Tulionusurika kufa maji tukutane hapa

Tulionusurika kufa maji tukutane hapa

Yaani hadi ukaweza kuruka juu pia ukiwa chini ya maji uku unajilazimisha kutembea kwa chini. Bado sipati picha. Labda umalizie story yako
Mkuu ni kweli sema tu swiming pool haikuwa pana sana, mahali nilipozama pia nadhani haikuwa kina kirefu sana huenda hata nywele zilikuwa juu ya maji ila uso mzima ndio umezama. Pia ni longtime siwezi simulia exactly ilivokuwa, ila nilitoka kwa staili hiyo ya kujirusha na kutupa mikono na kujivuta hadi ukingoni. Kutembea chini kwa chini huenda nimeongeza chumvi mkuu!!!
 
Nakumbuka 2016 July , nikiwa naogelea pale kipepeo beach. Nikiwa deep nilimwona jamaa mmoja kaja na Mke wake jamaa akakaa ktk vile viti vya karibu na mwanzo wa maji, ilikuwa ni msimu wa mawimbimbi makubwa. Yule mke wake ni wa umri kidogo, nikamwona anaingia kwenye maji

Kama bahati tu yule mama alifika maji ya kina cha kifuani kwake Mimi nikawa namwangalia bila sababu yoyote, Mara akaingia ndani ya maji. Nikawa najaribu kuangalia ili nione uzoefu wake,cha ajabu sioni akiibuka Juu, Kama dk 1 nzima hivi. Kwa sababu Mimi najua ni vigumu mtu kukaa ndani ya maji kwa dk 1 Kama siyo mzoefu, nikawa na Mashaka, nikapiga kelele kumstua Yule jamaa yake jamaa hasikii, na Mimi nilikuwa mbali kidogo deep sea. Ikabidi niyakate maji kwa kasi sana.

Nikafika pale alipozama namuita jamaa yake ndiyo anastuka. Alikuwa anachat. Nikazama ndani nikamuibua. Cha ajabu hapa alipozama ni maji ya kifuani tu. Nikamtoa alikuwa keshazimia. Nikamlaza ufukweni na jamaa yake sasa akawa anasaidia nikampamp kuifuani aka rushwa maji mdomoni Kama bomba la dawasco limepasuka. Akazinduka. Jamaa alinishukuru sana, alinipa Laki 3, Nilikataa zile pesa lakini jamaa alinisisitiza sana, nikachukua. Nilimwokolea mke wake. Kumbe Yule mama tangu azaliwe hajawahi kuongelea, ilikuwa Mara ya kwanza kwake.

Angalizo.
Maji Kama hujui kuogelea ni hatari sana, yanaweza kukua ndani ya dk 3 tu
 
Hii imewahi kunikuta..Nilikuwa sijui vizuri kuogelea..Uogeleaji wangu ilikuwa siangalii ninapokwenda..Kichwa kipo ndani ya maji macho nimefumba..Nikaanza kwenda wrong direction naelekea kwenye kina kirefu bila kujijua..

Imefika stage nataka nisimame miguu haifiki chini then naanza kuzama..Nilidata..Nikianza kupiga mbizi kwa kasi huku sijui naelekea wapi..Hapo nishapanic..Mungu alikuwa upande wangu,nilikuwa naelekea kwenye kina kifupi..

Baada ya kuchoka kabisa na kuona siwezi tena kuendelea nikaamua nisimamame..Nikagusa chini..Maji yapo kifuani..Nilitembea hadi nje nikabeba nguo zangu na kusepa bila kuaga washkaji...

Hii siku siji kuisahau kamwe..
Bila shaka siku hiyo ulijua kanuni ya kuogelea na kuheshimu maji..ukiona maji mazito toka usife..
Nadhani baada ya hapo ulikuwa muogeleaji mzuri
 
Hapo sawa mkuu. Nilitaka nishangae hapo kwenye kutembea chini kwa chini. Tupo Pamoja sana.

Binafsi mara ya kwanza ilikuwa Moshi kuna mto hapo mbali sana na Vunjo Sec kulikuwa na dimbwi. Mara zote nilizoea kuingia kwenye maji mnachezacheza tu maana ni padogo ila sasa kulikuwa na style watu wanakaa juu ya jiwe alafu wanajirusha. Mi nikaiga ila kosa nililofanya ni kuwa nilitanguliza kichwa nikashuka mpaka chini alafu nikakutana na jiwe. Nimeibuka nikajikuta nimepasuka na damu zinavuja sana. Nahisi nilipata madhara sana maana kichwa kilivimba sana wiki nzima na mbaya zaidi nyumbani sikusema ukweli. Nilidanganya kuwa nilikuwa naangua maembe jiwe likanidondokea kichwani.

Mara ya pili Coco beach nilijisahau nikaenda mbali alafu misuli ya miguu ikakaza. Kilichoniokoa ni jamaa walikuwa na boya jirani nikaliwahi vinginevyo ingekula kwangu
Mkuu ni kweli sema tu swiming pool haikuwa pana sana, mahali nilipozama pia nadhani haikuwa kina kirefu sana huenda hata nywele zilikuwa juu ya maji ila uso mzima ndio umezama. Pia ni longtime siwezi simulia exactly ilivokuwa, ila nilitoka kwa staili hiyo ya kujirusha na kutupa mikono na kujivuta hadi ukingoni. Kutembea chini kwa chini huenda nimeongeza chumvi mkuu!!!
 
Hapo sawa mkuu. Nilitaka nishangae hapo kwenye kutembea chini kwa chini. Tupo Pamoja sana.

Binafsi mara ya kwanza ilikuwa Moshi kuna mto hapo mbali sana na Vunjo Sec kulikuwa na dimbwi. Mara zote nilizoea kuingia kwenye maji mnachezacheza tu maana ni padogo ila sasa kulikuwa na style watu wanakaa juu ya jiwe alafu wanajirusha. Mi nikaiga ila kosa nililofanya ni kuwa nilitanguliza kichwa nikashuka mpaka chini alafu nikakutana na jiwe. Nimeibuka nikajikuta nimepasuka na damu zinavuja sana. Nahisi nilipata madhara sana maana kichwa kilivimba sana wiki nzima na mbaya zaidi nyumbani sikusema ukweli. Nilidanganya kuwa nilikuwa naangua maembe jiwe likanidondokea kichwani.

Mara ya pili Coco beach nilijisahau nikaenda mbali alafu misuli ya miguu ikakaza. Kilichoniokoa ni jamaa walikuwa na boya jirani nikaliwahi vinginevyo ingekula kwangu
Mkuu yaogope maji hata kama ni expert wa kuogelea, ukikaza msuri kama hamna mtu jirani ndio unaondoka hivo
 
Nakumbuka 2016 July , nikiwa naogelea pale kipepeo beach. Nikiwa deep nilimwona jamaa mmoja kaja na Mke wake jamaa akakaa ktk vile viti vya karibu na mwanzo wa maji, ilikuwa ni msimu wa mawimbimbi makubwa. Yule mke wake ni wa umri kidogo, nikamwona anaingia kwenye maji

Kama bahati tu yule mama alifika maji ya kina cha kifuani kwake Mimi nikawa namwangalia bila sababu yoyote, Mara akaingia ndani ya maji. Nikawa najaribu kuangalia ili nione uzoefu wake,cha ajabu sioni akiibuka Juu, Kama dk 1 nzima hivi. Kwa sababu Mimi najua ni vigumu mtu kukaa ndani ya maji kwa dk 1 Kama siyo mzoefu, nikawa na Mashaka, nikapiga kelele kumstua Yule jamaa yake jamaa hasikii, na Mimi nilikuwa mbali kidogo deep sea. Ikabidi niyakate maji kwa kasi sana.

Nikafika pale alipozama namuita jamaa yake ndiyo anastuka. Alikuwa anachat. Nikazama ndani nikamuibua. Cha ajabu hapa alipozama ni maji ya kifuani tu. Nikamtoa alikuwa keshazimia. Nikamlaza ufukweni na jamaa yake sasa akawa anasaidia nikampamp kuifuani aka rushwa maji mdomoni Kama bomba la dawasco limepasuka. Akazinduka. Jamaa alinishukuru sana, alinipa Laki 3, Nilikataa zile pesa lakini jamaa alinisisitiza sana, nikachukua. Nilimwokolea mke wake. Kumbe Yule mama tangu azaliwe hajawahi kuongelea, ilikuwa Mara ya kwanza kwake.

Angalizo.
Maji Kama hujui kuogelea ni hatari sana, yanaweza kukua ndani ya dk 3 tu
Aisee mbona balaa...!
 
Duuh! Noma sana, ndio alikuwa keshakufa huyu. Nadhani harudii tena
 
Huu uzi unatisha ngoja nisepe. Mimi zaidi ya kujisaidia haja kubwa pale coco enzi nikiwa primary sikumbuki lini nimeingia kwenye maji Tena.
 
Mwaka 1996 miezi ya mwanzo mwanzo kabla MV Bukoba haijazama ilikuwa Tabora hiyo, mjinga mmoja akanidanganya tukaenda kuogelea bwawa lipo sehemu moja inaitwa igombe, halafu akanificha kwamba lile bwawa lina mamba na viboko wengi sana.........kwa kweli kilichotokea huwa sitaki kukikumbuka kabisa na yule mjinga bahati nzuri alikufa, maana tofauti na hapo ningefanya kitu kibaya sana juu yake
 
Sisemi ni wapi ila nakumbuka hiyo siku niliendaa maahali mimi na jamaa zangu.

Tukawa tuna gonga vitu na siku hiyo tuliingia sehemu classic kidogo. Yaa watoto kama jeshi.

Basi bwana kwakuwa nilikuwa na aibu kidogo nikawa sina mzukaa na maji kuogelea baada ya kunywaa sana mzuka ukaja. Nikasema ngoja nikaogele na watoto kulee maana niliona majamaa wanajizolea tu.
Nikazama nikaanza kuogelea na hapo mimi si mtaalamu sana huwa natumia ile njia ya kubana pumzi nazama chinii [emoji1787][emoji1787] naibuka kama nyangumi, ila hii staili ya kawaida siwezi.

Nika zama bwana baada ya kuona watoto wanaeleweka nikawa najikaza na vinywaji vyangu kichwani. Bwana weeeee wimbi lili kuja likani piga nikazama chini huku nabilingita, kimoyo moyo nikasema nakufaa sasa ile kuibuka naona boxer kama yangu. Najishika chini lahaulaa !!!

Kweli maji sio poa.
Hahaaaa wewe mkuu kiboko
 
Mwaka 1996 miezi ya mwanzo mwanzo kabla MV Bukoba haijazama ilikuwa Tabora hiyo, mjinga mmoja akanidanganya tukaenda kuogelea bwawa lipo sehemu moja inaitwa igombe, halafu akanificha kwamba lile bwawa lina mamba na viboko wengi sana.........kwa kweli kilichotokea huwa sitaki kukikumbuka kabisa na yule mjinga bahati nzuri alikufa, maana tofauti na hapo ningefanya kitu kibaya sana juu yake
Daaah so jamaa aliliwa na mamba?
 
wengine tusikumbushie machungu. Ila niliishapiga vikombe ya kutosha kwenye maji chumvi ya bahari.
 
Mwaka 1996 miezi ya mwanzo mwanzo kabla MV Bukoba haijazama ilikuwa Tabora hiyo, mjinga mmoja akanidanganya tukaenda kuogelea bwawa lipo sehemu moja inaitwa igombe, halafu akanificha kwamba lile bwawa lina mamba na viboko wengi sana.........kwa kweli kilichotokea huwa sitaki kukikumbuka kabisa na yule mjinga bahati nzuri alikufa, maana tofauti na hapo ningefanya kitu kibaya sana juu yake

Tupe full story mkuu tujifunze. Ilikuaje mpaka ukaokoka?
 
Mkuu ni habari mbaya sana hiyo huwa sitaki kuifikiria japokuwa kwa sasa ina miaka 23 lakini nikiifikiria nahic kama ni ya juzi tu

Mkuu usitufanyie hivo mkuu. Kumbuka watu humu wanafunguka hata wenye stori mbaya kuliko yako. Humu ni eneo la kutema nyongo iliyoko mwilin. Hakuna naekufaham mkuu. Cha msingi ni ku skip eneo ambalo laweza kukufany ufahamike kwa wahusika
 
Duh miaka ya 1998 nikiwa darasa la nne nilipona kufa maji mara mbili huko Kajiado masaini ( olgulului).
mara ya kwanza tumeenda kundi kubwa la wanafunzi kufua na kuogelea mtoni mimi nikiwa sijui chochote kuhusu kuogelea. Nikafurahia watu wanavyoogela nikachojoa nguo nikajipaka sabuni nikawa nimesimama tu pembeni ya mto najiuliza nijitose nami au nichote maji na ndoo nikaoge pembeni? Ghafla mjinga mmoja akaona ninavyozubaa akaja nyuma yangu akanisukuma nikadumbukia kama jiwe. Sikuweza kufanya chochote kwa namna nilivyopanic ilikuwa nikiibukia napiga kelele mamaaa...maji yanazama mdomoni ya kutosha narudi chini..nilienda chini mara mbili ya tatu Brother mmoja akanidaka akanitoa nje niliokota nguo zangu nikakimbia uchi hadi karibu na shuleni ndo nikavaa na tangu siku hiyo nikifika mtoni nikawa naomba mtu anisaidie kuchota maji nikiwa umbali wa mita 10.
ya pili huko huko kwenye madimbwi ya wamasai wanaita silangee tumeenda kufua jamaa wakanisukumiza dimbwini nilikutana na bonge la tope hakuna rangi sikuona. Akajitokeza msamaria mwema akaja kuninasua akanitoa nje ile tunatoka tu mzee wa Kimasai kafika na fimbo zake tulichapwa balaa...kila akichapa fimbo yake (wanaita njibi njibi) inakata unashangaa damu inachuruzika...wote tulikimbia tukaacha nguo. It was terrible
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom