Duuh huu Uzi umenikumbusha mbali Sana
Ilikuwa mwaka 2011 nikiwa form six huko mwanga Kilimanjaro ,alikuja dada mzungu jirani na shule basi nikaja kumshobokea na viinglish vyangu vya broken.
Mtoto akaja kukolea akawa anakuja school asiponiona analia basi masela wananisaka Kila chimbo kwamba mzungu wako analia huko.
Basi siku moja kaja na wazungu wenzake Kama watatu wakasema tukaogelee, nikawabeba washkaji zangu Kama kumi ivi..
Kufika bwawa lenyewe la umwagiliaji limejengwa kwa sakafu,basi watu wakapunguza nguo wakaanza kuruka kwenye maji ,kiukweli mi sijui kuogelea nkabaki mwenyewe nje nawashangaa Mara wakaanza come on men sio parefu
Nkaona itakuwa aibu niende na watasha alafu wajue sijui kupiga mbizi Mara nkapunguza nguo nkasogea nyuma umbali wa Kama mita kumi nkakimbia nkajitosa kwenye bwawa bwaaaaa
Watu ohhh oyeeee hiooo ....Mara naibuka nazama ,naibuka nazama nikaona ndo mwisho tayari sasa
Ikafika hatua sasa nikiibuka kidogo nanyoosha mikono kuomba msaada tatizo sasa wenzangu wakajua ni manjojo daah nlikunywa maji machafu Kama Lita tano ivi nahisi
Basi akaja malaika wa mungu ,jamaa mmoja akatambua nimezidiwa akaja akaniokoa daaah
Niliumwa U.T.I Kama mwezi mzima ivi
"Ukitaka kujua maji sio uhai we Zama tu utapata mrejesho"
Kwa sasa ata maji ya beseni tu nayaogopa ..