Tulionusurika kufa maji tukutane hapa

Tulionusurika kufa maji tukutane hapa

Aisee, mwaka fulani nikiwa form 1 nilitaka kuagana na ugali kimasihara hivi.
Ilikuwa boarding skul, jioni tulikuwa na kawaida ya kwenda kuogelea ziwa Victoria..Nakumbuka hiyo siku ziwani kulikuwa kumechafuka sana, maji jirani na tulipokuwa twaogelea hayakutamanika kwa uchafu, hivyo tukaamua kusonga mbele zaidi ili tupate maji masafi, sikuwa mzuri sana katika kuogelea hivyo nikawa natumia dumu ya litre 5 kupata support (boya) nimefika umbali mrefu nikajaribu kupima kina cha maji, aisee nilihisi kama maji yananinyonga vile, kina kilikuwa kirefu nikakosa pumzi nikipiga yowe nakunywa vikombe vya kutosha, nikakata tamaa ya kuokoka, giza likatanda, nikaanza kujutia dhambi zangu, nikamkumbuka mamangu nyumbani, ndgu zangu, nikaikumbuka hadi ile siku naletwa shule kuripoti machozi yakanitoka nakufa kizembe[emoji22].

Kumbe katika purukushani zile wanafunzi wenzangu waliokuwa nchi kavu waliniona wakawa wanaduwaa hawajui wafanye nini, kuna sister mmoja (alikuwa form 2 alikuwa fundi wa kuogelea) kajitosa kuja kuniokoa....Kafanikiwa kuniokoa ingawa kwa mbinde maana kila alikuwa akijaribu kunipa mkono nimshike naambulia vikombe, ikabidi anyooshe mguu wake nikafanikiwa kuudaka, kafanya machachari yake mara niko mgongoni kwake[emoji120][emoji120][emoji120]

JACQUELINE popote ulipo Mwenyezi Mungu akujalie kila lililo jema. Bila roho mtakatifu kukuongoza giza lingetanda siku hiyo hiyo..
Aisee, pole sana.Niliimiss hii post.

Kale kafeeling unakokapata mara ya kwanza ukishajua hauna control ya maisha yako tena ni noma.
 
Aiseee... nimeponea scenario 2. Sitakaa nisahau.
Sisi wachagga mito yetu ilivyo na mawe kuogolea wapi na wapi kwamfano?

1. Enzi hizo tukienda moshi likizo bwana kila actuvity hutaki kumiss. Kuna vibarua walikua wanaenda shamba Ibukoni huko. Sina hata kilo za nyama enzi hizo kadogo tu. Bibi alibikataza sana kwani naelewa. Nataka nikale maembe huko mwai. Wooi, tukaenda na binamu yangu haooo tukafika shamba. Miye nahangaika tu huku na huku. Binam yangu alikua na mdogo wake pia mdogooo tena kunizidi. Binamu alikua mkubwa na ana mwili. Muda wa kurudi ukafika. Uuwuuii, mvua iliyokuja utasema huko mbinguni malaika wa zamu alibet mkeka ukachanika. Barabara zote zimejaa maji. Kumbuka hiyo ni kupanda. Nikawa naona kizunguzungu. Tukafika mahali kuna mfereji unaenda kuunganisha na bonde ni kama mto hivi linapeleka maji kenya. Mdogp wake binamu akavuka kwanza, huyoo akachukuliwaa, nikawa nayadharau yale maji. Na mimi nikavukaa. Weeee, nikajikuta hata kusema maa siwezi napambana kujiokoa. Aisee yule binam yangu kwa hofu alirukia kwenye maji akaanza nitoa mimi, then later akamtoa mdogo wake. Yaan angechelewa tukafija kwenye lile bonde ndo basi wangesubiria miili yetu kenya iletwe tena tz kutuzika.

2. Hii nilienda marangu mtoni kwa mamdogo wangu ameolewa huko. Ule mto na kwake pamepakana. Hata maji enzi hizo wanachota huko kuna mifereji ndo huchota maji yake. Siku moja wakawa wanaenda kuogelea. Watu woote wanaogelea. Mimi peke yangu ndo nimebaki kwenye jiwe nawaangalia wanavyodive. Hapo pia kadogo kweli. Nikasema jaman si na mimi naweza? Wooiii si na mimi nikajidumbukiza1[emoji23][emoji23][emoji23] nilikunywa maji apaaaa womii[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] sasa kuna binamu akiwa yuko ndani ya maji akahisi kama ameshika mtu maana miye hapo nasubiria kukata roho tuu[emoji23][emoji23] ila akawa anasita asije akamtoa nguva bure ila akajikaza kisabuni akasema liwalo na liwe, akaninyakua paaaap, kufika nje ya maji si huyu hapa fulani mungu wangu[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] msaada wa chap chap. Since then sitaki tabia mbaya na maji. Yaan hata uniue. Lama ni kuogelea natbeaga tu kwenye yale maji mafupu ya wet en world ama popote mahi mafupi
hahahahahah, aisee, pole sana Pendo.
 
Nikiwa Olevel tulifukuzwa ada tukaenda kudiba mtoni, sasa kuna msela angu alikua ajui kuogelea kimasiara masiara watu wakamtosa kina kirefu mara kikombe cha kwanza mara chapili, mi nkajitia ufundi nkamuokoe jamaa alikua mbavu alinipiga roba anapanda mwilin mwangu awe juu apumue mi niwe chini, kila nkitoa wap piga ngumi wap, mpaka nkapanic, thank to God nkapata akili ya kuzama chini ndo kuniachia nkapita chin kwa chini nkatoka njee tukamrushia mgomba ndo kumvuta nao......! nkuanzia siku iyo ukitaka ugonvi naewe zungumizia mambo ya kuogea
Niliwahi kusikia kuwa mtu anayezama ukimuwahi pale pale kumuokoa anaweza kukuzamisha wewe muokoaji...
 
hahaha asante,
ilikuwa coco beach 2011 wakati huo maji yalikuwa yamejaa sasa pale coco maji yakijaa mpaka kule kwenye ile mimawe mikubwa (rocks) kote maji yanakuwa full pia.
sasa watu wanajirusha kutokea juu ya yale mawe wanazama baharini hapo ndo tamaa iliponiingia, kumbuka sijui kuogelea hapo (yani sina uwezo kukaa kwenye kina kirefu) sasa ile najitupa kutokea juu ya mawe nikazama mpaka baharini baada ya kuona haya maji si size yangu nikapanic niwahi kutoka nje hapo ndo picha linaanza sasa.
ndo maana nikasema siku zangu zilikuwa bado, baada ya kutapatapa kupiga mbizi nikachoka na pale pale nika give up tena nilishahadia kabisa nikasema kwaheri ya kuonana hiyo.
bahati nzuri sasa, nikayaona yale mawe makubwa ambayo juu yake watu ndo wanaruka kuingia kwenye maji nikayafata ikawa kama boya langu nikaenda nalo kwa kulishika mpaka namefika ufukweni.
niliponea hivyo, ila nilipiga lita kadhaa ya maji ya chumvi acha mdomo upasuke.
Pole sana.Yaani pale unapoona maji yashakuzidi, kale kafeeling ni hatari sana.
 
hahaha asante,
ilikuwa coco beach 2011 wakati huo maji yalikuwa yamejaa sasa pale coco maji yakijaa mpaka kule kwenye ile mimawe mikubwa (rocks) kote maji yanakuwa full pia.
sasa watu wanajirusha kutokea juu ya yale mawe wanazama baharini hapo ndo tamaa iliponiingia, kumbuka sijui kuogelea hapo (yani sina uwezo kukaa kwenye kina kirefu) sasa ile najitupa kutokea juu ya mawe nikazama mpaka baharini baada ya kuona haya maji si size yangu nikapanic niwahi kutoka nje hapo ndo picha linaanza sasa.
ndo maana nikasema siku zangu zilikuwa bado, baada ya kutapatapa kupiga mbizi nikachoka na pale pale nika give up tena nilishahadia kabisa nikasema kwaheri ya kuonana hiyo.
bahati nzuri sasa, nikayaona yale mawe makubwa ambayo juu yake watu ndo wanaruka kuingia kwenye maji nikayafata ikawa kama boya langu nikaenda nalo kwa kulishika mpaka namefika ufukweni.
niliponea hivyo, ila nilipiga lita kadhaa ya maji ya chumvi acha mdomo upasuke.

Oh no. Pole sana.

Naona Malaika wa siku hiyo alikuambia tulia dogo sipo na wewe leo.😉😉
 
Sisemi ni wapi ila nakumbuka hiyo siku niliendaa maahali mimi na jamaa zangu.

Tukawa tuna gonga vitu na siku hiyo tuliingia sehemu classic kidogo. Yaa watoto kama jeshi.

Basi bwana kwakuwa nilikuwa na aibu kidogo nikawa sina mzukaa na maji kuogelea baada ya kunywaa sana mzuka ukaja. Nikasema ngoja nikaogele na watoto kulee maana niliona majamaa wanajizolea tu.
Nikazama nikaanza kuogelea na hapo mimi si mtaalamu sana huwa natumia ile njia ya kubana pumzi nazama chinii [emoji1787][emoji1787] naibuka kama nyangumi, ila hii staili ya kawaida siwezi.

Nika zama bwana baada ya kuona watoto wanaeleweka nikawa najikaza na vinywaji vyangu kichwani. Bwana weeeee wimbi lili kuja likani piga nikazama chini huku nabilingita, kimoyo moyo nikasema nakufaa sasa ile kuibuka naona boxer kama yangu. Najishika chini lahaulaa !!!

Kweli maji sio poa.
Kwamba boxer ilikuvuka?😀😀😀
 
Jana nimepita hapa. Usiku napigiwa CM watoto wawili wamekufa maji. Mmoja mtoto wako ndugu yangu. Imeniuma mno asee
 
Acha kabisa.....tangu 1996 sitaki kuyasikia maji yaani bahari naiangaliaga kwa Mbali tu
 
1988 Bagamoyo palikuwa na Beach ikiitwa nadhani BADECO Mwenyewe nimezoea maji ya mto Ruaha si nikavamia bahari huku nikiwa na konyagi kidogo kichwani halafu sifa kwa watoto wa kike tumekodi coaster kutoka Magomeni duh yaliyonikuta kwa kweli mpaka leo maji ya bahari mimi ni msindikizaji tu
 
Dah acha kabisa kifo cha Maji kilinikosa Mwaka 2000, nilikuwa nimeenda kuvua samaki MTO wenye kina kirefu wenye mamba. Sasa tumevua tumemaliza ile naenda kupanda mtumbwi tu nikateleza na kuzama kutokana na utelezi Wa mtumbwi kukaa na Maji. Nikapiga kikombe kimoja, Jamaa yangu akazama na kuniokoa.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom