MWAMBIENI JAJI MUTUNGI, TUTAJIPATA
Baada ya Lissu kuwa huru,
Tume Huru ya Uchaguzi,
Katiba Mpya.
Hatutajipata kwa warsha, kubambikikiwa kesi nyingi, kusingiziwa, kufungiwa kufanya siasa, na mikakati ya vitisho.
Huzuni upande wetu ni kubwa. Tuna watu wasio jua waume zao wako wapi kwa mamia; achilia mbali wanaotafuta miili ya wapendwa wao mpaka sasa. Tunajipata Kwa furaha Gani ?
Tunao mahabusu wa kutosha, wastani kila gereza mbeya Geita ,shinyangai,iringa,Mwanza,musoma,UKONGA Aliko Lissu , na mengine yanatutabasamia kila siku tunapopita, maana ndiyo tuzo mwajiri wake ameamua iwe yetu kwa miaka yake yote.
Na kesi rasmi sasa ni uhaini, ugaidi, uhaini, uhujumu uchumi... Tunajipataje?
Kwa mujibu wa Jaji Mutungi (Msajili wa Vyama vya Siasa), na kwa mujibu wa macho ya kichawa na husda, hiki ndicho chama alichokitaja kwenye vikao vyake na vyama anavyoviamini 18 kuwa bado kinajitafuta.
Maana yake hakijakamilika.
Inajulikana dhahiri kwa nini anasema kinajitafuta, maana lugha za chama hiki zinamkera mwajiri wake abadani. Kinazungumza na kusanua wananchi sana, naye hapendi masanusi ya namna tunavyoporwa na uhalifu wote wananchi wanaofanyiwa.
Kwa maono hayo, wananchi wote hawa wanajitafuta isipokuwa yeye na vyama vya flash disk 18 ndio wako kwenye njia sahihi.
Rai yangu na ushauri wangu kwako, Jaji Mutungi: Kusanya hivyo vyama 18 vilivyojipata, ongoza wewe msafara, njoo uongee na wananchi uwaeleze namna gani huielewi CHADEMA Tanzania na kwa nini huielewi. Labda utushtaki kwa wananchi; wanaweza kutuelewesha uliposhindwa wewe.
Lakini muhimu, sisi tumeamua kusimama na wananchi. Ndio tumeamua kujitafutia huku, sio kwenye korido za serikali na warsha za bahasha za kaki. Hizo tukizikwepa, msituone watukutu.
Tutajipata mkimwachia Lissu.
#FreeLissu
Tutajipata mkikubali tuwe na Tume Huru ya Uchaguzi.
Tutajipata baada ya kuwepo #KatibaMpya.
Mwl. Chacha Heche
Mwenyekiti wa Mkoa wa Mara