Serikali kutoitambua Shahada ya Maendeleo Vijijini (Bachelor of Rural Development) toka Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoinie (SUA)

displayname

JF-Expert Member
Feb 15, 2013
1,950
1,039

BURUA YA WAZI KWA MKUU WA CHUO CHA KILIMO CHA SOKOINE (SUA)

SERIKALI KUTO ITAMBUA SHAHADA YA MAENDELEO VIJIJINI (BACHELOR OF RURAL DEVELOPMENT) KATIKA AJIRA ZINAZOTOLEWA NA UTUMISHI WA UMMA KITENGO CHA SECRETARIET YA AJIRA TANGU SHAHADA HIYO ILIPO ANZISHWA MWAKA 2004.

Kwako Mheshimiwa Mkuu wa Chuo ninakusalimu kwa jina la jamhuri ya muungano wa Tanzania. Hongera kwa kuteuliwa katika chuo cha SUA kwa kua umeaminiwa kua una uwezo wa kukisimamia Chuo na Taaluma zake zote vizuri na kwa weledi mkubwa. Na mimi nimefurahi kupata mawasiliano yako na kuwasiliana na wewe na nakushukuru kwa kunisikiliza na kutaka kujua kuna nini katika tatizo hili na kufuatalia ili utatuzi uweze kupatikana.

Ninaandika barua hii kwako kuhusu serilikali kuto tambua Shahada ya Rural development na wahitumu wengi wa shahada hiyo tangu ilipo anza kufundishwa na Chuo chako mwaka 2004 mpaka sasa 2023. Kitengo kilichopo katika Ofisi ya Rais Utumishi wa Umma na utawala bora, kiitwacho Secretariet ya ajira imetunyima haki ya kupata ajira muda mrefu sasa, imetunyima haki hata ya kufanya Usahili mara kadhaa, hata kutuchagua kufanya usahili katika kazi mbalimbali zikiwemo kazi za Maendeleo ya jamii, Afisa Mipango, Ustawi wa jamii na nyinginezo nyingi.

Mheshimiwa Mkuu wa Chuo Katika hili sisi wahitimu wa shahada ya Rural Development wa miaka mbalimbali kwa wakati tofauti, tumetumia rasimali fedha na muda mwingi kufuatilia nini tatizo hasa serikalini, kujua kwanini shahada hii ifundishwe katika Chuo cha serikali na tena kikongwe na kinachoaminika sana na Umma na Serikali yenyewe, lakini wahitimu wake wakataliwe kupata fursa ya ajira Serikalini? sisi wahitimu tunaiona hii ni double standard. Tumekua tukijibiwa na wahusika wa vitengo vya ajira serikalini kama ifuatavyo miaka mingi.

Kwanza : Utumishi wa Umma pamoja na Secretariet ya ajira wanatoa sababu kua Shahada hii (Rural Development) tangu ianzishwe na kuendelea kufundishwa na SUA mwaka 2004 mpaka leo 2023 haijawahi kutambulika na serikali kwasababu haijasajiliwa na kuingizwa katika kitabu maalumu cha ajira cha serikali kinachojumuhisha shahada mbalimbali za inchi nzima kilichopo utumishi wa umma na secretariet ya ajira ambapo wao hutumia kitabu hicho tu kutangazia ajira na kuwapa watu ajira. Ikitokea shahada yeyote inatolewa na Chuo chochote kile kiwe cha serikali au binafsi hapa Tanzania lakini haijasajiliwa katika kitabu hicho basi shahada hiyo wahitimu wake wasitegemee kuajiriwa na serikali ikiwemo Rural Development ya SUA.

PILI: Utumishi Umma pamoja na Secretariat ya ajira wamekua mara kwa mara wakielekeza lawama nyingi kwa Uongozi wa chuo (SUA) wakisema kua, tangu shahada hii isajiliwe na chuo, chuo hakija weka nia dhabiti ya kufuatilia serikalini ili iweze kuingizwa katika kitabu cha ajira cha Tanzania. Hapa wao hutujibu sisi kua tatizo ni chuo na wanatutuma sisi kurudi kukaa chini na uongozi wa SUA ili uongozi ufanye ufuatiliaji wa kina serikalini ili kuwezesha shahada hii ijulikane serikalini kwa maana kuingizwa katika kitabu cha ajira la sivyo haitawezekana na tatizo hili litakua ni la kudumu.

TATU:Watumishi wa Utumishi wa Umma pamoja na Secretariet ya ajira hutujibu kua shahada hii (Rural Development) hufundishwa na chuo kama fashioni na wanafunzi wanaosoma shahada hii wanataka tuu wawe na cheti basi au wafanye kazi zingine katika sector binafsi na sio serikalini.

Mheshimiwa Mkuu wa Chuo na Staff wote wa SUA mimi na graduates wenzangu ni watoto wenu, kwa majibu ya hapo juu yanayotolewa na serikali, kwa muda mrefu tumeendelea kugugumia na kupata maumivu makali sana moyoni, tunalia machozi na kusononeka sana na kujilaumu wenyewe kwanini tulisoma rural development, tunapata msongo wa mawazo hasa pale ambapo hatuelewi nini hatima ya maisha yetu katika ajira na maisha yetu tumekuwa masikini sasa (tumekua Rural poor na sio Rural development tena) hasa tunapokataliwa kuajiriwa na Serikali kama muajiri mkuu inchini tunaona wenzetu tena waliosoma nyuma yetu shahada nyingine wanaajiriwa na serikali ila sisi tu ndio hatutakiwi kupata ajira. Sisi inatuuma saana, maana tumepoteza tumaini la kuishi kwa furaha kama graduates wa shahada zingine inchini.

Sisi (wahitimu wa Rural Development) tumekataliwa ajira serikalini kwasababu ya shahada hii wakati tofautitofauti na sehemu tofautitofauti miaka mingi sasa tangu kumaliza kwetu sisi wa 2012 na wanafunzi wa miaka mingine sasa, Mifano ni mingi kama hii miwili hapa chini.

MOJA Hivi karibuni April 2023 serikali kupitia secretariet ya ajira wametoa kibali na tangazo la ajira lenye Kumb. Na. JA.9/259/01/A/276 la tarehe 18 Aprili, 2023, ambapo ndani yake kulikuwemo ajira za MAENDELEO YA JAMII daraja la II nafasi 800, sisi wahitimu wa Rural development tumeomba nafasi hizi katika ajira portal na mfumo ukatukubalia lakini shahada hii haikutajwa katika tangazo lao, tujipa matumaini kua tungechaguliwa kufanya Usahili na wengi tulikua na matumaini tutapata kazi sasa maana ajira hizi ni nyingi, mheshimiwa Prof. bahati mbaya sana tarehe 01/07/2023 secretariet ya ajira wametoa majina ya walioitwa kufanya usahili ila hakuna hata mmoja aliechukuliwa wa shahada ya Rural Development tukiingia katika account zetu tumejibiwa kua “NOTSHORTLISTED Lacks Relevant Bachelor Degree Certificate as Per Advertisement” ikimaanisha kua sisi shahada yetu sio relevant katika ajira za maendeleo ya jamii, lakini pia Shahada hiyo haikutajwa katika advertisement yao ya tangazo la ajira ( hii ni tafsiri ya as per advertisement). Hii ndio imetuvunja moyo kabisa, na ndio maana tumeanza kuwasilian kwa kasi chuoni SUA tangua jumamosi asubuhi 01/07/2023 baada ya kukataliwa tena katika ajira hizi. Wafuatao ni mfano wa wengi ambao hawajachaguliwa kwenye Usahili unaotarajiwa kufanyika tarehe 08/07/2023 kwa sababu ya shahada haitambuliki na serikali.
S/N
NAME​
EMAIL ILIYOTUMIKA AJIRA PORTAL​
NAMBA YA SIMU​
1.
Rainery Denis Kayombo​
0757305310​
2.
Primus wilbald Mbote​
0682802424​
3.
Jasmin Ally Mchome​
0717009195​
4.
Tunzo Sulemani Sanga​
0757233580​
5.
Prima Nchasi Richard​
0657332254​
6.
Juliana Charles Matharo​
0673917718​
7.
Rehema Ramadhani Mtili​
0688817770​
8.
Nuru Basyagile​
0688787201​
9.
Christopher Juma Mtisi​
cjuma81882gmail.com​
0624362241​
10.
Emmanuela Kondrald Chikawe​
0656822070​
11.
Shukrani Mkongwa​
0787977897​
12.
Happiness Edward Nzigilwa​
0717574485​
13.
John Daudi Manase​
0623998952​
14.
Chilstobela Wilcharles Lyimo​
0657332254​
15.
Silvia Laurent Tsere​
0782869508​

PILI: Mwaka 2017 Serikali kupitia secretariet ya ajira walitoa tangazo la ajira lenye Kumb. Na. EA.7/96/01/ J/01 la tarehe 24 Agosti 2017, ambapo ndani yake kulikuwemo ajira za MAENDELEO YA JAMII DARAJA LA II nafasi 17, sisi wahitimu wa Rural development tuliomba nafasi hizo katika ajira portal na mfumo ukatukubalia lakini shahada hii haikutajwa katika tangazo lao, ila tibahatika kutwa kwenye Usahili Magogo chuo cha kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Dar-Es- Salaam tarehe 02/12/2017,Tukiwa Ukimbuni katika zoezi la uhakiki na ukaguzi wa vyeti watumishi wa secretarieat ya ajira walitukatalia kuingia ukumbini kufanya mtihani kwa sababu kua wametuita kimakosa na Shahada yetu haitambuliki na serikali hivyo tunatakiwa kuondoka ukumbini hapo na kurudi tulikotoka.

Hapa tulielekea wizara ya kazi ,ajira na maendeleo ya vijana ya wakati huo na baade Utumishi wa Umma Dododma kulalamika juu ya kile tulicho kiona na kutukuta katika ukumbi wa Usahili ndiko tuliko jibiwa majibu matatu ya ukurasa wa kwanza hapo juu. Baadae tulielekezwa na Utumishi wa Umma Dodoma kua turudi Chuoni kwa kua tatizo ni chuo kushindwa kuwasilisha serikalini mahitaji ya ajira za Rural development katika kitabu cha ajira cha Tanzania.

Mheshimiwa Mkuu wa Chuo Tuliwasiliana na Kiongozi wa college ya Social Science and Humanities Dr.Kabote ambae sasa ni Prof.Kabote, nae alituambia tuandike burua ya malamiko yetu na tuwasilishe SUA,ikatubidi kusafiri kutoka Dodoma mpaka Morogoro natukakabidhi barua katika kitivo hicho tulielekezwa tukutane na tukae mezani na maafisa wa idara ya social science and humanities akiwemo Dr.Boniface Masawe na Dr,Emmanuel Malisa. Tulikaa nao kujadiliana na kukabidhi barua hiyo na ilipokelewa tarehe 20/12/2017 mchana. Tuliahidiwa suala hilo litashughulikiwa kwa haraka na sisi tulijua kwakua Usahili wakati huo (2017 Decemba) ulikua umeshafanyika na muda umepita basi tutafaidika na utatuzi huo siku za mbeleni, kumbe hatukujua tatizo halikutatuliwa kati ya serikali na chuo na linaendelea mpaka sasa 2023 ikiwezekana hata mbeleni likawa bado ni tatizo, na ndio maana majina ya Usahili ya tarehe 08/07/2023 BRD hatumo hata mmoja wetu. Mheshimiwa Mkuu wa Chuo Hili tatizo limekua kubwa na sugu sasa tumefika mahali tunaona kua ni kama halitatuliki na limeshindikana kutatuliwa kwakua limejulikana miaka mingi sana, lakini limebaki vilevile.

Mheshimiwa Mkuu wa Chuo Nikwambie kitu pakuanzia suala hili, inawezekana wewe ni mgeni katika Chuo Cha SUA ila sina uhakika, Idara ya DSI (yaani Development studies Institute) ya wakati huo na sasa Facult of social science and Humanities imekua ikulijua suala hili kwa muda mrefu tangia 2008 miaka yote hii watumishi wa idara hii katika chuo chako wanalijua wote, ikiwezekana hata uongozi wa juu wa chuo wa nyuma kabla yako sio issue ngeni kwao akina prof. Kabote, prof.Kayunze,Prof,Chingonikaya,Prof. Jekonia na wengine wengi, na ndio maan hata barua yetu ya 2017 ya kulalamikia suala hili iliwafikia wao baada ya sisi kukosa mawasiliano ya moja kwa moja na mkuu wa chuo yaani vice Chancellor wa wakati huo. Kwahiyo kukosekana kwa majibu sahihi kati ya chuo na serikali suala hili limekua mwiba kwetu. Tukimwambia Prof.Kabote kama mkuu wa faculty ambapo shahada hii iko chini yake, yeye anatupia lawama serikali na anaonesha kuto kujali wala kufuatilia kwa makini na pia hatuoni kama anaweza kupush jambo hili kwa ufasaha zaidi mpaka tukajua mwisho wake maaan ni mda mrefu yapata miaka zaidi ya kumi suala hili limekua mezani kwake kama kiongozi wa idara ya Social science and humanities bila mafanikio, licha yay eye mwenyewe na idara yake kukabidhiwa barua ya maandishi ya suala hili tarehe 20.12/2023 na sis wahanga wa jambo hili, na tunaona kwamba suala hili likiachwa chini ya idara hii ya social science and humanities peke yao bado majibu yake hatapatikana ndio maana tunakumba wewe mkuu wa Chuo uingilie kati , tukuombe ukutane moja kwa moja na wahusika wa jambo hili serikalini ili lipate ufumbuzi ila likiwa cini ya idara ya Prof. Kabote basi nina uhakika hatutapata majibu kama barua yetu ya mwaka 2017 ambavyo haikuzaa matunda.

Naamini umepata mwanga shida iko wapi Mheshimiwa Mkuu wa Chuo Ni maombi yetu kwako baba yetu ambae ndiwe tumaini letu la mwisho kwa upande wa Chuoni SUA, utusidie yafutayo.

Tukuombe wewe mwenyewe sasa ulibebe hili suala kikamilifu kwakua umelijua na tatizo ambalo liko wazi na vielelezo vyake viko wazi katika kupitia barua hii na vyanzo vyako vingine vya habari. Hatukupangii ufanye nini kwa kua hatuna mamlaka hayo ila, tunakuomba utufanyie yafuatayo miongoni mwa mengi unayotufikilia kutusaidia katika hili.

MOJA.Uweze kuongea na Serikali ishughulikie shahada hii iingie katika kitabu cha ajira ili ijulikane na Utumishi wa Umma na Secretariet ya Ajira. Tatizo ni kile kitabu cha ajira cha shahada zote za Tanzania shahada yetu haimo mule ndani na mimi nilikiona kwa macho yangu nilioneshwa namtumishi mwenye upendo wa utumishi wa Umma tukiwa Dodoma.

PILI: Tunakuomba sana uingilie kati kadri uwezavyo kuishawishi serikali kuiamuru secretariet ya ajira iliyoko eneo la Asha Rose Migiro - Dodoma iweze kukubali kurudia kutushortlist sisi wa Rural development tuliomba na hatujatoka katika majina ya usahili utakaofanyika tarehe 08/07/2023, majina yetu yatoke kama majina ya nyongeza ya usahili kama ambavyo hua wnatoa wakati mwingine pale yanapojitokeza makosa katika mifumo yao. Hili linawezekana kufanyika kabisa kwa sababu mfumo ulitukubalia kuomba hii kazi na tuliomba ila tumenyimwa kwa sababu ya shahada hawaitambui.

Tunaomba haya yafanyike kwa mapenzi mema na maslahi mapana ya Chuo chetu kizuri cha SUA kuendelea kukijengea uaminifu, umaarufu na kuilinda heshima yake kwa watanzania wote na pia utulivu na furaha kwa wahitimu wake wa BRD ambao wengi wetu ni wahanga sasa turudi katika furaha ya matumaini tuliyokua nayo wakati tukisomea shahada hii.Wahitimu na wahanga wenzangu katika kundi lilopo whasap la BRD 2012 wametaka sana kulipeleka suala hili katika vyombo vya habari mitandaoni wengine wameenda mbali sana, mimi binafsi nimewaomba wasifanye hivyo kwa sasa kwa mara ya kwanza tumefanikiwa kupata mawasiliano ya moja kwa moja na wewe na tunaamini chini ya usimamizi wako suala hili litapata ufumbuzi ndani ya siku chache kabla ya usahili kufanyika.

Tumetumia rasilimali nyingi zikiwemo pesa, muda na mikopo wakati mwingine tumeuza hadi mashamba ya ukoo ili tusome, shahada hii ya Rural development, lakini kumbe tumepoteza rasimali na muda wetu, na wengine tumeingia hata kukopa mikopo ili kusoma na tupate kazi itusaidie katika maisha, wengi wetu mpaka sasa tunadaiwa na bodi ya mikopo mikopo tuliyosemea shahada hii lakini katika yote haya tunafika mwisho tunaambiwa hatuwezi kuajiriwa au kuajirika tumesoma shahada ambayo sio sahihi hili kwetu ni janga la kielimu na la kitaaluma. Ingelikua shahada hii inafundishwa na Chuo cha private/binafsi tungesema labda kwa kua ni binafsi lakini SUA ni Serikali na Serikali ni SUA jambo hili ni kweli kabisa limeshindikana? Mheshimiwa Mkuu wa Chuo sisi tunaona tunaumizwa sana. Jamii tunamo ishi wakiwemo wazazi wetu,wake na waume zetu na wengine wote wanatuuliza kwanini mlisoma shahada hii ambayo serikali inawakataa na kama ni hivyo kwanini bado serikali haitoi tamko kuhusu shahada hiyo, kwanini inaendelea kufundishwa tena ndio kwa muda mrefu imekua na wanafunzi wengi SUA. Haya maswali yote sisi wahitimu wa shahada hii tunakosa majibu tunabaki kujiona wanyonge, tusiotakiwa katika ajira za serikali Tanzania.

Tunashangaa, serikali kupitia wizara ya fedha kitengo cha bodi ya mikopo kwa muda mrefu wametoa na wanaendelea kuwapa mikopo wanafunzi wa shahada hii ya Rural Development wa SUA. Pia kwanini TCU waidhinishe shahada hii kufundishwa chuoni SUA. Lakini baadae wahitimu hawatakiwi kuajiriwa na hutujulikani sasa mikopo ya bodi ya mikopo tuliyoikopa tutairudishaje na je tutaishije.

Mheshimiwa Mkuu wa Chuo Tunakubali kua wachache wetu wamebahatika kupata ajira lakini katika mazingira ambayo bahati nasibu tuu na hili lili dhibitishwa tulipokua Utumishi Dodoma Kulalamika nao walisema hao walibahitika tuu ila hawakutakiwa kuajiriwa kwa kupitia shahada hiyo. Hivyo wnegi wetu tuko tuu hatujui mwisho wetu na hatuajiriki serikalini.

Mheshimiwa Mkuu wa Chuo Natambua wazi kua tangia jumamosi 01/07/2023 watumishi wa SUA wamepokea malalamiko mbalimbali kutoka kona mbali mbali juu ya suala hili nikiwemo mimi kuongea na wewe moja kwa moja kupitia simu ya mkononi kwa kua mimi nimebahatika kupata mawasiliano yako ila wao wanawasiliana na staff wengine hapo Chuoni ambao waliwafundisha. Tunakushukurowewekipekeekuguswa na suala hili na wafanyakazi wengine wa chuo kwani tunazo taarifa kua staff wako pia wamelalamika sana na wanalijua tatizo hili kwa kua limesikika na limeripotiwa hapo chuoni muda mrefu nao wanajiuliza kwanini hatua hazijachukuliwa mpaka sasa na halifiki mwisho? na wengime wameenda mbali hata kusema basi shahada hii ifike mahali ifutwe kama haiwasaidii watanzania kupata ajira na serikali inaikataa. Hawa wameumia kama sisi watoto wao tunavyoumia.

Tunashukuru kwa juhudi za awali kuwasiliana na wahusika serikalini juu ya jambo ambapo wewe Mheshimiwa Mkuu wa Chuo umelivalia njuga na kwmba leo tarehe 03/07/203 siku ya jumatatu zikiwa zimebaki siku tano tuu za usahil kufanyika,Chuo kitawasilisha Barua serikalini wizara ya Utumishi wa Umma na utawala Bora, Wizara ya maendeleo ya jamii na Wizara ya Elimu kwa utatuzi. Tunaomba kuwasilisha majina machache 15 tajwahapo juu yatumike kama ushahidi wa sisi kukosa ajira katika barua zitakazo andikwa na chuo lakini pia barua hii itumike kama kiambatanisho cha malalamiko ya wahitimu wa shahada yamaendeleo vijini kunyimwa ajira na serikali.

Kama tangazo la ajira llilotolewa 24 Augosti 2017 na 18 Aprili 2023 pamoja na majina ya usahili yaliyoitishwa yakitakiwa kama kielezo pia na barua ya 2017 tuliyoiwasilisha SUA dokumenti hizi zote tunazo tunaweza kuziwasilisha mara moja pale zitakapo hitajika kama kielelezo.

Ni mimi muhitumu wa Bachelor of Rural Development wa 2012, Kwa niaba ya wahitimu na wahanga wa ajira wote wa shahada hii naomba kuwasilisha kwako mheshimiwa asante sana.

Ahsante sana.
Rainery Denis 0757305310
kwa niaba ya wahitimu wote wa Bachelor of Rural Development
 
Mkuu ni kweli maana Mimi pia nilimsaidia ndugu yangu kuomba juzi naangalia nakuta hajachaguliwa yani ni majanga matupu now anamiaka 3 toka haitimu ila kila nikipiga wapi ataajiriwa ndo sione zaidi ya kuchonga mchongo huko sekta binafsi
 
Kuna tatizo kubwa kama hali ndio hii kwa hakika! Inakatisha tamaa na kusononesha!! na Kufifisha matumaini ya hao ma graduate!!!
 
Dah pole mkuu, kuna vitu ni ngumu kuvielewa aisee
Chuo cha Serikali, Kozi ya Chuo, na ni Serikali hiyohiyo inawakataa wahitimu kutoka katika chuo chake!!! Pia naona mentality ya wahitimu wengi ni ajira... na private competition ni ya kibabe so mkombozi ni Serikali na Serikali yenyewe inawakataa mbaya sana!!
 
Mkuu ni kweli maana Mimi pia nilimsaidia ndugu yangu kuomba juzi naangalia nakuta hajachaguliwa yani ni majanga matupu now anamiaka 3 toka haitimu ila kila nikipiga wapi ataajiriwa ndo sione zaidi ya kuchonga mchongo huko sekta binafsi
Kasome PhD in Rural Areas hapohapo SUA
 
Nina ndugu yangu kasoma kozi hiyo alipata kazi 2020 kama Afisa Ustawi wa Jamii kwenye wilaya moja.

Lakini alisita sana mtaani kuitwa kwenye interview za serikali.
Kozi nyingine ni ungese sana,watu wanapoteza muda bure.
 
Sema Nyie Jamaa wangewaajiri mnge add value sana maana mnaonekana kweli mna moyo wa Kuleta Mendeleo Vijijini
 
Vipi bado mpaka sasa hali ipo hivyo ?
Walisharekebisha shukrani ziende pia kw Prof C.I. Nombo KM huku Elimu nadhani. Alisaidie fanikisha jambo hilo pia vijana wakaajirikia vizuri tu sasa wanajivunia check namba zao.
 
Mkuu ni kweli maana Mimi pia nilimsaidia ndugu yangu kuomba juzi naangalia nakuta hajachaguliwa yani ni majanga matupu now anamiaka 3 toka haitimu ila kila nikipiga wapi ataajiriwa ndo sione zaidi ya kuchonga mchongo huko sekta binafsi
Kuna Pacha wake anaitwa BTM(Bachelor of Tourism Management) zote ziko mazimbu aisee najuta nilipoteza my 3good years , pesa na muda, degree yetu haiwi mentioned hata kwa kazi ambazo ukisoma majukumu yake unaona ni yetu kabisa, majanga sana .
 
Back
Top Bottom