Ni upi muda/umri sahihi wa mtu kufurahia maisha?

mlinzi mlalafofofo

JF-Expert Member
Apr 20, 2008
278
548
Ukiwa bado kijana mbichi unaambiwa - we mwana usichezee maisha - usubiri muda wako sahihi utafika uko mbeleni utakula maisha adi uchoke

Ukifika umri wa kati bado unakuta vibao vya hatari kila kona - unatahadharishwa usichezee maisha, ujijenge kwa baadae mara ooh taifa bado linakuhitaji.

sasa ukiamua kujitoa ufahamu kidogo ukawa unafanya tu mambo yako mwenyewe, unaonekana kama mtu aliyepoteza mwelekeo wa maisha na asiyejielewa kabisa.

Cha ajabu ukizubaa kidogo, kabla haujakaa sawa kule mbeleni utawaskia walimwengu haohao ooh huyu hana jipya, amezeeka - amepitwa na wakati/zama zake zimeshapita!

Sasa wakuu wakati gani ni muafaka kwa mtu kufurahia maisha kwa ubora wake bila vikwazo.
 
Itoshe kusema ukiwa mzima huumwi popote hiyo ni furaha ya kwanza na ndiyo ya msingi.

Mengine ni ya ziada tu,na hakuna kinachoitwa muda maalumu wa kuyafurahia maisha kwa binadamu anayepumua,hao akina Bahakresa tunaosikia ni matajiri wa taifa ukienda leo kuwauliza wanafuraha na maisha yao watakwambia hawana sababu kutaka kwao hela zijae kumewapa maradhi sukari pressure etc.
 
Itoshe kusema ukiwa mzima huumwi popote hiyo ni furaha ya kwanza na ndiyo ya msingi.

Mengine ni ya ziada tu,na hakuna kinachoitwa muda maalumu wa kuyafurahia maisha kwa binadamu anayepumua,hao akina Bahakresa tunaosikia ni matajiri wa taifa ukienda leo kuwauliza wanafuraha na maisha wanakwambia hawana sababu kutaka kwao hela zijae kumewapa maradhi sukari pressure etc.
Kabisa mkuu.mengine yatajisumbukia.
 
Itoshe kusema ukiwa mzima huumwi popote hiyo ni furaha ya kwanza na ndiyo ya msingi.

Mengine ni ya ziada tu,na hakuna kinachoitwa muda maalumu wa kuyafurahia maisha kwa binadamu anayepumua,hao akina Bahakresa tunaosikia ni matajiri wa taifa ukienda leo kuwauliza wanafuraha na maisha yao watakwambia hawana sababu kutaka kwao hela zijae kumewapa maradhi sukari pressure etc.
ni sawa, lakini hakuna ugonjwa mbaya kama umasikini, japo una tiba
 
ni sawa, lakini hakuna ugonjwa mbaya kama umasikini, japo una tiba
Kwenye uwanja wa utafutaji iko hivi,maskini akipata ya kula leo na nauli ya watoto kwenda shule kesho anashukuru analala anaacha maisha yaende kama yanavyotaka lakini tajiri anataka kile alicholala nacho leo kesho kiongezeke so wakati maskini anakoroma usiku kuupa mwili haki yake ya kupumzika tajiri anauchosha kwa kuwaza jinsi ya kuongeza kipato.

Mimi nikiwa na mzunguko wa hela kila saa kichwani kunazunguka ideas nifanyeje million moja izae nyengine ikija nataka tena tena na tena mwisho kule kuwaza sana kunauathiri mwili wangu naanza kukutana na maradhi,nina mdogo wangu (35yrs) ana Fuso tipper 3,Coaster za abiria mbili Noah 3 ameshaanza kutoka mvi na kipara kichwani yote ni anawaza jinsi ya kui-handle cash.

Nimekupa mfano huo,ukiwa maskini ni rahisi kuikubali hali (well umaskini siyo mzuri hata kidogo lakini una mazuri yake) lakini pia ukishaanza kuingia kwenye mfereji wa hela ni vigumu kutoka salama au kukaa salama maana ”ukizishika zikaisha zinakuachia maradhi na jinsi unavyokazana zijae zinakuletea maradhi”
 
Hapana mkuu Tatizo huwa Ni kwamba "Mgumba akipata Mimba lazima makorido Yajae mate na lazma avae nguo za kubana ili muone tumbo"
unaupenda huu msemo, mgumba akipata mimba atatema mate kila mahali mjue"
Kwenye uwanja wa utafutaji iko hivi,maskini akipata ya kula leo na nauli ya watoto kwenda shule kesho anashukuru analala anaacha maisha yaende kama yanavyotaka.

Mimi nikiwa na mzunguko wa hela kila saa kichwani kunazunguka ideas nifanyeje million moja izae nyengine ikija nataka tena tena na tena mwisho kule kuwaza sana kunauathiri mwili wangu naanza kukutana na maradhi,nina mdogo wangu (35yrs) ana Fuso tipper 3,Coaster za abiria mbili Noah 3 ameshaanza kutoka mvi na kipara kichwani yote ni anawaza jinsi ya kui-handle cash.

Nimekupa mfano huo,ukiwa maskini ni rahisi kuikubali hali (well umaskini siyo mzuri hata kidogo lakini una mazuri yake) lakini pia ukishaanza kuingia kwenye mfereji wa hela ni vigumu kutoka salama ni kusema ”ukizishika zikaisha zinakuachia maradhi jinsi unavyokazana zijae zinakuletea mahari”
mkuu ningechagua, bora nichague upara kuliko kupata leo kesho umekosa 😂
 
Ninachojua mimi ni kwamba kusubiria mpaka ndoa ili ufanye ngono ni ulimbukeni wa hali ya juu....

mengine watakuja kuongezea
Kwani kula .aisha ni ngono peke yake? Toto la zinaa hilo, linawaza ngono tu na ndio maana linachonga nyusi. Hakuna ulimbukeni katika kujitunza na kujiheshimu. Umalaya una hasara nyingi sana. Pole najua, una jina mahaba ndio yanakufanya useme hovyo.
 
Back
Top Bottom