Tumpe Rais Kikwete heshima yake

Tumpe Rais Kikwete heshima yake

ACHA UCHOCHEZI WEWE, WEWE JUHASIKIA MTU ANAUITA MWENZAKE WE MSUKUMA. MBONA UNAPENDA KUKUZA MAMBO, KAMA HUNA CHA KUANDIKA SIO MBAYA UKATULIA:nono:
 
Sio vibya labda yeye mwenyewe Muungwana aseme hataki kuitwa hivyo, na humu jamvini watani zake tuko weeeeeeeeeeeeeengi, by the way yeye mtu wa pwani utani sunna
 
Huu ni utani tu. Mkwere/Wakwere wana watani wengi sana kwa hiyo usijali. Mwenyewe amesema "Ukubwa jalala". Tulipokuwa shule kulikuwa na majina fulani tunawaita waalimu vilevile. Wasukuma, wangoni, wanyamwezi n.k. ni watani wa wakwere. Hata kuna usemi wa utani pia unaosema 'Mzigo mzito mpe mnyamwezi. Isiwe issue ndugu yangu.
 
POLENI WANA JF na smahani kama nitawakwaza wengine.
Nimekuwa nasoma post mbalimbali humu hasa zile za siasa hususani kuanzia mchakato,uchaguzi hadi matokoe yake.
Kifupi nimegundua member wengi wanaishabikia CHADEMA kama ambayo hata mimi naishabikia,naipenda na kuiamini.
Kutokana na kufuatilia post baadhi nikagundua wengi wanaochangia wana ukabila kwa kigezo kimoja. Kwamba baada ya mchakato mbovu uliomwingiza Kikwete madarakani na kwakua Kikwete alikuwepo madarakani na alikuwa kwenye nafasi ya kuweza kufanya mabadiliko lakini hakufanya kwa manufaa yake na chama chake,WATU wanamshambulia kama MKWERE*kabila* badala ya kama Kikwete au Rais aliyeshindwa kuleta matumaini aliyo ahidi 2005.
Wakati mimi naamini Kikwete ndiye anaeneza hofu ya UDINI,members wengi hapa wanaeneza UKABILA kwa hilo nililotaja hapo juu.
Members tujenge hoja za kutomtambua Kikwete kama rais bila kuhusisha kabila lake wala dini yake.
Hivi siku Wakwere wakisema mnalisema vibaya kabila lao kwa sababu ya Kikwete nao wakaanza Kulisema vibaya kabila la DR: SLAA au LIPUMBA,tutaweza kuvumilia na je ustawi wa nchi utakuwa wapi??[/QUOTE

Nawe pia ni MKWERE NINI???:teeth:
 
Mi pia naona haina tabu.. labda kwa sababu linasemwa kwa kiswahili ndo linasaundi kimajungu na kimazabe... SHAYCAS UNATAKA KUSEMA MTU AKISEMA MTANZANIA, MMAREKANI, MTANZANIA MWENYE ASILI YA KIMAREKANI, AU YA KIGANDA, AU YA KIHINDI....UTAUITA HUO UKABILA/UNCHI? hizi ni identity tu, ukizitumia vibaya zita-deliver ujumbe mbaya, & vaisi vesa..... MFANO KIHIYO LILIKUA JINA ZURI, LA HESHIMA KTK UTUMISHI WA UMMA, alipoLITUMIA VIBAYA... likawa fedheha... Kihiyo ikamaanisha kama unavojua (probably). so is everythng! SJUI UNATUELEWA????!!!
 
Wanaomwita kikwete Mkwere ni tofauti na wanaomwita Mzee Ruksa au Mchonga. Hii ya Kikwete imeanzishwa na wana Chadema hawa.

Kikwete anaitwa mkwere kwakuwa wakwere wanajulikana hawajasoma, kwahiyo wanamaanisha mkwere hastahili kuwa rais labda angekuwa mchaga!!!!
 
Wanao muita hivyo sijaona mahali wamemkashifu hivyo naamini kwamba hao ni watani zake kwani kwa TZ utani wa makabila ni kitu cha kawaida tu. Na hasa ukizingatia muungwana yu proud na kabila lake hivyo sioni tatizo kwenye matumizi ya kabila lake kama utambulisho wake.Sana sana naona kuna mapungufu katika kumuita mkwere bila kisifa ingependeza wakamwita "Mkwere One" ingekuwa na mjazo na ujiko zaidi.
 
mkwere ndo nickname yake mi ninayotumia it make me happy to use it
 
mkwere ndo nickname yake mi ninayotumia it make me happy to use it, siyo ukabila kumwita hivyo
 
upo sahihi,lakini kutoa kauli kama 'Mkwere nchi imemshinda, unafikiri ni sawa kwa ustawi wa nchi? Kwanini tusiseme tu kwamba Kikwete ameshindwa kuongoza nchi na badala yake anatakiwa afanye 1,2,3 nk?

Either "Mkwere nchi imemshinda" or "Kikwete ameshindwa kuongoza nchi" zote zinafikisha ujumbe maridhawa bila chenga.Kwani we mbona hapa unajulikana kama Shaycas wakati Jina lako Ni ........ Hamna mbaya, kwa kuwa yeye ni mkwere kweli and he must be proud of his tribe.At least I am.Aliyemaliza muda wake alijulikana kama Chinga na mambo yanasonga.
 
POLENI WANA JF na smahani kama nitawakwaza wengine.
Nimekuwa nasoma post mbalimbali humu hasa zile za siasa hususani kuanzia mchakato,uchaguzi hadi matokoe yake.
Kifupi nimegundua member wengi wanaishabikia CHADEMA kama ambayo hata mimi naishabikia,naipenda na kuiamini.
Kutokana na kufuatilia post baadhi nikagundua wengi wanaochangia wana ukabila kwa kigezo kimoja. Kwamba baada ya mchakato mbovu uliomwingiza Kikwete madarakani na kwakua Kikwete alikuwepo madarakani na alikuwa kwenye nafasi ya kuweza kufanya mabadiliko lakini hakufanya kwa manufaa yake na chama chake,WATU wanamshambulia kama MKWERE*kabila* badala ya kama Kikwete au Rais aliyeshindwa kuleta matumaini aliyo ahidi 2005.
Wakati mimi naamini Kikwete ndiye anaeneza hofu ya UDINI,members wengi hapa wanaeneza UKABILA kwa hilo nililotaja hapo juu.
Members tujenge hoja za kutomtambua Kikwete kama rais bila kuhusisha kabila lake wala dini yake.
Hivi siku Wakwere wakisema mnalisema vibaya kabila lao kwa sababu ya Kikwete nao wakaanza Kulisema vibaya kabila la DR: SLAA au LIPUMBA,tutaweza kuvumilia na je ustawi wa nchi utakuwa wapi??

Pumba kama za rais Mwizi.
 
Mkapa aka Chinga aliita wapinzani Kokoto nenda ukamshauri yeye kwanza manake huyo ndo alikosea.
 
Mbona huongelei kuhusu kuitwa kwake title kibao at a go? Mheshimiwa raisi Dr. Chifu Kikwete!
 
Mimi ni kati ya Watanzania ambao ninahofia sana maendeleo ya Tanzania kama wenzangu wengi sana hapa. Nina imani kuwa sababu za umasikini zinatokana na rushwa na ubinafsi mkubwa wa viongozi wetu wa serikali hasa CCM.

Lakini ndugu zangu Watanzania pamoja na hasira zetu Watanzania tumekuwa katika mazingira ya kuheshimiana hasa kwa wazee. Ndugu zangu naomba tuwache kumuita raisi majina na kimadongo na kikejeli kwasababu kufanya hivyo hakusaidii nchi!.

Nchi nyingi duniani kwa miaka kumi ijayo zitabadilika kwasababu uchumi wa dunia hasa kwa nchi zinazoendelea unakuwa kwa kasi hata Tanzania. Hivyo ningeshauri pamoja na kupigana na rushwa na mafisadi tujiulize je ni kitu gani tufanye au tushauri kuhimiza elimu, technologia, nishati, barabara na maji kwa watanzania wenzetu?.

Hatutaweza kuwa na maendeleo kama topic zote zitakuwa kumshambulia raisi kwa madongo bila kushauri serikali ifanye nini. Tatizo la Tanzania si Kikwete pekee kwani matatizo yalikuwepo kabla ya Kikwete!. Nahimiza kwamba Watanzania kuna matatizo mengine si ya kisiasa bali ni ya nchi mfano.

Tatizo la umeme limetokana na rushwa za viongozi hasa CCM lakini tatizo la nishati linarudisha nyuma nchi nzima si CCM pekee na tatizo la nishati halijaanza wakati wa kikwete!! ningeomba tufikirie bila siasa kwani hili sasa ni janga la Taifa!!. Ningeweza kutoa mifano mingi lakini ndugu zangu tuache kushambulia wanasisa kibinafsi bali ki agenda.
 
Mwambie jk ajipe yeye kwanza heshima kabla wengine hawajampatia. Yeye mwenyewe hajiheshimu, sembuse sisi, looooohhh!! Kama alidhani mtu yeyote anaweza kuwa rais basi alikosea sana. Hata uwaziri tu aliopewa na mzee mwinyi ilikuwa ni upendeleo tu. Kikwete alifaa akae kwenye kichama tena kwenye kitengo cha Tambwe Hiza. Hapo ndipo pangemfaa zaidi.
 
Back
Top Bottom