MamaSamia2025
JF-Expert Member
- Mar 29, 2012
- 10,090
- 22,370
Binafsi mimi ni kijana mdogo wa miaka 38 na mwanachama wa Chama Cha Mapinduzi. Huu uzi umeandikwa na kijana. Pamoja na kujitambulisha ila kama kichwa cha habari kinavyosomeka imefika sehemu kama taifa tunahitaji mjadala kuhusu upi ni umri sahihi wa mtu kuendelea kuitwa kijana tofauti na hali ilivyo kwa sasa. SABABU KUU YA KUULIZA ni kuwa karibu kila sekta utakuta kuna wazee wanaojiita vijana hali inayowanyima fursa wale vijana halisi kiumri. HII HAIKUBALIKI.
Kwa mfano huko CHADEMA utakuta kundi la Heche, Lema, Sugu, Halima Mdee, Hawa Bananga, Mnyika, na Cecilia Pareso nao wanatajwa kama vijana. Tena bila aibu hata wao hujiita viongozi vijana. Sio sawa. CCM utakuta mtu kama Kigwangala, Nchemba, Bashe, Silaa, Ridhiwani, hata Nape kwamba ni wabunge vijana.. inashangaza sana.
Ndugu wanaJF mnadhani ujana hukomea miaka mingapi?