nawshauri vijana hapo UDSM waachane na huyo SHY maanake huyu ni mtu wa kujikomba na anataka kuwaumiza wanafunzi wa UDSM.Eti,wataje majina halisi.Hivi huwezi kuwasaidia hawa watu hapa JF mpaka uonane nao na kujua weanafananaje ndio ujue cha kuwasaidia? SHy kama huwezi kuwasaidia hawa vijana just leave them alone maanake watu type yenu ndio mnatufanya tunakua nyuma kimaendeleo siku zote.

We huko UDSM muda wote uko huko kufuatilia maendeleo ya mgomo kiudaku udaku bila kutoa solution hapa.Kumbuka hii thread ni ya kuomba msaada wa wanajf,kwa hiyo ambae anatakiwa kupost ni yule mwenye solution otherwise ni upotoshaji wa thread
 
Moto utanza kuwaka na kuunguza magugu yaliyopo pale UDSM na haswa baada ya kunaswa kwa barua ya makamba kwa wakuu wa vyuo na jinsi ya kuendesha chaguzi za wanafunzi.

Kuna siri kubwa hapa na mnio lazima MKANDALA atasema kuwa ni kwa nini tangu aingie chuoni hapo hakuna fedfha za kuendesha chuo na pia mahesabu ya ofisi yake hayapelekwi kwenye Finance Committee ya council kama ilivyokuwa hapo awali.

Pili kuna kamcxhezo kanachezwa na vijana baadhi wa uv CCM kuwa wanataka mtu wao ili awasaidie kwenye kampeni zao hapo baadaer kidogo huku ni kuua sehemu ya ubongo ya kufikiri,nawataka vijana hao waache mara moja la sivyo tutaanza kutajana majina hapa bila aibu na kumbukeni jana mlikosea mkamshirikisha mwana JF kwenye kikao na bila kujua kuwa mtandao huu ni mpana basi tutaweka CD nzima hapa.....

Tuwasaidie hawa vijna kwai wanaumizwa kwa sababu za maagizo na za kisiasa zaidi kuliko ukweli.....
 
Hawa vijana wawe makini kwa kila move maanake maspy wapo kila kona otherwise wataishia kudhalilishwa.

Vijana daini haki zenu kwa kutumia nguvu ya umma.Kama mnazo hoja za nguvu msiogope na msikubali hata mwanafunzi mmoja kufukuzwa chuo.La sivyo wawafukuze wote,wasilete ukaburu hapa.

Hakikisheni mpaka kesho asubuhi hoja zenu zimeleweka kabisa na muanze kuhamasishana
 
Labda amewahi kuwa dean lakini si UDSM. Idara aliyoiongoza ni REDET ambayo kila mtu anafahamu ipo kwa ajili ya nani.

Kijana unaanza kunitia shaka kama wewe ni mwanafunzi wa Mlimani. Kama ni mwanafunzi wa mlimani kweli basi inabidi ukazane kidogo kujielimisha mambo ya chuo chako. Uliza mwalimu wako yeyote akueleze kidogo historia ya Mukandala hapo chuoni. Huyu alikuwa mkuu wa idara ya sayansi ya siasa na utawala na baadaye akawa mkuu wa kitivo cha sayansi za jamii na sanaa kwa muda mrefu sana.

Sasa ndio tunasema vijana wa sasa mnatia shaka sana kwenye usomi wenu maana kama hata historia fupi ya chuo chenu hamuielewi mtayajua kweli nyie mambo ya akina Che Guevera? Na kama mambo ya Che hamyajui, mnaweza kweli kufanya mgomo wa maana ambao jamii itawaunga mkono?
 
Jamani wanaJf.

Naungana nanyi katika kutafuta suluhisho la UDSM. Nakumbuka wakati nikiwa huko migomo ilikuwa mingi na sababu za msingi ila mwisho wa yote wachache huwa bangusilo (waliokuwepo na wasiokuwepo).

Mfano mgomo 2000 ambao Zitto, Kusaja, Mkili na wenzie walitimuliwa kisivyo halali, lakini kichekesho ilikua bwana mmoja aliitwa kwa jina Augustino Mrema alikuwa anasoma Sheria nae alifukuzwa simply jina lake ni kama la Mrema (TLP). Huyu bwana hakuhusika kwa namna yeyote katika mgomo ule lakini alipewa adhabu hiyo isiyomhusu kwa namna yeyote.

Nikirudi kwenye mada hii, inawezekana vijana wa DSM wanaomba msaada hapa wameshindwa kujieleza ama wanaogopa kujieleza maana nao linaweza likawakuta pamoja kutofahamu vizuri historia ya chuo na walimu wao.

Hivyo ni bora kwa wale waliopitia mlimani wanajua ukandamizaji unaofanywa na utawala wa chuo kuanzia juu hadi chini. Hivyo wale wanaopenda kusaidia sio lazima tutegemee maelezo ya huyu mtoa mada bali tutumie ndugu zetu, rafiki zetu na wengine kupata ukweli wa mambo na kutafuta ufumbuzi wa matatizo ili vijana wetu wasome
 
Back
Top Bottom