Tundu Antipas Lissu special thread (CHADEMA CHAIRMAN)

Tundu Antipas Lissu special thread (CHADEMA CHAIRMAN)

MAHAKAMA IMEANZA TUNDU LISSU ANAFANYAMAJUMUISHO YA MWISHO.

SEHEMU YA 1, TAREHE 25.9.2026.

Lissu ameshaingia Mahakamani, na Majaji nao wameingia Mahakamani tayari.

Karani wa Mahakama anajiandaa kusoma:

Criminal Session, Kesi Na. 19605 ya 2025
Jamhuri dhidi ya Tundu Antipas Lissu.

Nassoro Katuga anasimama kuwatambulisha wenzake.

Nassoro Katuga:
“Iwapendeze Waheshimiwa Majaji, naitwa Nassoro Katuga, Wakili wa Serikali Mkuu.

Nipo pamoja na:

1. Job Mrema — Wakili wa Serikali Mkuu
2. Ignas Mwinuka — Wakili wa Serikali Mkuu
3. Tawabu Issa — Wakili Mwandamizi
4. Cuthbert Mbilinyi — Wakili wa Serikali
5. Winiwa Kasara — Wakili wa Serikali

Waheshimiwa Majaji, jopo hili la Mawakili sita linaiwakilisha Jamhuri katika shauri hili leo.

Mshtakiwa yupo na anajiwakilisha mwenyewe.

Shauri limekuja kwa ajili ya mshtakiwa kuwasilisha hoja zake.

Upande wa Jamhuri tupo tayari.”

Jaji Ndunguru:
“Mshtakiwa?”

Lissu:
“Nipo tayari.”

Jaji Ndunguru:
“Tuendelee. Nakumbuka jana tuliishia pale ulipotaka kuanza hoja ya tano.”

Lissu:
“Waheshimiwa Majaji, nalazimika kujitetea mwenyewe.

Nipo gerezani mwaka mmoja na nusu.

Kile ambacho tungetumia muda wetu vizuri kukitumia kwa mwezi mmoja, nalazimika kutumia muda wangu wa final submission kwa wiki moja.

Kama kuna jambo nimelisahau jana, nitalirudia.

Nataka nianze; yapo masuala jana niliyasahau.”

Lissu:
“Ndiyo ilivyo hivyo. Nalazimika kufanya kazi ya mwezi mmoja kwa wiki moja.”

Jaji Ndunguru:
“Tuendelee.”

Lissu:
“Kuna kitu muhimu juu ya hoja niliyoimaliza jana.

Je, maneno yanatengeneza uhaini?

Nataka niongee kitu muhimu ambacho kitasaidia Mahakama inielewe na kufanya uamuzi sahihi sana.

Kwa nini Mahakama ya Rufani katika kesi ya Khatibu Ghandi ilisema, ‘Maneno matupu hayavunji mfupa’?

‘Mere words do not constitute treason.’

Ni kwa sababu Mahakama ya Rufani ilikuwa inafahamu historia yetu kuhusu uhaini.

Na msiwe na wasiwasi, sitotumia masaa matatu katika hilo.

Sheria yetu ya Jinai (Penal Code) ilitungwa mwaka 1930.

Na sheria yetu ilitungwa moja kwa moja kutoka Uingereza, wakati Waingereza walikuwa wanatutawala.

Mwaka mmoja kabla ya 1929, that is, Bunge la Uingereza lilipendekeza sheria za jinai kwa ajili ya Tanganyika, Kenya, Uganda na Nyasaland (Malawi ya sasa).

Bunge la Uingereza lilipendekeza sheria za jinai.

Ndiyo, mwaka 1930 Bunge la Uingereza likatunga sheria kutokana na draft ya Westminster.

Vifungu vinavyohusu uhaini vilichukuliwa moja kwa moja kutoka katika sheria ya Uingereza ya mwaka 1948.”
 
TUNDU LISSU ANAFANYA MAJUMUISHO YA MWISHO MAHAKAMANI

SEHEMU YA 2.

Hiyo sheria ya Uingereza inaitwa Treason Felony Act ya 1848.

Palikuwa na tofauti moja na sheria hiyo ya Treason Felony Act.

Kwenye ile sentensi inayosema katika kifungu cha 39(2)(d), kwenye sheria ya Uingereza inasema:

“Manifest such by publishing any writing or printing, or by open advice, speaking, or by any overt act or deed.”

Sasa, Waheshimiwa Majaji, sheria ya Uingereza ya mwaka 1848 ilikuwa imeweka uhaini kwa kuzungumza (kwa kutoa maneno).

Sasa, hicho kifungu kilichokuwa kinaruhusu maneno kuwa ni sehemu ya kosa la uhaini kiliwekewa ukomo wa maisha yake.

Ile sheria, kifungu chake cha 4, kilisema hicho kifungu kitatumika kwa miaka miwili tu.

Kwa hiyo, baada ya mwaka 1850, kifungu hicho kiliacha kutumika kama sababu ya kumtia mtu hatiani.

Na ilipofika mwaka 1891, The British Parliament amended that section by repeal.

The repealing Act was the Statute Law Revision Act of 1891 ya Westminster.

From that time to this day, English law on treason is counted as Section 39 of our Penal Code.

Our Penal Code was enacted in 1930 by British law.

Kwa vile English law ilishafuta uhaini wa maneno, ndiyo maana sheria yetu vilevile haijawahi kuwa na uhaini wa maneno.

Na ndiyo maana, Waheshimiwa Majaji, Marehemu Jaji Mkuu Francis Nyarali kwenye kesi ya Khatibu Ghandi alisema kuwa maneno matupu hayafanyi uhaini.

Alikuwa anajua hii sheria imetoka wapi.

Waheshimiwa Majaji, nimesema hiyo sheria ya uhaini kama ilivyopendekezwa na Uingereza kwa Tanganyika, Uganda, Kenya na Nyasaland.

Isipokuwa nchi mmoja imeongeza uhaini wa maneno.

Uganda, katika Penal Code yao, wameongeza uhaini baada ya Mwingereza kuondoka.

Kwa sheria yetu, hakuna uhaini wa maneno.

Napendekeza uamuzi wa Mahakama ya Juu ya Uingereza:

Regina v Her Majesty’s Attorney General (Ex parte Rusbriger and another) [2003] UKHL.

Wanataka kuingiza kitu kwenye kesi hii wakati Waingereza waliotuletea sheria hii waliachana nacho tangu mwaka 1890; wao wanataka kukileta leo.

Pia, lengo la upande wa mashtaka ni kuingiza uhaini wa maneno katika sheria zetu ambao haujawahi kuwa katika sheria zetu milele.

Na tatu, hoja hii ya upande wa mashtaka inapinga msimamo wa Mahakama ya Rufani ya Tanzania kwenye kesi ya Khatibu Ghandi, kwamba maneno matupu hayatengenezi uhaini.
 
TUNDU LISSU ANAFANYA MAJUMUISHO YA MWISHO MAHAKAMANI

SEHEMU YA 3️⃣

Rai yangu, Waheshimiwa Majaji, mtakapofanya uamuzi, msikubali mwaliko wao wa kuingiza katika sheria yetu ya uhaini mambo ambayo hayajawahi kuwepo kabisa.

Mambo ambayo Mahakama ya Rufani ilishayawekea msimamo.

“You are bound by what the Court of Appeal said: ‘Uhaini wa maneno haupo.’”

Sasa, kwa ridhaa yenu, Waheshimiwa Majaji, naomba nizungumze suala la PUBLICATION.

Swali ni: Je, mshtakiwa anayelalamikiwa alichapisha katika mtandao wa Jambo?

Waheshimiwa Majaji, hili ni suala muhimu sana.

Ni suala la kufa au kupona kwa kesi.

Both in Khatibu Ghandi and Gray Likungu Mattaka, ili upande wa mshtakiwa utiwe hatiani, ni lazima upande wa mashtaka uthibitishe printing or writing.

Na usipothibitisha, the case dies on arrival.

Kwenye ukurasa wa 132 wa rekodi, upande wa mashtaka ulituhumu siyo tu kwamba mshtakiwa alitoa maneno wanayoyalalamikia, bali pia alichapisha katika Jambo TV YouTube Channel.

Umma ukayatumia hayo maneno mara moja.

Kuna kitu kimoja hapa nataka niweke wazi.

Upande wa mashtaka haujanituhumu kuchapisha kupitia kwa mtu mwingine; tuhuma yao ni kwamba nilichapisha mwenyewe.

Sikusaidiwa wala sikutumia mtu mwingine.

Kwa hiyo, kusiwe na hoja kwamba, “Aha, ulitumia fulani?” Hapana. Wanatakiwa kuthibitisha kwamba nilichapisha mwenyewe.

Waheshimiwa Majaji, hii Publishing inayotajwa katika kifungu cha 39(2) cha Kanuni ya Adhabu, ambayo lazima ithibitishwe na upande wa mashtaka.

Huu uchapishaji unaozungumzwa hapa ni uchapishaji wa namna gani?

The term “Publishing” or “Publication” is not defined anywhere in the Penal Code.

The fact kwamba haijatafsiriwa haina maana kwamba haijulikani.

Tafsiri yake, Waheshimiwa Majaji, ilitolewa katika Mahakama ya Rufani kwenye Gray Likungu Mattaka, na hiyo decision ikawa affirmed na Khatibu Ghandi.

Kwenye ukurasa wa 509 hadi 510 wa Gray Likungu Mattaka, Mahakama ya Rufani ya Afrika Mashariki ilisema:

“The term publishing under section 39(2) of the Penal Code means sending out or sharing a writing or printing with a third party.”

Na huo uamuzi ukawa affirmed by our own Court of Appeal in Khatibu Ghandi.

Kitu kisichokuwa maandishi au chapisho kikisambazwa, hiyo siyo publishing kwa mujibu wa sheria.
 
TUNDU LISSU ANAFANYA MAJUMUISHO YA MWISHO MAHAKAMANI

SEHEMU YA 4.

Waheshimiwa Majaji, kama “publish” ni “sharing a writing or printing with a third party”, what about a video clip?

Waheshimiwa Majaji, video, pictures au television images are publication under the Cybercrimes Act.

Kwa bahati mbaya sijashitakiwa under the Cybercrimes Act (Sheria ya Makosa ya Mtandaoni), kwa hiyo “publishing” ya sheria ya makosa ya mtandaoni ibaki hukohuko.

Waheshimiwa Majaji, the term “publication” includes, under the Sheria ya Vyombo vya Habari, publication ina include usambazaji wa video.

Kwa bahati mbaya yao, sijashitakiwa chini ya Sheria ya Habari, kwa hiyo na hiyo “publication” ya Sheria ya Habari ifike hukohuko.

Waheshimiwa Majaji, nimeshitakiwa chini ya Penal Code, ambapo “publication” ni writings or printing.

Na hiyo Penal Code ipo chini ya Katiba, kwenye Ibara ya 13(6)(c), ambapo sisi raia tunalindwa na Katiba kwamba hatuwezi kushtakiwa kwa makosa yasiyokuwepo kwenye sheria.

Kama haikuwa makosa jana, hayawezi kuwa makosa leo.

Waheshimiwa Majaji, kwa heshima kubwa kwa mawakili ambao wamekuwa wakipambana na mimi kwa mwaka mmoja na nusu, kesi yao ilikufa siku ilipowasili — “dead on arrival”.

Kwamba mwaka mmoja na nusu tunajaribu kuthibitisha jambo lililotakiwa kujulikana siku ya kwanza.

Imenipa simanzi kubwa sana kuhusu mfumo wa haki jinai wa nchi yetu.

Mahakama zetu, polisi wetu.

Waheshimiwa Majaji, twende kwenye ushahidi wao sasa.

Swala hili limekuwa mojawapo ya maswala yaliyozua ubishi mkali mahakamani.

Kama nilivyosema, ilikuwa ni swala la kufa au kupona kwa kesi.

Ushahidi ukoje, Waheshimiwa?

Upande wa mashtaka waliita mashahidi wao:

PW1
PW2
PW3
PW16
PW17

Upande wa utetezi, mashahidi wote watano walipinga jambo hili.

Tuanze na ushahidi wao.

One notable thing in particular, with the exception of PW17, testified under oath that it was the accused who published a video on Jambo TV’s YouTube channel.

Ulikuwa ni mkanganyiko mtupu.

Walijichanganya, wakachanganyikiwa.

Tuanze na PW1, George Bagyemu.

Waheshimiwa Majaji, kwenye ukurasa wa 144 wa rekodi, PW1 anazungumzia hiyo video. Baada ya kuangalia vipande vipande vya hiyo video clip, aliamua kuwatafuta Jambo TV.

Maneno yanayofuata: “Who recorded the clip?”

Akiwatafuta Jambo TV walioirekodi hiyo video.

Kwa hayo maneno tu, hiyo video ilichapishwa na Jambo TV.

Ukurasa wa 144.

Na ukurasa wa 145 anasema aliyoambiwa na Jambo TV, kwamba anaijua/anaifahamu clip na kwamba hiyo imerekodiwa na mfanyakazi wake.

Anakubali mara ya pili kwamba aliyerekodi siyo mimi.

Anasema huyo mtu wa Jambo TV aliyerekodi yupo Dodoma.

PW1 alipiga simu kwa Kamishna wa Polisi Ng’anzi Dodoma kumjulisha aliyerekodi na eneo paliporekodiwa.

Kwa hiyo, PW1 chini ya kiapo anasema aliyerekodi siyo mimi.

WEKA EMOJI KAMA UNASOMA

SHARE ZAIDI UJUMBE UFIKE MBALI.
 
TUNDU LISSU ANAFANYA MAJUMUISHO YA MWISHO MAHAKAMANI

SEHEMU YA 5️⃣

Yote hayo yalijulikana tarehe 06 Aprili 2025. Kwamba nani alichapisha hiyo video tena siku tatu baada ya mkutano kufanyika.

Walijua vizuri nani alirekodi, ila kwa utaratibu wa Polisi wakasema, “Mpe kichwa.”

Waheshimiwa Majaji, tarehe 07 walimpata aliyeirekodi hiyo video.

Wakapata na nakala ya hiyo video yenyewe.

Na tarehe 07 hiyo hiyo wakapata pia maelezo ya aliyeirekodi.

Maelezo ya PW17 yapo Mahakamani kama Kielelezo D16.

Akaeleza kinagaubaga jinsi alivyoagizwa na boss wake, John Marwa.

Vifaa walivyokuwa navyo kama kamera Sony NHR 100.

Walikuwa watano.

Akaeleza walivyorusha moja kwa moja.

Akaeleza walivyopeleka kwenye mitandao ya Jambo TV kama YouTube, Instagram na X.

Akawaambia kwamba hajaziondoa; zipo mitandaoni hata sasa.

Hiyo ni tarehe 07, siku mbili kabla sijakamatwa.

Kwa sababu ya hayo, Mapolisi walikuwa na hamu ya kunikamata siku hiyo hiyo ya tarehe 07.

Walikuwa na ushahidi wa maandishi yake na memory card aliyokabidhi.

Baada ya siku mbili ndiyo wakanikamata kwa kuchapisha kwenye mtandao.

“They are not even ashamed! Shame on you. Shame on you, shame on you.”

Maneno niliyoyasema yapo ukurasa wa 145.

Na katika ukurasa wa 147, “It’s the accused who published with the intention to threaten the Executive.”

Mdomo mmoja, ndimi mbili.

Na katika cross-examination, PW1 alikiri kwamba ilipelekwa mtandaoni na PW17.

Alikiri pia kwamba amesoma maelezo ya shahidi.

Hata hivyo, aliendelea kung’ang’ania kwamba ni mshtakiwa ndiye aliyechapisha kwenye mitandao (ukurasa wa 159).

Waheshimiwa Majaji, PW1 aliendelea kuflip-flop.

Ukurasa wa 160 anasema, “It’s not true a Jambo TV employee recorded a clip.”

Akasema siyo kweli kwamba PW17 aliyechapisha mtandaoni peke yake ni pamoja na Tundu Lissu.

Alipozidi kubanwa, akabadilika tena, ukurasa wa 165 hadi 166.

Akasema PW17 ndiye aliyeniambia yeye kwamba amechapisha.

WEKA EMOJI KAMA UNASOMA

SHARE ZAIDI UJUMBE UFIKE MBALI.
 
🔴 TUNDU LISSU ANAFANYA MAJUMUISHO YA MWISHO MAHAKAMANI

SEHEMU YA 6️⃣

“Ndimi mbili kama nyoka. Nyoka ni hatari.” 🐍

Waheshimiwa Majaji, PW1 aliulizwa kwamba alikuwa na maana gani aliposema kwamba ni PW17 ndiye aliyechapisha.

Akasema, “Tumechapisha sisi, ila yeye ndiye aliyesababisha.”

Akaulizwa alikuwa na maana gani kusema Jambo TV ndiyo waliochapisha.

Akasema, “Nilikuwa na maana kwamba ni mshtakiwa ndiye aliyesababisha Jambo TV kuchapisha.”

Pia ni maneno ya Wakili Mkuu wa Serikali, Nassoro Katuga, kwamba “nilichapisha kupitia kwa wengine.”

Waheshimiwa Majaji, huo ndiyo ulikuwa ushahidi wa PW1, na ndiye aliyekuwa leading witness.

“Evidence was totally lost credibility.”

Waheshimiwa Majaji, twende kwenye ushahidi wa PW2, ukurasa wa 211 wa rekodi za Mahakama.

Ni confusion ile ile ya boss wake, George Byagemu.

PW2 katika ukurasa wa 214:

«“I don’t know who published the video in Jambo TV.”»

Huyu ni shahidi wa upande wa mashtaka.

Anasema hajui nani aliyechapisha video katika mtandao wa Jambo TV.

Lakini katika re-examination, ukurasa wa 222, Waheshimiwa Majaji, akasema ni mshtakiwa aliyechapisha hiyo video katika mtandao wa Jambo TV.

Akasema hivyo kwa sababu alialika waandishi wa habari.

Waheshimiwa Majaji, PW3 alikubali katika ushahidi wake kwamba hiyo video ipo katika mtandao wa Jambo TV.

Na akakubali kwamba aliikuta huko katika mtandao wa Jambo TV.

Ukurasa wa 276, akasema:

«“Katika uchunguzi wangu, sikugundua nani aliweka hiyo video katika mtandao.”»

Nilimuuliza kama inawezekana kujirekodi mwenyewe na wakati huo huo ukarusha matangazo wakati unahutubia.

Akajibu katika ukurasa wa 277:

«“Sijui kibinadamu kama inawezekana kujirekodi mwenyewe na wakati huo huo ukarusha matangazo wakati unahutubia.”»

Wakamleta Amani Mahamba, PW16, kuja kuokoa jahazi lao.

Ushahidi wa PW16 upo katika ukurasa wa 466 wa rekodi za Mahakama.

WEKA EMOJI KAMA UNASOMA

SHARE ZAIDI UJUMBE UFIKE MBALI.
 
TUNDU LISSU ANAFANYA MAJUMUISHO YA MWISHO MAHAKAMANI

SEHEMU YA 7️⃣

PW16 alisema kwa majigambo yafuatayo:

«“I testify it was you who published a video on Jambo TV.”»

«“It was you who transmitted a video on Jambo TV.”»

«“It’s you who circulated a video on Jambo TV channels.”»

«“It’s you who distributed the video on the Jambo TV YouTube platform.”»

Nilipoanza kumshughulikia hayo madai, yali-collapse.

Ukurasa wa 467, akasema:

“Sina uhakika kama wewe ni mfanyakazi wa Jambo TV.”

“Sina uhakika kama una password ya kutumia Jambo TV YouTube Channel.”

Akaendelea kusema:

“Nimesoma maelezo ya PW1 kwamba alikuwa ni mtu aliye-rekodi mkutano, na kwamba PW1 ndiye aliyerusha matangazo.”

Mwanzoni alikuwa anasema, “Ni wewe, ni wewe.”

Lakini kwenye cross-examination, akasema:

“Sina uhakika kama ni wewe.”

Ukurasa wa 467.

PW16 akaendelea kueleza Mahakama, Waheshimiwa Majaji, kwamba hata George Byagemu alisema:

«“That the video was recorded and live-streamed by a Jambo TV employee.”»

Amin Majamba anasema PW17 kwamba walielekezwa na Mkurugenzi wao, John Marwa, na ku-livestream hotuba yako.

Mahali pengine, PW16 alizungumzia kwa kirefu Inspector Andrew Chulu.

Nilipomuuliza kama amesoma maelezo ya Andrew Chulu, akasema:

“Nimesoma maelezo ya PW17 na Andrew Chulu,” katika ukurasa wa 469.

Katika maelezo yake, Askari Polisi Andrew Chulu na mwandishi wa habari wa Jambo TV wanasema ni waandishi wa habari wa Jambo TV ndiyo waliorekodi na kusambaza video katika mitandao ya Jambo TV.

Baadaye akabadilisha maelezo yake katika re-examination, ukurasa wa 466.

Waheshimiwa Majaji, niende kwa shahidi wao PW17.

Huyu ni star witness wa kesi yao.

Yeye ndiye anayeweza kusema ukweli—kama nina hatia au nimewekwa gerezani bure.

Maneno ya PW17, maelezo yake yapo katika ukurasa wa 490.

PW17 anasema yeye na wenzake walitumwa na boss wao kwenda Makao Makuu ya CHADEMA, Mikocheni, kwenda kutangaza mkutano.
 
TUNDU LISSU ANAFANYA MAJUMUISHO YA MWISHO MAHAKAMANI

SEHEMU YA 8️⃣

PW17 akaendelea kusema:

“Tulipofika Makao Makuu ya CHADEMA, we were prepared to cover the meeting and livestreaming.”

“We used the camera to footage to mainstream the meeting.”

📺 Kwa hiyo, walitumia mtandao wao wa Jambo TV kutangaza.

Na jina walilotumia kurusha matangazo lilikuwa Jambo TV.

Kwamba hilo wazo la kutangaza live lilikuwa la kwao, wala siyo la mtu mwingine.

Ukurasa wa 492.

Yote hii ni examination-in-chief ya shahidi wao.

Hapo alikuwa hajahojiwa na mimi hata kidogo.

Amekubali kula kitu. 😄

Waheshimiwa Majaji, katika mashahidi wote 17—mashahidi 12 wa upande wa mashtaka na 5 wa utetezi—huyu alikuwa shahidi mwepesi zaidi.

⚽ Kama ni goli la kujifunga wenyewe, ni kosa la kumleta shahidi PW17.

Tena goli la kisigino! 😂

Kwa jinsi huyu shahidi alivyojifunga, wala hawaku-re-examine.

The case was finito.

😂 MAHAKAMA KICHEKO!

Ushahidi huu unaiambia nini Mahakama?

Katika kesi ya Makonyo John @ Kibuna vs Republic, ushahidi huu, Waheshimiwa Majaji, siyo wa kuaminika.

Hakuna Mahakama inayoitwa Mahakama ya Sheria itakayotumia ushahidi huu.

Totally unreliable and completely not credible.

⚠️ Na hii siyo kesi ya kuku. Ni kesi ya uhaini, inahusu maisha ya watu.

Waheshimiwa Majaji, ushahidi wa utetezi ukoje?

Ushahidi wa utetezi ukinyooka.

Ukurasa wa 592 ni ushahidi wangu. Nilisema everywhere waliorusha matangazo siyo mimi.

Na vilevile upo ukurasa wa 621.

Na ukurasa wa 622.

(Oyaa huyu Lissu sio poa)

WEKA EMOJI KAMA UNASOMA

SHARE ZAIDI UJUMBE UFIKE MBALI.
 
TUNDU LISSU ANAFANYA MAJUMUISHO YA MWISHO MAHAKAMANI

SEHEMU YA 9️⃣

Ukaungwa mkono na DW2, DW3, DW4 na DW5.

Mashahidi wote wa utetezi walikuwa consistent kwamba walio-rusha matangazo na kadhalika walikuwa wafanyakazi wa Jambo TV.

Walisema hivyo katika examination-in-chief, na walisema hivyo pia wakati wa cross-examination.

Lakini kubwa kuliko yote, utetezi huu uliungwa mkono na PW17, aliyekuwepo katika mkutano na ndiye aliyerusha matangazo.

Waheshimiwa Majaji, nataka kufunga hoja hii kwa kusema machache tu juu ya sheria.

Hoja hii ya publication ya video/images, nimesema mwanzo, haipo kabisa katika sheria niliyoshtakiwa nayo.

Nataka kusema masuala ya habari yanaongozwa na Sheria ya Huduma za Habari ya mwaka 2016.

Mtu yeyote akitaka kujua nani anayewajibika katika kurusha matangazo ya redio na mitandao—

Kifungu cha 7(1) ndicho kinachosema nani mwenye haki ya kuhariri na kusambaza taarifa zinazorushwa katika televisheni.

Nani ana haki na matangazo hayo, na nani anayeyamiliki.

7.-(1) Every media house and journalist shall enjoy the following rights—

(a) freedom to collect or gather information from different sources;

(b) freedom to process and edit information in accordance with professional ethics governing journalists; and

(c) freedom to publish or broadcast news.

Kwa kifungu hiki, ile “nonsense” inayoitwa Constructive Publication imekufa on arrival.

Kwa sababu mwandishi au chombo kinachokusanya habari ndicho chenye habari.

Hakuna Constructive Publication hapa.

Waheshimiwa Majaji, hapa sitaki kuzungumzia maumivu ya kukaa gerezani mwaka mmoja na nusu.

Ina simanzi na ni masikitiko yangu kwa State Attorney kunishtaki kwa jambo ambalo halipo.

Ambapo siku ya kwanza wangeweza kuona kwamba hakuna kosa.

Na hii itaenda hadi kwenye compensation.

Wameniweka gerezani kwa hoja ya uongo.

Nina watoto na familia, nawekwa gerezani kwa kosa ambalo halipo.

Naishi kwenye kachumba ka futi sita, wakati nina nyumba nzuri tu.

Wanatungia watu makosa ya uongo.

Na mimi ninayeburuta miguu kwa kutembea, nikiwa na risasi mwilini, kwa nchi yangu nzuri.
 
TUNDU LISSU ANAFANYA MAJUMUISHO YA MWISHO MAHAKAMANI

SEHEMU YA 1️⃣0️⃣

“I can imagine kwa watu ambao sio wajanja kama mimi sijui wanafanywaje.”

Wanajua sijatenda kosa tangu siku waliponikuwa. Kila mtu anajua hilo.

JAJI NDUNGURU:
“Tuendelee, nimeshaandika.”

🗣️ LISSU:
Kwa hiyo nahitimisha kwa kusema hoja ya sita ni NEGATIVE.

HOJA YA SABA

Waheshimiwa Majaji, hoja ya saba ni:

Je, Serikali ilitishwa na hayo maneno?

Hoja hii inazungumzia matokeo ya nia ya kutenda uhaini chini ya kifungu cha 39(2).

Waheshimiwa Majaji, huwezi kuona hilo katika kesi ya Gray Likungu Mattaka.

Na watu wengi hawajui kwamba kesi ya Gray Likungu Mattaka ndiyo kesi ya Bibi Titi Mohamed.

Bibi Titi Mohamed alikuwa Mwenyekiti wa kwanza wa UWT na mpigania uhuru wa nchi hii.

Ule mtaa unaoitwa Bibi Titi Mohamed umepewa jina lake. Yeye ndiye aliyeshitakiwa kwa uhaini.

Tunaita kesi hiyo Gray Likungu Mattaka kwa sababu ndiye aliyekuwa mshtakiwa namba moja.

Mahakama ni mahali pa kuelimishana pia.

Katika kesi ya Gray Likungu Mattaka, haikufika katika hatua ya intention.

Na ndiyo maana juzi nilisema Mahakama hii ina nafasi ya kuweka historia.

Mahakama hii sasa inaweza kujielekeza katika kifungu cha 10(2).

Kama nia ni kutenda kosa, basi matokeo yaliyokusudiwa kutendwa na nia hiyo lazima yasemwe na yathibitishwe kwa ushahidi.

Waheshimiwa Majaji, kwa maana hiyo, upande wa mashtaka ulitakiwa kuonyesha kwenye hati ya mashtaka, inayotuhumu kwamba kulikuwa na nia ya kuitisha Serikali ya Jamhuri ya Muungano.

Walitakiwa kuonyesha matokeo ya nia hiyo—Serikali ya Jamhuri ya Muungano ilitishika au haikutishika.

Na walitakiwa kuonyesha katika Information kwamba, walipokuwa wakileta huo ushahidi, Serikali ya Jamhuri ya Muungano ilitishika au haikutishika.

Upande wa mashtaka haukuonyesha hilo kwenye hati yao ya mashtaka (Information).

Walifikiri unarusha mashtaka hivi, litakalompata na limpate.

Hawakubainisha katika mashtaka kwamba:

«“Any particular shown how the Executive of the United Republic has been intimidated.”»

That failure to show the results makes the case defective.

Essentials of the Information must be shown.

Lazima uonyeshe vielelezo vya mashtaka, na usipovionyesha, hati ya mashtaka ni batili.

Siyo tu kwamba hawakuonyesha vielelezo kwenye hati yao ya mashtaka; vilevile hawakuonyesha ushahidi wowote kuhusu jinsi Serikali ya Jamhuri ya Muungano ilivyotishika.

Serikali ya Jamhuri ya Muungano ipo katika Sura ya Pili ya Katiba.

Yote yanaelezea Serikali ya Jamhuri ya Muungano.

Serikali ya Jamhuri ya Muungano inaongozwa na Rais.

Ndiyo Kiongozi Mkuu wa Serikali na ndiye Amiri Jeshi Mkuu.

Akipaswa aje atoe ushahidi kama Serikali yake imetishika.

Mimi niliomba aitwe.

Walionishtaki wakapinga vikali, na Waheshimiwa Majaji mkanikubalia.

Mimi, ambaye nilishtakiwa, nilitaka aitwe, lakini hakuna.
 
TUNDU LISSU ANAFANYA MAJUMUISHO YA MWISHO MAHAKAMANI

SEHEMU YA 1️⃣1️⃣

Mimi nilijua kifungu cha 10(2) kinataka nini, lakini hakuna.

Vilevile, Waheshimiwa Majaji, Serikali ya Jamhuri ya Muungano ina Makamu wa Rais, na wakati ule alikuwa anaitwa Philip Isdory Mpango.

Mimi niliomba aitwe. Upande wa Serikali ulipinga vikali, kwa hiyo hakukuwa na ushahidi wake, na Waheshimiwa Majaji mliwakubalia.

Mtu wa tatu anayeunda Serikali, kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano, ni Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Wakati ule alikuwa anaitwa Majaliwa Majaliwa.

Yeye ndiye Kiongozi Mkuu wa Shughuli za Serikali na Kiongozi wa Bunge.

Mimi niliomba aitwe, lakini mkanikatalia.

Serikali inaundwa na Mawaziri; hakuna hata Waziri mmoja ambaye amekuja.

Serikali inaundwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, lakini hakuja.

Serikali inaundwa na Mkurugenzi wa Mashtaka, lakini hakuja.

Serikali inaundwa na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, lakini hakuna kiongozi hata mmoja kutoka Serikali ya Mapinduzi Zanzibar aliyekuja.

Serikali inaundwa na Wakuu wa Vyombo vya Dola, lakini hakuna hata mmoja aliyekuja.

Niliomba afike hapa Mkurugenzi wa Idara ya Usalama wa Taifa na Ujasusi, lakini Serikali ilipinga na Waheshimiwa Majaji mkawakubalia.

Mlinikubalia waje Mkuu wa Majeshi, IGP na Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai.

Kingai alikuja, lakini alinikatalia kutoa ushahidi.

Kwenye rekodi, hakuna hata mmoja aliyekuja kuthibitisha kama Serikali ilitishika.

Kama Serikali haikutishika, maana yake sina kosa.

Upande wa utetezi hatukuwa na burden yoyote kuthibitisha hili.

Burden ilikuwa kwao, lakini wameshindwa kuthibitisha, na hata kujaribu wameishindwa.

Tuna kesi ya uhaini, na wale wanaosema tumeitisha Serikali hawajajaribu hata kuthibitisha hata Mkuu wa Wilaya fulani.

Waheshimiwa Majaji, hawa nilio wataja kutokufika kwao Mahakamani kuna maana gani?

Maana yake ya kutokumwita ni kwamba walizuia asije, kwa sababu kesi yote imejengwa kwenye misingi ya uongo.

Kwa hiyo, Waheshimiwa Majaji, naiomba Mahakama iseme kwamba wangekuja wangesema ukweli, ndiyo maana hawakuitwa.

More importantly, jibu la swali la saba, Waheshimiwa Majaji, can only be NEGATIVE.

Jibu la swali hili ni:

SERIKALI HAIKUTISHWA.

🗣️ LISSU:
Wangekuwa wametishwa, wangeitwa Mahakamani.

Jibu la hili ni HAPANA, HAWAKUTISHIKA.

Naomba twende mapumziko, tutakuja kuzungumzia masuala mengine.

JAJI NDUNGURU:
“Upande wa mashtaka mnasemaje?”

NASSORO KATUGA:
“Waheshimiwa, hatuna pingamizi, isipokuwa hatujajua ni saa 1 au saa 1 na nusu.

Tuombe Mungu amalize akirudi.”

🗣️ LISSU:
“Saa 1 na nusu, Waheshimiwa Majaji.”

Off the record:
“Ni kwamba nakesha usiku kufanya kazi hii.

Ninapoomba kupumzika kwa saa 1 na nusu, ni ili nipate kupumzisha mwili kidogo.”

JAJI NDUNGURU:
“Kwa mengi hayo hayo, kwa leo tuishia hapa. Tuendelee siku ya Jumatatu saa 3:00 asubuhi.”

🚶🏾‍♂️ MAJAJI WANATOKA.
 
MARIDHIANO HAYAJI KWA NJIA ZA UTAPELI!

Mtu aliyetambulishwa kama Mwenyekiti wa Baraza la Wazee wa CHADEMA (BAZECHA) Kanda ya Kati (Morogoro, Singida na Dodoma, Acquilin Magalambula amenukuliwa akisema CHADEMA waingie maridhiano na serikali hata kama Lissu hajatoka gerezani.

Mtu ambaye aliyetambulishwa kama Katibu wa CHADEMA wa Mkoa wa Morogoro, Barnabas Okola amenukuliwa akiwashambulia Mhe. Jaji Joseph Warioba na Mhe. Anna Tibaijuka.

Lakini uchambuzi wa picha mjongeo (video) na mazingira ya mikutano yote miwili insonyesha kuwa ni mkutano mmoja kwa sababu mavazi ya wahudhuriaji yanafanana na watu wengine nyuso zao ni zile zile na kipaza sauti ni kile kile na hata wasambazaji wa video hizo ni watu au media zenye mrengo wa CCM.

Lakini waandaji wa mkutano huo ni watu wa ajabu sana. Wanasukuma maridhiano lakini hawataki Lissu atoke gerezani. Wanasukuma maridhiano lakini wanawashambulia Mhe. Jaji Joseph Warioba na Prof. Tibaijuka.

Lakini jambo lingine ni kuwa mikutano yote ya CHADEMA ina muktadha unaojulikana na hata hupambwa na bendera za chama chao na hukuwa wanachama wao wakivalia mavazi ya chama chao.

Pia, hata viongozi wa CHADEMA wakiwa katika mikutano yao lazima waseme kauli mbiu zao kama 'People's Power', nk. Lakini muktadha na mazingira ya mkutano huo au mikutano hiyo ni kinyume kabisa.

Sisi askofu tunataka kuwaeleza watu ambao wako nyuma ya mkakati huo wa kurubuni watu kwa kuwatumia watu ambao hujinasibu kama viongozi wa CHADEMA. Ujumbe wetu ni kuwa maridhiano ya kweli hayajengwi kwa kutumia njia za ulaghai, utapeli au udanganyifu. Kama CCM na serikali yake wanataka kweli kufanya maridhiano ya kweli waache kulaghai watu au kudanganya watu kwa njia hizo.

Kwa nini kauli za watu wanaohujumu ukweli na kukihujumu CHADEMA na viongozi wake pia zipate nafasi katika media za watu ambao ni wale walio karibu na CCM na serikali yake?
Je, nini kimekushangaza? Je, nini maoni yako?

Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!
Askofu Emmaus Bandekile Mwamakula
Itunge, Dar es Salaam; 9 Septemba 2026; Saa 5:55 usiku.View attachment 3667243
Wanao lazimisha CDM iingie kwa ujinga wa maridhiano ni matapeli hasaaa.

Hua wanatamba kua CDM hataidipokuepo wao wataridhiana tuu. Sasa nini kinawashinda ku move on bila CDM?
 
Wadau nikaomba muongozo wapi nitazipata update mkanikaushia😂.
Hatimaye nimefika hapa na nimezichakata nondo zote jana na leo tuombe uzima hiyo jtatu.
Ingekua si mambo ya vyama vyama huenda mamlaka zingeamua rasmi kuungana na wapinzani walau taifa lifaidi kichwa kinachojua sheria kama mshtakiwa 🙌.
Possibly upande wa mashtaka nao wamejipanga na hoja zao ila waliacha mianya mingi kwenye maandalizi ya kesi yao mwamba anayaanika tu.
 
Back
Top Bottom