MJADALA: Umuhimu wa Chanzo Dhidi ya Saratani ya Mlango wa Kizazi kwa Wasichana (Miaka 9-14)

JamiiTalks

JF Advocacy Team
Aug 7, 2018
648
1,000
Saratani.jpg

JE, WAJUA msichana anayeanza kushiriki ngono katika umri mdogo anakuwa katika hatari zaidi ya kupata Saratani ya Mlango wa Kizazi endapo atakuwa hajapata Chanjo ya HPV?

Takwimu za Wizara ya Afya Tanzania zinaonesha aina 4 ya Saratani zina idadi kubwa ya Wagonjwa nchini kulinganisha na Saratani nyingine

Saratani ya Mlango wa Kizazi inaongoza kwa 23% ya Wagonjwa ikifuatiwa na Saratani ya Mfumo wa Chakula 11%, Saratani ya Matiti 10.4% na Saratani ya Tezi Dume 8.9%

Ungana nasi leo Aprili 27, 2024, Saa 10:00 Jioni katika Mjadala utakaokuwa na Wataalamu wa Afya kutoka Wizara ya Afya na Chama cha Madaktari Wanawake Tanzania (MEWATA) kupitia XSpaces ya JamiiForums

Kushiriki Mjadala Bofya https://jamii.app/HPVSpaces

Chanjo ya Human Papillomavirus (HPV) inatolewa na Serikali kwa Wasichana wenye umri wa Miaka 9 hadi 14 kwa ajili ya kuwakinga dhidi ya Ugonjwa wa Saratani ya Mlango wa Kizazi

Saratani hiyo inaweza kuzuilika kwa kupata Chanjo na kutibika endapo Mgonjwa atawahi Matibabu

DKT. NTULI KAPOLOGWE (Mkurugenzi Kinga, Wizara ya Afya): Chanjo ilianza Mwaka 1975 hadi Mwaka 2024 tumekuwa na Chanjo 10 za kuweza kudhibiti Magonjwa 14.

Serikali imeamua kutoa Chanjo ya HPV kwa kuwa Saratani ya Mlango wa Kizazi imekuwa changamoto kubwa Nchini, inaongoza kwa kuwa na Asilimia 23 ya Wagonjwa tofauti na Saratani nyingine zote.

Kutibu au kujiuguza Saratani ni gharama kubwa ndio maana Serikali imeungana na Serikali nyingine Duniani kwa ajili ya kuhamasisha kupata Chanjo ya HPV ili kujikinga

Nchini Tanzania, Mkoa wa Kilimanjaro unaongoza kwa kuwa na Wagonjwa wengi ukifuatiwa na Dar es Salaam na Mwanza

DKT. FLORIAN TINUGA (Meneja Mpango Chanjo): Chanjo ya Saratani ya Mlango wa Kizazi ilianza kutolewa Mwaka 2014 Mkoani Kilimanjaro, baadaye Mwaka 2018 ikaelekezwa Nchi nzima

Chanjo ya HPV ilianza kwa dozi mbili za Chanjo kwa Wasichana wa Miaka 9-14

Mwaka 2024, kwa kuzingatia tafiti ilionekana kutoa dozi moja na mbili zote ni sawa

Tafiti hizo zilifanyiwa tathmini na Shirika la Afya Duniani na ukatolea mwongozo wa kutolewa Dozi moja

Kuanzia Aprili 2024 kulikuwa na mabadiliko kutoka Dozi mbili na kuwa Dozi moja

Umri umezingatiwa kwa kuwa Sayansi imeonesha katiks umri huo ni wakati ambao dozi ya chanjo inaweza kufanya kazi kwa usahihi zaidi.

Chanjo hii ni salama, ni hiyari na kundi kubwa inawalenga Watoto ambao wapo shule na ndio maana wakafuatwa huko

Hadi kufikia Aprili 26, 2024, walengwa wa chanjo waliofikiwa katika walikuwa 90%

Baada ya kumalizika kwa kampeni, Chanjo hii itaendelea kutolewa katika vituo mbalimbali hadi Septemba 2024

Pia, itambulike kuwa chanjo inatolewa katika vituo vya Serikali na vile vya Binafsi

DKT. NORMAN JONAS (Daktari Mkufunzi Wizara ya Afya): Virusi vya HPV vinaathiri Binadamu, na Maambukizi yake yanapotokea hayana dalili

90% ya Wagonjwa wa Saratani ya Mlango wa Kizazi wanatokana na virusi vya HPV

Saratani ya Mlango wa Kizazi kuna wakati pia inaweza kuitwa Shingo ya Mlango wa Kizazi, hivyo unaposikia hivyo isikuchanganye

Saratani inayotokea eneo hilo inatokana na HPV, kuna aina zaidi ya 200 za HPV

Maambukizi ya Saratani ya Mlango wa Kizazi yanaweza kusambaa kwa kujamiiana

Ni moja ya magonjwa yanayotokana na ngono na kuathiri watu wengi

Tafiti za Kisanyansi zinaonesha umri sahihi wa kutoa Chanjo ni miaka 9 hadi 14 ikiaminika ni umri ambao ni kabla ya balehe.

Maambukizi ya Saratani ya Mlango wa Kizazi yanaweza kusababisha maumivu ya nyonga au maumivu wakati wa tendo la Ndoa

Virusi wa HPV hawasababishi Saratani ya Mlango wa Kizazi pekee, wanaweza kusababisha Saratani ya Koo, Mdomo, na Uume pia

Saratani inaathiri Wanawake kwa asilimia kubwa ndio maana hata #Chanjo imeanza na wao

Chanjo ya #HPV ni kinga namba moja ya Saratani ya Mlango wa Kizazi, kinga namba mbili ni kutofanya Ngono wakati wa umri mdogo

Hii Kinga namba mbili ipo kimaadili zaidi, kwa kuwa inawaepusha na Maambukizi mengine mbalimbali

DKT. NORMAN JONAS (Daktari Mkufunzi Wizara ya Afya):Ni vizuri Mwanamke akaanza uchunguzi wa Saratani ya Mlango wa Kizazi mapema, tunawashukuru sana Chama cha Madaktari Wanawake Tanzania (#MEWATA) kwa kuwa mstari wa mbele kuongoza kampeni ya Chanjo

Chanjo hii ni ya hiyari na inapatikana bila malipo Nchi nzima

Utoaji chanjo wa HPV unatolewa kwa Kampeni za Kitaifa kama inavyofanyika wakati huu. Pia, unatumia kampeni ndogondogo mfano katika maeneo kama Wilaya au Mkoa

Utafiti ulianza tangu Mwaka 2017, na ulionesha Wasichana wadogo wanapokea kinga vizuri na inaweza kufanya kazi vizuri kuliko Watu wazima

Maambukizi ya HPV yanasambaa kwa kujamiiana, asilimia kubwa wanaopewa Chanjo kwa umri tulioutaja wanakuwa hawajaanza kujamiiana

JOHN CHANGALUCHA: Mtafiti Taasisi ya NIMR: Tafiti zilizofanyika zilionesha kuwa uwezo wa Dozi moja ni mkubwa katika kuweka kinga mwilini (dhidi ya Saratani ya Mlango wa Kizazi)

Wakati utafiti wetu unaendelea, upande wa pili Nchini Kenya kulikuwa na utafiti kwa Wanawake wenye umri mkubwa na baada ya ufuatiliaji wa Miezi 36 ikaonekana Wasichana wetu walikuwa na kinga zaidi kuliko wale wenye umri mkubwa

Sisi Watafiti tunaendelea na utafiti wetu na tunawafuatilia wahusika 930 tuliowachanja ambao tuliwagawa katika makundi matatu, huu ni Mwaka wa 7 na tutawafuatilia hadi watakapofikisha Miaka 9 tangu tulipowapa chanjo kuona kama kutakuwa na madhara yoyote

Mpaka sasa hakuna madhara yoyote makubwa yaliyowapata washiriki tofauti na yale ya kawaida kama homa ambayo inaweza kutokea kwa mtu mwingine yeyote anayepata chanjo.

DKT. NTULI KAPOLOGWE (Mkurugenzi Kinga, Wizara ya Afya): Kutokana na utafiti wetu uliofanyika kuhusu chanjo hii, Nchi kadhaa zilizoendelea zilikuja kwetu kupata uzoefu wa tulichokifanya ikiwemo Uingereza

Kuna Nchi kama Norway na Australia wameshaanza kutoa chanjo kwa Watoto wa Kiume

HPV inaweza kusababisha Saratani mbalimbali ikiwemo ya Mdomo hasa kwa ambao wanashiriki Ngono kwa kutumia Mdomo

Tumeanza na Chanjo ya Wasichana huku Serikali ikiangalia namna kwa ajili ya makundi mengine

DKT. JOHN CHANGALUCHA: Mtafiti Taasisi ya NIMR:Chanjo zinaweza kutolewa kwa Wasichana wenye umri zaidi ya Miaka 14, kilicholengwa ni kupunguza kuwapa chanjo ambao tayari wameshaanza kujamiiana kwa kuwa ufanisi wa chanjo unapungua pale mlengwa anapokuwa ameshaanza kujamiiana

Shirika la Afya Duniani (WHO) lenyewe limetoa mapendekezo kutolewa Chanjo kwa Wasichana wenye umri wa miaka 9 hadi 20, nchi nyingine zinatoa hata kwa zaidi ya hapo

Hakuna utafiti ulioonesha chanjo hiyo ikitolewa kwa Msichana mwenye umri wa chini ya hapo kama atapata madhara

MARY ROSE (Daktari Bingwa Afya ya Jamii – JHPIEGO): Utatifi ulifanyika Nchi 9 ikiwemo Tanzania ulionesha Wasichana wengi wanaanza kujamiiana wakifikisha umri wa Miaka 15 na kuendelea, ndio maana hata chanjo hii imeanza kwa Wasichana wenye umri wa Miaka 9 hadi 14

Wanawake wenye umri wa Miaka 30 hadi 50 hao ndio wapo kwenye hatari kubwa ya kupata maambukizi, wanashauriwa wafanye uchunguzi kila baada ya Miaka mitatu

Uchunguzi unatolewa bure katika Vituo vyetu, unachukua chini ya dakika 11

Kundi lingine lililo hatarini kupata Maambukizi ya Saratani ya Mlango wa Kizazi ni Watu wenye Maambukizi ya HIV, wanashauriwa kufanya uchunguzi kuanzia wakiwa na umri wa Miaka 25

Kulazimisha Mtoto achomwe Chanjo kwa kumpa vitisho ni kinyume kabisa na utaratibu na hilo halitakiwi kufanyika
 
Nilisikia chanjo hiyo inafanya wasichana wakifika umri wa kupata watoto anakuwa hawezi, yaani anakua mgumba, je ni kweli?
 
View attachment 2975215

JE, WAJUA msichana anayeanza kushiriki ngono katika umri mdogo anakuwa katika hatari zaidi ya kupata Saratani ya Mlango wa Kizazi endapo atakuwa hajapata Chanjo ya HPV?

Takwimu za Wizara ya Afya Tanzania zinaonesha aina 4 ya Saratani zina idadi kubwa ya Wagonjwa nchini kulinganisha na Saratani nyingine

Saratani ya Mlango wa Kizazi inaongoza kwa 23% ya Wagonjwa ikifuatiwa na Saratani ya Mfumo wa Chakula 11%, Saratani ya Matiti 10.4% na Saratani ya Tezi Dume 8.9%

Ungana nasi leo Aprili 27, 2024, Saa 10:00 Jioni katika Mjadala utakaokuwa na Wataalamu wa Afya kutoka Wizara ya Afya na Chama cha Madaktari Wanawake Tanzania (MEWATA) kupitia XSpaces ya JamiiForums

Kushiriki Mjadala Bofya https://jamii.app/HPVSpaces

Chanjo ya Human Papillomavirus (HPV) inatolewa na Serikali kwa Wasichana wenye umri wa Miaka 9 hadi 14 kwa ajili ya kuwakinga dhidi ya Ugonjwa wa Saratani ya Mlango wa Kizazi

Saratani hiyo inaweza kuzuilika kwa kupata Chanjo na kutibika endapo Mgonjwa atawahi Matibabu

DKT. NTULI KAPOLOGWE (Mkurugenzi Kinga, Wizara ya Afya): Chanjo ilianza Mwaka 1975 hadi Mwaka 2024 tumekuwa na Chanjo 10 za kuweza kudhibiti Magonjwa 14.

DKT. NTULI KAPOLOGWE (Mkurugenzi Kinga, Wizara ya Afya): Serikali imeamua kutoa Chanjo ya HPV kwa kuwa Saratani ya Mlango wa Kizazi imekuwa changamoto kubwa Nchini, inaongoza kwa kuwa na Asilimia 23 ya Wagonjwa tofauti na Saratani nyingine zote.

DKT. NTULI KAPOLOGWE (Mkurugenzi Kinga, Wizara ya Afya): Kutibu au kujiuguza Saratani ni gharama kubwa ndio maana Serikali imeungana na Serikali nyingine Duniani kwa ajili ya kuhamasisha kupata Chanjo ya HPV ili kujikinga

Nchini Tanzania, Mkoa wa Kilimanjaro unaongoza kwa kuwa na Wagonjwa wengi ukifuatiwa na Dar es Salaam na Mwanza

DKT. FLORIAN TINUGA (Meneja Mpango Chanjo): Chanjo ya Saratani ya Mlango wa Kizazi ilianza kutolewa Mwaka 2014 Mkoani Kilimanjaro, baadaye Mwaka 2018 ikaelekezwa Nchi nzima

DKT. FLORIAN TINUGA (Meneja Mpango Chanjo): Chanjo ya HPV ilianza kwa dozi mbili za Chanjo kwa Wasichana wa Miaka 9-14

Mwaka 2024, kwa kuzingatia tafiti ilionekana kutoa dozi moja na mbili zote ni sawa

Tafiti hizo zilifanyiwa tathmini na Shirika la Afya Duniani na ukatolea mwongozo wa kutolewa Dozi moja

DKT. FLORIAN TINUGA (Meneja Mpango Chanjo): Chanjo ya HPV ilianza kwa dozi mbili za Chanjo kwa Wasichana wa Miaka 9-14

Mwaka 2024, kwa kuzingatia tafiti ilionekana kutoa dozi moja na mbili zote ni sawa

Tafiti hizo zilifanyiwa tathmini na Shirika la Afya Duniani na ukatolea mwongozo wa kutolewa Dozi moja

DKT. FLORIAN TINUGA (Meneja Mpango Chanjo): Kuanzia Aprili 2024 kulikuwa na mabadiliko kutoka Dozi mbili na kuwa Dozi moja

Umri umezingatiwa kwa kuwa Sayansi imeonesha katiks umri huo ni wakati ambao dozi ya chanjo inaweza kufanya kazi kwa usahihi zaidi
Mada inawahusu hii mje, cocastic uje na wenzako na nyie wenye watoto Mshana Jr Bujibuji Simba Nyamaume johnthebaptist Robert Heriel Mtibeli GENTAMYCINE
 
Back
Top Bottom