Nadhani anaweza kukasirika zaidi Ridhiwani kusikia jina hilo, siyo wewe. Lakini nikueleze tu katika jamii ukiwa kiongozi ahata baba wa familia ama mama wa familia kulingana na matendo yako unaweza kupewa jina ambalo watoto wako wanaweza kukuita bila ya wewe kujua. Jina hili linaweza kutokana na tabia yako ya ulevi ama umalaya n.k. angalia katika ofisi fulani mabosi pia wamekuwa wakipachikwa majina kadha wa kadha sembuse MKWERE, fuatilia kwa watoto wako utakuwa umepewa jina na nadhani watakuwa wamekupachika jina la Unonko kulingana na jinsi ulivyoweka Post yako humu.
1. Nyerere= Mchonga, Mussa, Nyag'au
2. Mwinyi = Shemeji, Ruksa
3. Mkapa = Mr Clean, Shot
4. Kikwete= Msanii, mkwere, Boys II men
Mengine mnaweza kuongezea hapa......