Tundu Lissu amekataa kupiga magoti kwa wadhalimu, amekataa kuwapa mashetani ushindi, amekataa kutia huruma mbele ya majambazi, amewanyima furaha wale mumiani wanaofurahia maumivu ya watanzania yanayoyokana na umasikini na ufukara wa kutengenenezewa.
Amekataa udalali, amekataa kuibukia ikulu na kuungana na walaghai wanaotapanya kodi za watanzania bila kujali lolote.
Ameamua kusimama na kuwanyima heshima na utukufu wasiostahili, japo wanalazimisha sana kujipa heshima na utukufu bandia. Lissu amewanyima.
Sasa, hasira walizo nazo ni kubwa sana. Nathubutu kuamini wanatamani Lissu afe, kama walivyojaribu kumuua miaka 9 iliyopita, hata sasa naamini bado wanatamani hayo. Lakini watafanya nini?
Kilichobaki ni kuwaamrisha majaji watoe hukumu kwa Lissu ili kuendelea kumlazimisha awapigie magoti, wajifanye wamemsamehe ili wapate heshima na utukufu bandia, visivyostahili.
Bado simuoni Lissu wa kumpigia mtu magoti.
Ninachokiona, hukumu yotote kwa Lissu itakuwa na athari kubwa kwenye maadhimisho ya Oktoba 29.
Nawasilisha!
Dr. Chris Cyrilo.