Tulionusurika kufa maji tukutane hapa

Tulionusurika kufa maji tukutane hapa

Kuna siku naogolea coco kumbe Sasa jioni maji Yana kuja na yanarudi yakanipeleka mbali bila kujua nakuja kushtuka Niko mbali Seema uzuri palikuwa na watu wengi ilibidi nimshike braza mwenye tairi..WANAWAKE wanapelekwa mbali halafu wanabakwa utafanyaje jamaa anataka kukuacha anakwambia mpe kidogo akuokoe??[emoji1787]
Nilishuhudia Mara tatu pale raskazone tanga kuna mshikaji yeye anawafundisha kuogelea anawapeleka mbali then anaomba abatizwe Maji mengi Demu akikataaaaa jamaa anatishia kumwachia aisee.demu anaamua ambatize tuu mshkaji...na alisema yeye akitaka papuch anashuka beach
 
Nakumbuka niko Advance Tanga.... Friends zangu wapenda maji kama samaki, sisi most of week end days tunatoroka shule kwenda kuogelea, tukiwa na ela tunaenda Raskazone tukifulia tunaingia deepsea.......!

Ilikua kawaida tukiwa Raskazone tunaogealea mpaka meli zilipotia nanga, pana umbali kidogo sasa siku moja tunatoka kwenye nanga turud nchi kavu misuli ikakaza, kila nikistrech wap, dooohhh nilitoa macho nkaomba Mungu aniepushe na kifo cha maji ila kwaushirikiano ya washkaji na mabaharie wengine nilirud salama......!

Kuanzia siku iyo nkawa nikitakakupiga zoez la kuogelea nnaenda parallel na bahari....
ukibanwa na musles baharini, ziwani au mtoni, na ukapona ukitoka hapo kasali kabisa na katambike, wengi wale wanaojiita wataalamu wanakufa kwa kubanwa na muscles
 
Aisee mi pia naziheshimu swiming pool nilinusurika kuzama hoteli moja kule south afrika! Aisee, acha tu. Nilijirusha kumbe nimerukia kwenye kina kirefu, najaribu kusimama nikagundua sigusi chini! Nikapaniki! Ikabidi nikubali kuzama hadi nikakanyaga chini nikaanza kutembea kuelekea kwenye kina kifupi! Aah! Aisee siwezi sahau na nilikuwa peke yangu, kama pool ingekuwa pana sana hata sijui ingekuwaje, ni neema za Mwenyezi MUNGU tu ndio ziliniokoa
hahahaha, we ndio ulidandia daladala kwa mbele aisee,
 
Duuh huu Uzi umenikumbusha mbali Sana

Ilikuwa mwaka 2011 nikiwa form six huko mwanga Kilimanjaro ,alikuja dada mzungu jirani na shule basi nikaja kumshobokea na viinglish vyangu vya broken.

Mtoto akaja kukolea akawa anakuja school asiponiona analia basi masela wananisaka Kila chimbo kwamba mzungu wako analia huko.

Basi siku moja kaja na wazungu wenzake Kama watatu wakasema tukaogelee, nikawabeba washkaji zangu Kama kumi ivi..

Kufika bwawa lenyewe la umwagiliaji limejengwa kwa sakafu,basi watu wakapunguza nguo wakaanza kuruka kwenye maji ,kiukweli mi sijui kuogelea nkabaki mwenyewe nje nawashangaa Mara wakaanza come on men sio parefu
Nkaona itakuwa aibu niende na watasha alafu wajue sijui kupiga mbizi Mara nkapunguza nguo nkasogea nyuma umbali wa Kama mita kumi nkakimbia nkajitosa kwenye bwawa bwaaaaa
Watu ohhh oyeeee hiooo ....Mara naibuka nazama ,naibuka nazama nikaona ndo mwisho tayari sasa

Ikafika hatua sasa nikiibuka kidogo nanyoosha mikono kuomba msaada tatizo sasa wenzangu wakajua ni manjojo daah nlikunywa maji machafu Kama Lita tano ivi nahisi

Basi akaja malaika wa mungu ,jamaa mmoja akatambua nimezidiwa akaja akaniokoa daaah

Niliumwa U.T.I Kama mwezi mzima ivi
"Ukitaka kujua maji sio uhai we Zama tu utapata mrejesho"

Kwa sasa ata maji ya beseni tu nayaogopa ..
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Maji yote naogelea niko vizuri tu. Baharini saaana coco beach, Mbudya beach. Kunduchi beach.
Ziwani poa, swimming pool ndo kabisaa.

Kimbembe siku moja nimesafiri kwenda kijijini kwetu nikakuta vitoto vidoogo vinaogelewa mtoni maji mengi ila kama yanaenda taratibu, kumbe vinauzoefu na maji ya mto. Nikajisemea siwezi kushindwa na hivi vitoto ngoja nivionyeshe show 😀 😀 😀 .

Weeeee..... maji ya mto staki hata kuyasikia tena, Baada ya kujitosa kumbe yana kina na kasi ya ajabu kwa chini yalinizoa nilipambana nayo yakanipeleka kama mita 30 nikatokea upande wa pili wa mto.

Ndugu wee... nlitembea nimevaa boxer tu kama mita 500 kutafuta daraja nirudie nguo zangu upande nlikotokea. Toka siku hio maji yanayotembea MARUFUKU!!!
 
Mtoto Wa mwalimu, jirani yetu akiwa f6 uko shule yeye ndio alikuwa mwalimu wa kuwafundisha wasichana wenzake.kuogelea.

Siku hiyo shetani alikuwa kazini, alizama wenzake wakajua si ndo zake anaendaga mbali, kumbe maskini alipozama alikutana na jiwe, kabamiza kichwa akafia huko huko.

Wenzake wakasubiri mwalimu wao mbona harudi? Ikabidi warudi shuleni kutoka taarifa, kumbe aliisha kufa na kuibukia mtaa wa 7.
Mbaya zaidi mama yake alizaaga huyo mtoto pekee na umri ulishaenda hawezi kuzaa tena, yule mama alilia zaidi ya mwezi alichanganyikiwa tangu Siku hiyo ni zaidi ya miaka 15 mpaka sasa ni kama kichaa, unaweza kukuta yupo njiani anaongea mwenyewe, umsalimie asikujibu.

Ilibidi alazimishwe kustaafu, hakuwa na uwezo kufundisha tena.
 
Hahaha

Ko mzee baba. Kohogweeee
Shule yetu nzuri ya korogweee... kule st. C mashost kama wote tuition cilos enzi hizo.
Niligoma kbs kutoka government. Nilionja raha maisha yalivyokua huru[emoji23][emoji23] na vile nikawa waziri wa menu kwa ubabe wangu baasii sikua na tatizo la chakula. Mawe hayafai ya raskazone aisee. Hayafai hata kidogooo
Oooohh.... Nmewamc sana zile times tunacheza disco kwetu afu kwenu!

Kipind yule dada ameparamia gari ya basha wake akatuaribia shughuli ulikuepo.....?
 
ukibanwa na musles baharini, ziwani au mtoni, na ukapona ukitoka hapo kasali kabisa na katambike, wengi wale wanaojiita wataalamu wanakufa kwa kubanwa na muscles
100% true..... Good luck nilikua niko na kampan kubwa bila hivyo ingekua stori nyingine!
 
Oooohh.... Nmewamc sana zile times tunacheza disco kwetu afu kwenu!

Kipind yule dada ameparamia gari ya basha wake akatuaribia shughuli ulikuepo.....?
Hahaha hapana kwakweli, nilikua nishagraduate. Ila alogongesha si yule mpuuz hata hajui kuendesha alikua anataka waoshea wenzake? Ndo keshampa kilema mwenzake cha milele na wengine kupoteza maisha. Very sad.

Ila tabia yenu ya kuazimana mashati ya tomato bwana[emoji23][emoji23][emoji23] mynakuja TYCS.

Sad enough mito yote pale ko una mamba[emoji23][emoji23] unaogelea wapiii
 
Nakumbuka niko Advance Tanga.... Friends zangu wapenda maji kama samaki, sisi most of week end days tunatoroka shule kwenda kuogelea, tukiwa na ela tunaenda Raskazone tukifulia tunaingia deepsea.......!

Ilikua kawaida tukiwa Raskazone tunaogealea mpaka meli zilipotia nanga, pana umbali kidogo sasa siku moja tunatoka kwenye nanga turud nchi kavu misuli ikakaza, kila nikistrech wap, dooohhh nilitoa macho nkaomba Mungu aniepushe na kifo cha maji ila kwaushirikiano ya washkaji na mabaharie wengine nilirud salama......!

Kuanzia siku iyo nkawa nikitakakupiga zoez la kuogelea nnaenda parallel na bahari....

Bila shaka umesoma galanos
 
Aisee, mwaka fulani nikiwa form 1 nilitaka kuagana na ugali kimasihara hivi.
Ilikuwa boarding skul, jioni tulikuwa na kawaida ya kwenda kuogelea ziwa Victoria..Nakumbuka hiyo siku ziwani kulikuwa kumechafuka sana, maji jirani na tulipokuwa twaogelea hayakutamanika kwa uchafu, hivyo tukaamua kusonga mbele zaidi ili tupate maji masafi, sikuwa mzuri sana katika kuogelea hivyo nikawa natumia dumu ya litre 5 kupata support (boya) nimefika umbali mrefu nikajaribu kupima kina cha maji, aisee nilihisi kama maji yananinyonga vile, kina kilikuwa kirefu nikakosa pumzi nikipiga yowe nakunywa vikombe vya kutosha, nikakata tamaa ya kuokoka, giza likatanda, nikaanza kujutia dhambi zangu, nikamkumbuka mamangu nyumbani, ndgu zangu, nikaikumbuka hadi ile siku naletwa shule kuripoti machozi yakanitoka nakufa kizembe[emoji22].

Kumbe katika purukushani zile wanafunzi wenzangu waliokuwa nchi kavu waliniona wakawa wanaduwaa hawajui wafanye nini, kuna sister mmoja (alikuwa form 2 alikuwa fundi wa kuogelea) kajitosa kuja kuniokoa....Kafanikiwa kuniokoa ingawa kwa mbinde maana kila alikuwa akijaribu kunipa mkono nimshike naambulia vikombe, ikabidi anyooshe mguu wake nikafanikiwa kuudaka, kafanya machachari yake mara niko mgongoni kwake[emoji120][emoji120][emoji120]

JACQUELINE popote ulipo Mwenyezi Mungu akujalie kila lililo jema. Bila roho mtakatifu kukuongoza giza lingetanda siku hiyo hiyo..
 
Nikiwa Olevel tulifukuzwa ada tukaenda kudiba mtoni, sasa kuna msela angu alikua ajui kuogelea kimasiara masiara watu wakamtosa kina kirefu mara kikombe cha kwanza mara chapili, mi nkajitia ufundi nkamuokoe jamaa alikua mbavu alinipiga roba anapanda mwilin mwangu awe juu apumue mi niwe chini, kila nkitoa wap piga ngumi wap, mpaka nkapanic, thank to God nkapata akili ya kuzama chini ndo kuniachia nkapita chin kwa chini nkatoka njee tukamrushia mgomba ndo kumvuta nao......! nkuanzia siku iyo ukitaka ugonvi naewe zungumizia mambo ya kuogea
Inasemekana unapotaka kumuokoa mtu anaye kunywa vikombe majini muaache Hadi akose nguvu kabsa ndo uende , la sivyo utazamishwa ww
 
Hahaha hapana kwakweli, nilikua nishagraduate. Ila alogongesha si yule mpuuz hata hajui kuendesha alikua anataka waoshea wenzake? Ndo keshampa kilema mwenzake cha milele na wengine kupoteza maisha. Very sad.

Ila tabia yenu ya kuazimana mashati ya tomato bwana[emoji23][emoji23][emoji23] mynakuja TYCS.

Sad enough mito yote pale ko una mamba[emoji23][emoji23] unaogelea wapiii
Haaaa.... Atuaziman zile tunazo for special occasion, Sasa Xul yenyewe ipo town mnaachaje kua smart...!

Sasa hivi ukienda mton uende na wajuvi wakupiga mbizi usijepotelea mto Nana!
 
Inasemekana unapotaka kumuokoa mtu anaye kunywa vikombe majini muaache Hadi akose nguvu kabsa ndo uende , la sivyo utazamishwa ww
Yah man!..... Nilishaskia case moja Ziwani walikufa muanga na muokoaji wakakutwa wamekumbatiana
 
Haaaa.... Atuaziman zile tunazo for special occasion, Sasa Xul yenyewe ipo town mnaachaje kua smart...!

Sasa hivi ukienda mton uende na wajuvi wakupiga mbizi usijepotelea mto Nana!
Hahaha munaazimana bana na kuyaloweka kwenye blue.

Ule mto pale tunaitaga ruvu ula naskia ni pangani. Na uba mamba kama wote. Na wenyeji pale wanakuambua ni wa mazindiko pale wanaoingia ni wenyeji tu na waliozindikwa. Usicheze na kilole[emoji23][emoji23] pale ndipo anatoka rais wa wachawi. Hata kychota maji walikua wanatuchotea wenyeji na siyo sisi. Yaan wale mamba wanasema wapo wa asili na wa wananchi wa pale[emoji23][emoji23]
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom