UDSM: Tunaomba msaada wenu JF!

kitumtui

New Member
Oct 11, 2007
2
0
Ninapenda kupitia hapa niweze kuzungumzia mtafaruku uliopo Chuo kikuu cha DSM. Mkuu wa chuo Prof Mkandara aliwasimamisha wanafunzi 25 hapo chuo akiwemwo waziri mkuu na mpaka sasa wanafunzi wote wapo kimya na hakuna kinachoendelea kudai kurudishwa kwa wanafunzi wenzao... NINI SASA sio kwamba wanafunzi wako kimya bali ni hila na jinsi mkuu alivyoamua kutumia UBABE NA NDIKTETA kuzuia any movement ambayo inaweza kuwarudisha pale chuo.

Ikumbukwe kwamba mkuu huyo yupo pale kisiasa na siyo kivingine na anapoaana matakwa ya chama chake hayafanikiwi anatumia njia mbadala za kuumiza umma wa chuo.

KWANINI NATUMIA JF: nia makusudi yangu kwamba tukitoa sauti ya nguvu kuwasaidia wanafunzi waliosimamishwa chuo eti kwa kuhatarisha amani ya chuo wanaweza kurudi.

Wanafunzi hapa leo walitaka kuanzia mgomo lakini kuna kina hali yawao kushindwa kwa maana kila mtu anayeonekana kuleta move anaitwa na Mgaya(PRof) anampiga biti na kumtukana tena kumwambia atamfunga.

Inaniuma sana pia nikifikiria Uongozi wa chuo unahaonga hata waandishi wahabari ili wasitoe sauti yao

Tupo Chuo kujifunza jinsi ya kutetetea maisha ya watanzania ambao wengi ni masikini tunaomba mtuunge mkono kwani bila msaada wenu hatutaweza...

Mwnakijiji, Invisible na wote wale nyie ni wanaharakati na mnajua nini maana ya haya yote tupeni sapoti ili tuweza kukikomboa chuo chetu then kiweze kuitetea nchi.

Tunamkumbuka Chachage ambaye alikuwa mtetezi wa wanafunzi Siyo hawa kina SHIVJi wanaomuenzi Nyerere bila kufuata yale yote aliyoyataka.

REVOLUTION FOR CHANGES
 
Tupo Chuo kujifunza jinsi ya kutetetea maisha ya watanzania ambao wengi ni masikini tunaomba mtuunge mkono kwani bila msaada wenu hatutaweza...
kitumtui,

Mradi umefikisha ombi lako, toa muda kidogo na kuwa tayari kujibu ama kutoa ushirkiano utakapoombwa kufanya hivyo.

JF si Invisible wala Mwanakijiji pekee... Ni mkusanyiko wa watanzania wengi... baadhi ni wakufunzi wako!

Nakuoneeni huruma lakini amini kuwa jitihada zitafanyika. Muhimu ni uwepo wako ili kujibu baadhi ya hoja na kutoa mwanga pale panapohitajika.

Watanzania, nakaribisha maoni, mapendekezo na maelekezo ya namna ya kuwasaidia vijana wenu.

Invisible
 
Wanafunzi wa UDSM ni wazembe period!

wanayo access ya internet 24/7 sasa mmeshindwa vipi kuwa active humu au kuwa na forums zenu?

anywa..ombi lenu tumeliona lakini kwa sasa tuko bizee na Mustafa Mkullo
 
Inasikitisha kuwa hawa wanafunzi hawaonyeshi kwamba kweli ni wasomi wachanga. wanachojua wao ni kugoma tu pale mambo yao yanapoharibika. Yanapotokea masuala makubwa ya kitaifa sijawasikia hata wakitoa tamko tu!

Ebu onyesheni usomi wenu kwa kuitafuta njia muafaka ya kumaliza matatizo yenu. Kwa nini muuige ubabe wa Mukandara? Jionyesheni kuwa ninyi ni tofauti na wao, inabidi mutafute njia ya kutafuta suluhu ya matatizo yenu na mui-present hapa ili kuona mtasaidiwaje. Sasa mnaomba msaada gani haswa? Na sisi tuje tugome kama ninyi?
 
Wanafunzi wa UDSM ni wazembe period!

wanayo access ya internet 24/7 sasa mmeshindwa vipi kuwa active humu au kuwa na forums zenu?

anywa..ombi lenu tumeliona lakini kwa sasa tuko bizee na Mustafa Mkullo

Ila kabla ya kuwasaidia, Basi Vijana Muwe na Nidhamu hasa mtu kama Mtatiro na wengine, katika historia ya Chuo kikuu cha Dar es salaam haijawahi kutokea wanafunzi kuandamana mpaka kwa mkuu wa Chuo, hii ilionesha kukosa nidhamu na mnataka kuhatarisha hata familia yake ambayo haisuki.. Tulieni Mmalize masomo na nyie kazi yenu ni kuchagua viongozi, waacheni wanaotaka madaraka waitishe uchaguzi na nyie mpige kura.

Suala la kugoma sababu ya uchaguzi si jambo la Busara hata kidogo, nyie ndio mnajenga jamii ya machafuko ambayo watanzania tusiongependa itokee hata kidogo, tutumie diplomasia kuyamaliza mambo na sio Jazba zisizo na Msingi.

Mkuu Gt,
Yes Us said, and am Saying Mkullo Should Go Out from the Cabinet,
Yes Mwanakijiji You Sais, Msolla should Go out
YEs Mwafrika wa kike you said, Othman Rashid should Resign
 
Tatizo sisi watanzania tulio wengi hua hatuchukui tahadhari ila yanapotimia ndio tuna jibu mapigo kwa ghadhabu kitu ambacho hakisadidii badala ya kukuza tatizo kua kubwa.Hili swala la udsm liliongelewa kabla lakini reaction ikawa zero.

Mimi nafikiri migomo mmejaribu sana na mara zote hua haiwaletei majibu mema na hata hivyo migomo imepitwa na wakati.

Mimi ningewashauri nendeni mahakamani huko ndio itabidi watoe vielelezo jinsi gani wamehatarisha usalama wa chuo .Na mkiwashinda kesi itabidi wawalipe fidia.
DARUSO ina fedha ya kuendesha kesi hii Ni ushauri tu.
 
Hawa si ndio waliandama kuwaunga mkono mafisadi sijui CCM na ma T-Shirt yao ya kijani na njano? Anyway naamini kabla ya kugoma mliangalia legal framework ya huo mgomo and I hope mliona sheria iko upande wenu na any consequence mngeweza kuichallenge in the court of law. Kama mlijua ni illegal na hakuna any law mnayoweza kuitumia kuwabeba basi inabidi muumie tuu, nawashauri vitu kama hivi muanze kutumia mahakama maana migomo sasa sio popular sana na mara nyingi uzoefu unaonyesha mnaishia kufukuzwa tuu
 
Hawa si ndio waliandama kuwaunga mkono mafisadi sijui CCM na ma T-Shirt yao ya kijani na njano?
Mkuu, wawie radhi... Wako katika nyakati za kuchanganyikiwa kwa sasa. Nashukuru kwa maoni yako na mapendekezo.

Muhimu hapa ni kuwapa ushauri juu ya nini wafanye ili kurejea masomoni. Kama ni kuuangukia uongozi wa chuo ndiyo njia muafaka basi pia tuwaelekeze ni kwa namna gani wafanye hivyo. Ni vijana wetu, wana mapungufu yao... GT, waonee huruma hawa... Kuna wakati watagundua mapungufu yao na watajirekebisha (japo huenda wakawa wamechelewa).

Invisible
 
Jamani hadi inafikia hatua ya kuomba msaada sio kwamba hatujajaribu njia nyingine. Labda tu ni kwamba aliyeomba msaada ameuwasilisha vibaya kwa kuomba msaada wa kugoma. Ila kama mahakamani hata katika uchaguzi wa mwaka jana tulijaribu kwenda mahakamani ila tarehe za kesi zilivyopangwa tukajua hapa hatutapata kitu. kuhusu hii ishu ya mwaka huu tulijaribu kufikiri kususua uchaguzi lakini nahisi kuna watu watafaidika zaidi. NDIO MAANA TUNALETA KWENU TUPATE MAWAZO ZAIDI YA KULITATUA HILI TULILONALO SASA HIVI.
 
Ila Wanafunzi majority wa Chuo kikuu wanudhi sana, leo wanalia wanaonewa kesho Makamba akiitisha mkutano Diamond Jubilee hawa jamaa watavalishwa Tshirt za Kijani Wakiwa wamepandishwa kwenye Mabasi wakiimba nyimbo za Kumsifu Makamba, ni lazima kwanza wabadilike hawa Watoto,
 
NDIO MAANA TUNALETA KWENU TUPATE MAWAZO ZAIDI YA KULITATUA HILI TULILONALO SASA HIVI.
Na katika mawazo yote jaribu kutumia usomi wako kuchambua cha kukusaidieni. Connect the dots and you'll succeed. Wajibu wangu ni kukuombeeni kwa wadau wajaribu kuwapa namna mbadala za kupata suluhu ya tatizo lenu.

Great to have both of you here.

Invisible
 
Jamani hadi inafikia hatua ya kuomba msaada sio kwamba hatujajaribu njia nyingine. Labda tu ni kwamba aliyeomba msaada ameuwasilisha vibaya kwa kuomba msaada wa kugoma. Ila kama mahakamani hata katika uchaguzi wa mwaka jana tulijaribu kwenda mahakamani ila tarehe za kesi zilivyopangwa tukajua hapa hatutapata kitu. kuhusu hii ishu ya mwaka huu tulijaribu kufikiri kususua uchaguzi lakini nahisi kuna watu watafaidika zaidi. NDIO MAANA TUNALETA KWENU TUPATE MAWAZO ZAIDI YA KULITATUA HILI TULILONALO SASA HIVI.

Nendeni mahakamani
msitafute njia za mkato,hizi njia za mkato ndio maana kila mwaka mna mgogoro na uongozi na hatimaye kurudishwa nyumbani kila mara.

Huko mahakamani uchaguzi unaweza simamishwa mpaka hapo kesi itakapoamuliwa.
 
wanayo access ya internet 24/7 sasa mmeshindwa vipi kuwa active humu au kuwa na forums zenu?
Hawa nao cjui namna gani utawakuta muda woote wakichat kutafuta mademu tu.Kuna wengina hata anuani za barua pepe hawana!
 
Ila Wanafunzi majority wa Chuo kikuu wanudhi sana, leo wanalia wanaonewa kesho Makamba akiitisha mkutano Diamond Jubilee hawa jamaa watavalishwa Tshirt za Kijani Wakiwa wamepandishwa kwenye Mabasi wakiimba nyimbo za Kumsifu Makamba, ni lazima kwanza wabadilike hawa Watoto,

Jamani tuwe werevu kidogo hivi kama hapa JF inakuja hoja ya ufisadi na baadhi ya wanaJF wanaifagilia na kuwatetea mafisadi itakuwa sahihi kusema wanaJF wote hawana maana? UDSM kuna wanafunzi zaidi ya 10,000 sasa Makamba akija kuondoka na wake 1000 wanaotaka kupewa fulana na elfu tano-tano je itakuwa halali kuwaadhibu na hawa wengine waliobakia?
 
Wanafunzi Wa Chuo Kikuu Cha Dar Es Salaam Udsm Wameanza Mgomo Wao Rasmi Sasa Hivi Tu Kuanzia Saa Sita Kamili Mchana , Hapa Ninapoandika Sasa Hivi Nipo Chumbani Na Internet Karibu Zote Za Hapa Ndani Ya Chuo Wamefungia Wanafunzi Wengine Ndani Kwa Sababu Kuna Vikundi Vya Wanafunzi Vimeanza Kufanya Vurugu Za Hapa Na Pale , Wanafunzi Wengi Kwa Sasa Wamekusanyika Ndani Ya Ukumbi Wa Yombo Wanapiga Kelele Na Hata Kufikia Baadhi Kuanza Kutwangana Makonde Njiani Wakati Wanatokea Kituo Cha Basi Kinachoitwa Bondeni

Na Mawe Wameshaanza Kurusha Wanafunzi Wanakimbia
 
Hawa nao cjui namna gani utawakuta muda woote wakichat kutafuta mademu tu.Kuna wengina hata anuani za barua pepe hawana!

Mtu ,umenichekesha sana..nakumbuka enzi zetu tunasoma hata maendeleo ya Intenert yalikuwa chini sana..kulikuwa hakuana hata wirelss ila kwa sasa pale Mlimnai kuna Access ppoint kibao...karibuni Jf.
 
Mgomo wenye kuhatarisha maisha na mali sio tabia ya wanafunzi wa Mlimani. Hii ni miaka nenda rudi.

Mgomo walioufanya wa kuharibu mali za Chuo, kuvamia nyumba ya Mkuu wa Chuo na hata kuvunja/kuingia kwenye mabweni ya wasichana - hii sio tabia inayotegemewa kutoka kwa wasomi wetu. Hizi ni tabia za vibaka na mabaradhuli waliokubuhu!

Hatua ya kuwapeleka Polisi ilikuwa ni sawa kabisa. Hilo la uchaguzi - nadhani mahakama ndio mahali sawia pa kulimaliza.
 
Back
Top Bottom