Abdulhalim
Platinum Member
- Jul 20, 2007
- 17,217
- 3,123
Kwa hiyo tukimpa heshima ndio matatizo yetu yatayeyuka!!??
Hiyo saini yako Hamad Rashid anaikumbuka kweli?ilia ni kweli wanakula woteHeshima gani unayomwombea ile ya kuilipa Dowans pale Movenpick au ile ya kuiba kura au ile ya kuua waandamanaji ni ipi iliyo nafuu unayoiona wewe tuanze nayo kumpa heshima, you must be joking.
Kamundu, nakuunga mkono rais aheshimiwe ndio maana anaitwa rais. Japo humu jamvini anadhaulika na kuitwa kwa kila aina ya majina. in reality kiukweli ukweli heshima yake kama rais iko pale pale, akipita sote huwa tunasimama tupende tusipende hizi lugha za kejeli humu jukwaani hazimkoseshi usingizi kwa sababu JK ni mtoto wa mujini na hizi ndizo lugha zake.
Kamundu said:uchumi wa dunia hasa kwa nchi zinazoendelea unakuwa kwa kasi hata Tanzania.
Kusimama wakati anapita si heshima Pasco you are missing the meaning of heshima hata train ikipita huwa tunasimama ipite hiyo si heshima. Hata Hitler alipokuwa akipita wote walikuwa wanasimama, heshima inatokana na busara ulizonazo towards wale wanaokuzunguka haitokani na uwezo ulionao.Kamundu, nakuunga mkono rais aheshimiwe ndio maana anaitwa rais. Japo humu jamvini anadhaulika na kuitwa kwa kila aina ya majina. in reality kiukweli ukweli heshima yake kama rais iko pale pale, akipita sote huwa tunasimama tupende tusipende hizi lugha za kejeli humu jukwaani hazimkoseshi usingizi kwa sababu JK ni mtoto wa mujini na hizi ndizo lugha zake.
read me in btn the lines. Nimesema raisi ni raisi heshima mbele ya kusimama akipita tunampa hizi lugha za kejeli humu jukwaani ndizo stahili yake maana yeye ni mtoto wa mijini au to be more specific, JK ni mtoto wa kihuni, hizi lugha ndizo lugha zake hazimkoseshi usingizi!.Kusimama wakati anapita si heshima Pasco you are missing the meaning of heshima hata train ikipita huwa tunasimama ipite hiyo si heshima. Hata Hitler alipokuwa akipita wote walikuwa wanasimama, heshima inatokana na busara ulizonazo towards wale wanaokuzunguka haitokani na uwezo ulionao.
Definition yako ya heshima ni ya mitaani zaidi maana hata mtoto mdogo akiwa na pesa kukuzidi utampa heshima hata kumwamkia(shikamoo).
KAMUDU
Nakubaliana na wewe kuwa Rais tuliye naye IS THE BEST PRESIDENT na ana mapenzi ya dhati kuhusu maslahi na ustawi wa nchi yetu na sio vizuri kumlaumu ilhali wa kulaumu ni sisi wenyewe. Kwa bahati mbaya watanzania tunajulikana kwa ufundi wa kulaumu na kutopenda kufanya kazi. Wengine hata wanauliza UHALALI wa RAis kama vile wao ndio kipimo cha uhalali. Sisi tulio na kumbu kumbu tunakumbuka kuwa hata Baba wa Taifa walikuwa wakimlaumu sana ingaWA SASA utawasikia wakimsifia (someni maandiko yao, yanawasuta).
Watanzania ni wepesi kwa kulaumu wengine bila kujiuliza binafsi kama sisi watanzania tunachapa kazi kwa bidii, tunaweka akiba na kuwekeza. Marekani na NCHI NYINGINE ZILIZOPIGA HATUA KUBWA ZA KIUCHUMI HAZIKUJENGWA na watu kila kukicha wanatafuta mchawi wa kulaumu. Hao CCM unaolaumu ni wananchi wengi wa kawaida ambao ni maskini na hawana uwezo. Ndugu zetu wa Kenya, Uganda na Rwanda wanatujua sisi watanzania kuwa ni watu wa maneno matamu na tusiopenda kufanya kazi. Bila kila mmoja wetu kufanya kazi kwa bidii, kujisomea kwa bidii, kulipa kodi, kuhakikisha kodi zinatumika katika kuwekeza katika elimu, uwezeshji na miundo mbinu, kupunguza kupiga soga, kupunguza kulaumu nchi yetu haitaendelea na kulaumu. Mchawi wetu ni tabia zetu sisi watanzania. Sisi ni wavivu na wepesi wa kulaumu wengine. Kwa sasa tutalaumu CCM, lakini yeyote atakayepata nafasi ya kuongoza Tanzania tutamlaumu tuu.
Wote tunajua kuwa nchi yetu inahitaji uwekezaji ili ipate mitaji ya kujenga nafasi za ajra na KIUCHUMI. Lakini Watanzania tunajulikana kwa kulaumu na kuwalaani wawekezaji.