Wengi wa watanzania ni walalamikaji tu, hawawajibiki kwa makosa yao wenyewe. Mimi sioni sababu ya kumsema vibaya rais wetu Mpendwa JK. Kwani hana makosa.
Watanzania wengi wanatumia uchaguzi vibaya na hawataki kuwajibika kwa makosa wafanyayo katika uchaguzi. JK hakujichagua mwenyewe, wala hakuchaguliwa na CCM tu. Bali alichaguliwa na watanzania wote na hivyo mnapomlaumu ni sawa na kujilaumu wenyewe, lakini kumlaumu kikwete ni kumbebesha mtu mzigo usio wake. Hapa watu wenye kustahili lawama ni watanzania waliomchagua.
Kama huamini hii subili Uchaguzi ujao pamoja na haya yote bado kikwete atashinda kwakishindo. Hebu tujiulize ni nani atakayemchagua? Kama si hawa hawa wanaolaumu leo. Mimi sioni sababu ya kulaumu na tukimlaumu yeye tunamuonea, tuwalaumu waliomchagua. Sisi tunapaswa kuchapwa na hali ngumu ya maisha. Kwani hakuna mwalimu mzuri duniani kama Maisha.
Wengi wa watu wanaolaumu hata hawapigi kura, kazi yao ni lawama tu. Kitu ambacho ni sawa na kelele za chura ambazo hazimzuii Tembo kunywa maji. Mtu muhimu kwa mwanasiasa ni mpiga kura, mpiga kura si mtu tu aliye na akili timamu namwenye kitambulisho cha mpiga kura. Mpiga kura ni mtu anaye piga kura anayeshiriki kupiga kura toka ngazi ya chama mpaka taifa. Kwani viongoza wanatoka kwenye chama, sasa wewe unasubili chama kikuchagulie halafu ukiletewa mbovu, hupigi kura. Hapa unaishia kulaumu tu.
Kila mtu ukimuuliza uchaguzi ujao vipi? Pamoja na kumlaumu sana atakuambia kuwa kikwete anashinda tu, wanasahau kuwa maneno huumba. Wakiisha umba wanarudi tena kulaumu. Ni bora kukaa kimya tu. Maana hata unaposema kikwete atashinda tu ni kuumba tu, wanakatisha watu tamaa ya kuleta mabadiliko. Utasikia CCM wanaiba kura, Je unapiga kura? Ni swali la kwanza kujiuliza.
Uchaguzi mwema.
kasyabone tall, mkubwa ni jalala, asipolaumiwa yeye, alaumiwe nani?.
Unapokuja na utetezi wa fulani dhidi ya shutuma au lawama dhidi yake, lazima kwanza uzipangue pili utoe wasifu wake, hivyo ili umtee vizuri rais wetu Kikwete, pangua hizo shutuma zake na lete mazuri yake yanayostahili sifa/pongezi.
Yes October, atachaguliwa tena kwa ushindi wa kishindo, sio kwa sababu ndie rais bora, ni kwa sababu tuu ya mazoea, Hata Rostam atachaguliwa tena Igunga, hata Chenge atachaguliwa tena kwa kishindo, vivyo hivyo kwa Lowassa, Dr. Msabaha na Karamagi, hata Mramba na Yona akiamua kugombea tena. Hata Mgonja.
Hata Liyumba angeachiwa jana, angegombea kupitia CCM na angeshinda sambamba na Rajabu Maranda, yoyote atakayegombea CCM kwenye maeneo ya Mazezeta, lazima ashinde, sio kwa sabanu ni msafi, bali kwa sababu Watanzania walio wengi bado ni mazezeta.
Good news, hawawezi kuwa mazezeta miaka yote, kuna siku wataamshwa na wataamka na kuacha uzezeta. Hiyo siku inakuja na haiko mbali sana, kama sio 2015 basi mwisho ni 2020!.