Ni muhimu kuwa na ukomo wa umri wa mtu kuwa Rais Tanzania

OLS

JF-Expert Member
Oct 12, 2019
419
670
Nchi kadhaa zimekuwa na mijadala juu ya ukomo wa umri ambao rais anatakiwa kutovuka ili kuendelea kutawala. Hata hivyo, baadhi ya marais wamekuwa wakibadili katiba zao ili kuhakikisha wanabaki madarakani. Hii sio shida lakini ni muhimu ukomo wa umri uwepo ili kutokuwa na marais wazee ambao maamuzi yao yanaweza kuathiri taifa kama ilivyotokea kwa nchi kadhaa barani Afrika.

Katiba ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Ibara ya 39(1)(b) imeweka kwamba mgombea urais ni lazima awe aliyetimiza miaka 40. Katiba hiyo hiyo haijataja ni je mtu akizidi umri upi hatofaa kugombea urais. Hili jambo ni muhimu sana kuwa nalo.

Kwa sasa Life Expectancy ya mtanzania ni miaka 66, lakini mara nyingine tumechagua watu waliozidi umri huo kwa kuwa hakuna ukomo wa umri wa mgombea urais. Hii sio tu inasema tutakuwa na marais wazee bali pia uzee unaambatana na magojwa na sisi tuna huduma mbovu za awafya ambazo zitatufanya tuwe tunafanya uchaguzi mara kwa mara au kuwafanya watu wengine kuwa marais baada ya wengine kufariki.

Tukiangalia mfano wa waliogombea urais mwaka 2015, wale waliokuwa vinara wagombea urais mwaka 2015, wengi wao walikuwa na miaka zaidi ya 60. Aidha imekuwa ni kama tamaduni sasa kwamba mtu akiwa na miaka isiyozidi 50 akigombea urais akaitwa 'kijana' na inaweza kuwa kikwazo hata kama katiba imeruhusu kugombea. Hebu fikiria Kikwete kuitwa kijana kwa sababu ya umri wake alioingia nao kwenye urais.

Suala la kutokuwa na ukomo wa urais limetengeneza tamaduni isiyoandikwa ya kuwa mtu kugombea urais lazima awe na miaka isiyopungua sitini. Mimi naona ni muhimu katiba iseme Rais asizidi miaka 65. Yaani aingie na miaka ambayo hata akitoka anakuwa hajafikia umri wa ukomo, ili tusije chagua mtu mwenye miaka 65 akakaa madarakani hadi akafika miaka 75, hatari inakuwa ni ile ile.

Nawasilisha.
 
Hii sio shida lakini ni muhimu ukomo wa umri uwepo ili kutokuwa na marais wazee ambao maamuzi yao yanaweza kuathiri taifa kama ilivyotokea kwa nchi kadhaa barani Afrika.
Hujafafanua maamuzi yapi yanayoweza kuathiri taifa kutokana na umri
Katiba ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Ibara ya 39(1)(b) imeweka kwamba mgombea urais ni lazima awe aliyetimiza miaka 40. Katiba hiyo hiyo haijataja ni je mtu akizidi umri upi hatofaa kugombea urais. Hili jambo ni muhimu sana kuwa nalo.
Hata miaka 40 sikubaliani nayo. Ni kigezo gani kimetumika kubaini kwamba umri huo ni muafaka kwa nafasi ya Urais.
Nyerere alikuwa Kiongozi wa Taifa Tanganyika akiwa na umri wa miaka 39, kwa maana kwamba miaka 10 alitumia katika mobilization. Ni wazi alianza harakati za kudai Uhuru akiwa na miaka 29. Kwanini tudhani miaka 40 ni muafaka.

Baraza la Mawaziri la Kwanza la Nyerere waliokuwa na miaka 40 ni wawili kama sikosei. Waliobaki walikuwa chini ya hapo wengine wakiwa na miaka 28 n.k.

Hoja ya ukomo ina mantiki, kwa bahati mbaya haiwezi kufikiriwa kwasababu 'watuhumiwa' bado wanavizia nafasi

Hoja yako itakuwa na mantiki kama tutaanza na KATIBA ili kipengele hicho kiingizwe.
Nakubaliana nawe kabisa kuhusu ukomo, lakini huwezi kupata suluhu hadi Katiba mpya

Nasikitika kwamba Vijana wanaotakiwa kuliona hili kwa jicho la katiba ndio wamejivika vyeo vya 'uchawa'
 
Kiafrika Rais ana nguvu kubwa sana, mtu akizeeka uwezo wake wa maamuzi hupungua, hivyo kuwa na marais wazee ni kujiingiza kwenye hatari zaidi ya kupata maamuzi mabaya yatakayoathiri taifa kutokana na nguvu ya rais na umri wa rais.

Suala la tuanze na umri gani kwa mtu kuwa rais, kwanini miaka 40. Hii ni hoja nyingine, hata hivyo kwa kuwa rais ni ngazi kubwa ya kimaamuzi tunaweza kutumia vigezo vya kiuzoefu kupata rais, lakini tukawa na ukomo wa umri.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom