Tulionusurika kufa maji tukutane hapa

Tulionusurika kufa maji tukutane hapa

Hahahahaha
Mi maji yalikua yaniue Jangwani sea breeze. Nimeenda na cousin wangu mmoja na ndugu wengine wawili kufika wao wanaogelea kwa raha. Mimi nikaingia pia nikaanza kuogelea bana acha nikanyage chini kuteleze. Sasa namna ninavyoteleza nazidi kuelekea kwenye kina kirefu. Nikawa nazama naibuka namwita cousin akawa sijui hanielewi. Yani nilijump moja nikamshika tukazama wote ndo alipojua kwamba nazaama huku. Niliishia kuogelea kwenye kabwawa ka watoto. Kwa kweli bado sijayachoka maji natamani kujua kuogelea aisee
 
Aisee, mwaka fulani nikiwa form 1 nilitaka kuagana na ugali kimasihara hivi.
Ilikuwa boarding skul, jioni tulikuwa na kawaida ya kwenda kuogelea ziwa Victoria..Nakumbuka hiyo siku ziwani kulikuwa kumechafuka sana, maji jirani na tulipokuwa twaogelea hayakutamanika kwa uchafu, hivyo tukaamua kusonga mbele zaidi ili tupate maji masafi, sikuwa mzuri sana katika kuogelea hivyo nikawa natumia dumu ya litre 5 kupata support (boya) nimefika umbali mrefu nikajaribu kupima kina cha maji, aisee nilihisi kama maji yananinyonga vile, kina kilikuwa kirefu nikakosa pumzi nikipiga yowe nakunywa vikombe vya kutosha, nikakata tamaa ya kuokoka, giza likatanda, nikaanza kujutia dhambi zangu, nikamkumbuka mamangu nyumbani, ndgu zangu, nikaikumbuka hadi ile siku naletwa shule kuripoti machozi yakanitoka nakufa kizembe[emoji22].

Kumbe katika purukushani zile wanafunzi wenzangu waliokuwa nchi kavu waliniona wakawa wanaduwaa hawajui wafanye nini, kuna sister mmoja (alikuwa form 2 alikuwa fundi wa kuogelea) kajitosa kuja kuniokoa....Kafanikiwa kuniokoa ingawa kwa mbinde maana kila alikuwa akijaribu kunipa mkono nimshike naambulia vikombe, ikabidi anyooshe mguu wake nikafanikiwa kuudaka, kafanya machachari yake mara niko mgongoni kwake[emoji120][emoji120][emoji120]

JACQUELINE popote ulipo Mwenyezi Mungu akujalie kila lililo jema. Bila roho mtakatifu kukuongoza giza lingetanda siku hiyo hiyo..
Sio vizuri ila nimecheka mpaka machozi yamenitoka bro kwa namna ulivyosimulia. Maji nayaheshimu kwa heshima zote aisee
 
Nilichogundua hapa wengi wanasema '"nilienda kina kirefu nikazama".Hao wote ni waogaji maji sio waogeleaji.
Ukijua kuogelea huna haja ya kujua kina cha maji,yaani unakuwa na uwezo wa kuelea juu ya maji.

Wapo wanaopatwa na dharula kwenye maji wakafa au kudhurika,japo ni waogeleaji wazuri kutokana na kubanwa na misuri.
 
sitosahau siku nlikuwa naogelea nkiwa kwenye kina kirefu swimming pool pale jangwani sea breeze daaah kimbembe kilikuja jamaa mmoja alinishika mjuu ko nkawa siwez kusimama nlikunywa vikombe mbaya kabisa. baada ya hapo nlienda jitapisha ila kwanzia siku hyo sijawah ogelea pakiwa na watu wengi
 
Teh teh..Ilikuwaje mkuu
Anasema wakati anaogelea aliteleza nafikiri lilikua halijasafishwa vizuri. Pamoja na kujua kuogelea vizuri ilibidi washkaji zake waingie wamtoe na tayari ashakunywa lita za kutosha tu maana anasema alipanick.
 
Anasema wakati anaogelea aliteleza nafikiri lilikua halijasafishwa vizuri. Pamoja na kujua kuogelea vizuri ilibidi washkaji zake waingie wamtoe na tayari ashakunywa lita za kutosha tu maana anasema alipanick.
Kwenye hatari mara nyingi kinachowaua watu ni panic..Mtu unashindwa kufanya maamuzi sahihi kwa wakati ukishapanic.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom