Igombe fisherman
JF-Expert Member
- Apr 28, 2017
- 2,262
- 4,052
Ah kumbe ni simulizi za mabwawa na beach? Nilidhani ni kule tunakoenda kufuata sangara
[emoji23][emoji23][emoji23]Ilikua pande za bahari beach kwa kando hivi.
niko na marafiki zangu wanapata msuba mi nikaona isiwe mambo ngoja nikapige mbizi.
Basi nikawa naogelea maji ya level yangu baada ya muda hivi nikawa narushrusha miguu na mikono nikawa naelea elea nikajiona yes nishajua kuogelea. Nikawa nafanya hivyo nikichoka nakanyaga chini. Sasa nilielea kwa muda mrefu kidogo kumbe maji yalishanipeleka kwenye kina kirefu. niliposema nishushe miguu nikanyage chini ndio balaa lilipoanza. Miguu haifiki chini na nishakunywa vikombe kadhaa. Nikaanza kutapatapa piga maji kama sina akili nzuri nilitoka niko hoi washkaji wanafurahi eti duh unayakata maji. kumbe mwenzao nimeponea tundu ya sindano.
Day one nmeingia Raskazone nkafanya yng ile natoka kucheki mguuni nkajiona kama nmekatwa na kiwembe...kumbe ni hiyo mimawe[emoji848]Hahaha ni epamiss tangaaa, ila yale mawe ya raskazoni yanakata miguu hapana aisee[emoji23][emoji23]
Hahaha poleee. Yanakata balaaa. Yanakata mnoo[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] sitasahauDay one nmeingia Raskazone nkafanya yng ile natoka kucheki mguuni nkajiona kama nmekatwa na kiwembe...kumbe ni hiyo mimawe[emoji848]
Daah hatari sana aisee...yani ndo unanisanua sa hivi eti...nlikuwa sijui mkuuHahaha poleee. Yanakata balaaa. Yanakata mnoo[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] sitasahau
Wewe ndio yule jamaa wa arusha?nimenusurika kusombwa na maji ya mfereji meeen
Ni mawe yale mwayaDaah hatari sana aisee...yani ndo unanisanua sa hivi eti...nlikuwa sijui mkuu
[emoji16][emoji16][emoji16] mkuu mita 500 kutafuta daraja ungepambana tu uibukie upande wa pili ila Pole SanaMaji yote naogelea niko vizuri tu. Baharini saaana coco beach, Mbudya beach. Kunduchi beach.
Ziwani poa, swimming pool ndo kabisaa.
Kimbembe siku moja nimesafiri kwenda kijijini kwetu nkakuta vitoto vidogo vinaogelewa mtoni kumbe vizoefu na maji ya mto. Nkajisemea siwezi kushindwa na hivi vitoto ngoja nivionyeshe show 😀 😀 😀 .
Weeeee..... maji ya mto staki hata kuyasikia tena, kumbe yanakina na kasi ya ajabu kwa chini yalinizoa nlipambana nayo yakanipeleka kama mita 30 nikatokea upande wa pili wa mto.
Ndugu wee... nlitembea nimevaa boxer tu kama mita 500 kutafuta daraja nirudie nguo zangu upande nlikotokea. Toka siku hio maji yanayotembea MARUFUKU!!!
Muongo sana we jamaa.Aisee mi pia naziheshimu swiming pool nilinusurika kuzama hoteli moja kule south afrika! Aisee, acha tu. Nilijirusha kumbe nimerukia kwenye kina kirefu, najaribu kusimama nikagundua sigusi chini! Nikapaniki! Ikabidi nikubali kuzama hadi nikakanyaga chini nikaanza kutembea kuelekea kwenye kina kifupi! Aah! Aisee siwezi sahau na nilikuwa peke yangu, kama pool ingekuwa pana sana hata sijui ingekuwaje, ni neema za Mwenyezi MUNGU tu ndio ziliniokoa
Hadi leo huwa naenda mahotel mengi tu lkn sina urafiki na swiming pools kabisa.
Umenichekesha sana we jamaa. Hivi enzi za Biafra hatukuwahi kwenda Coco pamoja kweliDaah Nakumbuka Ilikuwa 1993 maeneo ya Mabibo Chumbwinchu au Beach Kidimbwi kwa sasa lilipo Kanisani Katoliki Yohana Mbatizaji Luhanga, Ilikuwa mida ya km saa 5 asubuhi hivi tuko Kama 4 hivi, wenzangu wanajua kuogelea Maji yalikuwa yapo mengi Enzi zile na masafi Ambayo Yale yameanzia kule Tabata TIOT inaitwa nadhani mto kigogo au mto Tenge,Basi Bwana wenzangu wakaingia kuogelea, nawaona wanavyoyakata Maji nikaona Kumbe Rahisi hivi, si ndio Nami nikajituma niingie, Maji mengi na yanatembea kwa speed, Ile Naingia tu, nikazama mazima, nikazama nikaona maluweluwe, nikaibuka juu, nikazama tena, ndio wakastuka Kuwa Mimi Sijui kuogelea, ikabidi waniwahi haraka kunishika na kunitoa nje, natetemeka, ikabidi turudi home muda huo huo, ikapita wiki sijasimulia home, jamaa nilioenda nao ndio wakasimulia mtaani
Hahaha, ww jamaa nimekudanganya nini mkuu? Hiyo ni true story bro it was 2014 mji mmoja unaitwa mulders drift nje kidogo ya johanessburgMuongo sana we jamaa.
Umedanganya hapo uliposema kuwa ukaamua kuzama mpaka chini then ukaanza kutembea kuelekea kina kifupi.Hahaha, ww jamaa nimekudanganya nini mkuu? Hiyo ni true story bro it was 2014 mji mmoja unaitwa mulders drift nje kidogo ya johanessburg
Acha hizo kamba mkuuSisemi ni wapi ila nakumbuka hiyo siku niliendaa maahali mimi na jamaa zangu.
Tukawa tuna gonga vitu na siku hiyo tuliingia sehemu classic kidogo. Yaa watoto kama jeshi.
Basi bwana kwakuwa nilikuwa na aibu kidogo nikawa sina mzukaa na maji kuogelea baada ya kunywaa sana mzuka ukaja. Nikasema ngoja nikaogele na watoto kulee maana niliona majamaa wanajizolea tu.
Nikazama nikaanza kuogelea na hapo mimi si mtaalamu sana huwa natumia ile njia ya kubana pumzi nazama chinii [emoji1787][emoji1787] naibuka kama nyangumi, ila hii staili ya kawaida siwezi.
Nika zama bwana baada ya kuona watoto wanaeleweka nikawa najikaza na vinywaji vyangu kichwani. Bwana weeeee wimbi lili kuja likani piga nikazama chini huku nabilingita, kimoyo moyo nikasema nakufaa sasa ile kuibuka naona boxer kama yangu. Najishika chini lahaulaa !!!
Kweli maji sio poa.
Yule ni mwehu wa ngono...Vipi khs maradhi? Yeye haogopi?
Mkuu ni swiming pool sio bahari, infact sijakusimulia yote, nilipata tabu, kupiga hatua kwenye maji ni kazi, nikawa nikifika chini naruka juu kutafuta pumzi huku naendelea kupiga vikombe kadhaa. Ni bahati tu niliufikia ukingo wa swiming pool mapema ila chamoto nilikiona. Siku hiyo ndio nilijua kwanini mfa maji haachi kutapatapa, maana nilitapatapa sana hadi kuufikia ukingo.Umedanganya hapo uliposema kuwa ukaamua kuzama mpaka chini then ukaanza kutembea kuelekea kina kifupi.
Hiyo kitu haipo mkuu
Yaani hadi ukaweza kuruka juu pia ukiwa chini ya maji uku unajilazimisha kutembea kwa chini. Bado sipati picha. Labda umalizie story yakoMkuu ni swiming pool sio bahari, infact sijakusimulia yote, nilipata tabu, kupiga hatua kwenye maji ni kazi, nikawa nikifika chini naruka juu kutafuta pumzi huku naendelea kupiga vikombe kadhaa. Ni bahati tu niliufikia ukingo wa swiming pool mapema ila chamoto nilikiona